MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday, 26 July 2014

TAARIFA YA: Jeshi la Polisi Tanzania tunapoelekea kipindi hiki cha sikukuu ya Eid-El-Fitr


index 
Jeshi la Polisi Tanzania linapenda kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wote, vyama vya siasa, taasisi mbalimbali za serikali, madhehebu ya dini, asasi za kiraia na vyombo vya habari kwa ushirikiano wa dhati katika kusimamia masuala ya amani na usalama hapa nchini.
Tunapoelekea kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini na kusheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu umeonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu.
Jeshi la Polisi linapenda kuwaondoa hofu wananchi wote kuwa, limejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi kote nchini wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote, aidha, tunapenda kuwatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara, kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.
Katika kuhakikisha usalama kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi. Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya starehe, hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, yakiwemo maduka, hoteli na maeneo ya benki. Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza wale ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji endapo uhalifu unatokea.
Vilevile, wazazi wawe makini na watoto wao na hasa disko toto, ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.
Aidha wananchi wachukue tahadhari watokapo kwenye makazi yao wasiache nyumba wazi ama bila mtu na watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya bali watoe taarifa haraka kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu nao au kwa namba ya simu ifuatayo 0754 785557, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.
Imetolewa na: Advera John Bulimba – SSP Msemaji wa Jeshi la Polisi.

Kanali Ngemela Lubinga awataka madiwani kusimamia miradi kwa ukaribu

???????????????????????????????
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga  akifungua kikao mkutano mkuu wa mwaka wa baraza la madiwani Halmshauri ya NSIMBO Mbele ya wajumbe wa kikao hicho pamoja na watalaam wa Halamshauri hiyo
……………………………………….
Na Kibada Kibada –Nsimbo Katavi.
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga amewataka madiwani kusimamia kwa ukaribu miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yao kwa kuwa wao wana dhamana kubwa katika jamii wanayoingoza kama wawakilishi wa wananchi kwenye Vikao vya maamuzi hivyo ni wajibu wao kutimiza wajibu huo. Kanali Lubinga aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Fedha uliokwisha wa 2013/2014.na kueleza kuwa uwakilishi ni dhamana kubwa katika jamii ambayo ni wananchi unaowawakilishi hivyo wanatakiwa kuwatendea haki kwa kutimiza wajibu wako waliokabidhiwa katika jamii ya uwakilishi ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa umakini utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoko kwenye Halmashauri katika eneo husika.
Alisema matatizo yaliyoko kwenye eneo la diwani unatakiwa kuyatambua na kuyapatia maamuzi mfano wizi unatokeo kwenye eneo lako kama wizi wa Soral Kijiji cha Ugala pale upo uongozi upo kuanzia ngazi ya Kijiji,Kata na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo katika Kata ni Diwani na wataalamu wake wapo pia na Diwani yupo katika eneo , kweli kama upo uwajibikaji na kutimiza wajibu wananchi wangeweza kutoa ushirikiano na mali kama hiyo isingeibiwa kwa kuwa wanaona ni mali ya jamii kwa manufaa ya jamii lazima watailinda kwa gharama yeyote ili ila kama hakuna uwajibikaji na ushirikiano basi wananchi hwawezi kutoa ushirikiano.. Akasema siwajibu wa viongozi kuktaa watu bali wanasimamiwa ukiwasimamia kwa ukaribu matatizo yaliyopo kwenye eneolako utayafahamu na kutafuta njia ya kuyapatia ufumbuzi kabla hayajawa makubwa .
Akizungumzia suala la ujenzi wa Maabara alieleza kuwa Halmashauri ya Nsimbo iko nyuma katika utekelezaji wa agizo la Rais na agizo la Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe lakuzitaka halmashauri zote kukamilisha ujenzi wa Maabara kwa shule za Sekondari ifika mwezi Novemba hali ya ujenzi inakwenda kwa kusuasua mno tofauti na maeneo mengine katika Mkoa.
Mkuu huyo wa wilaya ameitaka Halmashauri kuwatumia na kutumia fursa zilizopo katika Hlamshauri hiyo hasa makampuni ya uchimbaji madini nay ale ya nayojishughulisha na unuzi wa tumbuka kuhakikisha wanawashirikisha wasaidie katika ujenzi wa Maabara.
Akasisitiza kuwa Mkoa wa Katavi na Halmashauri ya Nsimbo wanaoutajiri wa kutosha watumieni hawa watu waweze kuwasidia katika kujenga maabara hizo hawa wanachuma mali kwenye halmashauri yetu haiwezekana na wao wasisaidie watalaam tumieni Talaam zenu kuwasiadia wananchi hao. Akasema hataki kusikia shule hazina madawati katika Wilaya yake na ameisha agiza mamlaka inayohusika kutoa kibali au leseni ya kuvuna kupasua mbao katika Wilaya yake mvuna huyo lazima achangie madawati 300 hiyo ni lazima kwa kuwa ni agizo lasivyo asipewe leseni hiyo ya kupasua mbao kama hataki kuchangia madawati hayo. Katika hatua nyingine amewaagiza watendaji wa Halmashauri hasa Idara ya utumishi kuondoa kero na manunguniko kwa watumishi wanaolalamikia kututendewa haki kwa kulipwa masilahi yao nap engine posho zao akasema iwapo malalamiko yatazidi watu watachukia na kuichukia serikali yao vita ya namna hiyo siyo lahisi kuishinda ni vyema watu wakasilikizwa na kupewa haki zaowanazodai kama madai yao mbalimbali katika Halmashauri.
Kwa upande wake Mweyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo Mohamed Assenga alieleza kuwa kuwa kwa kuwa wote ni viongozi watajitahidi kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ili kuhakikisha maendeleo katika Halmashauri yanakwenda kama inavyotakiwa kwa kuwaletea wananchi maendeleo kwa mstakabali wa Taifa. Katika kikao hicho ambacho kilikuwa ni Mkutano Mkuu wa mwisho wa Mwaka wa fedha unaoishia 2013/2014 Taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli nyingine ziliwasilishwa na kujadiliwa na kupatiwa majibu.

MH. EDWARD LOWASSA AWAANDALIWA FUTARI WAUMINI WA MONDULI

Mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowassa akizungunza na waumi wa dini ya kiislam (hawapo pichani), katika hafla aliyofuturisha katika Msikiti Mkuu wa Monduli mjini.
 Shekh wa Wilaya ya Monduli Shekh Mwinshehe Mwinyi akizungumza na waumini wakati wa futari iliyoandaliwa na Mh. Lowassa.
 Baadhi ya waumini wakipata futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa.
 Mke wa mbunge wa jimbo la monduli Regina Lowassa akizungumza katika ghafla ya futari  iliyoandaliwa na mbunge wa jimbo hilo Edward Lowassa iliyofanyika katika msikiti wa monduli.
 Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akiwa na Shekh wa Wilaya ya Monduli Shekh Mwinshehe Mwinyi wakati wa futari aliyoiandaa kwa ajili ya waumini wa dini ya kiisalamu wilaya Monduli.
 Shekh wa Wilaya ya Monduli Shekh Mwinshehe Mwinyi akizungumza na waumini wakati wa futari iliyoandaliwa na Mh. Lowassa.
 Waumini wakipata fuatari.
 Meza Kuu wakipata futari.
 Waumini wakipata futari iliyoandaliwa na mbunge wa jimbo laMonduli Mh. Lowassa.
 Mke wa mbunge wa jimbo la Monduli, Regina Lowassa akizungumza katika hafla ya futari  iliyoandaliwa na mbunge wa jimbo hilo Edward Lowassa iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Monduli.
 Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha, Namelock Sokoine akizungumza katika hafla ya futari iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Monduli.
 Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Arusha Namelock Sokoine akiwa na mke wa Lowassa katika hafla ya futari iliyofanyika katika Msikiti wa Monduli..

RAIS KIKWETE ATUNUKU WAHITIMU WA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI KATIKA MAHAFALI YA KOZI YA PILI

1
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kanali James Ruzibiza Stashahada ya Usalama na Stratejia (Diploma in Security and Strategic Studies) katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Kanali Ruzibiza, ambaye anatokea Rwanda, ni mmoja wa washiriki tisa wa kozi waliotoka nchi za nje. Washiriki wengine kutoka nje y nchi walitoka Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Uganda, zambia na Zimbabwe. Jumla ya wahitimu 30, wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. 
2
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku Luteni Jenerali C.L. Makakala Shahada ya Uzamili ya Falsafa ya Usalama na Stratejia katika mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014. Luteni jenerali Makakala, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi wa kwanza, amekuwa mtunukiwa wa kwanza wa Shahada hiyo hapo chuoni.
  4
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia baada ya kutunuku shahada katika  mahafali ya Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014.Jumla ya wahitimu 30 wamehudhuria kozi hiyo wakiwemo maafisa wandamizi katika utumishi wa umma, ambapo 11 wametoka JWTZ na 10 kutoka vyombo vingine vya usalama na idara mbalimbali. Washiriki wengine tisa wametoka  nchi za nje ambazo ni Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda Uganda, Zambia na Zimbabwe.
5
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwaambia kuwa sasa ni zamu yao kupiga picha ya kumbukumbu bila yeye wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014   8
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika  picha ya kumbukumbu na wahitimu wa Kozi ya Pili ya Chuo Cha Taifa cha Ulinzi (NDC) chuoni hapo Kunduchi jijini Dar es salaam leo Julai 26, 2014

RAIS KIKWETE, WAZIRI MKUU PINDA NA JAJI MKUU WAKARIBISHWA FUTARI KWA MAKAMU WA RAIS DKT BILALI


b1
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sawa  kanzu ya Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kabla ya kushiriki katika futari waliyoandaliwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Ijumaa jioni Julai 25, 2014
b2
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman wakiwasili kushiriki katika futari waliyoandaliwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Ijumaa jioni Julai 25, 2014

 

Marekani yamua kufunga ubalozi Libya wafanyakazi wake wote wamehamishiwa nchi jirani,


Athari za mapigano uwanja wa ndege wa Tripoli, LIbya
Marekani imefunga ubalozi wake wa Libya kwa muda na wafanyakazi wake wote wamehamishiwa nchi jirani, Tunisia.
Walipelekwa huko kwa magari huku wakilindwa na ndege za Marekani.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Marekani piya imewasihi raia wote wa Marekani waondoke nchini humo.
Jengo la ubalozi wa Marekani mjini Tripoli liko katika eneo ambalo limeathirika na mapambano kati ya makundi ya wapiganaji yanayozozana, ambayo yamekuwa yakigombania kudhibiti uwanja wa ndege wa kimataifa wa Libya.
Waziri wa mashauri ya nchi za nje, John Kerry, alisema kulikuwa na hatari hasa ikiwakabili wafanyakazi wa ubalozi huo, lakini alisisitiza kuwa shughuli za ubalozi zinasimamishwa kwa muda tu.
Miaka miwili iliyopita balozi wa Marekani aliuwawa pale ofisi ndogo ya ubalozi wa Marekani katika mji wa Benghazi, mashariki mwa Libya, iliposhambuliwa na wapiganaji Waislamu.

Tamasha la Saba la Muziki wa Cigogo 2014 Larindima Chamwino Ikulu, Dodoma

???????????????????????????????
Tamasha la saba la Muziki wa Cigogo 2014, lililoanza jana  Julai 25, kwenye kijiji cha Chamwino Ikulu, Mkoani hapa linarindima kwa kishindo na kufanya nji wote kuwa na shamrashara za aina yake.
 
Tamasha hilo ambapo jana lilizinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi,  linashirikisha vikundi zaidi ya 30 vikiwasha moto wa ngoma na muziki wa kitamaduni.
 
Kwa mwaka huu tamasha hilo ni la msimu wa  Saba (7) likifahamika kama (Wagogo music festival 2014)  lenye kauli mbiu  ‘Utamaduni na Amani’  linarindima kwa siku tatu na hiyo kesho Julai 27 linatarajia kufikia tamati.
 
Mkurugenzi mkuu wa tamasha hilo, Dk. Kedmon Mapana,  wa Kituo cha Sanaa Chamwino (Chamwino Arts Center-CAC) wandaaji wa tamasha hilo alisema wanatarajia Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, ndiye atakayelifunga rasmi tamasha hilo hiyo kesho.
 
“Kesho Julai 27, ndiyo tunafikia tamati na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino anatarajia kuwa mgeni rasmi.” alisema Dk. Kedmon.
 
Tamasha hilo tokea kuanza kwake limekuwa katika mwangaza mpana wa kukuza na kuinua utamaduni wa Cigogo, ambapo kwa mwaka huu limeweza kukusanya wasanii zaidi ya 700 na wageni mbalimbali katika mji huo wa Chamwino Ikulu.
Aidha, alivitaja vikundi vinavyoshiriki tamasha hilo ni pamoja na kutoka Dodoma kuwa ni New Pendo, Yelusalem, Inueni mioyo, Yeriko, Nyota njema, Ushirikiano, Nyerere na Ebenezer.
 
Vikundi  vilivyo vijiji vya Wilaya ya Chamwino ni  Upendo (Kijiji cha Dabalo),  Imani, Sinai  (Kijiji cha Membe).  Mchungaji mwema, (Kijiji cha Nzali), Juhudi, Muhubiri (Kijiji cha Kawawa), Nyota njema, Safina, Ndagwa (Kijiji cha Msanga).
Msifuni (Kijiji cha Mlimwa), Nyota, Ufunuo (Kijiji cha Majeleko), Simba (Kijiji cha Mbele zungu) na Inueni mioyo (Kijiji cha Mgunga).
 
Vikundi kutoka Wilaya ya Kongwa imani ( Kijiji cha Mkutani), Faru (Kijiji cha Songambele) na  Safina (Kijiji cha Chigwingili), Pia  kikundi cha Uvuke na Upendo  (kutoka  Manispaa ya  Dodoma mjini).
 
Vikundi vingine ni Mandoo/Tasuba kutoka Bagamoyo  Mkoa wa Pwani, Nazareti (Dar es s Salaam), Muungano (Manyoni, Singida) na  Zanzibar.

Waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) wanataka taifa hilo ligawanywe kati ya Waislamu na Wakristo.


 
kundi la wapiganaji nchini CAR
Waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR wamekataa makubaliano ya kusitsisha vita na kutaka taifa hilo ligawanywe kati ya Waislamu na Wakristo.
Afisa mkuu wa waasi wa kundi la kiislamu la Seleka ameiambia BBC kwamba wapiganaji wake watapuuza makubaliano hayo yalioafikiwa siku ya jumatano kwa kuwa yalifanywa bila wao kuhusishwa.
Joseph Zoundeiko amewalaumu Wakristo wa Kusini mwa taifa hilo kwa kushindwa kuleta amani na kusema kuwa taifa hilo ni sharti ligawanywe mara mbili.
Mapigano ya miezi kadhaa kati ya makundi ya Wakristo na yale ya Waislamu katika taifa hilo yamesababisha mauaji ya maelfu ya watu huku mamilioni wakiwachwa bila makao.
Kundi la waasi wa Seleka lilivunjwa rasmi mwaka uliopita.
lakini kundi la Human Rights Watch linasema kuwa wapiganaji hao wameelekea katika maeneo ya mashambani na kwamba wameanza kuzishambulia jamii za Wakristo.
Wakristo na wamelipiza kisasi na hivyobasi kusababisha maafa zaidi kutoa pande zote mbili.

BAHATI BUKUKU APATA AJALI maeneo ya Kongwa Dodoma usiku wa kuamkia leo.



Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku.
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Bahati Bukuku amepata ajali ya gari akiwa na dereva wake, Eddy maeneo ya Kongwa Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Akiongea kwa simu Bahati amesema: “Ni Mungu tu aliyetuokoa, tulikuwa tunaelekea Kahama kwenye huduma ghafla tukagongana uso kwa uso na lori, gari yetu aina ya Toyota Nadia  iliruka na kubiringika kama mara tatu hivi, tumetoka tukiwa tumeumia sana.(P.T)
“Hapa siwezi kusimama wala kukaa na dereva wangu kaumia sana mguu. Gari yangu imeumia sana wala huwezi kuamini kama kuna mtu katoka salama.”
Taratibu za kumhamishia Bahati kutoka Hospitali ya Kongwa kuja Muhimbili zinafanywa na ndugu pamoja na marafiki.
Tunakuombea upone haraka Bahati.
Chanzo:http://www.globalpublishers.info/

PIGO KWA LIVERPOOL, ADAM LALLANA AUMIA GOTI NA ATAKUWA NJE WIKI SITA

MATUMAINI ya Adam Lallana kuanza kwa kishindo Liverpool yamepata pigo baada ya kuumia goti ambalo litamfanya awe  nje ya Uwanja kwa wiki sita.
Kiungo huyo wa England, ambaye amekuwa akifanya mazoezi na Liverpool kwa siku nne baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 23.6 kutoka Southampton, atakosa mechi tatu za kwanza za Ligi Kuu ya England — ukiwemo mchezo wa nyumbani dhidi ya klabu yake ya zamani na mechi za ugenini dhidi ya Manchester City na Tottenham.
Na pia anaweza kukosa mchezo wa ufunguzi wa kufuzu Euro 2016 dhidi ya Uswisi Septemba 8 ugenini. Lallana aliumia mazoezini Alhamisi na wasiwasi wa Liverpool umeongezeka baada ya majibu ya vipimo alivyofanyiwa. 
Pigo kubwa: Brendan Rodgers atamkosa mchezaji mpya, Adam Lallana mwanzoni mwa msimu