Saturday, 8 February 2014

WAZIRI FENELLA AFUNGUA MASHINDANO YA DAR COMMUNITY CUP

 
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Idd Azzan (kushoto) akimpa matibabu mchezaji wa  Shule ya Sekondari Kawe Thomas Ibrahim aliyeumia wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya Dar es Salaam Community Cup leoo katika viwanja vya shule ya msingi Turiani. PIX1 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Henry Lihaya akimkaribisha  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara(wa pili kushoto waliokaa0 wakati wa uzinduzi wa ligi ya Dar es Salaam Community Cup leo katika viwanja vya shule ya msingi Turiana Magomeni jijini Dar es Salaam. Ligi hiyo inashirikisha timu 12 kutoka shule za Sekondari za jiji la Dar es Salaam. PIX2. 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na washiriki wa mashindano ya Mpira wa miguu yajulikanayo kwa jina la Dr es Salaam Community Cup leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua rasmi mashindano hayo, kushoto ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. PIX4 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akipiga penati kuashiria uzinduzi rasmi wa mashindano ya Mpira wa miguu yajulikanayo kwa jina la Dr es Salaam Community Cup leo jijini Dar es Salaam , aliyeko gorini ni  ni Meneja wa Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
PIX6 
Mchezaji wa Shule ya Sekondari Turiani akidhibiti mpira wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano hayo.
Picha zote na Frank Shija – Wizara ya Habari

0 comments: