MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Tuesday, 22 March 2016

Utata Mwingine Wagubika Waliokufa Kwa Kunyongwa Gesti wilaya ni kyela mkoani mbeya

 


Hatimaye kitendawili cha watu watatu walionyongwa kisha kuchomwa moto kwenye Gesti ya Mexico mjini Kyela, kimetenguliwa baada ya ndugu kujitokeza na kuwataja kwa majina halisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema baada ya vyombo vya habari kuandika tukio hilo, ndugu na jamaa wa marehemu walijitokeza na kugundua majina waliyoandika na maeneo wanayotoka ni uongo.

Msangi alisema ndugu wa marehemu baada ya kusoma na kusikia kwenye vyombo vya habari, walianza kuwapigia simu jamaa zao na mmoja wao aligundua kwamba ndugu yake anayeitwa Rogers Mwaka (49), ambaye ni Wakala wa Kampuni ya Vodacom hapatikani na hakuonekana nyumbani.

“Kwa mtandao huo pia tuliweza kufanikiwa kuwapata ndugu wa marehemu wengine, ambao wamewatambua kwa alama na majina yao halisia,” alisema.

Alisema mwanamke aliyeuawa kwenye tukio hilo na kutambuliwa kwa jina la Mariam Hassan, kwa sasa ametajwa kwa majina halisi kwamba ni Zauda Hussein Omary mzaliwa wa Mbarali na mkazi wa Veta jijini hapa wala hatoki Songea.

Msangi alisema marehemu mwingine ametambuliwa kwa jina la Baraka Chaula (27), ambaye ni mdogo wa Zauda kutokana na kuchangia mama, lakini baba tofauti na mkazi wa Mbarali alikuwa akifanya kazi za kilimo na biashara.

Akizungumza kwa uchungu ndugu wa marehemu Zauda na Baraka, aliyejitambulisha kwa jina la Riziki Chaula mkazi wa Mbarali, alisema alifika Kyela baada ya kugundua simu za mdogo wake hazipatikani.

Riziki alisema Zauda ni mke wa Abdallah Malifyuma, anayeishi Mbeya na kwamba alimuaga mumewe kwamba alikuwa akielekea Tukuyu wilayani Rungwe kibiashara.

Mkazi wa Ilomba jijini hapa, Sebastian Amani ambaye alifika Kyela alisema aliamua kupanda gari baada ya simu za Rogers kutopatikana licha ya kuaga kwamba anakwenda Chunya.

Amani alisema chanzo cha mauaji hayo hakijajulikana na kwamba yamewaweka kwenye wakati mgumu jinsi yalivyotokea.

Jana hiyo, Riziki alishirikana na mume wa Zauda, Malifyuma kuchukua miili ya marehemu hao wawili ilhali Aman ‘akibeba msalaba’ wa kusafirisha mwili wa Rogers.

MSANII LINAH SANGA AMZIMIKIA STAA WIZKID KIMAPENZI. KUTOKA NIGERIA

wiz45

Msanii wa bongo fleva nchini Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa alikuwa anatamani na bado anatamani sana kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii Wizkid kutoka nchini Nigeria.
Akipiga stori kwenye kipindi cha eNEWS kinachorushwa na ting’a namba moja kwa vijana (EATV) Linah Sanga alisema kuwa toka kipindi cha nyuma alikuwa anatamani kuwa na msanii huyo kama mpenzi wake, ingawa anadai mpaka sasa ndoto yake hiyo haijaweza kukamilika mpaka dakika hii.
“Unajua nilikuwa namu admire Wizkid toka muda mrefu, na ndiyo mwanaume ambaye hata ukiniuliza ni msanii gani wa kiume katika bara la Afrika ambaye ungependa kuwa naye au ambaye nampenda nitakwambia ni Wizkid, siwezi kukataa ila ndiyo hivyo tena maana mwenyewe natamani ingekuwa kweli” alisema Linah Sanga.
Katika hatua nyingine msanii huyo kwa sasa anasema ameamua kufanya tu kazi na kuachana na masuala ya mapenzi na kusema kuwa akichanganya kazi na mapenzi mwisho wa siku hata kazi yenyewe anaweza kuharibu.
Linah amedai mpaka sasa ana mipango ya kufanya kazi na Wizkid ingawa anadai kwa sasa alimwambia yupo ‘busy’ kidogo mpaka siku za usoni ndipo wanaweza kukamilisha kazi hiyo.
CHANZO Eatv.tv

Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi Toka Uganda Hadi Tanzania Uko Palepale soma ujue msimamo Dk Magufuli

 
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limesema mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda mpaka Bandari ya Tanga utafanyika kama marais wa nchi hizo mbili walivyokubaliana.

Wameeleza kuwa kwa sasa makubaliano yako katika hatua za mwisho ili ujenzi wa mradi huo kuanza huku nchi za Kenya na Uganda wakiendelea na mazungumzo katika kufikia mwafaka wa jambo hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dk James Mataragio alisema hivi karibuni kumekuwa na taarifa za mradi huo kukwama kutokana na Kenya kudaiwa kukubaliana na Uganda kupitisha mradi huo nchini mwao.

Akizungumzia suala hilo, Dk Mataragio alisema ni kweli awali kulikuwa na makubaliano ya nchi hizo mbili kupitisha mradi huo Kenya kutoka Hoima hadi Bandari ya Lamu, lakini kwa sababu mbalimbali Uganda waliamua kupitisha Bandari ya Tanga.

Alieleza ingawa umbali kutoka Uganda hadi bandari za Kenya ni karibu kwa kilometa chache kuliko Tanga zipo sababu zilizofanya bomba hilo kufikishwa Tanga. Sababu hizo ni pamoja na gharama kubwa za ujenzi kwenda Kenya na bandari ya Tanga kuwa na kingo za asili hivyo kuweza kusafirisha mafuta mwaka mzima.

Alisema pia ujenzi wa bomba hilo hadi bandari ya Tanga haupiti sehemu yenye makazi ya watu wengi hivyo kupunguza gharama, huku bomba likipita maeneo mengi ya tambarare bila kuwa na miinuko inayofanya kuongeza gharama za kupampu.

Alisema tayari timu za wataalamu zimekutana na kukubaliana masuala kadhaa ya ujenzi huo pamoja na kusaini mpango wa utekelezaji wa mradi. 

Dk Mataragio alisema kuhusu gharama ni kawaida siyo kubwa kama inavyoelezwa na baadhi ya watu hivyo ni vema watanzania wakaelewa kuwa hakuna tatizo la kukwama kwa mradi huo kwa sababu yoyote.

Kampuni zinazozalisha mafuta nchini Uganda ni Tullow kutoka Ireland, Kampuni ya Ufaransa ya Total na Kampuni ya CNOC kutoka China.

Wakati hayo yakielezwa hivi karibuni, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki, Javier Rielo alimueleza Rais John Magufuli kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi huo haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

Bomba hilo la kutoka Tanga hadi Uganda litakuwa na urefu wa kilometa 1,410 na litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga na litajengwa kwa gharama ya Dola za Marekani bilioni nne.

Unatarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000 huku ukitarajia kukamilika baada ya miaka mitatu hadi minne.

Kauli ya (CCM) kumpongeza Dk Ali Mohammed Shein Kwa Ushindi wa Kishindo Alioupata



Baada ya Dk Ali Mohammed Shein kutangazwa mshindi kwa zaidi ya asilimia 90, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hatma ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa itaamuliwa na Rais kwa kufuata matakwa ya Katiba ya Zanzibar.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM, Waride Bajari Jabu alisema Dk Shein ataongozwa na Katiba ya Zanzibar pamoja na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika mkutano huo ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya kumpongeza Dk Shein kuchaguliwa tena kwa mara ya pili na wananchi wa Zanzibar, Jabu alisema maelekezo yote ya kuundwa kwa SUK yamefafanuliwa kikatiba.

Alisema CCM inaamini kuwa katiba ndiyo msingi wa uendeshaji wa nchi, hivyo jambo ilo wanaliachia liamuliwe kwa kufuata matakwa husika ya Katiba ya Zanzibar.

“Rais ataunda serikali yake kikatiba, imefafanua kila kitu,” alisema Jabu wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari. 

Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 inataka Serikali inayoundwa iwe ya umoja wa kitaifa kwa kuwa na Rais, Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye anatoka chama kikubwa cha upinzani na Makamu wa Pili wa Rais anayeteuliwa kutoka katika miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Hata hivyo, katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, CCM imeshinda majimbo yote ya uchaguzi kutokana na hatua ya Chama cha Wananchi (CUF) kutangaza kutoshiriki katika uchaguzi huo wa marudio.

Dk Shein alitangazwa kuwa mshindi kwa kupata asilimia 91.4 na mgombea aliyemfuatia ni wa ADC, Hamad Rashid Mohamed aliyeambulia asilimia tatu ya kura zilizopigwa.

Kutokana na kutokuwepo mgombea urais aliyepata zaidi ya asilimia 10 ya kura za urais na kutokuwepo kwa chama kilichoingiza wajumbe wengi Baraza la Wawakilishi, CCM imejikuta inabaki pekee yenye sifa zote kikatiba.

Jabu pia alituma salamu za pongeza kwa Dk Shein kwa kuchaguliwa tena kuwatumikia Wazanzibari kwa kipindi cha miaka mitano.

Akitoa salamu hizo, Jabu alisema ushindi wa Dk Shein umedhihirisha namna Wazanzibari wanavyoridhishwa na utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kumuamini kwao.
Kwa upande wao, Umoja wa Vijana (UVCCM) umesema ushindi alioupata Dk Shein ni kielelezo cha kuimarika kwa msingi ya demokrasia Zanzibar na kukubalika kwa mgombea huyo kwa wapiga kura na wananchi wa Zanzibar.

Kaimu Katibu Mkuu alisema aina ya uongozi wa Rais Dk Shein ni wa kipekee na kwamba kama angekuwa si mtawala mwenye maarifa mapana na uvumilivu wa kisiasa serikali hiyo anaamini ingevunjika mapema

Acheni Kumuonea Huruma Chidi Benz Anavuna Alichokipanda. -Faiza Ally


Katika ukurasa wake wa Instagram Faiza ameandika huku akiwapondea wale wanaomsikitikia, na kusema kuwa Chid amejichagulia mwenyewe kuwa hivyo kwani kabla hajaanza kutumia alikuwa anafahamu madhara yake.
“Kila mtu anamsikitikia Chidi kwa nini? Chidi sio mtoto ni maisha aliyo chagua, pengine unaweza kumsikitia mtoto aliye jifunza akiwa chini ya miaka 18 lakini sio mtu mzima! Kila siku mifano tunaiona jinsi gani madawa yana haribu watu inaama hawaoni ? Hawasikii ?"
Faiza ameendelea kuandika
 "Hapana kwa kweli mimi naona unavuna unachokipanda. Unapo sema ugumu wa maisha ndiyo umekupeleka kuvuta madawa au kuuza - hivi mnazani wote tunao cheka maisha yetu mepesi? Kwa kweli ni uzembe......! acheni kabisa kuwahurumia watu kijinga, lazima wajue wamekosea sio kuwa peti peti”.

Pamoja na hayo Faiza ameonekana kuchukizwa na kitendo cha biashara ya madawa ya kulevya inayoendelea nchini, na kutaka watumiaji na wauzaji pia wafungwe iwapo watathibitika, ili kudhibiti matumizi ya madawa ya kulevya.
“Hivi kwa nini wanao nunua madawa pia wasifungwe ??? Kwa sababu mtazamo wangu unaona mnunuzi na muuzaji wote ni wahalifu!

Kati ya hawa watu wawili wote wanafanya biashara maana kama hamna mnunuzi hakuna muuzaji, kama hakuna muuzaji hamna mnunuzi”, aliandika Faiza.

Pamoja na hayo Faiza amemtakia heri Chidi Benzi katika mapambano yake na kuachana na madawa ya kulevya, ili aweze kurudi kama zamani.

Waziri Lukuvu Awatia Kitanza shingoni shilika la nyumba (NHC)



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameiagiza bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa Nyumba (NHC) kuacha kuanzisha miradi mipya ya ujenzi hadi kukamilishwa kwa miradi iliyokwishaanza.

Akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo Dar es Salaam jana, Lukuvi alisema hakuna haja ya kuanzisha miradi mipya wakati iliyopo haijakamilika.

“Nadhani miradi iliyopo mnaijua na tarehe za kukamilika ujenzi wake wote tunafahamu, hivyo nitoe agizo kuanzia leo hakuna kuanza kwa mradi mpya wowote mpaka imalizwe iliyokwishaanza,” alisema.

Lukuvi pia aliiagiza bodi hiyo kutopandisha kodi za nyumba zake bila ridhaa yake huku akisisitiza gharama zipangwe kwa kuzingatia uwezo wa wananchi.

“Hamuwezi kusema nyumba ya gharama nafuu wakati ina vyumba viwili na inauzwa kwa Sh52 milioni, hainiingii akilini na wala Mtanzania wa kawaida hawezi kuona unafuu wowote hapo,” alisema Lukuvi.

Huyu ndiyo mkuu wa wilaya aliye Amuomba Rais Magufuli Ampumzishe Ukuu wa Wilaya



Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote.

Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti.

Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zinazodorora kutokana na kubanwa na majukumu ya ukuu wa wilaya.

“Pamoja na ukuu wa wilaya, mimi pia ni mbunge na wakati huohuo ni mfanyabiashara; haya ni majukumu mengi kutekelezwa na mtu mmoja kwa wakati moja,”alisema Mayenga 
Aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Nyamilangano, wilayani Ushetu kuwa biashara zake nyingi zilizopo mkoani Shinyanga zimedorora kutokana na kukosa usimamizi wake.

“Ombi hili nililitoa binafsi kwa Waziri Mkuu ambaye alinishauri kusubiri uteuzi; isitafsiriwe kwamba nimeogopa kasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano.Hapana! Nimeona ni vyema nibaki na ubunge na biashara zangu,” alisema Mayenga ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari.

Baadhi ya wanachama wa UWT waliohudhuria mkutano huo walimpongeza kwa uamuzi huo wakisema unapaswa kuigwa na viongozi wengine wenye majukumu mengi kwa kuachia watu wengine nafasi za kutumikia umma badala ya kung’ang’ania nafasi zote.

“Nampongeza Mheshimiwa Mayenga kwa uamuzi wake wa kuomba asiteuliwe tena kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya kwa sababu itatoa fursa kwa watu wengine kutumikia nafasi hiyo,”alisema Selina Mkula.

Katika mkutano huo ambao Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa alitoa msaada wa mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Nyamilangano na Mitonga pamoja na Shule ya Sekondari Kisuke, wanachama wapya 55 walijiunga na UWT.

Mbunge huyo pia aliahidi kutoa vyerehani 20 kwa makatibu kata wa UWT ili kusaidia harakati za maendeleo ya wananchi kwa kuanzisha vikundi vya kiuchumi katika kata zao.

Cech mchezaji bora wa mwaka

Image captionMchezaji bora nchini Czech Peter Cech
Golikipa wa kimataifa ya Jamuhuri ya Czech Petr Cech ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa nchi hiyo.
Cech Mwenye umri wa miaka 33,alichaguliwa na makocha, wachezaji na viongozi wa timu kutwaa tuzo ya nane ya uchezaji bora nchini mwake.
Golikipa huyu amewazidi wachezaji wenzake wa timu ya taifa Mshambuliaji wa Sparta Prague David Lafata, na kiungo wa Vladimir Darida anayeichezea Hertha Berlin.
kipa huyu wa klabu ya Soka ya Arsenal ameichezea timu ya taifa michezo 118 tangu alipoanza soka la kimataifa mwaka 2002.

