MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Thursday, 5 September 2013

KAMATI YA UTENDAJI YANGA YAKUTANA LEO KUMJADILI KATIBU MKENYA




Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga, itakutana leo jioni katika kikao cha dharura kilichoitishwa kujadili suala la katibu mkuu mpya raia wa Kenya aliyetimuliwa na wazee wa klabu hiyo.

Kikao hicho kimeitishwa ikiwa ni siku moja tu baada ya wazee kumtimua Patrick Naggi raia wa Kenya ambaye alikwenda klabuni hapo na kujitambulisha ndiye katibu mpya.


Imeelezwa kamati hiyo itajadili masuala mengine kadhaa, lakini agenda namba moja na kubwa ni hiyo inayomhusu Naggi.

Naggi aliyewahi kuwa mkugenzi wa ufundi wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) alipewa saa 24 awe ameondoka na kutogusa tena katika klabu hiyo.

Taarifa zimekuwa zikieleza kwamba aliletwa na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf manji lakini bado hakuna utuhibitisho na taraifa zilieleza Manji alikuwa nje ya nchi katika kazi zake za kibiashara.

Mkenya alituhumiwa na wazee hao kwamba hakueleza aliyempeleka klabuni hapo, badala yake akajitambulisha kwamba anachukua nafasi ya Lawrence Mwalusako.

MJANE ANAOMBA MSAADA WA KUTIBIWA MKONO BAADA YA KUJERUHIWA NA NYOKA

Tunomba radhi kwa picha zilizo wekwa kwenye mtandao huuu

Mwanamke Mjane FAINES NAMBEYE KAONGA [60] Mkazi wa kijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI Wilaya ya CHUNYA Mkoani MBEYA anawaomba wasamaria kumchangia pesa kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kujeruhiwa  na nyoka alipokuwa amelala  chumbani kwake.
Hivi ndivyo mkono wake ulivyo kwa sasa



Mwanamke mmoja Mjane aliyefahamika kwa jina la FAINES NAMBEYE KAONGA [60] Mkazi wa kijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI Wilaya ya CHUNYA Mkoani MBEYA anawaomba wasamaria kumchangia pesa kwa ajili ya kupata matibabu baada ya kujeruhiwa  na nyoka alipokuwa amelala  chumbani kwake.

Mjane huyo alijeruhiwa mkono wa kushoto na nyoka alipokuwa amelala chumbani kwake hivi karibuni na kusababisha ngozi kutoka hali iliyomsababishia maumivu makali ambapo alikimbizwa Hospitali ya Wilaya ya CHUNYA na kupatiwa matibabu lakini mpaka sasa hali inazidi kuwa mbaya.

FAINES  amesema pamoja na kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya na kuruhusiwa kurudi nyumbani mkono umezidi kuliwa na sumu na kusababisha ngozi kutoka hadi mfupa kutokeza nje ya ngozi hali inayomtia hofu siku hadi siku.

Mama huyo hana pesa za kuweza kupata matibabu zaidi kutokana nayeye kufiwa na mumewe na wanawe hawana uwezo wa kugharamia matibabu katika Hospitali nyingine hivyo kuwaomba wasamaria wema kumsaidia ili aweze kuokoa maisha.

Baadhi ya majirani wamesema mama huyo ameumwa na nyoka siku za hivi karibuni akiwa amelala chumbani kwake na alipopelekwa kupatiwa matibabu hajapata ahueni na afya yake imezidi kuzorota siku hadi siku hali akishindwa kufanya kufanya shughuli za kiuchumi

Picha na Ezekiel Kamanga
kwa hisani ya Mbeya yetublog

Kwa atakae guswa  kumsaidia mjane huyu wasiliana 
na

0754 49 07 52
AU
0754 37 44 08

MTALII ASHAMBULIWA NA KUUAWA NA TEMBO HIFADHI YA TAIFA YA TARANGIRE

Raia mmoja wa Marekani, Thomas Vardon Mcaffe mwenye umri wa miaka 58, ameuawa baada ya kushambuliwa na kundi la tembo wakati akifanya shughuli za utalii katika hifadhi ya Taifa Tarangire iliyoko mkoani Manyara

Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Manyara, Mussa Marambo, ameiambia TBC kuwa, tukio hilo limetokea juzi saa 2 asubuhi wakati mtalii huyo kutoka Jimbo la Califonia nchini Marekani akiwa na wenzake wawili walipokuwa wakitalii katika hifadhi hiyo.

Kamishna Msaidizi wa Polisi Marambo amebainisha kuwa watalii hao walikimbizwa na kundi la tembo wapatao 50 wenye hasira, ambapo katika jitihada za kujihami, marehemu Thomas alikwama kwenye tope na kushambuliwa kwa kukanyagwa na tembo hao huku wenzake wawili wakifanikiwa kujiokoa.

Jitihada za kuokoa uhai wa marehemu baada ya kukimbizwa katika zahanati ya Tarangire ziligonga mwamba kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata wakati wa tukio hilo.

Mwili wa Merehemu umesafirishwa kwa ndege na kuhifadhiwa katika hospitali ya Selian, Arusha kwa uchunguzi zaidi wakati taratibu za kuukabidhi mwili wake kwa  ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa ajili ya kuurejesha kwao inafanywa.

Benny Mwaipaja, 
TBC - Manyara.

WABUNGE WA CCM WATUHUMIANA RUSWA


SIKU moja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Muswada wa Sheria ya Vyama vya Ushirika, baadhi ya mawaziri na wabunge wanatuhumiwa kuhongwa na wafanyabiashara wakubwa wa makampuni ya pembejeo za kilimo ili kushinikiza kupitisha muswada huo.

Habari za kuaminika ambazo MTANZANIA imezipata jana kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilichokuwa chini ya Uenyekiti wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, zinasema baadhi ya wabunge walimtuhumu Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangwalah (CCM) kuwa amehongwa na Chama Kilele cha Ushirika (APEX), ili apinge hoja ya Serikali kwa nguvu.


Katika kikao hicho, Dk. Kigwangwalah alituhumiwa kuwa ni miongoni mwa watu ambao wamepewa tenda ya kusambaza pembejeo za kilimo cha wakulima wa tumbaku kupitia kampuni yake binafsi.

Kutokana na mjadala huo kuwa moto, wabunge hao walilazimika kutoka na azimio la kuifuta APEX kama njia ya kunusuru kupitishwa kwa muswada huo.

Chanzo cha kuaminika kililiambia MTANZANIA kuwa kutokana na hoja hizo, ikiwemo tuhuma dhidi ya wabunge na mawaziri kuhongwa na wenye makampuni kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kusambaza pembejeo za kilimo, ilimlazimu Pinda kutumia busara ili kumaliza malumbano hayo.

Baada ya mvutano huo, Dk. Kigwangwalah aliomba nafasi ya kujitetea mbele ya Waziri Mkuu.

Alisema hajawahi kuhongwa na wenye makampuni ya watu wanaosambaza mbolea kwa lengo la kuipigia debe APEX.

“Kilikuwa ni kikao moto, maana ziliibuka tuhuma nzito nzito mno kwa baadhi ya wabunge na mawaziri kuhongwa ili kuweza kufuta APEX kwa lengo la kuwabeba wasambazaji wa pembejeo za kilimo kutoka nje ya nchi.

Mbali ya hilo, MTANZANIA iliambiwa kuwa kutokana na ukali waliokuwa nao wabunge wengi wa CCM, kikao hicho kilimpa onyo Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso (CCM), kutokana na tuhuma zake alizozitoa bungeni dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB), Vita Kawawa pamoja na Makamu wake, Said Nkumba.

Viongozi hao wanadaiwa kuidhinisha mamilioni ya fedha dhidi ya Mkurugenzi Mtendaji wake.

Kutokana na tuhuma hizo, MTANZANIA ilimtafuta Dk. Kigwangwalah ili kupata ukweli kuhusu tuhuma zake za kuhongwa kwa madai kuwa amepewa tenda ya kusambaza pembejeo kupitia Mwenyekiti wa APEX, Moshi Kakoso, ambaye pia ni mbunge wa Mpanda Vijijini (CCM). Alisema hatua ya Bunge kupitisha muswada huo wa sheria ipo siku madudu yataibuka na dhambi itawarudia wabunge waliopitisha, huku wakiifuta APEX kwa maslahi yao binafsi na si ya taifa.

“Daima ninachotaka kusema kuwa mimi ni mfanyabiashara, hata kama ni kutajirika sikutajirika kupitia Bunge, ila kwa kipindi kirefu nilikuwa nafanya biashara ya pamba, lakini hili la kampuni yangu kupewa tenda na APEX si kweli na kama wao wana ushahidi waseme ni kampuni gani.

“Niliapa mbele ya Waziri Mkuu na kikao cha wabunge wa CCM kuwa kama yupo mtu mwenye ushahidi mbele yangu na ajitokeze.

“Mbona kuna taarifa za baadhi ya mawaziri na wabunge kuhongwa ili waweze kupitisha muswada huu na kuifuta APEX. Huu ni ukoloni mamboleo, sasa unarejeshwa nchini kwa mlango wa nyuma,” alisema Dk. Kigwangwalah.

Wakati wa kuhitimishwa kwa mjadala huo jusi, wabunge wa CCM walivuana nguo kwa kutoleana siri zao za ndani, huku Mbunge wa Sikonge, Said Nkumba (CCM), akijibu mapigo kwa kumtuhumu Mwenyekiti wa APEX, Moshi Kakoso, alisababisha ufujaji wa Sh bilioni 16 za wakulima wa tumbaku 


chanzoMtanzania
Alhamisi, Septemba 05, 2013 
  Na Bakari Kimwanga, Dodoma

Wednesday, 4 September 2013

HAYA NDIYO MADAWA YA KULEVYA ALIYOKAMATWA NAYO MNAIGERIA JIJINI DAR ES SALAAM

 
“Baada ya kumhoji ametueleza kuwa dawa hizo alizinunua maeneo ya Magomeni, kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi na mahojiano zaidi.” Clemence Jingu 
Na Fide lis Butahe  


Dar es Salaam. Mwanamke ambaye ni raia wa Nigeria, amekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akiwa na kete 99 za dawa za kulevya.
Hata hivyo kete hizo hazikujulikana ni za aina gani.

Kukamatwa kwa raia huyo, kumekuja wiki tatu tangu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kutangaza vita dhidi ya watu wanaopitisha dawa za kulevya katika idara na taasisi zilizoko chini ya wizara yake.
Akizungumza na Mwananchi jana, Meneja Usalama wa uwanja huo, Clemence Jingu, alisema mtuhumiwa alikamatwa jana saa 8:00 mchana

Alisema kete hizo alikuwa ameziweka katika makopo ya poda na mafuta.
“Kete hazijajulikana ni za aina gani, kwa sasa tunafanyika utaratibu wa kutambua aina yake,” alisema.

“Kwa sasa hapa JNIA kuna mitambo ya kisasa ya kuweza kuwabaini wanaopitisha dawa hizi, tulimkamata akiwa na kete 99, kati ya hizo kete 30 alikuwa ameweka katika kopo la mafuta ya nywele, kete nyingine alikuwa ameweka katika kopo la poda za watoto,” alisema.
Alisema kuwa raia huyo wa Nigeria alikuwa akielekea Roma, Italia kupitia Paris, Ufaransa kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

“Baada ya kumhoji ametueleza kuwa dawa hizo alizinunua maeneo ya Magomeni, kwa sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi na mahojiano zaidi,” alisema.
Alisema kuwa binti huyo aliingia nchini Agosti 30mwaka huu, akitokea nchini Nigeria.

ANGALIA WABUNGE WA CHADEMA,NCCR-MAGEUZI NA CUF WALIVYO TOKA NJE YA BUNGE

 
Wabunge wa Vyama vya CUF, NCCR-Mageuzi, na Chadema wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge kupinga muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba bungeni dodoma jana.Picha na Fidelis Felix 



Dodoma.Wabunge wa Kambi ya Upinzani Bungeni jana jioni walitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge, baada ya kupuuzwa kwa mwongozo wao wa kutaka kuahirishwa kujadiliwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, hadi hapo Zanzibar itakaposhirikishwa.

Wabunge waliotoka bungeni jana yapata saa 12.15 ni kutoka vyama vya Chadema, CUF na NCCR- Mageuzi huku Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP, Augustine Mrema akiendelea kubaki ukumbini.

Kitendo cha wabunge hao wa upinzani kilionekana kuwakera baadhi ya wabunge wa CCM, ambao walisikika wakiwakejeli kwa kupiga meza huku wakisema: “Kwendeni zenu, tumewazoea.”
Wakati wabunge hao wakiondoka, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alikuwa akiwasisitiza wabunge wanaobakia wawe watulivu, maana kuna usalama wa kutosha ndani ya ukumbi huo.
“Mnaotoka nimewaona wote na mnanijua,” alisikika Naibu Spika Ndugai akiwatahadharisha wabunge wa upinzani waliosusa mjadala huo.

Wabunge wa CCM waliendeleza vituko ambapo baada ya wapinzani kutoka, wabunge Juma Nkamia (Kondoa Kusini), Hilary Aeshi ( Sumbawanga Mjini) na Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini) walikwenda kukaa katika viti vya kambi ya upinzani.

Kabla ya kutoka kwa wabunge hao wabunge wawili kutoka CUF waliomba mwongozo wa Spika, wakitaka muswada huo kuondolewa ili kuwapa nafasi Wanzanzibar kutoa maoni yao.
Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mohamed Mnyaa (CUF) aliomba mwongozo akitaka muswada huo uondolewe, hadi hapo Wazanzibar watakaposikilizwa.

Alisema kuwa kwa maoni ya Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala wamesikiliza maoni ya wadau wengi, lakini Zanzibar hawakwenda kuwasikiliza wadau wa eneo hilo.

“Na hili suala zima katika masuala ya katiba linahitaji usawa wa washirika, tunazungumza kitu kinachohusiana na Zanzibar na Tanzania Bara, ili kupata maoni ya nchi nzima kuna uhalali gani wa Bunge hili kuendelea na mjadala huu?” alihoji.

Hata hivyo, alikatizwa na kelele za Mbunge wa Viti Maalumu, Pindi Chana (CCM), ambaye alitoa taarifa kuwa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ilialika wajumbe mbalimbali ikiwamo Zanzibar.
“Miongoni wa wajumbe walioalikwa ni pamoja na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na wadau mbalimbali ambao walikuja mbele ya Katiba,” alisema Pindi ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo.
 
Na Waandishi Wetu   Mwananchi
Posted  Jumatano,Septemba4  2013  

JWTZ YAKAMATA WANAJESHI WANNE WA RWANDA WALIOKUWA KONGO WAKIWASAIDIA WAASI WA M23

 

SKARI wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini Kongo (Monusco), wakiongozwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamedai kuwakamata maofisa wanne wa jeshi la Rwanda, katika mapigano ya wiki iliyopita nchini Kongo.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano kwa sharti la kutotajwa jina, mmoja wa askari aliyepo ndani ya kikosi cha JWTZ huko nchini Kongo, alisema maofisa hao wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Taarifa hizi za sasa zinakuja wakati ambapo kumekuwa na madai ya muda mrefu, ambayo yamekuwa yakitolewa na Umoja wa Mataifa pamoja na Marekani kwamba, Rwanda imekuwa ikiwasaidia waasi wa kundi la M-23.

