MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Sunday, 3 August 2014

LIGI KUU MIEZI MINNE YA MSIMU, HAKUNA MASHINDANO MENGINE YOYOTE HUYO MCHEZAJI FITI ATATOKEA WAPI?


LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, msimu wa 2014/2015 inatarajiwa kuanza Septemba 20 mwaka huu, na ratiba itatolewa mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo.
Yaani tutarajie wakati wowote kuanzia Agosti 20 ratiba ya msimu mpya wa Ligi Kuu itatoka.
Hiyo itafuatia kukamilika kwa zoezi la usajili, hatua ya kwanza ikikamilika Agosti 17 mwaka huu ikifuatiwa na kipindi cha uhamisho kitakachokamilika Agosti 17 mwaka huu wakati pingamizi itakuwa kati ya Agosti 19 hadi 26 mwaka huu. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itathibitisha usajili kati ya Septemba 1 na 2 mwaka huu.

Zoezi la uhamisho wa kimataifa, usajili wa wachezaji huru, na utatuzi wa dosari za usajili litafuatia ambalo linatakiwa liwe limekamilika hadi Septemba 7 mwaka huu kabla ya uthibitisho wa hatua ya mwisho ya usajili kufanywa Septemba 15 mwaka huu.
Tangu Juni mwaka huu klabu zimekuwa zikisajili na hadi Septemba 15 zoezi hilo litakapokamilika rasmi, itakuwa ni miezi mitatu.
Hata Ligi Kuu isingechelewa na ikaanza mwishoni mwa Mei kama kawaida, bado zoezi la usajili lingechukua si chini ya miezi miwili.
Lakini kwa kawaida, kwa misimu iliyotangulia, Ligi Kuu imekuwa ikianza mwishoni mwa Agosti au Septemba mwanzoni, na kumalizika Novemba.
Maana yake mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu unachezwa kwa miezi miwili au mitatu- tumemaliza kazi.
Baada ya hapo wachezaji wanakwenda kupumzika hadi watakaporejea kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu, mwishoni mwa Januari au mwanzoni mwa Februari.
Na kutoka hapo watacheza mzunguko huo wa pili wa Ligi Kuu ya timu 14 hadi mwishoni mwa Aprili au mapema Mei, ligi inakuwa imemalizika na bingwa amekwishapatikana, timu za kushuka Daraja zimekwishajulikana.
Siri kubwa ya kufanikiwa kumaliza ligi haraka ni kuikimbiza, kuichezesha haraka kila wiki, kila timu inacheza wastani wa mechi mbili au tatu.
Pamoja na miundombinu yetu mibovu, lakini timu itasafiri kutoka kituo kimoja hadi kingine mara tatu ndani ya wiki moja.
Mfano Azam FC, mabingwa wa msimu uliopita, waliimalizia wiki Tanga katikati ya wiki wakacheza mara mbili Mlandizi na mwishoni mwa wiki wakacheza Mbeya.
Baada ha kumalizika kwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Azam wakiwa mabingwa, zaidi ya wachezaji waliokwenda timu ya taifa, Taifa Stars- wachezaji wengine wa klabu za ligi hiyo hawakupata mashindano mengine yoyote ya kushiriki hadi watakaporudi kwenye ligi mwezi ujao.
Unaweza ukajiuliza iko wapi faida ya kuikimbiza Ligi Kuu kwa kasi hiyo ikiwa hakuna mashindano mengine mbele? Kitaalamu, mchezaji anatakiwa kucheza sana ili kuwa fiti, lakini kwa mchezaji wa Tanzania anayecheza Ligi Kuu kwa miezi minne hadi sita ya msimu, unatarajia nini?
Ndiyo maana kila siku tunawamezea mate wachezaji wa nchi jirani kama Kenya naUganda, kwa sababu wanacheza Ligi ndefu na bado wana mashindano mengine kama Kombe la FA na kadhalika.
Sisi ukisikia mashindano mengine ni ya ujanja ujanja tu ya wiki mbili mbili kama Kombe la Mapinduzi kule Zanzibar, sasa saa ngapi unategemea kumjenga mchezaji katika kiwango cha ushindani?
Hapo hapo unamsikia mtu mwingine anahoji, hivi kwa nini wachezaji wa Taifa Stars watoke Azam, Simba na Yanga pekee, hakuna timu nyingine?
Anasahau kwamba Azam, Simba na Yanga ndizo ambazo kwanza zinasajili wachezaji waliong’ara kutoka timu nyingine- na pili ndizo ambazo zinacheza mechi nyingi kidogo kuliko timu nyingine.
Kutoka timu hizo tatu ndipo hupatikana wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Kagame, Ligi ya Mabingwa Afrika hata Kombe la Shirikisho- sasa kwa vyovyote lazima mchezaji wa timu ya taifa atokane na timu hizo.
Naziona jitihada za rais mpya wa TFF, Jamal Emil Malinzi katika kuhakikisha analeta mabadiliko kwenye soka ya Tanzania na kwa hakika anaonyesha matumaini.
Najua ni mengi ambayo anayafanyia kazi kwa sasa, na hili la ligi ya miezi minne hadi sita ndani ya msimu, vyema akalitupia jicho nalo, je kwa mtaji huu tutampata wapi mchezaji fiti? Asanteni.  

MAN UNITED YAWAFUMUA REAL MADRID 3-1 KOMBE LA KIMATAIFA MAREKANI


MANCHESTER United imewafunga mabingwa wa Ulaya, Real Madrid mabao 3-1 katika Kombe la Kimataifa Uwanja wa Michigan mjini Ann Arbor, Detroit nchini Marekani. 
Shujaa wa United alikuwa ni winga Ashley Young aliyefunga mabao mawili- huku bao pekee la Real likifungwa Gareth Bale.
Young alifunga bao la kwanza kwa kikosi cha Louis van Gaal dakika ya 20, kabla ya Madrid kusawazisha kwa penalti kupitia kwa Bale dakikan ya 27.
Lakini Young tena akamuinua kitini kocha Van Gaal dakika ya 37 akiunganisha vizuri krosi kumtungua kipa Iker Casillas. Nyota wa zamani wa United, Cristiano Ranaldo ambaye kabla ya mcheo huo alisema hajawahi kukataa kurudi timu hiyo, aliingia dakika ya 74, lakini akashindwa kuisaidia timu yake. 
Umati wa mashabiki 109,00 ndani ya Michigan mjini Ann ArborBurst of pace: Gareth Bale draws a foul from Michael Keane inside the penalty area
Gareth Bale akimtoka Michael Keane Dictating play: Rooney put in a good performance for Van Gaal's side as they upset Madrid in Detroit
Rooney aling'ara jana mjini Detroit Friendly: Danny Welbeck and Pepe challenge for a cross as United have the best of the early exchanges
Danny Welbeck akipambana na beki 'mtata' PepeStar turn: The Portugal captain did not push himself too hard as he continues his preparations for the season
Ronaldo alishindwa kuiepusha na kipigo Real janaStill a threat: Shaw and Tyler Blackett keep a close eye on Ronaldo as he dribbles with the ball for Madrid
Shaw na Tyler Blackett wakitafuta mbinu za kumpokonya mpira Ronaldo 
Javier Hernandez ‘Chicharito’ akawafungia Mashetani Wekundu bao la tatu dakika ya 80 mbele ya mashabiki 109,318 waliotapisha Uwanja wa Michigan.
Kikosi cha United kilikuwa; De Gea, Keane, Jones, Evans/Blackett dk45, Valencia/Lingard dk61, Herrera/Cleverley dk45, Fletcher, Young/Shaw dk45, Mata/Kagawa dk61, Welbeck/Zaha dk41 na Rooney/Hernandez dk61.
Real Madrid; Casillas, Arbeloa/Ronaldo dk73, Pepe, Ramos, Fernandez, Alonso/De Tomas dk55, Carvajal, Illarramend, Modric, Bale na Isco.

LIVERPOOL YAWAFUMUA AC MILAN 2-0...NI WAO NA MAN UNITED KESHO MIAMI


KLABU ya Liverpool itakwenda Miami kupambana na wapinzani Manchester United Jumatatu kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya AC Milan mjini Charlotte.
Mabao ya Joe Allen na Suso yameifanya timu ya Brendan Rodgers ishinde mechi ya tatu katika Kombe la Kimataifa nchini Marekani.
Liverpool tayari ilikuwa imejihakikishia kuongoza kundi lake kufuatia kipigo chaManchester City kwa penalti 5-4 kutoka kwa Olympiacos baada ya sare ta 2-2.

Mwanzo mzuri: Joe Allen akipongezwa na Rickie Lambert baada ya kuifungia bao la kwanza Liverpool dhidi ya AC Milan

MAN CITY HAWAKUAMINI MACHO YAO MAREKANI



Balaa gain hili!: Wachezaji wa Manchester City wakiwa wamejichokea baada ya kutolewa kwa penalti 5-4 na Olympiacos mjini Minneapolis katika Kombe la Kimataifa kufuatia safe ya 2-2Shot stopper: Roberto Jimenez Gago was the hero for the Greek side in the shootout
Kiboko yao: Kipa Roberto Jimenez Gago alikuwas shujaa wa timu ya Ugiriki baada ya kucheza penalti

Usain Bolt aisaidia Jamaica kuwika


  
Usain Bolt
Bingwa wa michezo ya Olimpiki katika mbio za mita 100 Usain Bolt ameiongoza Jamaica kushinda medali ya dhahabu katika michezo ya jumuiya ya madola nchini Scotland.
Bolt alikimbia mita mia moja za mwisho baada ya kupokezwa kijiti ambapoJamaica ilishinda kwa urahisi na kuweka rekodi mpya katika michezo hiyo ya sekunde 37.
Ilikuwa medali ya kwanza ya mwanariadha huyo.
Mbio hizo za kupokezana vijiti ndio zilizokuwa za mwisho na zenye msisimuko mkubwa katika mpango

Mlipuko wa bomu Mogadishu wawauwa 3


  
Mlipuko mjini Mogadishu

Bomu moja lililokuwa limefichwa katika mfuko wa plastiki limelipuka katika mji mkuu wa Somali ,Mogadishu na kuwauwa takriban wanawake watatu waliokuwa wakilisafisha jiji hilo huku wengine 11 wakijeruhiwa.
Mfuko huo ulikuwa umechanganywa na takataka karibu na soko moja ambapo wafanyikazi wa kulisafisha jiji hilo hukutana.
Haijulikani ni nani aliyeegesha bomu hilo,lakini kundi la Alshabaab limetekelza mashambulizi kadha katika mji wa Mogadishu katika kipindi cha hivi karibuni.

Shambulizi la Israel lawaua watu 10



Gaza
Ripoti za hivi karibuni zinaarifu kuwa shambulizi la angani laIsrael limewauwa watu saba katika shule moja ya umoja wa mataifa katika mji wa Rafah.
Walioshuhudia wanasema kuwa kombora hilo lilipiga eneo moja karibu na mlango wa shule hiyo.
Usiku kucha Israel ilirusha makombora 13 ya angani yaliowauwa watu 13 waliuawa huku makombora mawili ya roketi yakirushwa nchini Israel.
Msemaji wa Jeshi la Israel Luteni kanali Peter Lerner amesema kuwa baadhi ya wanajeshi wanaondolewa katika eneo la Gaza ,lakini oparesheni hiyo itaendelea.
Wajumbe wa Hamas wamewasili katika mji mkuu wa cairo nchini Misri kwa mazungumzo ya kusitisha vita.
Israel imesema kuwa haipelekwa wawakilishi wake.
Wakati huohuo Msemaji wa umoja wa mataifa katika eneo la Gaza ameonya kuwa maafa makubwa ya kiafya huenda yakazuka katika eneo la Gaza kufuatia wiki tatu za mapigano katika eneo hilo.
Chris Gunness kutoka shirika la umoja wa mataifa linalosimamia misaada amesema kuwa maafisa wa afya katika eneo la Gaza wanaendelea kulemewa.
Amesema kuwa hospitali,zahanati na ambulansi zimeharibiwa na kwamba zile zinazotoa huduma zimezidiwa huku asilimia 40 ya maafisa wa afya wakishindwa kufika kazini.

Saturday, 2 August 2014

KIONGOZI TFF ASHUHUDIA YANGA SC ‘INAVYOLALIWA’ MSUMBIJI, ASEMA...


 
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau leo ameshuhudia namna klabu ya Yanga SC inavyohujumiwa nchini Msumbiji.
Asubuhi ya leo, Kidau ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo, nchini hapa alikutana kijana mmoja akiwa amevalia jezi Yanga ambayo amenunua kwa watu wanaouza bila idhini ya klabu hiyo.
Kidau alifika Uwanja wa Ndege kuwapokea washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC waliokuja kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji, Msumbiji kesho.
Kidau kushoto akiwa na raia wa Msumbiji aliyenunua jezi ya Yanga SC mjini Beira

Kijana huyo raia wa Msumbiji, Magnum alisema kwamba jezi hiyo aliinunua Beira na anafahamu kwamba Yanga SC ni timu ya Tanzania, lakini haijui.
“Nimependa jezi nzuri, rangi nzuri nikanunua,”alisema kijana huyo ambaye alifika uwanja wa ndege kupata huduma za kibenki.
Alisema amenunua jezi hiyo kwa thamani ambayo ni sawa na fedha za Tanzania Sh. 15,000 na kwamba watu wengine pia wananunua kwa wingi na kuvaa jezi hizo nchini Msumbiji.
Kidau alisema kwamba Yanga SC na watani wao Simba SC wanapoteza fedha nyingi kutokana na kupuuza bishara ya jezi na bidhaa nyingine zenye nembo zao.
“Sasa watu ambao wanajua kama hii ni bishara nzuri, ndiyo wanajipatia fedha nyingi kirahisi namna hii, hii ni biashara kubwa sana, klabu nyingi Ulaya zinanufaika mno kwa biashara hii,”alisema kiungo wa zamani wa Milambo ya Tabora, Simba SC na timu ya Taifa, Taifa Stars.
Pamoja na ukweli huo kwamba jezi za timu ni biashara inayoziingizia fedha nyingi hata klabu kubwa Ulaya, lakini bado viongozi wa Yanga SC  hawajaonyesha kutaka kutumia fursa hiyo kuinufaisha klabu yao kiuchumi.
Jezi za Yanga pamoja na mahasimu wao, Simba SC zinapatikana karibu Afrika Mashariki yote na nchi nyingine jirani ikiwemo Msumbiji.
Wapembuzi yakinifu wa masuala ya biashara hiyo wanaamini, kwa mwaka Simba na Yanga zinakosa si chini ya Sh. Milioni 500 kila klabu kwa kupuuza biashara ya jezi pekee.

Kenya yakata rufaa ya marufuku ya CAF


 
Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche
Kenya imekata rufaa ya marufuku ya mwaka mmoja iliyopewa kocha wa timu ya taifa Adel Amrouche na shirikisho la soka barani Afrika CAF.
Amrouche alipigwa marufuku hiyo baada ya kudaiwa kumtemea mateafisa msimamizi wa mechi baina ya Harambee Stars ya Kenya naComoros mwezi Mei.
katibu wa Shirikisho la soka la Kenya FKF Michael Esakwa ameiambia BBC kuwa tayari wameshatuma ombi la kukata rufaa kwa shirikisho la CAF .
Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche
"baada ya kuona video ya tukio hilo linalodaiwa kutokea baada ya mechi nina hakika kuwa hakuna aliyetemewa mate ''.
Sadfa ni kuwa kocha mkuu wa Comoros Amir Abdou amepuzilia mbali uwezekano wa tukio hilo akisema haiwezekani kuwa Amrouche alimtemea mate afisa huyo.
''Mimi mwenyewe nili kuwepo na pia nilitazama video na kwa hakika ninaunga mkono FKF maanake hii ilikuwa ni mechi ambayo tulishiriki.''
Ujumbe huo wa kocha Abdou ulimpiga jeki Esakwa ambaye anasema kuwa taarifa hiyo itakuwa kati ya habari watakazopendekeza kutumiwa katika rufaa hiyo.
Kenya imekata rufaa ya marufuku ya kocha Adel Amrouche
Kufuatia marufuku hiyo ya Amrouche, Kenyasasa inamtegemea Kocha mbadala James Nandwa kuiongoza Kenya katika mechi ya mkondo wa pili ya kufuzu kwa mechi ya kuwania kufuzu kwa dimba la mabingwa wa Afrika dhidi ya Lesotho.
Mechi hiyo itachezwa wikiendi hii mjini Nairobi.
Kenya ilishindwa katika mkondo wa kwanza kwa bao moja kwa nunge ugenini.

Bolt aisaidia Jamaica kufuzu


   
Usain Bolt
Bingwa wa mbio za mita 100 duniani Usain Bolt amelisadia taifa lake la Jamaica kufuzu katika fainali za 400 m x 100m hii leo licha ya tishio na kusisitiza kuwa amefurahi kuwa Glasgow.
Bolt amelazimika kukana madai kwamba alitoa matamshi mabaya dhidi ya mashindano hayo,ambapo nusra jamaica ishindwe baada ya mmoja ya wakimbiaji wake katika mbio za 400m X100m kupata jeraha.
Hatahivyo Bolt aliweza kuwasaidia wenzake na kushinda mbio hizo.
Bolt baadaye alikiri kwamba alifikiri kuna tatizo mahala .
Anasema kuwa alikuwa na wasiwasi lakini mwanariadha kimmari wa jamaica aliyeanza mbio hizo na kupata jeraha alimpokeza mwenzake kijiti cha kukimbia.
''Kocha wangu kwa mara nyingi hutuambia tukimbie na uchungu'',alisema Bolt.

Libya:Uingereza kuufunga ubalozi wake.


 
Ubalozi wa Uingereza mjini Tripoli,Libya

Uingereza inatarajiwa kuufunga ubalozi wake kwa mda katika mji mkuu wa Tripoli nchini Libya kufuatia mapigano makali katika mji wa Benghazi.
Zaidi ya watu mia mbili wameuawa katika miji hiyo miwili katika kipindi cha majuma mawili yaliopita.
Wizara ya maswala ya kigeni nchini Uingereza imesema kuwa oparesheni za ubalozi huo zitasitishwa baada ya siku ya jumatatu.
Imesema kuwa inafanya mipango ya kuwaondoa raia wa Uingereza ambao wanataka kuondoka nchini humo.
Mataifa mengi ya Magharibi ikiwemo Marekani tayari yamewaondoa wajumbe wao.
Siku ya ijumaa maelfu ya waandamanaji walifanya maandamano katika barabara za mji wa Tripoli na Benghazi ili kuwapinga wapiganaji ambao wamekuwa wakikabiliana na vikosi vya serikali ya Libya.

W.H.O:Ebola inaweza kuwa janga baya


 
Mgonjwa wa ebola abebwa
Mkurugenzi wa shirika la afya duniani Margeret Chan amesema kuwa kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola Magharibi mwa Afrika kunaweza kusababisha janga baya iwapo hautazuiwa.
Akizungumza mjini Conakry baada ya kukutana na marais wa Guinea,Liberia na Sierra Leone,amesema kuwa ugonjwa huo unasambaa kwa kasi ikilinganishwa na juhudi za kuudhibiti,lakini akaongezea kuwa unaweza kusitishwa kutokana na usaidizi wa kimataifa.
Marekani imesema kuwa raia wawili wa taifa hilo wa kutoa msaada wanaougua ugonjwa wa ebola watasafirishwa hadi nchini Marekani mapema wiki ijayo ili kupewa matibabu katika eneo lililotengwa.
Kisa hicho cha ugonjwa huo kitakuwa cha kwanza kutibiwa marekani.

Gaza:Mashambulizi ya Israel yawaua 100


 
Gaza

Maafisa wa matibabu katika eneo la Gaza wanasema kuwa zaidi ya wapalestina 100 wameuawa na makombora ya Israeltangu kukiukwa kwa makubaliano ya kusitisha vita siku ya ijumaa.
Vifo vingi vimetokea katika eneo la Rafah kusini mwa Gaza ambapo wanajeshi wawili wa Israel waliuawa na mwengine wa tatu kudaiwa kutekwanyara baada ya kuvamiwa na wapiganaji wa Hamas.
Kundi la wapiganaji wa kipalestina Hamas limesema kuwa halina habarizozote kuhusu mwanajeshi aliyetoweka Hadar Goldin na kwamba huenda aliuawa katika mapigano.