Arsenal yawafunza soka watoto wanaokimbia vita Iraq

Image captionArsenal ikifunza watoto nchini Iraq
Watoto wanaotoroka vita nchini Iraq wanafunzwa soka na kilabu ya Arsenal ambayo inashirikiana na shirika la Save the Children kuwajengea viwanja katika kambi za watu wasio na makao.
Mpango huo kwa jina Victoria Derbyshire uliandamana na nahodha wa kikosi cha timu ya wanawake wa Arsenal Alex Scot ambaye alifanya mazoezi na watoto hao.
Arsenal wana matumaini kwamba mradi huo utawasaidia watoto walio katika hali mbaya kuona furaha inayosababishwa na soka.
Esra ambaye sio jina lake rasmi alitoroka karibu na mji mkuu wa Iraq,Baghdad wakati vita hivyo vilipotokea katika maeneo aliyokuwa akiishi.
Aliiwacha nyumba kubwa pamoja na bustani ambayo alikuwa akiangalia yeye na babaake na sasa anaishi katika kambi ya Alwand One huko Kurdistan,kaskazini mwa Iraq ambayo ni makao ya zaidi ya watu 6000.
Image captionWatoto wa Iraq wanaofunzwa soka na Arsenal
''Tumelazimika kuishi kwa kuwa mabomu na milipuko imekuwa ikitokea na tuliogopa kwamba huenda moja likalenga nyumba yetu''.
''Roketi zilikuwa zikirushwa kwa hivyo tukalazimika kuondoka kwa haraka.Niliwaaga rafiki zangu wawili'',wengine sikuwaona,alisema mtoto huyo wa miaka 12.
''Mara ya kwanza nilichanganyikiwa,sikujua vile ningeondoka nyumbani kwangu na kusafiri hadi hapa,lakini ni saa chache kutoka mahali vita vilikuwa vikiendelea''.
Katika eneo linalodhibitiwa na wapiganaji wa islamic State.Tangu Januari 2014,mapigano yamewaacha zaidi ya watu milioni tatu kuwacha makao yao nchini humo na nusu yake ni watoto.
Na alipoulizwa ni nini kizuri kuhusu kambi hiyo,Esra alijibu:Shule na uwanja huo wa Soka.
Image captionKambi ya wakimbizi nchini Iraq
Alex ambaye ameichezea timu ya soka ya Uingereza anasema kuwa ijapokuwa hawezi kufananisha hali yake na ilivyo sasa,soka ilimsaidia wakati alipokuwa akikuwa.
Viwanja hivyo vilivyo na nyasi za kijani vinatoa mandhari nzuri ya rangi katika eneo lililojaa vumbi na kuwapatia watoto hao eneo salama la kucheza.
Kufikia sasa watoto 2500 wamepata fursa ya kucheza katika viwanja hivyo.
Huku Alex akiwafunza na kucheza na wasichana, wavulana wanaonekana wakiangalia katika upande mwengine wenye uwa.
Image captionWatoto wanaofunzwa soka na Arsenal nchini Iraq
''Wavulana wanatamani kuingia'',alisema Esra huku akionyesha ujuzi wake anavyosakata soka.
Wakiwa na furaha wasichana wanaonekana wakionyesha ujuzi wao wa soka kabla ya kuvaa jezi za mechi.Mbali na Alex Arsenal ilituma kocha ambaye amefunza save the Children katika kambi hizo.
Mpango huo unawalenga wavulana na wasichana na kuwahamasisha watoto kuanzisha timu zonazovunja migawanyiko ya kihistoria.
"Mbali na kupata mda wa kucheza,nidhamu na muelekeo aambayo ni vitu muhimu ,kuna wazo muhimu haswa miongoni mwa watoto kwamba watu unaowapenda,pia wanakupenda zaidi'',alisema Mkurugenzi mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis.

Rubani wa Ukraine jela miaka 22 Urusi kwa kosa la .......?


Image copyrightAFP
Image captionRubani wa Ukraine jela miaka 22 Urusi

Rubani kutoka Ukraine anayetuhumiwa kwa mauaji ya wanahabari wawili kutoka Urusi amehukumiwa kifungo cha miaka 22 gerezani.
Nadiya Savchenko alipatikana na hatia ya kufyatua makombora yaliyowauwa wanahabari hao waliokuwa wakipeperusha habari kutoka eneo la vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga wanaoaminika kuungwa mkono na Urusi.
Kisa hicho kilitokea mwezi juni mwaka wa 2014.
Savchenko aliangua kicheko punde baada ya majaji hao kumaliza kusoma hukumu yao.
Alianza kuimba nyimbo za kitamaduni za kizalendo kama njia yake ya kupinga uamuzi huo.
Savchenko alikanusha madai dhidi yake.

Image copyright 
Image captionNadiya Savchenko alipatikana na hatia ya kufyatua makombora yaliyowauwa wanahabari 2 wa Urusi

Mara baada ya hukumu hiyo kutolewarais wa Ukraine Petro Poroshenko alipuzilia mbali uhalali wake na kusema kuwa yuko tayari kubadilisha rubani huyo shupavu na wanajeshi wawili wa Urusi waliokamatwa.
Aidha waziri wa maswala ya kigeni wa Ukraine aliahidi kuendelea na harakati za kutafuta uhuru wa rubani huyo.
Kulitokea makabiliano baada ya mashabiki wa rubani huyo kujaribu kupeperusha bendera ya Ukraine ndani ya mahakama.
Kiongozi wa mashtaka alisema kuwa bi Savchenko alikuwa na chuki sana dhidi ya Urusi na hiyo ndiyo iliyompelekea kuwashambulia waandishi habari hao,.ambao hawakuwa wamejihami.
Kesi hiyo iliendeshwa katika mji wa mpakani wa Donetsk.