MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Tuesday, 3 September 2013

KASHFA YALIKUMBA JESHI LA POLISI TENA....... CAMERA ZA CCTV ZAZIMWA KURUHUSU UJAMBAZI



SIKU chache baada ya tukio la wizi mkubwa wa fedha katika Benki ya Habibu mjini Dar es Salaam, siri nzito zimeanza kuvuja kuwa polisi wanadaiwa kuhusika katika tukio hilo kwa kuhujumu kamera za usalama za CCTV zinazomilikiwa na jeshi hilo.
 
Katika tukio hilo, watu wanaodaiwa kuwa majambazi walipora dola za Marekani 20,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 32 za Tanzania.

Katika tukio hilo, Polisi Mkoa wa Ilala inamshikilia askari mmoja kwa kosa la kuhusika katika tukio hilo kutokana na kushindwa kuchukua hatua za haraka wakati tukio linatokea.

Habari za uhakika kutokana ndani ya jeshi hilo, zinasema siku ya tukio polisi waliokuwa zamu kuongoza mitambo hiyo, kwa namna moja au nyingine wanadaiwa kufanya hujuma hiyo, kwa lengo la kupoteza mawasiliano na maeneo mengi ya polisi.

Chanzo chetu hicho, kiliongeza kuwa siku ya tukio eneo lote la mzunguko wa barabara ya Uhuru na maeneo ya jirani na Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL), sehemu zote hazikuwa na huduma ya kamera za usalama, jambo ambalo si la kawaida kutokea.

“Hatua iliyofikia sasa ni mbaya, huwezi amini siku ya tukio kamera za CCTV zinazotumiwa na polisi zilizimwa kabisa, kitendo hiki kilisababisha polisi makao makuu wasijue nini kinachoendelea pale.

“Ndiyo maana utaona kuna askari mmoja anashikiliwa katika tukio lile, haiwezekani kituo kikuu kishindwe kubaini uwapo wa tukio hili, wakati kuna mawasiliano ya kutosha, umefika muda wa kulisafisha jeshi letu kwa kasi,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho, kilisema mitambo ya kamera hizo, ilizinduliwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa mwaka 2004 na imekuwa ikifanya kazi bila matatizo yoyote.

“Nimekuwapo hapa tangu mwaka 2004, kamera hizi zilipozinduliwa rasmi na hazijawahi kuharibika hata siku moja, iwe siku ya tukio zisifanye kazi,” kilihoji chanzo chetu.

Askari aliyekamatwa katika tukio hilo, anadaiwa anafanya kazi katika kituo cha Oysterbay Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alithibitisha kukamatwa kwa askari huyo.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipoulizwa na MTANZANIA jana, alisema ameipokea taarifa hiyo na wanaifanyia kazi haraka iwezekanavyo.

“Taarifa hii tumeipokea, tunaifanyia kazi haraka sana ili kupata ukweli, naomba tuwe na subira,” alisema kwa kifupi Kamishna Kova.

Alisema bado polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba watu waliokamatwa watafikishwa mbele ya vyombo vya dola
.
CHANZO MTANZANIA.

NYAMLANI NA MALINZI, WAPITISHWA KUWANIA NAFASI YA URAIS TFF

 



NYAMLANI (MWENYE TAI)

Wagombea wawili, Athumani Nyamlani na Jamal Malinzi wamepitishwa kuwania nafasi ya Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

MALINZI

Malinzi na Nyamlani ambaye anashikilia nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, wamepitishwa baada ya usaili uliofanyika jijini Dar es Salaam.

 
Upinzani kati ya Nyamlani na Malinzi umekuwa mkali sana tokea walipotangaza tu kugombea.


Katika nafasi hiyo kulikuwa na wagombea wanne na wawili kati yao hawakupita ambao ni Omary Mussa na Richard Lukambula.
Kwa upande wa umakamu wa urais, Wallace Karia na Iman Madega, mwenyekiti wa zamani wa Yanga, ndiyo waliopitishwa kuwania nafasi hiyo.
 

Wakati huohuo, usaili huo pia umemng’oa Shaffi Dauda aliyekuwa nawania ujumbe.

HIZI NDIZO TUHUMA NA KASHFA ZA UFISADI WA MALI ASILI

Imeandikwa na Danson Kaijage, Dodoma, Tanzania Daima — 
WAKATI mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), Mchungaji Peter Msigwa, akimtuhumu Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, kuibeba kampuni ya uwindaji ya Leopard Tours Ltd, mwenyewe amejibu mapigo akidai mbunge huyo hajafanya utafiti.

Msigwa aliwaambia waandishi wa habari jana mjini Dodoma kuwa Kagasheki alitumia nafasi yake kuiarifu kampuni hiyo kuipatia ekari tano kwa gharama ya dola za Kimarekani 30,000 nusu ya gharama za kawaida dola 60,000 kwa ekari kumi.

Mbunge huyo ambaye pia ni msemaji mkuu wa kambi ya upinzani kwa wizara hiyo, alisema kuwa Kagasheki anaendesha wizara kwa kukiuka sheria na taratibu akitumia mamlaka vibaya.

Msigwa alisema kuwa Kagasheki tangu alipoingia madarakani na kuivunja Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), sasa hifadhi inaendeshwa bila bodi jambo ambalo ni kinyume.

Alidai kuwa waziri huyo alifanya maamuzi
hayo ya kuibeba kampuni hiyo ya uwindaji bila kuzingatia sheria na kanuni za ugawaji wa vitalu na kwamba alivunja sheria kwa kufanya uamuzi wa moja kwa moja na Leopard Tours wa kushusha viwango vilivyowekwa kisheria bila kutoa tangazo la serikali.

Source: kwa habari zaidi bonyeza hapa www.wavuti.com

HOFU YA NJAANCHINI ZIMBABWE ZAIDI YA MILION MOJA NA NUSU WAKABILIWA NA NJAA



WFP linasema kuwa bei ya nafaka imepanda sana ikiwa moja ya sababu ya upungufu wa chakula

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa linasema kuwa zaidi ya watu milioni mbili nchini Zimbabwe wanakabiliwa na tisho la njaa katika miezi michache inayokuja.
Shirika hilo la , WFP, linasema kuwa mtu mmoja kati ya watu wanne katika maeneo ya vijijini wanahitaji msaada wa chakula.

Idadi hii ya watu wanaohitaji msaada inasemekana kuwa kubwa zaidi kushuhudiwa tangu mwaka 2009 wakati ambapo zaidi ya nusu ya wananchi walihitaji msaada kama huo.

Tatizo hilo ni mbaya zaidi Kusini mwa Zimbabwe ambako mavuno hayakuwa mazuri mwaka huu.
WFP linasema kuwa tisho la uhaba wa chakula limesababishwa na hali mbaya ya anga , bei ghali ya nafaka na ukosefu wa mbegu za hali ya juu, mbolea na mahitaji mengine ya kilimo bora.

Ili kukabiliana na hali nchini Zimbabwe, shirika la WFP na washirika wake litaweza kutoa nafaka, mafuta na mboga kwa watakaokabiliwa na hali mbaya zaidi.

Mnamo mwaka 2012,kwa mara ya kwanza serikali ya Zimbabwe ilitoa mbegu za thamani ya dola milioni 10 kwa wakulima kutokana na mradi walioshirikiana nao na shirika la WFP na washirika wake wengine kwa wilaya 37.

Ili Kuwasaidia watu kukabiliana na njaa, shirika la WFP limekuwa likiendesha mpango wa kuwapa watu pesa badala ya chakula katika maeneo ya vijijini tangu mwezi Juni.
Chini ya mpango huu jamii ambazo zinakabiliwa na tisho kubwa zaidi hupokea chakula au pesa wakati wakijihusisha na miradi ya kusaidia jamii kama vile ujenzi wa mabwawa.

WACHIMBA MIGODI WAANZA MGOMO AFRIKA KUSINI


Mgomo huu unatishia kuathiri sekta ya madini nchini Afrika Kusini
Takriban wachimba migodi 80,000 wa dhahabu nchini Afrika Kusini wanatarajiwa kuanza mgomo kudai nyongeza ya mishahara.
Chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa migodini kinataka waongezwe mishahara kwa asilimia sitini.
Wafanyakazi hao wiki jana walikataa pendekezo walilopewa la nyongeza ya asilimia 6 ambacho ni kiwango cha mfumuko wa bei kwa sasa.

Sekta ya madini ya dhahabu ndio moja ya sekta kubwa duniani lakini imekuwa ikikumbwa na misukosuko katika miaka ya hivi karibuni huku ile ya madini ya platinum ikijikwamua kutokana na athari za migomo iliyokumba sekta hiyo mwaka jana.

Inakisiwa kuwa migomo hiyo ya wachimbaji migodi ikiwa itafanyika, itapotezea nchi hiyo zaidi ya dola milioni 30 kila siku.

Wamiliki wa migodi wanaonya kuwa migomo hiyo huenda ikasababisha migodi ya dhahabu kufungwa na maelfu kupoteza kazi zao kufuatia kushuka kwa bei ya dhahabu.
Wanasema kuwa gharama za uchimbaji dhahabu zimepanda kwani wamelazimika kutumia pesa nyingi zaidi katika shughuli nzima za uzalishaji.

Kwa miezi mingi Afrika Kusini ilikuwa nchi yenye kuzalisha zaidi dhahabu ikiwa inazalisha asilimia 68 ya dhahabu yote duniani katika miaka ya sabini.
Lakini kwa sasa iko katika nafasi ya tano katika uzalishaji wa madini hayo ikiwa ni asilimia sita pekee ya dhahabu yote duniani ingawa bado ni sekta muhimu sana katika uchumi wa nchi hiyo.
Rais Jocob Zuma ametaka pande zote mbili kwenye mgogoro huu kuafikiana ili kuzuia hasara kwa pande zote mbili.

Wafanyakazi watalazimika kuondoka kazini saa sita asubuhi kwa mujibu wa msemaji wa chama cha wafanyakazi hao, alisema Lesiba Seshoka.

Hata hivyo alikanusha madai kuwa nyongeza wanayotaka ya asilimia 60 ni kubwa sana. Chama cha wafanyakazi cha NUM kinawakilisha asilimia 64 ya wafanyakazi 120,000 wanaochimba dhabahu migodini.

Wananchi wa Afrika Kusini walishangazwa sana mwaka jana wakati polisi walipowaua wachimba migodi 34 wa Platinum waliokuwa wamefanya mgomo haramu uliokuwa umeitishwa na chama chao na kutuhumu NUM kuwa na uhusiano wa karibu na serikali.

Mwandishi wa BBC Mike Wooldridge mjini in Johannesburg anasema kuwa huku uchaguzi ukisubiriwa mwaka ujao,
serikali inatumai kuwa itaweza kukabili migomo hiyo, katika msimu huu ambapo watu wengi wanaomba nyongeza ya mishahara.

MISRI YAFUNGA VITIO 4 VYA TELEVIONI VINAVYO PENDELEA CHAMA CHA BROTHERHOOOD

 
Jeshi linasemekana kudhibiti hali ya usalama Misri

Mahakama moja nchini Misri, imeamuru kufungwa kwa vituo vinne vya televisheni, ambavyo vimetuhumiwa kupendelea chama cha Muslim Brotherhood.
Vituo hivyo ni pamoja na kituo cha chama hicho, Ahrar 25 na tawi la kituo cha Al-Jazeera kinachopeperushia matangazo yake nchini Misri.
Wakati huohuo, jeshi la Misri, limefanya mashambulizi ya angani dhidi ya maeneo yanayoshukiwa kuwa ngome za wapiganaji wa kiisilamu katika rasi ya Sinai na kumuua mtu mmoja.
Jeshi linajaribu kuonyesha kuwa lina udhibiti wa eneo hilo linalopakana na Gaza.
Kufungwa kwa vituo hivyo, kunakuja baada ya serikali kufanya msako dhidi ya vyombo vya habari vinavyoonekana kuunga mkono rais aliyeondolewa mamlakani Mohammed Morsi, aliyepinduliwa na jeshi tarehe 3 mwezi Julai.

Vituo kadhaa pia vililazimia kufunga kufuatia hatua za kijeshi.
Sasa mahakama mjini Cairo, imeamuru stesheni ya Al-Jazeera, Mubashir Misr kufungwa na Ahrar 25 pamoja na vituo vingine Al-Quds na Al-Yarmuk.

Siku ya Jumatatu , Misri iliwafurusha waandishi watatu wa habari wa kigeni waliokuwa wanafanya kazi na Al-Jazeera ikisema kuwa hawakuwa na stakabadhi zinazohitajika kufanya kazi nchini humo.

Bwana Morsi amezuiliwa akisubiri kufunguliwa mashtaka .
Viongozi wa mashtaka walitangaza wiki jana kuwa atashtakiwa kwa kosa la kuchochea mauaji ya waandamanaji mwaka jana.

Vuguvugu la Muslim Brotherhood limeitisha maandamano chini ya kauli mbiu 'Mapinduzi ni ugaidi'.
Shirika la habari la serikali Mena, linasema kuwa maafisa wa usalama wameziba baadhi ya barabara huku magari ya kijeshi yakisemekana kuziba sehemu za kuingilia medani ya Rabaa al-Adawiya na Tahrir.

Monday, 2 September 2013

FELLAIN ATUA RASMI MAN UNITED, NA YAMSAJILI COENTRAO KUTOKA MADRID



Manchester United hatimaye imefanya kweli na kumsajili Marouane Fellaini kutoka Everton kwa dau la pauni milioni 27.5.
Awali Man United ilikuwa ikihaha na wengi walilalama kuhusu kiungo chake na sasa Kocha David Moyes aliyeonekana butu katika usajili amefanikiwa kumpata kijana wake huyo wa zamani.


Manchester United pia imemsajili Fabio Coentrao kutoka Real Madrid kwa mkopo nah hii ni baada ya kumkosa Baines wa Everton.
 


WATOTO WAWILI WAIBA FUNGUO ZA GARI WAENDESHA NA WAPATA AJALI MMOJA AFARIKI

Jiweke katika nafasi ya mzazi, fikiria una watoto wawili wadogo ambao hawajatimu miaka kumi.

Unaamka kuwatizama watoto, huwaoni. Unatizama kote kote, unagundua na gari nalo halipo.

Ni rahisi sana kufikiri kuwa watoto hao wametekwa na mtu aliyetumia gari lako. Kwa hiyo jambo la haraka ni kupiga simu polisi ili kupata usaidizi.

Lakini fikiria mshangao utakaokuwa nao baada ya kutambua kuwa watoto wako wenyewe ndiyo walioamua kujiendesha barabarani.

Hicho ndicho kilichotokea jijini Phoenix, Arizona siku ya Jumatano ya wiki jana.

Akiwaeleza askari polisi kwa uchungu, mama wa watoto wawili, mmoja wa kiume wa umri wa miaka 8 na mdogo wake wa kike mwenye umri wa miaka 6, anasema alishituka sana alipofahamishwa kuwa mwanaye
wa kiume ndiye aliyekuwa akiliendesha gari barabarani wakati binti yake akiwa ameketi kwenye kiti cha abiria.

Kutokana na kutokuwa na mafunzo yoyote ya udereva, mtoto huyo aliendesha gari hilo hovyo barabarani, jambo lililosababaisha madereva wengine wa magari wapige simu 911 kuwaeleza kinachoendelea. Kwa bahati, jirani wa watoto hao aliwaona walipolichukua gari na kuingia barabarani, hivyo akaamua kuwafua huku akizungumza na 911 kuwaeleza hatua kwa hatua kuhusu kinachotokea.

Baada ya mama mzazi kupiga simu kuripoti, askari polisi walifuatilia gari hilo wakidhani kweli limetekwa, lakini baada ya ajali waling’amua kuwa watoto hao hawakuwa wametekwa, bali mkubwa ndiye aliyekuwa akiliendesha. 
 
Gari hilo liligonga mlingoti barabrani na kupata ajali iliyomsababishia majeraha makubwa binti ambaye hakuwa amejifunga mkanda na kwa bahati mbaya airbag ya upande alikokaa haikufunguka wakati wa ajali ili kumlinda. Kaka yake yeye alivunjika kiwiko cha mguu, alikuwa amefunga mkanda na airbag ya upande wake ilifunguka na kumkinga.

Bado haijafahamika sababu ya watoto hao kuamua kuendesha gari hilo wenyewe na taarifa za awali za polisi zimesema hawana sababu ya kumfungulia mtu yeyote mashitaka kutokana na kisa hicho.

Polisi wamewaasa wazazi kuwa waangalifu na makini kuhakikisha kuwa wamezificha vyema funguo za magari yao ili kuepusha urahisi wa watoto kuzichukua na kuamua kuendesha gari bila ujuzi wowote.

 

UMOJA WA AFRIKA WATAFUTA SULUHISHO LA KIDIPLOMASIA DRC KWA MAPIGANO MAKALI YANAYO ENDELEA NCHINI HUMO

PictureMary Robinson
Imeandikwa na Mwandishi Maalum — Kufuatia  kurejea tena kwa mapigano makali yaliyotokea wiki iliyopita kati ya majeshi  ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo  (FARD) yakisaidiwa na Jeshi la MONUSCO na kundi la waasi  la M23. Umoja wa Mataifa sasa  unajaribu kutafuta suluhu ya kidiplomasia inayolenga katika kujaribu  kuweka sawa hali ya mambo.

Mapingano  hayo ambayo  siyo tu  yanasadikiwa kuliondoa kundi la M23 katika ngome yake ya vilima vya Kibati Magharibi ya Kivu yamelaaniwa vikali na Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu Ban ki  Moon hasa baada ya kundi hilo la M23 kusababisha  kifo cha  mwanajeshi Mtanzania na kujeruhi wengine kumi wakiwamo wanajeshi  kutoka Afrika ya Kusini.

Mchakato huo wa   kisiasa  unafanywa  na Mjumbe Maalum  wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Kanda ya Maziwa Makuu, Bi. Mary  Robinson, ambaye amewasili katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya  jumapili na kutoa  rambirambi zake kwa wahanga wa  mapigano hayo.

Source: kwa habari zaidi www.wavuti.com

UGOMVI WA MKE NA MUME WASABABISHA KIFO CHA MTOTO

Mtoto mmoja aliyefahamika kwa jina la Aines Zacharia mwenye umri wa miezi mine mkazi wa kijiji cha Ivuna wilayani Momba mkoani Mbeya, amefariki dunia Septemba Mosi majira ya saa saba mchana alipokuwa akiendelea kupata matibabu katika kituo cha afya Kamsamba kutokana na jeraha alilolipata kichwani baada ya kupamizwa ukutani.

Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Barakael Masaki alisema awali kulikuwa na ugomvi kati ya mama wa mtoto huyo aliyemtaja kwa jina la Priscar Willson aliyekuwa amembeba mgongoni na mumewe Steven Cletus. Alisema ugomvi huo ukiendelea, Cletus alimsukuma mwanamke huyo na ndipo wakajikuta wanamgongesha mtoto ukutani na kumsababishia jeraha kubwa kichwani.

Mtuhumiwa alikimbilia kusikojulikana baada ya tukio hilo na Polisi wanaendelea kumtafuta.

FRANCIS CHEKA APOKELEWA KWA SHANGWE KUBWA MJINI MOROGORO

Bondia Francis Cheka akiwa sambamba na Mkanda wake aliokabidhiwa Agost 30 baada ya kumtwanga Mmarekani Phil William  mwishoni mwa wiki ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar,pichani bondia huyo akiwa na mashabiki wake wakati alipokuwa akiwasili mkoani Morogoro anakoishi mapema jana jioni.
                 Msafara kuelekea katikatika ya mji ukiendelea

Cheka akizungumza na umati mkubwa wa watu uliofurika kwenye ukumbi wa Old Vai jana majira ya saa 12 jioni kwenye mapokezi hayo ya Cheka kulikuwa na vituko kibao kikiwemo cha Mlemavu wa miguu aliyenusurika kugongwa na gari alipotaka kumshika mkono Cheka baada ya kuona tukuio hilo Cheka alisimamisha msafara huo na kumshika mkono Mlemavu huyo kwa habari na picha za tukio hilo la kuhudhunisha zitawajia hivi punde

PICHA ZOTE NA KWA HISANI YA DUSTAN SHEKIDELE,MOROGORO-

MISS TANZANIA BRIGITTE ALFRED AONDOKA LEO KWENDA MISS WORLD INDONESIA


Mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Urembo ya Dunia, Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Lymo, ameondoka nchini leo kwenda nchini Indonesia katika kambi ya Miss World 2013. Pichani juu ni Brigitte akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jioni hii tayari kwa safari hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka nchini akiwa uwanjani hapo Brigitte ameahidi kufanya vyema katika mashindano hayo huku akiwaomba watanzania kumpa suport kwa kumpigia kura pindi zoezi hilo liytakapo anza kupitia tovuti ya Miss World.
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, kupitia kampuni ya Lino International Agency, Hashim Lundenga akimwelekeza machache mrembo huyo kabla ya kuondoka.
 Lundenga akizungumza huku Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfed na mama yake wakisikiliza.
 Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege hii leo.
  Baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na mrembo huyo uwanja wa Ndege hii leo.
Mama na Mwana....Miss Tanzania akilamba picha na mama yake kabla ya kuruka kwenda Indonesia hii leo

chanzo   fatherkidevu blog

ARSENAL IMEKUBALI KUMSAJILI MESUT OZIL KWA PAUNI MILION 42.4

 
Mesut Ozil
Kunako siku ya mwisho kwa vilabu vya mpira wa miguu kukamilisha usajili wa wachezaji klabu ya Arsenal imeafikiana na mchezaji Mesut Ozil wa Ujerumani anayechezea klabu ya Real Madrid kwa kitita cha pauni za Uingereza milioni £42.4.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, klabu ya Arsenal imekubaliana na Real Madrid kuilipa pauni za Uingereza milioni £42.4m sawa na Euro milioni 50 kumsajili Mjerumani Mesut Ozil.

Kijana huyo menye umri wa miaka 24 amefikia makubaliano na Arsenal kuhusu maslahi yake binafsi ingawa sharti apitie mchakato wa vipimo vya afya yake kabla ya Arsenal kukamilisha usajili ambao katika historia ya klabu hio haujawahi kufanyika kumsajili mchezaji kwa zaidi ya pauni milioni 22.
Mesut Ozil wa Ujerumani

Kwa wakati huu Ozil yuko pamoja na kikosi cha Timu ya Taifa ya Ujerumani na itabidi afanyiwe vipimo huko huko Ujerumani.
Kwa kipindi cha msimu wa likizo na usajili wa wachezaji Arsenal imeshindwa kuwasajili wachezaji wa kiwango anachokitaka Arsene Wenger kama mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez na Gonzalo Higuain, mchezaji mwingine aliyekua huko Real Madrid.
Lakini kwa sasa yumkini Ozil anaelekea uwanja wa Emirates kufuatia usajili wa Gareth Bale kwa kitita kikubwa cha pauni milioni 85.3.

Kabla ya kujiunga na Real Ozil alikua akichezea klabu ya Werder Bremen alikosajiliwa na Real kwa takriban pauni milioni 12.4 na kuichezea Real mara 155.
Wakati Arsenal ikijitahidi kusajili kabla ya dakika ya mwisho ya shughuli ya usajili Liverpool pia imetiliana saini na Mamadou Sakho na Tiago Ilori kwa jumla ya pauni milioni 25.
Sakho mwenye umri wa miaka 23 ameichezea Timu ya Taifa ya Ufaransa mara 14 France na amegharimu pauni milioni £18m kutoka klabu ya Paris St-Germain.
Ilori alizaliwa mjini London na ameiwakilisha Timu ya Ureno ya vijana ingawa bado anaweza kuiwakilisha England.

Liverpool haikuishia hapo ila imemzoa Mnaijeria Victor Moses kutoka Chelsea.
Mshambuliaji huyo alifunga mabao 10 akishiriki mechi 42 za Cheslea lakini amekabiliwa na ushindani mkali wa kuweza kuingia uwanjani kufuatia usajili wa mcheza kiungo kutoka Brazil Willian, Mjerumani Schurrle pamoja na mkongwe wa Cameroon Samuel Eto'o.

MANDELA AREJEA NYUMBANI KUTOKA HOSPITALINI


 
Mandela akitoka hospitaliMandela akitoka hospitali
Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Nlson Mandela amemaliza siku moja nyumbani kwake Johansberg baadha ya kuondoka hospitalini alikokuwa amelazwa kwa zaidi za miezi mitatu akipokea matibabu kwa maambukizi ya mapafu anayougua.
Nelson Mandela kwa sasa anendelea kupata nafuu nyumbani. Serikali ya Afrika Kusini imesema atakuwa akipata huduma sawa za zile alizokuwa akipewa hospitalini jijini Pretoria.
Maafisa wa serikali wameongezea kuwa nyumba yake imekarabatiwa kuwezesha madakatari kumtibu akiwa humo. Madakatri wataalam ambao wamekuwa wakimshughulikia wataendela kumtibu nyumbani mwake, lakini ikiwa hali yake ya afya itahitaji huduma za hospitali basi atarejeshwa humo bila kuchelewa.

Inasemekana kurudi nyumbani kwa Mandela kumetia matumaini kwa familia yake pamoja na taifa la Afrika Kusini. Hata hivyo Mzee Mandela bado anaonekana mwenye afya dhaifu.

Serikali ya Afrika Kusini ilisema hapo jana kuwa Mandela, alitolewa hospitali ambako amekuwa akitibiwa mapafu tangu mwezi Juni.

Taarifa katika tovuti ya rais wa Afrika Kusini ilieleza kuwa Bwana Mandela bado ni mahtuti na hali yake wakati mwengine inabadilika.

Lakini madaktari wake wanaamini akiwa nyumbani kwake mjini Johannesburg atapata matibabu sawa na yale ya hospitali.
Serikali imesema inamtakia mema wakati akiendelea na matibabu.

MORSI KUFUNGULIWA MASHTAKA YA UCHOCHEZI

 
Wafuasi wa Morsi wamekuwa wakiandamana wakitaka aachiliwe
Kiongozi wa mashtaka nchini Misri, amependekeza kuwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi afunguliwe mashtaka kwa kosa la kuchochea mauaji ya waandamanaji.
Tuhuma hizo zinahusiana na ghasia zilizotokea nje ya ikulu ya rais mjini Cairo Disemba mwaka jana ambapo angalau watu saba waliuawa kwenye makabiliano.
Wanachama wengine 14 wa vuguvugu la Muslim Brotherhood pia wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka kuhusiana na makosa hayo hayo.

Bwana Morsi amekuwa akizuiliwa katika eneo lisilojulikana tangu kuondolewa mamlakani mwezi Julai .
Anakabiliwa na mashtaka kadhaa ingawa pendekezo hii la yeye kushtakiwa ni la kwanza tangu sokomoko kuanza Misri baada ya kuondolewa kwake mamlakani.

Tangu aondolewe mamlakani serikali ya sasa inayoungwa mkono na jeshi, imekuwa ikiwasaka wanachama wa vuguvugu la Brotherhood wanaotaka bwana Morsi arejeshwe mamlakani.
Mwezi jana mamia ya waandamanaji walifariki wakati vikosi vya usalama vilipovamia kambi zilizokuwa zimekaliwa na wafuasi wa Morsi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, mnamo siku ya Jumapili mwendesha mkuu wa mashtaka alipendekeza kuwa Morsi afunguliwe mashtaka.

Walisema Morsi anashtakiwa kwa kuchochea mauaji na ghasia mnamo mwezi Disemba mwaka 2012.
Hata hivyo haijulikani ni lini kesi hiyo inayohusiana na makabiliano yaliyotokea nje ya Ikulu ya Rais Disemba mwaka 2012, itasikilizwa.

Maelfu ya waandamanaji walikuwa wakipiga kambi nje ya jengo hilo usiku wa kuamkia terehe 4 Disemba wakilalamika kuwa rais Morsi amejipa mamlaka makubwa kupita kiasi na pia wakipinga mpango wake wa kutaka kubadilisha katiba ya nchi.

