Monday, 6 January 2014

CAPITAL ONE CUP: JUMANNE NUSU FAINALI SUNDERLAND v MAN UNITED!

>>JUMATANO NI MAN CITY v WEST HAM!
KOMBE la LIGI, sasa likiitwa CAPITAL ONE CUP, Jumanne na Jumatano Usiku, litakuwa na MechiCAPITAL_ONE_CUP-BEST zake za Nusu Fainali ambazo huchezwa kwa mtindo wa Nyumbani na Ugenini. Jumanne Usiku Mabingwa wa England, Manchester United, watakuwa Stadium of Light kucheza na Sunderland na Jumatano Usikum huko Etihad, Man City watacheza na West Ham.
Marudiano ni Januari 21 na 22
++++++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP
NUSU FAINALI
[Saa 4 Dakika 45 Usiku]
Jumanne Januari 7
Sunderland v Man United
Jumatano Januari 8
Man City v West Ham
Marudiano
Jumanne Januari 21
West Ham v Man City
Jumatano Januari 22
Man United v Sunderland

DONDOO MUHIMU:
Sunderland v Man United
Manchester United hawajafungwa katika Mechi 20 dhidi ya Sunderland kwa Kushinda Mechi 16 na Sare 4 lakini mara ya mwisho kufungwa na Sunderland ilikuwa kwenye Kombe hili Msimu wa 2000/01.
Mara ya mwisho kukutana ni Mwezi Oktoba kwenye Ligi Kuu England huko Stadium of Light ambako Man United walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kushinda Bao 2-1 kwa Bao za Adnan Januzaj alizofunga ndani ya Dakika 6 katika Kipindi cha Pili.
Man City v West Ham
Katika Mechi 7 zilizopita kati ya Manchester City na West Ham, City hawajafungwa hata Mechi moja na wameshinda Mechi 5.

DONDOO MUHIMU:
-KLABU 92 za BPL [Klabu 20] na Ligi za Madaraja Matatu ya chini [Championship, Ligi 1 na 2, Jumla Klabu 24 kila Ligi] hushiriki Raundi 7 za Mashindano.
-NUSU FAINALI huchezwa kwa Mtindo wa Mtoano wa Nyumbani na Ugenini.
-KLABU ZA BPL HUANZA kushiriki Raundi ya Pili lakini zile ambazo zinacheza Mashindano ya UEFA ya CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI huanza kucheza Raundi ya Tatu.
-FAINALI ITACHEZWA TAREHE 2 MACHI 2014 Uwanja wa Wembley na Bingwa hushiriki UEFA EUROPA LIGI Msimu unaofuata.
-MFUMO:
Raundi ya 1: Wiki ya kuanzia Agosti 5
Raundi ya 2: Wiki ya kuanzia Agosti 26
Raundi ya 3: Wiki ya kuanzia Septemba 23
Raundi ya 4: Wiki ya kuanzia Oktoba 28
Raundi ya 5: Wiki ya kuanzia Desemba 16
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: Wiki ya kuanzia Januari 6
Nusu Fainali-Marudiano: Wiki ya kuanzia Januari 20
Fainali: Jumapili 2 Machi 2014

0 comments: