>>LOWASSA AELEZA MATUMAINI YAKE TFF KUUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS KIKWETE KUINYANYUA NCHI KISOKA!
SOMA ZAIDI:
SOMA ZAIDI:
Release No. 009
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Januari 20, 2014
MALINZI AELEZEA MIKAKATI YAKE KWA LOWASSA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema shirikisho lake limepanga malengo
ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya mkakati wa kuendeleza na
kuinua kiwango cha mchezo huo nchini.
Malinzi ameeleza mikakati hiyo ya
uongozi wake leo (Januari 20 mwaka huu) wakati alipomtembelea Waziri
Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Amesema uongozi wake umepanga malengo
hayo ikiwemo kuandaa mashindano maalumu ya kutafuta vipaji mikoani ili
kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) kuundwa na wachezaji
kutoka katika klabu chache tu.
Kwa upande wake Lowassa ambaye pia ni
Mbunge wa Monduli ameelezea matumaini yake kwa uongozi mpya wa TFF
katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kuimarisha na
kuinyayua Tanzania katika ramani ya mpira wa miguu duniani.
PICHANI: Rais wa TFF,
Jamal Malinzi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani Edward
Lowassa ambapo alimwelezea mikakati ya shirikisho lake katika kuinua
kiwango cha mpira wa miguu Tanzania. Mkutano huo umefanyika leo (Januari
20 mwaka huu) ofisini kwa Lowassa jijini Dar es Salaam.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)












0 comments:
Post a Comment