Tuesday, 21 January 2014

CHUKI ZAANZA NDANI YA CCM,SHINYANGA,MUNDULI,MGEJA,LOWASA

 chukiclip1 a1fd5
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, Hamisi Mgeja ameonya baadhi ya viongozi wa chama hicho kuwajengea chuki wanachama kadhaa na viongozi kwa madai wako karibu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa. (HM)
Hatua ya Mgeja imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku 'Msukuma' kumkana na kumshutumu, Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai kuwa anawalazimisha kuwa nyuma ya Lowassa wakati sivyo ilivyo.
Hata hivyo, Msindai alikanusha madai hayo kuwa hakuwahi kuwazungumzia wenyeviti wa CCM wa mikoa kuwa nyuma ya Lowassa zaidi ya kusema kuwa wanamuunga mkono katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza Mgeja alimtetea Msindai kuhusu suala la wenyeviti wa CCM kuwa nyuma ya Lowassa katika urais. Alisema: "Nataka kutoa angalizo kwa viongozi ndani ya chama, Tanzania kwa ujumla, kumejitokeza tabia ya baadhi ya watu kuchukiana eti tu kwa sababu wako nyuma ya Lowassa," alisema na kuongeza:
Mgeja alisema, kazi kubwa inayotakiwa kufanyika kwa wabunge, mawaziri na viongozi wa kada mbalimbali ni kukaa chini na kuwatumikia wananchi kwa kuhakikisha wanapata maji safi, dawa hospitalini na elimu kuliko kutumia muda mwingi kuangalia nani anampenda Lowassa.
Mgeja aliwataka wanaCCM kutulia na kutafakari mambo ya maendeleo kwa kuwa hakuna mtu aliyejitangaza urais akiwamo Lowassa zaidi ya kuanzisha safari ya matumaini ambayo ndani yake kuna mafanikio katika elimu, huduma za afya, ajira kwa vijana na mambo mengi," alisema.
Msindai alisema wanamwangalia Lowassa kutokana na uwezo wake katika kusimamia mipango yake ya maendeleo na zaidi katika kupigania elimu pana kwa Watanzania. 
Chanzo: Mwananchi

0 comments: