>>ADAI: “NGUMU KUJUA NANI 4 BORA, NGUMU ZAIDI KUJUA BINGWA NANI!”
>>UEFA YAMTEUA ‘BALOZI WA MAKOCHA!’
Sir Alex Ferguson anaamini Manchester United bado inayo nafasi ya kutetea Ubingwa wake Msimu huu.
Hivi sasa Man United wako Nafasi ya 7 Pointi 14 nyuma ya Vinara Arsenal na Mechi zimebaki 16.
Lakini, Ferguson, ambae alistaafu kama Meneja wa Man United mwezi Mei, amesisitiza Mabingwa hao bado wamo mbio za Ubingwa.
FERGUSON NA MATAJI YAKE MAN UNITED:
LIGI KUU ENGLAND: 1993, 1994, 1996, 1997, 1999, 2000, 2001, 2003, 2007, 2008, 2009, 2011, 2013.
FA CUP: 1990, 1994, 1996, 1999, 2004
LIGI CUP: 1992, 2006, 2009, 2010
UEFA CHAMPIONZ LIGI: 1999, 2008
UEFA KOMBE LA WASHINDI: 1991
FIFA CLUB WORLD CUP: 2008
UEFA SUPER CUP: 1992
INTER-CONTINENTAL CUP: 1999
FA CHARITY/COMMUNITY SHIELD: 1990, 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011
Akiongea na Wanahabari, Ferguson, mwenye Miaka 72, alisema: “Simtoi yeyote kwenye Ubingwa.”
Pia, Ferguson alisisitiza Man United,
ambayo sasa iko chini ya David Moyes, Siku zote huwa na nguvu na kasi
zaidi kwenye Mzunguko wa Pili wa Ligi.
Pia Ferguson amezisifia Timu 6 za juu
kwenye Ligi ambazo ni Arsenal, Manchester City, Chelsea, Spurs, Everton
na Liverpool na Man United wako nyuma yao wakiwakimbiza.
Msimu huu, chini ya Moyes, Man United
imekuwa ikisuasua na imeshatolewa kwenye FA CUP na CAPITAL ONE CUP
ingawa bado wamo kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI wakiwa Raundi ya Mtoano ya
Timu 16 ambapo Februari wataivaa Olympiacos ya Greece.
Pia, Man United walikutana na kipigo cha
Mechi 3 mfululizo kwa mara ya kwanza tangu 2001 katika Siku 7 za mwanzo
wa Januari walipofungwa na Spurs, kwenye Ligi, Swansea, FA CUP, na
Sunderland, CAPITAL ONE CUP.
Hivi sasa Man United wapo Pointi 6 nyuma
ya Timu ya 4 Liverpool na wapo hatarini kuikosa UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa
mara ya kwanza tangu 1992.
Akifafanua msimamo wake, Ferguson
alisema: “Naona ni ngumu kuchagua zipi zitakuwa 4 Bora. Ni ngumu zaidi
kusema nani atakuwa Bingwa wa Ligi!”
Jana Ferguson aliteuliwa kuwa Balozi wa UEFA wa MAKOCHA.
Pia Ferguson ameonyesha kukerwa kwake na
Klabu zinazobadilisha Mameneja mara kwa mara na kusema haelewi ni
kwanini wanafanya hilo kitu ambacho huathiri Klabu zenyewe.
Ferguson amesisitiza Man United haiwezi kupitia njia hiyo na kusema: “Inaonyesha ni upumbavu kwangu!”
Wakati Ferguson anachukua hatamu Old
Trafford, alishwahi kutwaa Mataji 10 akiwa na Aberdeen ya Scotland
lakini ilimchukua Misimu 6 mpaka alipotwaa Ubingwa wake wa Kwanza wa
Ligi.
Kabla ya hapo, Man United chini ya
Ferguson, ilimaliza kwenye Ligi Nafasi za 11, Nafasi ya Pili, 11, 13, 6
na 2 kabla Ferguson kutwaa Ubingwa.
Baada hapo Mataji 12 ya Ubingwa yalifuata na kumalizika kwa Taji lake la mwisho alipostaafu Msimu uliopita.
Lakini Ferguson, ambae sasa ni
Mkurugenzi Man United, amekiri hajapata kuona Ligi kama Msimu huu na
amesema: “Mwaka huu, kwa mara ya kwanza, inaonyesha Timu 5 au 6 zipo
kwenye Mbio za Ubingwa, na hii inafanya Ligi Kuu iwe bora. Hii si Ligi
rahisi kushinda. Nadhani Gemu ya England ni ya kweli zaidi na ngumu
zaidi kushinda! Unaweza kufungwa na Timu yeyote!”












0 comments:
Post a Comment