Pamoja na kwamba Rwanda imekuwa ikipinga madai hayo, kitendo chake cha wiki iliyopita cha kuamua kupeleka bataliani mbili zenye wanajeshi 1,700 ili kukabiliana na kile kinachodaiwa kuwa ni kishindo cha vikosi vya Umoja wa Mataifa vyenye jukumu la kulinda amani katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa kirasilimali, kinatokana na waasi wa M23 kupata kipigo kikali.

Chanzo chetu hicho kutoka uwanja wa mapambano nchini Kongo, kililidokeza gazeti hili kuwa maofisa hao wa Jeshi la Rwanda waliwakamata katika mapigano hayo yaliyodumu kwa zaidi ya wiki moja, ambayo tayari yamewakimbiza waasi wa M23.

“Askari wa Rwanda tuliowakamata, ni maofisa wa ngazi za juu kabisa jeshini, tena walikuwa na sare za jeshi hilo… walikuwa wakiwasaidia hao M23, lakini kwa kuwa sisi tulikuwa makini tulifanikiwa kuwatandika hadi tukawakamata,” kilisema chanzo chetu hicho.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vya habari vya kuaminika zinaeleza kwamba, hatua hiyo ya kuwakamata maofisa hao pamoja na kuondoka kwa waasi wa kikundi cha M23, imefanikisha kushinda vita hiyo kwa zaidi ya asilimia 95.

Mtoa taarifa wetu huyo kutoka Kongo, ameliambia gazeti hili kuwa, tayari Monusco wanaoongozwa na JWTZ wameanza kufurahia ushindi huo na kwamba sasa hivi wanasubiri tamko kutoka kwa wakuu wao, ili kufahamu kinachofuata baada ya kufanikisha hatua hiyo.

MAPIGANO YALIVYOKUWA
Akielezea namna walivyofanikiwa kutoa kibano kwa M23, askari huyo kwanza alikiri kuwa mapigano yalikuwa makali, kutokana na kikundi hicho cha waasi kusheheni vifaa vya kisasa na msaada wanaoupata kutoka Serikali ya Rwanda.

“Kwa kweli mapigano yalikuwa makali sana, lakini kwa upande wetu sisi tulikuwa tunajiamini kutokana na vifaa ambavyo pia ni vya kisasa hususani ikizingatiwa jeshi letu ni la Umoja wa Mataifa.

“Tulifanikiwa kuteka ngome yao kwa kutumia mbinu mbalimbali za kijeshi na kuwafanya watawanyike kabisa katika eneo hilo.

“Ngome yao ilikuwa ni kubwa sana, ina ukubwa wa zaidi ya viwanja vitatu vya mpira… na katika eneo hilo kulikuwa kumesheheni vifaa vyao vya kivita, kama makombora, mafuta, mizinga pamoja na vifaa vingine kama magari na baadhi ya silaha nyingine kubwa kubwa za kivita,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, sasa hali ni shwari ndani ya nchi hiyo ya Kongo.

“Baada ya kuwasambaratisha sasa wamekimbilia eneo moja lililopo karibu na mpaka wa Uganda. Kama unavyofahamu hawa jamaa walikuwa wakitumia mbinu za kujihami kwa kurusha mabomu katika eneo la Rwanda, ili ionekane kuwa sisi tumerusha,” alisema askari huyo.

“Lakini tunamshukuru Mungu, tupo salama ingawa tumempoteza askari mmoja na askari wengine wenzetu wa Tanzania ambao ni wanne, wamepata majeraha kidogo lakini wanaendelea vizuri.

“Hivyo nawaomba Watanzania wenzangu waendelee kutuombea turudi salama, kwa sababu kazi sasa imeshakamilika,” alisema askari huyo.

Juhudi za gazeti hili kumpata msemaji wa Monusco, Luteni Kanali Prosper Basse kuzungumzia juu ya taarifa hizo, zilishindikana.

Taarifa ambazo tumezinasa kwa siku kadhaa sasa kutoka uwanja wa mapambano na ambazo zimegusa vichwa kadhaa vya habari zinaeleza kuwa, brigedia maalumu ya vikosi vya UN yenye dhamana ya kujibu mashambulizi (FIB), katikati ya wiki iliyopita iliendesha operesheni kubwa iliyoharibu kabisa ngome muhimu ya waasi wa M23, hali inayotajwa na wachambuzi wa mambo kuwa ndiyo iliyoishtua Serikali ya Rwanda ambayo inatuhumiwa kuwasaidia waasi hao.

Taarifa za kijeshi zinaeleza kuwa, FIB ambayo inaundwa na wanajeshi wapatao 3,000 kutoka Tanzania na Afrika Kusini chini ya Azimio Namba 2098 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limejizatiti kwa zana za kisasa za kivita zikiwamo mizinga na helikopta za kivita.

Taarifa kutoka mashariki ya Kongo zinaeleza kwamba, mashambulizi dhidi ya waasi wa M23 ambao hivi karibuni waliripotiwa kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa Tanzania aliye katika jeshi la UN, yamesababisha waasi hao kukimbilia katika eneo la milima lililopo umbali wa kilomita tano kutoka mji mdogo wa Kanyaruchinya Mashariki mwa Goma.

M23 WAZUNGUMZA
MTANZANIA Jumatano jana lilifanikiwa kuzungumza na Rais wa M23, Bertrand Bisiimwa, ambapo pamoja na mambo mengine alieleza sababu za vikosi vyao kuondoka katika ngome yao ya kivita sambamba na taarifa za kuibuka kwa mapigano mapya ya hivi karibuni.

Katika hilo, Bisiimwa alikiri kikosi chake kurudi nyuma siku nne zilizopita, huku akiitaja sababu ya kufanya hivyo kuwa ilitokana na wao kutotaka vita baada ya majeshi ya Kongo kuanza kuwarushia mabomu kwenye kambi yao.

“Sisi tuliamua kurudi nyuma tusiendeshe vita, tunajua aliyetupa hayo mabomu ambayo yalifika mpaka Rwanda, tunaitaka Umoja ya Mataifa ikuje ifanye uchunguzi wake…wakuje waangalie vifaa yetu waone kama inaweza kurusha mabomu hadi Rwanda,” alisema.

Hata hivyo, Bisiimwa alisema kuwa sio kweli kama majeshi ya Umoja wa Mataifa yakiongozwa na JWTZ yaliwasambaratisha katika ngome yao.

“Sio kweli walikuja Kanyaruchina tukiwa tumeondoka na tuliondoka si kwa sababu ya kuwakimbia, hapana tulitaka UN wafanye uchunguzi yake juu ya kurushwa mabomu, kwa sababu wanataka kutuvalisha mambo ya uongo mchafu,” alisema Bisiimwa.

Bisiimwa alijigamba kuwa majeshi ya Kongo hayawawezi na kwamba walikwishawashindwa, lakini akakiri kwamba majeshi ya Umoja wa Mataifa wanaweza kuwaondoa.

“Ninakiri hiyo kwa sababu Umoja wa Mataifa inaweza kututoa, unajua inakuwa na nguvu ya hatari,” alisema Bisiimwa kwa Kiswahili cha tabu.

CHANZO-Mtanzania

WAFUASI WA MORSI WAFUNGWA JELA NCHINI HUMO


 
Morsi angali anazuiliwa akisubiri kufunguliwa mashtaka
Mahakama ya kijeshi nchini Misri imetoa hukumu ya vifungo vya muda mrefu jela kwa wafuasi wa Rais aliyepinduliwa Mohammed Morsi.
Watu hao walihukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kushambulia wanajeshi.
Mmoja wa washukiwa alifungwa jela maisha, wengine watatu wakipewa vifungo vya kati ya miaka 5, 15 na 45, kwa mujibu wa taarifa za jeshi.
Walishtakiwa kwa kuwafyatulia risasi wanajeshi wakati wa ghasia na vurugu katika mji wa bandarini wa Suez mwezi jana.
Vurugu hizo zilitokea baada ya msako mkali uliofanywa na maafisa wa usalama dhidi ya wafuasi wa Moris waliokuwa wamepiga kambi mjini Cairo.

Mamia ya watu, wengi wao wanachama wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, waliuawa wakati wafuasi wa Morsi walipokuwa wamepiga kambi nje ya msikiti wa Rabaa al-Adawiya na katika medani ya Nahda wakitaka Morsi aachiliwe, ingawa waliondolewa kwenye kambi hizo tarehe 14 mwezi Agosti.
Vurugu zilizotokea mjini Suez, Mashariki mwa Cairo, kati ya tarehe 14 na 16 mwezi Agosti zilisababisha vifo vya zaidi ya watu 30.

Hata hivyo haijulikani ikiwa wale waliohukumiwa Jumanne ni wanachama wa Brotherhood. Lakini ikiwa ni wanachama wa vuguvugu hilo, hukumu walizopewa bila shaka zitaathiri sana chama hicho hasa ikizingatiwa ni za kwanza kutolewa kwa vugu vugu hilo tangu kuondolewa mamlakani kwa Morsi.
Viongozi wa mashtaka walitangaza tarehe 1 Septemba miezi miwili baada ya kuzuiliwa kwa Morsi kuwa anatufunguliwa mashtaka kwa kuchochea mauaji.

RAIS MPYA WA MALI AAPISHWA RASMI

 
Rais mpya wa Mali Ibrahim Boubacar Keita

Rais mpya wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, ameapishwa kama rais wa nchi hiyo mjini Bamako.
Sherehe kubwa zaidi ambapo rais wa Ufaransa Francois Hollande amealikwa zitafanyika baadaye mwezi huu.

Wanajeshi wa Ufaransa walisaidia jeshi la Mali kupambana na wapiganaji wa kiisilamu waliokuwa wameteka eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo mapema mwaka huu.

Mtangulizi wa Keita ambaye kwa sasa ni kaimu rais, 
Dioncounda Traore, alisema mnamo Jumatatu kuwa tayari amekabiliana na changamoto kubwa sana ikiwemo kuandaa uchaguzi wa amani na kuweza kudhibiti maeneo yaliyokuwa yametekwa na waasi.

Duru zinasema kuwa bwana Keita atastahili kukabiliana na maswala muhimu zaidi kama vile kuleta uthabiti katika eneo la Kaskazini na kuleta mageuzi katika jeshi pamoja na kupambana na ufisadi.

MGOGORO WA WAFUGAJI NA WANAKIJIJI WA IGUNDU KATA YA SANGAMBI WILAYA YA CHUNYA MBEYA UMEMALIZIKA

Hatimaye mgogoro baina ya wanakijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI wilaya ya CHUNYA Mkoani MBEYA na jamii ya WAFUGAJI umemalizika baada ya serikali wilayani humo kuzikutanisha pande hizo na kuondoa tofauti zao.

 Baada ya mwenzao kuuwawa na maiti kuibwa hospitali wafugaji wakiandamana kuelekea eneo la tukio kujua kulikoni


Mweyekiti wa kijiji  cha IGUNDU EMMANUEL MBUGHI akijaribu kuwatuliza wafugaji hao kuwa watulie na wakae chini na kujadili huo mgogoro wao
Hakika wafugaji wakatulia na kusubiri viongozi ili waanza kujadili swala lao
Afisa Tawala Wilaya ya CHUNYA AMIMU MWANDELILE ambaye alilaani vikali kitendo kilichofanywa na vijana hao kwani kitendo hicho hakikubaliki na jamii kwani kinaondoa utu wa Mtanzania.

Mwenyekiti wa Wafugaji SAMWEL LAURENT  akielezea jinsi mgogoro huo ulivyoanza
Baada ya majadiliano ya muda mrefu Mweyekiti wa kijiji  cha IGUNDU EMMANUEL MBUGHI alipatanishwa na Mwenyekiti wa Wafugaji SAMWEL LAURENT ambao walipatanishwa na Afisa Tawala Wa Wilaya ambapo pande hizo ziliahidi kukomesha vitendo hivyo na kwamba wananchi wa IGUNDU waondoe hofu wao kama wafugaji hawatalipiza kisasi na waendelee na shughuli za uzalishaji mali
Hakika hali ya amani imerejea tena sasa nifuraha tu


Hatimaye mgogoro baina ya wanakijiji cha IGUNDU Kata ya SANGAMBI wilaya ya CHUNYA  Mkoani MBEYA na jamii ya WAFUGAJI umemalizika baada ya serikali wilayani humo kuzikutanisha pande hizo na kuondoa tofauti zao.

Mgogoro huo uliodumu kwa wiki moja kufuatia baadhi ya vijana wa kijiji hicho kumuua mfugaji aliyefahamika kwa jina la SAID PETRO kwa kipigo kutokana na vijana hao kumtaka awape pesa naye kushindwa kutekeleza takwa lao ndipo walianza kumpiga.

Kabla ya kupatanishwa wafugaji hao walikutana faragha kutoa msimamo wao juu ya vitendo vilivyokithiri kutoka kwa wanakijiji cha IGUNDU wakidai hilo ni tukio la tano kutokea na serikali ya kijiji haijachukua hatua yoyote kukomesha vitendo hivyo.

Baada ya mjadala mrefu wafugaji walikubali kusogea meza ya mazungumzo yaliyoongozwa na Afisa Tawala Wilaya ya CHUNYA AMIMU MWANDELILE ambaye alilaani vikali kitendo kilichofanya na vijana hao kwani kitendo hicho hakikubaliki na jamii kwani kinaondoa utu wa Mtanzania.

AMIMU amesema vitendo vya uhalifu kijijini hapo vinachangiwa na unywaji wa pombe kupita kiasi na utumiaji wa madawa ya kulevya ambapo vijana wanatafuta njia ya mkato kutafuta pesa  ikiwemo kucheza kamali badala ya kufanya kazi.

Aidha amesema kuwa serikali haitafumbia macho vitendo hivyo atahakikisha wale wote waliohusika na vitendo hivyo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwani hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria hivyo anayevunja sheria hatavumiliwa kabisa.

Kwa upande wake AMIMU alichukua fursa hiyo kuwapongeza wafugaji hao kwa moyo wa uvumilivu kwa kutolipa kisasi pamoja na vitendo vya kikatili walivyofanyiwa wafugaji hao zaidi ya mara tano hata kupelekea wengine kujeruhiwa na wengine kuuawa.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu Mweyekiti wa kijiji  cha IGUNDU EMMANUEL MBUGHI alipatanishwa na Mwenyekiti wa Wafugaji SAMWEL LAURENT ambao walipatanishwa na Afisa Tawala Wa Wilaya ambapo pande hizo ziliahidi kukomesha vitendo hivyo na kwamba wananchi wa IGUNDU waondoe hofu wao kama wafugaji hawatalipiza kisasi na waendelee na shughuli za uzalishaji mali,

Picha na Ezekiel Kamanga
Kwa hisani ya Mbeya yetublog

RAMOS ATOA YA MOYO WAKE KUHUSIANA OZIL


Beki kisiki wa Real Madrid, Sergio Ramos, ametoa ya moyoni kuhusiana na kuondoka kwa kiungo Mesut Ozil aliyejiunga na Arsenal.


Ramos amesema kama angekuwa ndiyo anayetoa uamuzi katika suala hilo, basi Ozil angebaki katika kikosi chao.



“Nasema wazi kuwa nimeumia kwa kuwa Ozil ni mtu mzuri, mchezaji hodari na rafiki yangu mkubwa. Sina la kuongeza kwa kuwa yeye na klabu wamefikia uamuzi.



“Namtakia kila la heri kwa uamuzi wake aliouchukua na nitaendelea kumkumbuka kama rafiki wa kweli,” alisema.


Pamoja na Ramos, wachezaji kadhaa wa Madrid walionyesha wazi kutofurahishwa na kuondoka kwa Ozil.


Mashabiki walipiga kelele wakati wa utambulisho wa Gareth Bale wakiusisitiza uongozi kufanya juhudi za kumbakiza kiungo huyo Mjerumani

BONDIO ALIYEPIGWA NA CHEKA NI KINYOZI KWAO MAREKANI

 


Bondia Phil Williams aliyedundwa na Francis Cheka katika kuwania ubingwa wa dunia uzito wa Super Middle unaotambuliwa na WBF ni kinyozi kwao Marekani.

Williams alipigwa na Cheka baada ya majaji wote watatu kumpa ushindi Mtanzania huyo ambaye ameweka rekodi ya kuwa wa tatu kuchukua ubingwa wa dunia baada ya Rashid Matumla na marehemu Shaaban Magoma.


Mitandao mbalimbali inaonyesha Williams aliyezaliwa Julai 12, 1977 katika Kitongoji cha Queens, New York nchini Marekani, amekuwa akifanya kazi kama kinyozi katika mji wa Minneapolis ambako anaishi kwa sasa.

Pambano kati ya Cheka na bondia huyo lilikuwa na mvuto zaidi kwa kuwa wawili hao kazi zao za nje si za ofisini kwa kuwa hata Cheka huuza chupa za plastiki zilizotumika katika Mji wa Morogoro.

Kabla ya kupigwa na Cheka kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Williams maarufu kama The Drill, alikuwa amepoteza pambano lake la mwisho kwa kushindwa na bondia kutoka Poland, Andrzej Fonfara katika raundi ya tatu.

Mmarekani huyo alionyesha ushindani mkali kwa Cheka ambaye amekuwa bondia Mtanzania asiyeshindwa katika kipindi hiki, hasa nyumbani.

Taarifa nyingine zimeeleza, Williams alikuwa akisotea malipo yake kutoka kwa promota aliyeandaa pambano ambaye pia alikuwa akilia ‘kupigwa’ kutokana na rundo la tiketi feki.
 
chanzo saleheblog

MGONJWA HUYU ANAOMBA MSAADA WAKO MTANZANIA ANAITWA ZUBERI M. ZUBERI

Assalaam Alaykum.

Kufuatia kichwa cha habari kilichopo hapo juu, nachukua fursa hii kutoa Historia fupi ya Kijana huyu anako toka na jinsi ugonjwa alionao ulivyo gundulika mpaka hivi sasa.

Zuberi Mgeni Zuberi alizaliwa Mwaka 1995 katika Kijiji cha Kwale Kata ya Kwale Wilaya [mpya] ya Mkinga Mkoa wa  Tanga. Alifanikiwa kumaliza Shule ya Msingi kwenye Kata yake hiyo na akabahatika kuchagulia Mwaka 2010 kuendelea na Masomo ya Sekondari ambayo ipo kwenye kata hiyo. Lakini hakuweza kuendelea na Masomo hayo kwa ajili ya Ugonjwa huo. Mwandishi wa habari hii ni Ndugu wa karibu wa Mama yake Zuberi.Bado wanaishi pamoja na Baba mzazi wa Zuberi hadi leo na jina lake ndilo hilo Mgeni.

Shughuli wanazofanya ni uvuvi na ukulima mdogo. Kipato chao ni cha hali ya chini kiasi wali shindwa kumfanyia uchunguzi Kijana wao ili wafahamu ni kipi kinacho msumbua Mtoto huyo ambaye mara kwa mara alikuwa akisumbuliwa na Tumbo hivyo kufikiria kuwa ndiyo Maradhi yanayo msibu, kwa hiyo walikuwa wa
kimpatia Dawa za Tumbo ambazo hazikua zikitoa nafuu ya moja kwa moja na ilibidi awachishwe kundelea  na Masomo ya Sekondari ndipo hapo Mwandishi wa Habari hii ambaye wakti huo alikuwa akiishi Kisiwani Pemba kwa shughuli za Ujenzi wa Barabara alipo fahamishwa na akatoa msaada wa ushauri na fedha ili Kijana apelekwe kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bombo Mjini Tanga kwa Uchunguzi na tiba husika mwaka 2011, mwezi Juni.

Hapo ndipo alipo gundulika kuwa anasumbuliwa na Ugonjwa ndani ya Moyo wake hivyo Hospitali hiyo ikampa Rufaa ya Kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amekuwa na Kliniki hadi leo. Cha kusikitisha ni kuwa Madaktari wa Hospitali hiyo wameshindwa kumpa Rufaa ya kwenda Nchi za nnje kwa Matibabu kamili baada ya wao kutokuwa na vifaa au ujuzi wa tiba hiyo, hivyo ilibidi kutafutwa njia nyengine kwenye Hospitali Binafsi ikiwemo Regency ambao baada ya utafiti wao wakasema anahitajika kwenda India kwa Matibabu na Gharama kwa kipindi hicho zilihitajika wastani wa Dola 6,000 za Kimarekani sawa na Shs. 9,600,000/= za Tanzania. Zikipatikana anaweza kusafirishwa na msaidizi wake mmoja.

Maelezo Mengine kwa kina yana weza kupatikana kwa kuwasiliana na Mwandishi wa Habari hii [Mjomba] moja kwa moja kwa kutumia nambari zifuatazo:- 0777 980492 au 0714 980492. Jina lake ni Bwana Yunus Ally Chui  na mshirika wake wa karibu ni Bwana Feisal Y. Chui Nambari yake ni 0773 449662.

Msaada wa kifedha unaweza kutumwa kwenye akaunti zifuatazo: 5753735527 kwa Fedha za Kitanzania na 5753735502 kwa fedha za kigeni Bank ya Exim tawi la Tanga kwa Jina la Yunus Ally Chui.

Ina ambatanishwa kwenye Barua hii Picha ya Zuberi ili kuthibitisha namna gani Ugonjwa huu ulivyo mbadili Umbile lake.

SHUKRAN

Yunus Chui. 

 

Tuesday, 3 September 2013

HABARI ZA HIVI PUNDE UHAMISHO WA FABIO COENTRAO KWENDA MAN U WASHINDIKANA

BAADA YA MADRID KUKATAA KUMTOA KWA MKOPO DAKIKA YA MWISHO

Manchester United imeshindwa kumnasa beki wa kushoto wa Real Madrid Fabio Coentrao, imethibitishwa.
 

Manager David Moyes alijaribu kumpata beki huyo mwenye miaka 25 baada ya kushindwa kumnyakua beki wa kushoto wa Everton Leighton Baines.
Mpaka leo asubuhi klabu hiyo ya jijini Manchester ilishindwa kuthibitisha kwamba wameweza kufanikisha dili la usajili wa Coentrao.

Lakini jioni hii imethibitishwa kwamba usajili huo haukukamilika.


Kwa maana hiyo ni  Marouane Fellaini pekee kutoka Everton kwa ada ya uhamisho wa £27.5m, ambaye ameongezwa kwenye kikosi cha cha Moyes katika dirisha hili la usajili lilofungwa jana.


Inaaminika kila kitu kilifanyika kabla ya muda wa dirisha la usajili kufungwa - hivyo kukawa kuna saa moja ya ziada kwa klabu hizo mbili kukamilisha taratibu nyingine vizuri.


Lakini Madrid wakasitisha dili hilo wakati jaribio lao la kumsajili beki wa kushoto Guilherme Siqueira kutoka Granada, kushindikana baada ya mchezaji huyo kuamua kujiunga na Benfica.

KATIBU MKUU WA YANGA LAWRENCE MWALUSAKO AACHIA NGAZI YANGA,



Katibu Mkuu Yanga, Lawrence Mwalusako ameamua kuachia ngazi baada ya kukaimu kwa mwaka mmoja.

Mwalusako amesema amefanya hivyo kwa kuwa makubaliano yao yalilikuwa ni kukaimu nafasi hiyo kwa mwaka mmoja.

“Haya ndiyo yalikuwa makubaliano yetu na sasa muda mwafaka umefika wa kufanya hivyo,” alisema hivi punde.


Lakini uchunguzi wa Blog hii umeonyesha kuwa Yanga imeleta Mkenya kuchukua nafasi yake hiyo na tayari ameanza kazi.
Mkenya huyo anajulikana kwa jina Patrick Naggi kuchukua nafasi hyo.
Taarifa hizo zinaaleza Naggi amewahi kuwa Technical Director wa Shirikisho la Soka la Kenya (KFF) na CEO wa Tusker ya  Kenya.
 
Chanzo salehejembe blog

WAFANYAKAZI WA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI WAFUNGIWA NJELICHA YA MKUU WA MKOA WA DSM KUWATAKA KURUDI KAZINI LEO

 

WAFANYAKAZI HAO WAKIWA NJE YA OFISI HIZO WASIJUE LA KUFANYA BAADA YA UONGOZI KUWAFUNGIA




MIJADALA YA HAPA NA PALE IKIENDELEA YA NINI KIFANYIKE



NYUSO ZILIZOPOTEZA MATUMAINI (picha na ujiji raha)
Mgomo wa wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam ya Strabag,umeingia katika sura nyingine leo baada ya  uongozi wa kampuni hiyo kuwafungia wafanyakazi nje na kuwazuia kuendelea na kazi licha ya tamko la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick kuwataka kuendelea na kazi.

chanzo mwaipayablog