Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kushoto) akimkaribisha mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa pili kulia) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (mwenye koti la drafti) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Kulia niRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (wa tatu kulia) akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (wa tatu kushoto) mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam. Wa pili kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakipanda jukwaani kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang wakiwa katika jukwaa kwa ajili ya kuimbiwa nyimbo za Taifa kabla ya kukagua gwaride 9 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (mwenye tai nyekundu) akikagua gwaride la heshima katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016.
Mke wa Rais wa Vietnam, Bi. Mai Thi Hanh akipokea zawadi ya ua toka kwa mtoto mara alipowasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 akiwa amefuatana na mmewe kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbali kati ya Tanzania na Vietnam.
Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan Sang (kushoto) pamoja na mkewe mama Mai Thi Hanh wakiwasili viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam 9 Machi, 2016 kwa ajili ya mazungumzo ya kuendeleza mahusiano katika nyanja mbalimbalikati ya Tanzania na Vietnam.
0 comments:
Post a Comment