>>“QUENELLE" YA NICOLAS ANELKA YAWATOA MKUKU ZOOPLA WBA!!
VIKUMBO
vya Uhamisho wakati huu wa Dirisha la Uhamisho la Mwezi Januari
vimeshamiri huku huko West Bromwish Straika wa France, Nicolas Anelka,
akizua balaa kubwa.
SOMA ZAIDI:
LACINA TRAORE: EVERTON WAKARIBIA KUMSAINI MKOPO TOKA MONACO
Straika wa Monaco Lacina Traore anatarajiwa kupimwa Afya yake Klabuni Everton ili kumalisha Uhamisho wake wa Mkopo.
Awali iliaminika Straika huyo kutoka
Ivory Coast mwenye Miaka 23 na Urefu wa Futi 6 Inchi 8 anakwenda West
Ham baada Klabu hiyo ya London kumwombea Kibali cha Kazi cha Nchini
Uingereza lakini Meneja wa West Ham, Sam Allardyce, ametoboa kuwa
Straika huyo hataenda tena kwao.
Monaco wamemsaini Traore kutoka Anzhi
Makhachkala ya Urusi ambako alicheza pamoja na Samuel Eto'o akitokea
Kuban Krasnodar Juni 2012.
Kwenye Msimu wa 2012/13, Traore alifunga Bao 12 katika Mechi 24.
SUNDERLAND YAMSAINI KWA MKOPO SANTIAGO VERGINI
Sunderland imemsaini Beki wa Argentine Santiago Vergini kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu.
Vergini, Miaka 25, anatokea Klabu ya Uruguay Atletico Fenix ingawa alikuwa kwao Argentina akichezea Estudiantes kwa Mkopo.
Sentahafu huyo, ambae alianza kuichezea
Timu ya Taifa ya Argentina Mwaka 2012, pia ameshaichezea Klabu ya Italy
Verona na ile Klabu maarufu huko Argentina, Newell's Old Boys.
Vergini ni Mchezaji wa Pili kusainiwa na
Sunderland Mwezi huu Januari na mwingine ni Beki kutoka Fiorentina ya
Italy, Marcos Alonso, ambae pia yuko kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu.
“QUENELLE" YA NICOLAS ANELKA YAWATOA MKUKU ZOOPLA WBA!!
Wadhamini wa West Brom, Zoopla, wameamua
kuachana na Klabu hiyo mwishoni mwa Msimu kufuatia kitendo cha Nicolas
Anelka kutumia Saluti iitwayo “Quenelle" ambayo inahusishwa na
Mafashisti wa Nazi na Ubaguzi kwa Mayahudi.
Anelka, Miaka 34, alitoa Saluti hiyo
ambayo Mkono mmoja unanyooshwa chini na mwingine kupita Kifuani na
kuugusa mwingine, wakati alipofunga Bao kwenye Mechi na West Ham hapo
Desemba 28.
Zoopla, ambae mmoja wa Wamiliki wake ni
Myahudi Alex Chesterman, na ambao walikuwa wamalize Mkataba na WBA
mwishoni mwa Msimu huu, Mkataba ambao ulianza 2012, wamesema watasaka
Soko jingine.
Kitendo hicho cha Anelka bado
kinachunguzwa na FA, Chama cha Soka England. Mwenyewe Anelka, mbali ya
kuiahidi WBA kutoitumia tena, amekanusha Saluti hiyo kuhusishwa na
Ufashisti na Ubaguzi na kubainisha inaitwa ‘Quenelle’ na ni kwa ajili ya
kumsapoti Rafiki yake wa France, Dieudonné M'Bala M'Bala, ambae ni
Mchekeshaji, anaesakamwa Nchini humo kwa kudaiwa Mbaguzi.
Lakini Anelka si Mwanasoka wa kwanza
kupigwa Picha akitoa hiyo ‘Quenelle’ kwani Samir Nasri wa Manchester
City na Mamadou Sakho wa Liverpool walishanaswa wakiwa pamoja na
Dieudonné wakitoa Saluti hiyo ingawa Sakho baadae alisisitiza hakujua
maana yake na alihadaiwa kuitumia.












0 comments:
Post a Comment