Tuesday, 14 January 2014

Kagame: Tutamshughulikia yeyote anayeisaliti Rwanda

Rais Paul Kagame wa Rwanda ameonya kwamba yeyote atakayewasaliti Wanyarwanda na Serikali yake anastahili kuchukuliwa hatua kali na kwamba amejitolea maisha yake kuijenga na kuhakikisha Rwanda inakuwa salama dhidi ya wote wasio na mapenzi mema.Akizungumza katika ibada maalumu ya kuliombea taifa juzi, Kagame aliwataka Wanyarwanda wote kuungana katika kusimamia misingi sahihi na msimamo wao kama taifa, bila kujali tetesi zinazotoka katika mataifa ya nje kuhusu wale waliotangaza kuisaliti Serikali yake.
Japokuwa hakutaja moja kwa moja kuhusu tuhuma zinazoikabili Serikali yake kuhusiana na mauaji ya aliyewahi kuwa Mkuu wake wa Ujasusi aliyeuawa Januari mosi akiwa hotelini huko Afrika Kusini, Patrick Karegeya, alisema wale wote wanaoigeuka nchi yao na kuchagua kuua raia wasio na hatia kwa sababu zao binafsi wanastahili kushughulikiwa ipasavyo.
"Sitakuwa na huruma na watu ambao wanasahau namna Rwanda ilivyowatengeneza na kuwa hapo walipo na hatimaye wanaamua kuisaliti kwa kuua raia wa Rwanda wasio na hatia, wakiwemo kinamama na watoto," aliongeza.
Alisema Rwanda haina sababu ya kuhusishwa au kuwajibishwa kwa ajili ya wale walioamua kuchukua njia zaidi na kufanya mambo yao kwa nia ya kuharibu yale yaliyofanyika kwa ajili ya kuliimarisha taifa la Rwanda. 
Soma zaidi...

0 comments: