Mwandishi Mmarekani Steven Sotloff aliyeuawa kwa kunyongwa na wapiganaji wa kiisilamu
Rais wa Marekani Barack Obama amesema kuwa Marekani haitatishwa na 
mauaji wa mwandishi mwingine wa habari Mmarekani na kundi la Islamic 
state.
Akiongea na waandishi wa habari nchini Astonia Rais obama amesema kuwa 
mauaji hayo yanaichochea Marekani kukabiliana ziani na magaidi
Video hiyo iliyotolewa na kundi la wanamgambo wa Islamic State inamuonyesha mwanamme aliyejifunika uso wake na kisu mkononi akisimama juu ya Sotlof.Mapema Marekani ilisema kuwa kanda ya video inayoonyesha kuchinjwa kwa mwandishi huyo Steven Sotloff ni ya ukweli
Nchini uingereza waziri mkuu David Cameron ameongoza mkutano wa kamati 
ya dharura ya serikali kujalidili jinsi itakavyojibu tishio la kutaka 
kumuua mateka raia wa uingereza.
Kwenye video hiyo mwanamgambo aliyejifunika uso na anayezungumza 
kiingereza anayaonya mataifa ya kigeni na kuyataka kusitisha harakati 
zao dhidi ya kundi la Islamic State.
Sotlof ni mwandishi wa pili wa Mmarekani kuuawa kwa kukatwa kichwa ndani
 ya mwezi mmoja baada ya mwandishi mwingine James Foly kuuawa kwa 
kukatwa kichwa mwezi uliopota na wanamgambo wa ISIS.












0 comments:
Post a Comment