Iliarifiwa kuwa Morsi aliwataka wafuasi wake kupitia kwa waziri anayesimamia idara ya polisi kukomesha maandamano ya kutaka aachiliwe huru lakini wakakataa.
Inaarifiwa walinzi wa Morsi waliwataka wafuasi wao kuja kuvunja maandamano hayo. Angalau watu saba waliuawa kwenye makabiliano hayo.

Wafuasi wa Morsi wanasema kuwa walikuwa wanalinda eneo hilo baada ya kushambuliwa na wafuasi wa upinzani.

RICARDO KAKA AICHA RASMI REAL MADRID, ARUDI AC MILAN KUUNGANA NA BALOTELLI


Baada ya kukaa Real Madrid bila ya mafanikio, Ricardo Kaka amerejea katika kikosi cha AC Milan na kusaini mkataba wa miaka miwili.



Kabla Kaka aliihama AC Milan mwaka 2009 na kujiunga na Real Madrid kwa dau kubwa la pauni milioni 56, lakini ameshindwa kufanya vizuri na sasa amerejea tena Milan ikiwa ni hatua za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Nyota wa kikosi cha Milan kwa sasa ni Muitaliano mweusi, Mario Balotelli.

TAARIFA KWA UMMA MWALIKO IKULU KWA WADAU KUCHANGIA MAONI KATIKA ZOEZI LA SERIKALI KUJITATHMINI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS – IKULU

TAARIFA KWA UMMA

MWALIKO KWA WADAU KUCHANGIA MAONI KATIKA ZOEZI LA SERIKALI KUJITATHMINI (SELF ASSESSMENT) KATIKA UTEKELEZAJI WA  MPANGO WA UENDESHAJI SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP)
Mwaka 2011, Serikali ya Tanzania ilijiunga na Mpango wa Kimataifa wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership - OGP).  Uamuzi huu wa kujiunga na Mpango wa OGP unalenga katika kuongeza juhudi za Serikali katika kuweka uwazi zaidi katika uendeshaji wa shughuli zake; kushirikisha wananchi katika upangaji na utekelezaji wa shughuli za Serikali; kuimarisha uwajibikaji katika utendaji wa Serikali; kuimarisha juhudi za kuzuia na kupambana na rushwa na kuweka umuhimu wa matumizi ya teknolojia na ubunifu.

Kwa kuanzia Serikali imeanza kutekeleza ahadi (commitments) zilizoainishwa katika Mpango Kazi wake katika
sekta tatu za kipaumbele za huduma za Afya, Elimu na Maji.  Serikali imetekeleza ahadi zilizoainishwa katika Mpango Kazi wake kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai, 2012 hadi Julai, 2013.  Kwa mujibu wa matakwa ya Mpango wa OGP, Serikali kwa kushirikiana na Asasi za Kiraia (Civil Society Organizations) inatakiwa kufanya zoezi la tathmini (Self Assessment) kujua ni kwa kiwango gani ahadi zilizoainishwa zimetekelezwa.

Kwa hiyo wadau wote na wananchi kwa ujumla wanakaribishwa kuchangia maoni ya jinsi mipango kazi ya OGP ilivyotekelezwa kwa kujaza fomu iliyopo kwenye tovuti www.ega.go.tz/ogp.

Maoni hayo ni muhimu katika kufanikisha zoezi la Serikali la kujitathmini na pia katika kuboresha maandalizi ya Mpango Kazi utakaotekelezwa katika kipindi kinachofuata cha miaka miwili kuanzia 2014 – 2016.  Maoni yawe yamewasilishwa kabla ya tarehe 18 Septemba, 2013.

OFISI YA RAIS, IKULU 

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
PRESIDENT’S OFFICE – STATE HOUSE


PRESS RELEASE

CALL FOR STAKEHOLDER VIEWS ON THE GOVERNMENT SELF ASSESSMENT EXERSICE ON IMPLEMENTATION OF OPEN  GOVERNMENT PARTNERSHIP
Year, 2011, the government of Tanzania joined the global initiative of Open Government Partnership that aims at promoting transparency, empowering citizens, fighting corruption and encouraging use of new technologies to improve governance.

The Government started implementing its OGP commitments which were translated to action plans.  During Phase I of OGP implementation, commitments were directed to three priority sectors which include Health, Water and Education.  Hence, the one year plans which were implemented from July, 2012 to July, 2013 focused on the above mentioned priority sectors. 

In accordance with OGP Regulations, after implementation for the period of one year, the government in collaboration with the Civil Society Organizations is required to conduct a Self Assessment Exercise to determine how the Programme was implemented.

Therefore, citizens are cordially invited to contribute their views and opinions on how the OGP action plans were implemented.  All comments are to be presented in the forms which are found in the website www.ega.go.tz/ogp.

The Public views are crucial to facilitate government self assessment exercise in OGP implementation.  Also the views will be used for developing next OGP action plans to be implemented between 2014/15 and 2015/16.

The views should be submitted through the above referred website before 18th Sept, 2013.

PRESIDENT’S OFFICE, STATE HOUSE

 

ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KULAWITI

JESHI la Polisi mkoani Singida linamtafuta kijana mmoja mkazi wa Kibaoni katika manispaa hiyo kwa tuhuma za kumlawiti mwenzake na kumharibu vibaya sehemu za haja kubwa baada ya kumnunulia pombe kali aina ya viroba jogoo tisa.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Geofrey Kamwela, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku eneo la soko la Kibaoni, kata ya Kindai, na kumtaja mtuhumiwa huyo kwa jina moja la Athuman.

Alisema kuwa baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, kijana aliyelawitiwa (jina tunalihifadhi) alimweleza mtuhumiwa kuwa amelewa kupindukia na hivyo kila mmoja arejee nyumbani kwao.

“Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia mtuhumiwa amwache hapo ili apumzike kwa vile
pombe ilikuwa imemzidi sana lakini ghafla alianguka chini na kisha kupoteza fahamu,” alisema.

Baada ya muathirika kupoteza fahamu, mtuhumiwa alitumia fursa hiyo na kuanza kumwingilia kimwili kinyume cha maumbile. Alisema kuwa wasamaria wema walimshuhudia mtuhumiwa akiendelea kufanya unyama huo dhidi ya rafiki yake lakini walipojaribu kumkamata, aliwaponyoka na kukimbilia kusikojulikana.

“Raia wema hao walimbeba muathirika na kumpeleka nyumbani kwake na baadaye aliweza kupata fahamu ndipo alianza kusikia maumivu makali sehemu yake ya haja kubwa,” alisema.

Alisema muathirika alipelekwa hospitali ya mkoa wa Singida ambako alibainika kuharibiwa vibaya sehemu zake za haja kubwa.


---chanzo  Hillary Shoo, TANZANIA DAIMA, Singida.

 

ANGALIA MABOSI WANAVYOTUMIA VYEO KULAZIMISHA NGONO MAKAZINI

 
Mikao kama hii huchangia hamasa ya ngono sehemu za kazi. Picha ya Maktaba. 


Licha ya harakati mbalimbali za kumkomboa mwanamke, bado kuna mabosi nchini wanawanyanyasa wanawake kwa kuwalazimisha kufanya nao ngono.
Wapo wanaonyanyaswa au hata kuteswa ikiwemo kusemwa maneno machafu au kutishiwa kufukuzwa kazi kwa sababu tu wamekataa kutoa penzi kwa bosi.

Wale wanaokubali, wengine wanaishia kupewa ahadi hewa za kufundishwa magari, kupelekewa kozi mbalimbali. Hata hivyo mbaya zaidi ni kwamba mabosi wengine hata kama wameoa, hupenda kuwamiliki wanawake hao kana kwamba ni wake zao kwa kuwafuatilia sana nyendo zao.
Ukahaba wa mabosi hufanywaje?

Baadhi ya wanaume kwa mwonekano ni vigumu kuamini kama ndiyo wanaofanya vitendo vichafu kwa wafanyakazi wao. Wanaposimama kwenye vikao, utasema mtu huyu, lakini wafanyakazi wa kike wamekuwa ni wenye kuwanyanyasa mno.
Baadhi ya mabosi wamekuwa wakitoa vitisho kuwa ‘kama hunipi penzi nitakuporomosha cheo au hata kukufanyia visa vyovyote hadi uhame’.

Katika baadhi ya ofisi badala ya mabosi kutumika kama washauri wa  wafanyakazi wao kuzipenda ndoa na nyumba zao, ndio wamekuwa wakitumia fedha zao kuwahonga wanawake hata magari, huku makatibu muhtasi wakidaiwa kuwa ndio wanaosumbuliwa zaidi.

Wapo mabosi huwaingia wanawake wakiwemo wake za watu kwa kuwapangia safari za mikoani au nje ya nchi hasa wanapoona hawana wepesi wa kukubaliana na matakwa yao.
“Nakumbuka kuna bosi mmoja katika ofisi moja nyeti aliwahi kudaiwa kumnunulia gari mke wa mtu kabla ya kuhama chombo hicho,” anasema mkazi mmoja wa Kimara.

Bosi aliweza kumpa safari ya nje mwanamke na kisha kumnunulia gari zuri kuliko la mumewe.
Hii ni moja ya kati ya matukio mengi ya mabosi kuwaingiza wafanyakazi wao katika ngono badala ya kuwa ndio washauri wema kwa wafanyakazi ili waweze kuziheshimu ndoa zao.

 Na Waandishi wetu, Mwananchi 
Posted  Jumatatu,Septemba2 


WATAKA ZANZIBAR IJITEGEMEE KWA KILA KITU

 
Aliyekuwa Mwakilishi wa Kiembesamaki, Mansour Yusouf Himid akizungumza katika kongamano la wazi lililoitishwa na Kamati ya Maridhiano Zanzibar ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipovuliwa uanachama wa CCM. Picha na Talib Ussi 


Zanzibar.  

Kamati ya Maridhiano imetoa maoni yake ya Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutaka Zanzibar ijitegemee karibu kwa kila kitu.
Maeneo inayotaka yaondolewe kwenye Muungano ni uraia na uhamiaji, sarafu na Benki Kuu, mambo ya nje na usajili wa vyama vya siasa.

Kamati hiyo inayounga mkono muundo wa muungano wa Serikali tatu inayoongozwa na mwanasiasa mkongwe, Hassan Nassor Moyo, iliwasilisha mapendekezo hayo juzi katika Ofisi za Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kusema kuwa maoni hayo ndiyo mawazo ya Wazanzibari wengi.
Mapendekezo hayo yalisomwa na Mwakilishi wa Mji Mkongwe ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo, Ismail Jussa katika Kongamano la Katiba lililoandaliwa na kamati hiyo.
Msimamo wa kamati hiyo unaelezwa kuwa chanzo cha mmoja wa wajumbe wake, Mansour Yussuf Himid kuvuliwa uanachama wa CCM, Agosti 26 mwaka huu.

Akisoma mapendekezo hayo, Jussa alisema kwa kuwa Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar uliziunganisha nchi zilizokuwa huru, unatakiwa kuitwa Muungano wa Jamhuri za Tanzania, kusisitiza kuwa rasimu hiyo inatakiwa kueleza wazi kwamba nchi nyingine zinaweza kuingia kwenye muungano huo.
Alisema kamati hiyo imependekeza kuwa mambo ya nje yasiwe suala la muungano na badala yake nchi washirika zisimamie zenyewe eneo hilo.

