Thursday, 9 January 2014

KIKONGWE JIMBONI KWA MBUNGE PROF MSOLLA AJINYOGA KWA UGUMU WA MAISHA



SUBIRA  ya maisha  bora  kwa  kila mtazania  imeanza  kuleta majanga mkoani Iringa  baada ya  kikongwe mmoja kutoka   jimbo la Kilolo  linaloongozwa na mbunge wake Prof Peter Msolla  kuamua kujitanguliza kuzimu  kwa kile alichodai ni ugumu wa maisha .

Kikongwe  huyo mkazi wa  kijiji   cha Matumbuka kata  ya  Ilole tarafa ya Mazombe wilaya ya  Kilolo Bw Gaudence Mtete  (84) alikutwa akiwa amejinyonga  ndani ya  nyumba yake  kwa kutumia kamba ya Chandarua  kutokana na  kile kinachoelezwa  kuwa ni ugumu  wa maisha  

Kamanda  wa  polisi mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi ameuthibitishia  mtandao huu  wa www.matukiodaima.com juu ya  kifo cha kikongwe  huyo  na kuwa tukio hilo lilitokea manano  tarehe 6 majira  usiku mwaka  huu.

0 comments: