Monday, 6 January 2014

YANGA SAFARINI UTURUKI KUPIGA KAMBI WIKI MBILI NA WACHEZAJI WAKE WOTE! KASORO CHUJI?


YANGA_UTURUKIMABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga, wanatarajiwa Alhamisi hii kuondoka Nchini kuelekea Uturuki kwa Kambi ya Mazoezi ya Wiki mbili huku wakiwa na Kikosi chao chote.
Hii itakuwa mara ya pili kwa Yanga kwenda Uturuki kufuatia Ziara kama hii Mwezi Desemba Mwaka 2012 walipopiga Kambi Mji wa Antalya ulio Kusini Magharibi mwa Uturuki.CHARLES_BONIFACE_MKWASA
Walipokuwa huko, kwenye Ziara iliyomalizika Januari Mwaka Jana, Yanga walicheza Mechi kadhaa za Kirafiki dhidi ya Timu kubwa za Nchi hiyo na kutia fora kwa Kandanda lao.
Kwenye Ziara hii huenda Yanga isimchukue Kiungo wao Athumani Idd ‘Chuji’ ambae inadaiwa anakabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu kwenye pambano la Nani Mtani Jembe ambalo Yanga ilifungwa 3-1 na Simba.
Inadaiwa kwenye Mechi hiyo Chuji alipobadilishwa katika Kipindi cha Pili hakukaa Benchi na moja kwa moja alielekea Vyumba vya Kubadili jezi na kisha kutokomea nje ya Uwanja.
Kwa vile Yanga wapo kwenye mchakato wa kusaka Kocha Mkuu baada ya kumwondoa Ernie Brandts kutoka Uholanzi, Ziara hii ya Yanga huko Uturuki itakuwa chini ya Kocha Msaidizi Charles Boniface Mkwasa na Kocha wa Makipa, Juma Pondamali ni mahsusi kwa ajili ya Raundi ya Pili ya Ligi Kuu Vodacom inayoanza Januari 25, Mashindano ya CAF CHAMPIONZ LIGI, ambayo Yanga itacheza na Klabu ya Comoro, Komorozine, Mwezi ujao na pia Kagame Cup, Kombe la Klabu Bingwa Afrika ya Mashariki na Kati.
LIGI KUU VODACOM
MSIMAMO:
NO
TEAMS
P
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Young Africans
13
8
4
1
31
11
20
28
2
Azam FC
13
7
6
0
23
10
13
27
3
Mbeya City
13
7
6
0
20
11
9
27
4
Simba SC
13
6
6
1
26
13
13
24
5
Kagera Sugar
13
5
5
3
15
10
3
20
6
Mtibwa Sugar
13
5
5
3
19
17
2
20
7
Ruvu Shootings
13
4
5
4
15
15
0
17
8
Coastal Union
13
3
7
3
10
7
3
16
9
JKT Ruvu
13
5
0
8
10
16
-6
15
10
Rhino Rangers
12
2
4
6
9
16
-7
10
11
JKT Oljoro
13
2
4
7
9
19
-10
10
12
Ashanti United
13
2
4
7
12
24
-12
10
13
Tanzania Prisons
12
1
5
6
6
16
-10
8
14
Mgambo JKT
13
1
3
9
3
23
-20
6
RATIBA
RAUNDI YA PILI
25 Januari 2014
Ashanti United v Yanga
Azam FC v Mtibwa Sugar
Coastal Union v JKT Oljoro
Kagera Sugar v Mbeya City
Tanzania Prisons v Ruvu Shootings
JKT Ruvu v Mgambo JKT
Simba v Rhino Rangers

0 comments: