ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 25
[Saa za Bongo]
[Cape Town Stadium]
1800 Morocco v Nigeria
2130 Mali v Zimbabwe
MASHINDANO
ya CHAN 2014, ambayo ni michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji
wanaocheza ndani ya Nchi zao, yanayochezwa huko Afrika Kusini, leo
yanaanza hatua za Robo Fainali kwa kuchezwa Mechi mbili.
Hii leo, Mechi zote zitachezwa Uwanja wa
Cape Town Stadium Jijini Cape Town kwa Morocco kucheza na Nigeria na
kufuatia Mali na Zimbabwe.
Morocco ndio walimaliza Kundi B wakiwa
kileleni kwa kushinda Mechi 1 na Sare 2 wakati Nigeria walimaliza Kundi A
wakiwa Nafasi ya Pili, nyuma ya Vinara Mali, kwa kushinda Mechi 2 na
kufungwa Mechi moja, kwenye Mechi yao ya kwanza, walipopigwa 2-1 na
Mali.
Nao Mali, waliomaliza Vinara Kundi A,
walishinda Mechi mbili na Sare 1 huku wapinzani wao Zimbabwe walitoka
Kundi B wakiwa Nafasi ya Pili kwa kushinda Mechi 1 na Sare 2.
Kesho Jumapili pia zipo Mechi mbili za Robo Fainali.
ROBO FAINALI
[SAA za Bongo]
Jumapili Januari 26
1800 Gabon v Libya [Peter Mokaba Stadium]
2130 Ghana v Congo DR [Free State Stadium]
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 29
1800 Mali/Zimbabwe v Gabon/Libya [Free State Stadium]
2130 Ghana/Congo DR v Morocco/Nigeria [Free State Stadium]
Jumamosi Februari 1
1800 Mshindi wa Tatu [Cape Town Stadium]
2100 Fainali [Cape Town Stadium]












0 comments:
Post a Comment