MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday, 7 June 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MWANDAMIZI WA MAMBO YA NDANI NA NJE WA SINGAPORE

l3 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano. l4 
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo  na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.PICHA NA IKULU

TFF YAPEREKA RAMBIRAMBI KWA MSIBA WA GEBO PETER

 


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Simba na Taifa Stars, Gebo Peter kilichotokea usiku wa kuamkia leo (Juni 6 mwaka huu) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Gebo aliyezaliwa mwaka 1961, pia aliwahi kuchezea timu za Sigara ya Dar es Salaam, CDA ya Dodoma na kombaini ya Mkoa wa Dar es Salaam (Mzizima United). Hadi mauti yanamkuta alikuwa akijishughulisha na biashara, kubwa ikiwa ya vifaa vya michezo.

Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu nchini kwani, Gebo enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa akiwa mchezaji na baadaye kiongozi katika timu ya Manyema ya jijini Dar es Salaam.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Gebo Peter, klabu ya Manyema na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Msiba upo nyumbani kwao Vingunguti karibu na Kanisa Katoliki ambapo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia.

Marehemu ambaye ameacha mjane na watoto watatu anatarajiwa kuzikwa kesho (Juni 7 mwaka huu) nyumbani kwao Kigurunyembe, mjini Morogoro.

Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

KIUNGO WA UJERUMANI MARCO REUS HATARINI KUZIKOSA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA

Down and out: Germany midfielder Marco Reus holds his left ankle in pain after injuring himself against Armenia 
Hoi : Kiungo wa Ujerumani,  Marco Reus akiwa ameshika kifundo chake cha mguu wa kushoto baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Armenia
Ouch: Reus grimaces as he is helped to his feet by medical staff late in the first half 
  Reus akitibiwa na madaktariwa timu ya taifa ya Ujerumani.
 PIGO!,  Marco Reus hatihati kucheza fainali za kombe la dunia baada ya jana kupata majeruhi ya kifundo cha mguu katika ushindi wa mabao 6-1 ambao Ujerumani ilivuna dhidi ya Armenia ikiwa ni pasha pasha kabla ya kuanza  kombe la dunia wiki ijayo.
Nyota huyo Borussia Dortmund alianguka chini baada ya kugongana na kiungo wa Armenia, Artur Yedigaryan na kuambulia kuumia na kuzua hofu kubwa kwa mashabiki wa Ujerumani na benchi zima la ufundi.
Kusoma zaidi bofya 

MASHABIKI WAZOMEA BRAZIL KWA KIWANGO KIBOVU BAADA YA KUTOKA 1-0 NA SERBIA KTKMCHEZO WA KIRAFIKI

 
To the rescue: Fred scored the only goal of the game in Brazil's final warm-up before the World Cup
Aliwaokoa: Fred aliifungia bao pekee Brazil katika pasha pasha ya kombe la dunia.
Fred flicked the ball home in the 58h minute to open the scoring at Morumbi Stadium
Fred akichukua mpira katika dakika ya 58 na kufunga bao kwenye uwanja wa  Morumbi
WAZEE wa Samba, Brazil,  jana usiku walibanwa mbavu na kuanza vibaya kipindi cha kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Serbia na kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 wakati huu zikisalia zimesalia siku tano tu kuanza fainali za kombe la dunia.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki waliofurika uwanjani waliwazomea wachezaji wa Brazil baada ya Fred kufunga bao hilo pekee katika dakika ya 58.
Kusoma zaidi bofya

Serikali yawapa uraia wakimbizi wa Kisomali 1,514,

 PIX 1
Felix Mwagara
SERIKALI imewapa uraia wa Tanzania Wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu 1,514 waliokuwa wanaishi katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Wakimbizi hao ambao walikimbia nchi yao Somalia baada ya vita kutokea mwaka 1990 ambapo baadhi yao 3,000 walikimbilia nchini kwa kutambua kuwa ndipo mababu zao walikotoka, Serikali iliwapokea na kuwahifadhi katika Kambi ya Mkuyu iliyopo Mkoani Tanga ambapo walikuwa wakipata msaada kutoka Shirika la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR).
Akizungumza jana baada ya kuwapa vyeti vya uraia wakimbizi hao ambao kwasasa ni raia halali wa Tanzania, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alisema wakimbizi hao walihamishwa na Serikali mwaka 2003 kutoka Kambi ya Mkuyu kuja katika Makazi ya Chogo ili wapatiwe mashamba kwa ajili ya kujishughulisha na kilimo ili waweze kujitegemea.
“Nachukua nafasi hii kuwapongeza wote waliopewa uraia wa Tanzania, wajisikie kuwa wao ni raia huru sawa na Watanzania wengine. Hata hivyo nawasihi muwe waadilifu na watiifu kwa sheria zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Chikawe.
Chikawe pia alitoa pongezi kwa UNHCR kwa kujenga miundombinu muhimu katika makazi hayo ya Chogo na pia kuwawezesha wakimbizi hao kuishi maisha ya kujitegemea wenyewe kabla hata ya kuwa raia.
Hata hivyo, Waziri Chikawe aliwataka wakimbizi 150 katika makazi hayo ya Chogo ambao hawakuomba kuwa raia wa Tanzania kwa nia ya kurudi nchini Somalia pale hali ya amani itakapopatikana wanapaswa kuendelea kutii sheria za nchi zinazotawala hifadhi ya ukimbizi nchini.
Aidha, Mwakilishi Mkazi wa UNHCR, Joyce Mends-Cole katika hafla hiyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuwapa uraia wakimbizi hao na Shirika lake litaendelea kutoa misaada mbalimbali kwa wakimbizi waliobaki katika makazi hayo pamoja na sehemu nyingine nchini.
Hafla hiyo ya ugawaji wa vyeti vya uraia ilihudhuriwa na Maofisa wa Idara ya Wakimbizi na Uhamiaji zilizopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwakilishi wa Mkuuu wa Mkoa wa Tanga na Serikali ya Kijiji cha Chogo pamoja na Maofisa wa UNHCR

Friday, 6 June 2014

UZI MPYA WA PUMA ARSENAL HUU HAPA, KITU BLUU

JEZI mpya za msimu ujao wa 2014/2015 za Arsenal zimevuja na aina zote tatu zilizotengenezwa na Puma zimeonekana. Zitazame 

Rangi ya Bluu: Jezi ya mechi za genii za Arsenal
Gunner wear it? This could be the Arsenal kit for next season - their first Puma strip
Nyekundu ndiyo yenyewe? Hii itakuwa jezi ya mechi za nyumbani msimu ujao Arsenal

KIKOSI CHA ITALIA NDANI YA BRAZIL, UTAWATAKAAA

WACHEZAJI tisa wa Italia walilazimika kukaa situ za daraja la pili, baada ya kuambiwa ndege ni ndogo wakielekea Brazil kwenye Kombe la Dunia.

The Azzurri imewasili leo mjini Riona kuelekea katika kambi yao mjini Mangaratiba, umbali wa maili 75 kusini mwa mji huo.
Lakini karibu nusu ya wachezaji wao waliambiwa hakuna nafasi katika daraja la kwanza kwenye ndege ya Alitalia maarufu na wakatumia saa 12 angani wakiwa wameketi kwenye siti 'za kawaida'.
Watanashati: Kikosi cha Italia kikiwa kwenye ndege kwa safari ya Brazil kwenye Kombe la Dunia

STAA BALOTELLI NDANI YA BRAZIL KWA KOMBE LA DUNIA

Kichaa ndani ya suti: Mshambuliaji wa Italia, Mario Balotelli akiwasili mjini Rio de Jeneiro, Brazil na timu yake ya taiga ya Italia tayari kwa Fainali za Kombe la Dunia

AFA KWA KUGONGWA NA KUGONGWA NA TELA ALILOKUWA AKILILINDA





Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Lameck Mashaka (38) mlinzi na mkazi wa kijiji cha Mgowelo mkoani Iringa amefariki dunia baada ya kugongwa na tela alilokuwa akililinda.



Akizungumza na mtandao huu wa   ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoani hapa ACP Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 4 Juni majira ya saa 7:30 usiku huko maeneo ya Kware Ruaha Mbuyuni barabara kuu ya Iringa – Moro iliyoko wilaya ya Kilolo.



Kamanda Mungi alisema gari aina ya Scania yenye namba za usajili T. 903 ARK iliyokuwa ikiendeshwa na Rajabu Aungalipa (36) mkazi wa Mbagara Dar es salaam liliacha njia na kasha kuigonga Tela lenye namba T. 894 BDQ iliyokuwa imeegeshwa kando ya barabara.



Alisema mbali na mtu mmoja kufariki dunia pia ajali hiyo ilisababisha majeruhi watatu ambao ni Ramadhani Dunia (23) ambaye ni fundi magari, Rajabu Aungalipa (36) ambaye ni dereva wa scania pamoja na Farid Ruben ambao wote wamelazwa katika hospitali ya Tandika iliyopo jijini Dar es Salaam.      


CHANZO 
www.matukiodaima.com

NA DIANA BISANGAO WA   IRINGA

WAKAZI WA MKOANI IRINGA WAASWA KUJIINGIZA KATIKA KILIMO



  Wakulima wa mazao mbalimbali mkoani Iringa  wametakiwa kutumia mbegu za kisasa ili kuboresha shughuli za kilimo na kupata mazao ya kutosha.

Afisa miradi  wa muungano wa wakulima  vijijini Bw  William Maja
aliyasema hayo  akiwa na baadhi ya wakulima katika ukumbi wa shule ya msingi Chemi Chemi  iliyopo katika manispaa ya Iringa ambapo aliwataka wakulima walime zao la mtama.

Hata hivyo alisema kuwa wakulima wanapaswa  kushirikiana  katika kilimo na kuacha dhana ya kutegemea watu wachache  katika kilimo ili kufanikiwa zaidi.

Aidha  alisema  kuwa wakulima pindi wanapopanda  mazao watumie mbolea husika ili waweze  kupata mazao ya kutosha.
 


NA DIANA BISANGAO WA  IRINGA

MBUNGE MGIMWA AANZA KUTIMIZA AHADI ZA MAREHEMU BABAKE KWA KASI KUBWA


Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Magubike Bi Lenatha Mbilinyi kushoto akipokea msaada wa saruji mifuko 100 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa leo ,wanaoshuhudia  kulia ni katibu menezi wa CCM wilaya Denis Lupala na diwani wa kata ya Nzihi katikati Bw Stivin Mhapa
........................................................................................

MBUNGE  wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa  Godfrey Mgimwa ameanza  kutimiza ahadi  zake kwa  wananchi  wa  jimbo la kalenga  kwa  kukabidhi mifuko zaidi ya 150 ya  saruji katika  kijiji cha Magubike na kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi  yenye  thamani  ya zaidi ya Tsh milioni 2.5


Saruji  hiyo mifuko 100 kwa ajili ya  kusaidia ujenzi wa jengo la utawala shule ya  sekondari Dimitrios katika  kijiji  cha Magubike  na mifuko 50 kwa ajili ya shule ya sekondari Kidamali.


Mgimwa alisema kuwa lengo la kutimiza ahadi  yake  hiyo ni kama njia ya  kuwashukuru  wana Kalenga kwa kumchagua katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni pia kutimiza ahadi mbali mbali binafsi ambazo alizitoa mbunge aliyefariki marehemu Dr Wiliam Mgimwa.


Alisema ataendelea  kutimiza ahadi  binafsi zilizotolewa na marehemu Dr Mgimwa kulingana na uwezo  wake  na zile  za  kitaifa ambazo zipo katika Ilani ya CCM atahakikisha anaikumbusha  serikali  ya CCM ili  kutimiza ahadi hizo kwa  wakati.

“Ndugu  zangu wananchi  mbali  ya  kuwa  ubunge  wangu ni  wa  mwaka mmoja  ila  tayari  mimeanza  kutimiza ahadi  bila  ya kuchelewa  na  ninawahakikishieni  sita  waangusha  nitaendelea  kufanya  hivyo  zaidi  mniombee  uzima”


Alitaja  maeneo  ambayo tayari  amekabidhi  ahadi  zilizotolewa na mbunge aliyefariki  kuwa ni pamoja  na Kiwere shule ya msingi mifuko 80 ya saruji,shule  ya msingi wangama bati 100 na  saruji mifuko 50,shule ya msingi Negabii bati 100 ,shule ya msingi Mibikimitali bati 50 ,Kijiji cha Isupilo bati  50 na saruji mifuko 50 na maeneo mingine mengi.


Pia amekabidhi kiasi cha  Tsh 500,oo kwa ajili ya kuchangia kuwezesha  kusajili  timu ya  kata ya Nzihi na nyingine  kwa ajili ya ukarabati wa soko

TAIFA STARS YA MART NOOIJ KUINGIA KAMBINI JUNI 11 KUIWINDA MSUMBIJI


1
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Kikosi cha Taifa Stars kinaingia tena kambini Jumatano (Juni 11 mwaka huu) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itakayochezwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na kambi ya siku tatu jijini Dar es Salaam ikijumuisha wachezaji 28. Kwa mujibu wa programu ya Kocha Mart Nooij, Stars itaingia tena kambini Juni 24 mwaka huu.
Wachezaji wanaotakiwa kuripoti kambini ni Deogratias Munishi, Aishi Manula, Benedictor Tinoko, Kelvin Yondani, Said Moradi, Nadir Haroub, Joram Nason, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Edward Charles, Aggrey Morris na Pato Ngonyani.
Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Amri Kiemba, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Said Juma, Haruna Chanongo, Himid Mao, Said Ndemla, John Bocco, Simon Msuva, Kelvin Friday, Ramadhan Singano, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Mwegane Yeya.

FABREGAS,NA PIQUE `DILI LIMEKAMILIKA KWA PAUNDI MILIONI 26.8` ASEMA JOSE MOURINHO


Done deal: Cesc Fabreagas has moved to Chelsea, according to Spain team-mate Gerard Pique
Imechapishwa Juni 6, 2014, 
KOCHA `mbwatukaji` Jose Mourinho amekiri kuwa Chelsea inavutiwa kumsajili Cesc Fabregas kutoka klabu ya FC Barcelona, huku mchezaji mwenzake wa Hispania Gerard Pique amesema dili hilo limekamilika kwa paundi milioni 26.8.
Kocha huyo amesema kuwa ni wazi Fabregas anataka kurudi ligi kuu ikiwa ni miaka mitatu imepita tangu aondoke Asernal, hivyo anafuatilia kwa makini ili kumsajili baada ya kombe la dunia.
Wakati huo huo Chelsea wako tayari kumpa ofa ya mshahara wa paundi milioni laki mbili kwa wiki winga wao hatari,  Eden Hazard ili kuwaziba mdomo Paris Saint-Germain wanaoiwinda saini yake.
Admission: Chelsea boss Jose Mourinho admitted the club are interested in the former Arsenal star
"Kuna mchakato huko anakotaka kuondoka, anataka kuja England kwasababu ni taifa analopenda kucheza. Tunavutiwa kufuatilia hali halisi".
Wakati huo huo, Pique kwa upande wake anasema dili hilo limekalimika. Beki huyo wa Hispania alinaswa na Kamera mjini Washington akimwambia kocha wa Hispania , Vicente del Bosque kuwa  Fabregas ataondoka Barcelona kwa dau la paundi milioni 26.8 baada ya klabu hiyo kumalizia msimu bila kikombe.
Revelation: Gerard Pique was caught on camera telling Spain coach Vicente del Bosque about the move
 Gerard Pique alinaswa na kamera akimwambia kocha wa Hispani Vicente del Bosque kuhusu kuondoka kwa Fabregas.
Team-mates? Fabregas could join Spanish striker Diego Costa at Stamford Bridge next season

HOT NEWS:WAFANYA KAZI WA NDANI WA WILFRED LWAKATARE WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI

 

Polisi & CCM na hila za ugaidi CHADEMA: Wakamata house boys na girl wa Lwakatare usiku...

Taarifa ya awali...
Katika hali ile ile ya mwendelezo wa kutumikia maelekezo na maslahi ya CCM dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa chama hicho, Jeshi la Polisi usiku huu limevamia nyumbani kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare na kumkamata housegirl wake.

Kama hiyo haitoshi, jeshi hilo la polisi limewakamata wafanyakazi wengine wawili (house boys) wa Lwakatare. Hadi muda mfupi uliopita vijana hao wawili, walikuwa wako Kituo cha Polisi Mbezi huku msichana wa kazi wakizunguka naye kwenye gari la patrol bila kumfikisha kituoni.

Jeshi hilo la polisi kupitia kituo hicho cha Mbezi lilikuwa linawatisha kila mtu anayekwenda hapo kituoni kuulizia sababu za vijana hao kukamatwa, lakini hatimaye mmoja wa watu walioko kituoni hapo ametonya kuwa polisi wanasema mmoja wa vijana hao kesi yake iko Arusha!

Kijana anayetaka kubambikiwa kesi huko Arusha ni mwanagenzi kabisa mjini. Hata ukimwambia aende Chalinze au Wami hawezi kupajua.

Hatimaye mbinu za CCM kupitia jeshi la polisi ya kutaka kukichafua CHADEMA au viongozi wake kwa kutumia kes za kubambikia ugaidi imerejea tena...

Tutawaletea taarifa kamili...

                           CHANZO JF

WANANDINGA UHOLANZI TABASAMU TUPU...WAKWEA PIPA KUELEKEA BRAZIL


Departure: Wesley Sneijder (left) poses with wife Yolanthe as the Holland squad head to Brazil

Up for the Cup: Dirk Kuyt (left) says farewell to his wife and children at the Holtel Huis ter Duin in Holland
Dirk Kuyt (kushoto) akimuaga mke na mtoto wake.
Safe hands: Swansea goalkeeper Michel Vorm joined the Dutch squad for their journey to Brazil
Key man: Holland fans will be hoping Robin van Persie (centre) can recover from a slight groin strain
Wish us luck: Dutch boss Louis van Gaal waves to fans as he prepares to board the flight to Brazil
Here we go: Arjen Robben (centre) arrives at Schiphol airport near Amsterdam

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KIWANDA CHA COCACOLA MWANZA

 


1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Mwanza na wa Kiwada cha Cocacola, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014. Picha na OMR 02Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Mwanza na wa Kiwada cha Cocacola, wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014. Picha na OMR 04Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa ubora wa Mazingira na Usalama Kazini, Peter Simon, kuhusu jinsi wanavyo tunza mazingira kwa kutotupa maji machafu ambayo hutengenezwa na kuwa masafi  na kutumika upya kwa baadhi ya shughuli za kiwandani hapo kama kumwagia bustani, kuoshea magari na n.k,  wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014. Picha na OMR 06Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa ubora wa Mazingira na Usalama Kazini, Peter Simon, kuhusu jinsi wanavyo tunza mazingira kwa kutotupa maji machafu ambayo hutengenezwa na kuwa masafi  na kutumika upya kwa baadhi ya shughuli za kiwandani hapo kama kumwagia bustani, kuoshea magari na n.k,  wakati alipowasili kwenye Kiwanda hicho kwa ajili ya kutembelea na kujionea mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza katika Viwanja vya Furahisha, jana Juni 5, 2014. Picha na OMR 6_1 
 Makamu akiagana na wafanyakazi wa kiwanda hicho baada ya ziara yake. Picha ya pamoja

MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO WAASWA KUTOA TAARIFA ZINAZOHUSU TAASISI ZAO KWA WAKATI

 
IMG_2358  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakati wa Semina ya Mafunzo iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na Kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Innocent Mungy. IMG_2365Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel wakati wa Semina ya Mafunzo iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Leo Jijini Dar es Salaam. IMG_2369Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Sylvia Lupembe akitoa neno la shukrani kwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga, wakati wa Semina ya Mafunzo iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Leo Jijini Dar es Salaam. IMG_2384Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel  akiwasilisha mada kuhusu huduma kwa mteja kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wakati wa Semina ya Mafunzo iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Leo Jijini Dar es Salaam. IMG_9760 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel  akifurahia jambo na Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Innocent Mungy, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Sylvia Lupembe na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Bw. Abel Ngapemba.

ZIARA YA MH.KINANA WILAYANI SIMANJIRO MKOANI ARUSHA

KINANA ASHUHUDIA MCHIMBAJI MDOGO WA TANZANIATE ANAVYOSAIDIA WENZAKE KWA KUWAUZIA KWA BEI NAFUU VIFAA VYA UCHIMBAJI MADINI HAYO MERERANI

Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite  kwenye machimbo ya Mererani wilayani Simanjiro,  Mahmoud Karia (kulia) akimuonyesha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahmahn Kinana vifaa vya kisasa vya uchimbaji madini hayo, ambavyo huviuza kwa wachimbaji wengine kwa gharama nafuu. Karia alipata fursa ya kuonyesha vifaa hivyo Kinana alipomtembelea kwenye eneo la machimbo la mchimbaji huyo mdogo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi mkoani Manyara, mapema wiki hii. Wapili kushoto ni Mbunge wa Simnanjiro, Christopher Ole Sendeka na anayerekebisha miwani ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye. (Picha na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog

BAADA YA PICHA ZA MH KOMBA ZA MAHABA KUSAMBAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII ADAI ZIME TENGENEZWA.


    Default


  1. PICHA za Capt. Komba zenye utata zasambazwa kwenye mitandao ya kijamii!





    Picha zinazomwonyesha mh. Captain John Komba zenye mapozi tofauti na mabinti tofauti zimeanza kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii hapa Tanzania.

    Kuna picha nyingine nyingi lakini kutokana na maadili hatuwezi kuziweka hadharani; hizi ni baadhi tu

    =======
    UTETEZI WA KOMBA:

    Kuhusiana na hizi picha 2 zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuznia asubuhi ya leo, zikimuonyesha Mheshimiwa Mbunge huyo wa CCM Kapteni John Komba akiwa kwenye mahaba na Mwanadada mmoja anayeishi Kinondoni.
    Mbunge huyo amesema kwamba picha hizi zimetengenezwa na maadui wake wa kisiasa na kwamba yeye sio Kiongozi wa hovyo hovyo namna hiyo.

    Kapteni Komba amesema kwamba anawakaribisha wataalamu wa Picha na Mitandao kutihibitisha ukweli wa picha hizo zinazoonyesha Mwana-Dada akiwa na kipande cha khanga tu huku Mbunge huyo akiwa pembeni yake akionyesha kutokuwepo kabisa kwenye Mahaba yanayotakiwa kuwa yanaendelea baina yao.

    Mbunge huyo ameuliza zaidi iweje awe kwenye mapenzi kama picha zinavyo onyesha halafu awe na nguo zake zote huku msichana akiwa na khanga tu?

    Kapteni Komba amesema kwamba kama kweli Taifa hili limefikia hapa pa kuchafuana namna hii kisa mitizamo tofauti ya kisiasa ya namna ya kuongoza Taifa letu basi kama Taifa tumefikia pabaya sana.

    Mbunge huyo amemalizia kwa kusema kwamba wale wote wanaomuamini kama Kiongozi shupavu wa Taifa, wasikatishwe tamaa na wajinga wachache wenye mawazo ya kitumwa ambao wanadhani wanaweza kummaliza kisiasa kwa kumtengenezea picha chafu kama hizi picha 2 za leo!