Mstahiki meya wa halmashauri ya
manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi akifungua kikao kwa maombi katika baraza la
madiwani lilofanyika mwishoni mwa wiki kushoto ni naibu meya Gervas Ndaki na
kulia Mkurugen Theresia Mahongo kikao kilichofanyika katika ukumbi
wa halmashauri ya Manispaa. (picha na Denis Mlowe)
Madiwani wa halmashauri ya Manispaa
ya Iringa wakiwa katika kikao cha baraza kilichofanyika katika ukumbi wa
halmashauri mwishoni mwa wiki. (picha na Denis Mlowe)
MIONGONI mwa watu 6003
mkoani hapa waliopima afya zao kwa hiyari katika kipindi cha Oktoba hadi
Disemba mwaka jana, watu 379 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya
ukimwi (VVU).
Akizungumza katika kikao
cha utekelezaji wa shughuli za ukimwi zilizotekelezwa na Kamati ya Kudhibiti
Ukimwi mbele ya baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya pili Oktoba na
Disemba mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naibu Meya Gervas Ndaki,
alisema kati ya waliojitokeza kupima na kupata ushauri nasaha, wanaume walikuwa
3074 wanawake 2,929.
Ndaki alisema kati ya
watu 379 waliopima kwa hiari na kukutwa na maambukizi,146 ni wanaume na
wanawake ni 233.
Alisema huduma ya kuzuia
maambukizi ya vvu/ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, wajawazito 1,287
walijitokeza na kupata ushauri wa nasaha na kati yao, 84 sawa na asilimia 6.5
walikutwa na maambukizi.
Ndaki alisema mapambano
ya ukimwi yanaambatana na huduma za tiba sahihi ya magonjwa ya ngono na
jumla ya watu 361, wanaume 110 na wanawake 251, walipata tiba sahihi ya
magonjwa ya ngono
“Maambukizi ya ugonjwa
wa ukimwi yanaendelea kuwepo na tunajitahidi sana kuwahamasisha wananchi
kujitambua na kutumia sana kondom na pia tumefanya sana kampeni kwa wananchi
wanaotakiwa kwenda tohara kujitokeza kwenda katika hospitali na vituo vya afya
vinavyotambulika kutoa huduma ya tohara” alisema Ndaki
Aliongoza kuwa huduma ya
kitabibu ya tohara kwa wanaume ilitolewa kwa jumla ya wanaume 171 walitahiriwa na
kati ya waliopima vvu wanaume 160 na hakuna aliyekutwa na maambukizi.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi aliwataka watendaji kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa kuwasisitiza wananchi kwa kuwapa elimu kuondokana na maambukizi mapya.
alisema mkoa wa Iringa una nafasi kubwa sana wa kuwa wa mwisho kama kila mmoja atatumia nafasi yake kuelimisha vijana kwa wazee katika mapambano dhidi ya ukimwi.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi aliwataka watendaji kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa kuwasisitiza wananchi kwa kuwapa elimu kuondokana na maambukizi mapya.
alisema mkoa wa Iringa una nafasi kubwa sana wa kuwa wa mwisho kama kila mmoja atatumia nafasi yake kuelimisha vijana kwa wazee katika mapambano dhidi ya ukimwi.
Na Denis Mlowe,Iringa
0 comments:
Post a Comment