Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwa Amelazwa Pembeni baaada ya kupewa msaadaAjali
mbaya imetokea mda si mrefu eneo kati ya wami na segera,ajali hiyo
imesababishwa na gari aina ya Noah ambayo ilikuwa inatokea Moshi mjini
kuelekea Dar,Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hiyo na pia
dereva alikuwa anasinsiza hali hiyo iliyopelekea kuacha njia na kuenda
kuivaaa gari ya mizigo kwa mbele.Gari hiyo Noah pia ilikuwa imebeba
abiria kupita uwezo wake ambapo abiria zaidi ya kumi na mbili walikuwa
ndani ya gari hiyo.Mpaka chanzo chetu kinaondoka eneo la tukio hakuna
aliyepoteza maisha bali kuna majeruhi walioumia vibaya sana.
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA DJ SEK BLOG
Huyu pia ni mmoja wa majeruhi ambaye ameumia vibaya sana kwenye mguuu wake
Hii ndi gari aina ya Noah ambayo imepata ajali ikiwa imeharibika vibaya kwa mbele

Watu wakiendelea kutoa msaada kwa majeruhi wa ajali hiyo
Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akiwa amelazwa pembeni ya barabara
















0 comments:
Post a Comment