Alisema kwa kuwa muungano umetokana na nchi mbili  zilizokubali kuungana na kuunda shirikisho,  msingi wa uraia wa shirikisho utokane na msingi wa mtu kuwa raia wa nchi mshirika na si kinyume chake.
“Kila nchi mshirika (Zanzibar na Tanganyika), ibakie na uraia wake na mtu kuwa na uraia wa nchi mshirika ndiko kumpe uhalali wa kuwa raia wa shirikisho,” alisema.

Pia kamati imependekeza Rais wa muungano ambaye atakuwa na madaraka ya juu katika shirikisho lote kwa mambo yote ya Muungano, hivyo nchi washirika zinapaswa kuwa na haki sawa katika kutoa watu wa kushikilia Baraza la Mawaziri la Muungano, Bunge na Mahakama.
Alisema rasimu inatakiwa itamke wazi kwamba urais wa Muungano utashikwa kwa zamu na kwa kupokezana baina ya nchi washirika yaani Tanganyika na Zanzibar na kwamba Rais atangazwe mshindi 

baada ya kupata kura zaidi ya asilimia 50 kutoka Tanganyika na Zanzibar.
Alisema badala ya kuendeleza mfumo uliopo sasa wa Makamu wa Rais kupatikana kutokana na mgombea mwenza, marais wa nchi washirika (Zanzibar na Tanganyika) moja kwa moja wawe makamu wa kwanza  na makamu wa pili wa Rais wa Muungano.


Na Fidelis Butahe, Mwananchi
Posted  Jumatatu,Septemba2  2013

MTANZANIA ALIYESAJILIWA QATARI MAFANIKIO YAONEKANA MWINYI KAZIMOTO APIGA BAO MBILI


Na Saleh Ally
Neema imeanza kumjaa kiungo wa zamani wa Simba, Mwinyi Kazimoto baada ya kupiga mabao mawili safi akiwa na timu yake mpya ya Al Markhiya ya Qatar.

Kazimoto amefanikiwa kufunga mabao mawili katika mechi tano alizoichezea timu hiyo inayoshiriki daraja la pili nchini Qatar.


Pamoja na kufunga mabao hayo mawili katika mechi tano za kirafiki alizocheza, Kazimoto amefanikiwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

Kocha wa zamani wa Simba, Hassan Afif aliyemsaidia Kazimoto kujiunga na timu hiyo nchini Qatar ameliambia Championi Jumatatu kwamba kocha wake kutoka nchini Serbia amemhakikishia namba katika kikosi cha kwanza.

“Kweli amefunga mabao mawili katika mechi hizo tano, walikuwa wamekwenda kuweka kambi nchini Tunisia na sasa wameisharejea hapa Doha tayari kwa ajili ya ligi itakayoanza wiki mbili zijazo.

“Kweli Kazimoto ameonyesha uwezo mkubwa sana kwa kweli, mabao aliyofunga ni mazuri. Kilichomvutia zaidi kocha ni kwamba, katika mechi zote tano hajacheza dakika 90 katika kila mchezo lakini amefanya vizuri.

“Wakati mwingine alianza au kuingia katika kipindi cha pili, kocha alifanya hivyo kwa ajili ya kujaribu wachezaji lakini inaonekana kama amejihakikishia namba katika kikosi cha kwanza na kocha ametaka aendelee na juhudi hizo,” alisema Afif.

Akiyaelezea mabao ya Kazimoto, Afif alisema: “Sijayaona lakini kocha kaniambia ni mazuri na moja lilikuwa ni la shuti kali nje ya eneo la kumi na nane. Imemfurahisha sana.”

Kazimoto amejiunga na Al Markhiya akitokea Simba ambayo ameichezea kwa misimu miwili, kabla ya hapo alikuwa kiungo tegemeo wa JKT Ruvu.

Kazimoto ambaya amechipukia kisoka mkoani Mwanza alikozaliwa, anasifika kwa kupika mashuti makali pia pasi za uhakika zinazozaa mabao

AZAM TV KUTENGENEZA MAMILIONI KUPITIA LIGI KUU YA TANZANIA BARA


TORRINGTON (KULIA) AKIFURAHI MARA BAADA YA KUSAINI MKATABA WA KUONYESHA MOJA KWA MOJA MECHI ZA LIGI KUU, KULIA KWAKE NI MAKAMU WA RAIS WA TFF, ATHUMAN NYAMLANI, NAYE 'AKIANGUKA'
Uongozi wa runinga ya Azam Tv umesema unatarajia kutengeneza mamilioni ya fedha kupitia Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini ukakataa kuelezea kwa undani zaidi.

Akijibu maswali ya waandishi hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Tv, Rhys Torrington alisema matarajio yao ni kuingiza mamilioni ya fedha, lakini hawawezi kuweka hadharani mipango yao ya biashara.

“Kweli tunatarajia kuingiza mamilioni ya fedha kupitia ligi kuu, hii ni sehemu ya mikakati ya kutengeneza fedha lakini hatuwezi kuanika mipango yetu.

Hata hivyo, Torrington aliwataka Watanzania kujivunia Azam Tv kwa kuwa ni chombo kinachimilikiwa na Mtanzania.
“Ushauri wangu ni kwenu kujivunia Azam Tv kwa kuwa ni ya Mtanzania na sasa itaonyesha mechi za ligi kuu. 

Tutaanza majaribio hivi karibuni na siwezi kuruhusu matangazo yaende hewani bila ya kuwa na kiwango bora ninachotaka,” alisema.

Azam Tv inatarajia kuanza majaribio yake wiki hii na kama bosi huyo atakuwa ameridhika na kiwango itaanza kurusha matangazo yake.

Azam Tv imeingia mkataba miaka mitatu wa pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na bodi ya ligi ambao thamani yake ni Sh bilioni 5.6 na kila klabu itakuwa ikipata Sh milioni 100 kila msimu.
   CHANZO  Salehjembeblog