
Ndugu zangu,
Kama wengi wenu, nami nimepokea kwa masikitiko usiku huu, taarifa za kifo cha ghafla cha Ndugu George Liundi ambaye alikuwa Msajili wa kwanza kwa vyama vya siasa hapa nchini.
Kama wengi wenu, nami nimepokea kwa masikitiko usiku huu, taarifa za kifo cha ghafla cha Ndugu George Liundi ambaye alikuwa Msajili wa kwanza kwa vyama vya siasa hapa nchini.
Kwa mujibu wa maelezo ya mwana wa marehemu, Taji Liundi, Ndugu Liundi amefariki leo mchana.
Mwezi Agosti mwaka jana, mara tu
baadada ya Jaji Mutungi kuteuliwa kushika nafasi ya Ndugu John Tendwa
kama msajili wa vyama, niliandika makala juu ya tukio hilo. Hii hapa
chini ni sehemu ya makala hiyo iliyomhusu Ndugu George Liundi pia...
"Miaka 20 iliyopita nilipata bahati ya
kukutana na Msajili wa kwanza wa Vyama Vya Siasa. Ni Bw. George Liundi.
Ni mwaka 1993, ilikuwa ni katika mwaka wake wa kwanza kama Msajili.
Nakumbuka vema, nikiwa kijana mdogo tu, George Liundi alinipokea kwenye
ofisi zake pale Mtaa wa Shaaban Robert. Tulikunywa chai na kuongea kwa
kirefu.
Sijui George Liundi yuko wapi siku
hizi, hakika ningependa nikutane nae nimkumbushe juu ya mazungumzo yetu
yale. Maana, baadhi ya changamoto za mfumo wa vyama vingi tulizoziongea
na Bw. Liundi miaka 20 iliyopita ndio zinazoonekana sasa.
Nakumbuka Liundi alikuwa mtu muwazi
sana. Alionyesha hata wakati huo, wasiwasi wake juu ya vyama
kufichaficha mambo yao ya ndani na kuwa vingine vilikuwa ni kama NGO ya
mtu au kikundi cha watu. Kwamba kulikuwa na tatizo la uwepo wa
demokrasia ya ndani ya vyama- Intra party democracy.
Hata wakati ule, niliona kupitia
mazungumzo yangu na Liundi, kuwa dhana ya kuwa Msajili wa Vyama
ilionekana kwenye macho ya Chama Dola na jamii kwa ujumla kuwa ni kuwa
mlezi wa vyama vinavyoanzishwa. Kwamba CCM ni chama kikongwe na
hakikuhitaji ' kulelewa' na Msajili.
Kwa wakati huo vyama vilivyosajiliwa
havikuonekana kuwa na impact sana na hata kuwa tishio kwa CCM. Vingi
vilikuwa kwenye ugomvi wa ndani kitu ambacho CCM kwa wakati huo haikuwa
kabisa na tatizo hilo.
Nilichokipata kwenye mazungumzo yangu
na Liundi miaka 20 iliyopita ni ukweli, kuwa hakukufanyika review ya
kina juu ya katiba za vyama kabla ya kusajiliwa. Ndio maana, masuala
kama haya ya vyama kuwa na vikosi au vikundi vyake vya ulinzi yalipaswa
kupigwa marufuku na Msajili tangu wakati huo bila kujali kama CCM wana
Green Guards." ( Raia Mwema)
Mungu Amlaze Mahali Pema Peponi Ndugu George Liundi.
Maggid Mjengwa, Dar es Salaam.
Imenukuliwa kutoka mjengwa blog












0 comments:
Post a Comment