MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Sunday, 2 March 2014

REAL MADRID NA ATLETICO MADRID ZATOKA DROO YA 2-2 BAADA YA RONADO KIUINUSURU REAL MADRID

 
>>REAL YABAKI KILELENI!!
Usiku huu, kwenye Dabi ya Jiji la Madrid, maarufu kama El Derbi Madrileono, iliyochezwa Estadio VicenteRON_WITH_ATLETICOCalderon, Wenyeki Atletico Madrid walitoka Sare ya Bao 2-2 na Real Madrid kwenye Mechi ya La Liga.
Real walitangulia kufunga Bao mapema kupitia Karim Benzema na Atletico kuamka na kupiga Bao 2 kupitia Koke na Arenas na kuongoza 2-1 hadi Mapumziko.
Huku jahazi likielekea kuzam, Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, aliisawazishia Real katika Dakika ya 82.

MAGOLI:
Atletico Madrid 2
-Koke Dakika ya 28
-Arenas 45
Real Madrid 2
-Karim Benzema Dakika ya 3
-Ronaldo 82

Matokeo haya yamewabakisha Real kileleni mwa La Liga wakiwa na Pointi 64 wakifuatiwa na Atletico wenye Pointi 61 na Barcelona wapo Nafasi ya Tatu wakiwa na Pointi 60.
VIKOSI:
Atlético de Madrid: Courtois, Juanfran, Godín, Miranda, Filipe Luis, Suárez, Gabi, Arda, Koke, Raúl García, Diego Costa.
Real Madrid: Diego López, Arbeloa, Pepe, Ramos, Coentrao, Xabi Alonso, Modric, Di María, Bale, Benzema, Ronaldo.
LA LIGA:
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumapili Machi 2
Villarreal CF 1 Real Betis 1
Atletico de Madrid 2 Real Madrid CF 2
2100 Sevilla FC v Real Sociedad
2300 FC Barcelona v UD Almeria
2300 Rayo Vallecano v Valencia
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Real Madrid CF
26
20
4
2
73
26
47
64
2
Atletico de Madrid
26
19
4
3
61
21
40
61
3
FC Barcelona
25
19
3
3
70
20
50
60
4
Athletic de Bilbao
26
15
5
6
49
30
19
50
5
Villarreal CF
26
13
5
8
47
31
16
44
6
Real Sociedad
25
12
7
6
46
35
11
43
7
Levante
26
9
9
8
26
31
-5
36
8
Sevilla FC
25
9
8
8
43
41
2
35
9
Valencia
25
10
5
10
38
36
2
35
10
RCD Espanyol
26
9
6
11
29
32
-3
33
11
Celta de Vigo
26
8
6
12
32
37
-5
30
12
Elche CF
26
7
8
11
23
37
-14
29
13
Osasuna
26
8
5
13
24
39
-15
29
14
Granada CF
26
8
3
15
22
36
-14
27
15
Getafe CF
26
7
6
13
23
40
-17
27
16
Malaga CF
26
6
8
12
24
35
-11
26
17
UD Almeria
25
7
5
13
24
42
-18
26
18
Real Valladolid
26
4
11
11
28
44
-16
23
19
Rayo Vallecano
25
6
2
17
25
59
-34
20
20
Real Betis
26
3
6
17
21
56
-35
15

VPL:ANGALIA RATIBA, MATOKEO NA MSIMAMO WA VPL BAADA YA SIMBA YAICHAPA RUVU SHOOTING!!


VPL_2013-2014-FPBao mbili za Amisi Tambwe na moja la Haruna Chanongo zimewapa Simba ushindi wa Bao 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom iliyochezwa Leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba walitangulia kufunga Bao 2 kupitia Tambwe na Said Dilunga wa Ruvu Shooting kuipa Timu yake Bao la kwanza
Haruna Chanongo aliifungia Simba Bao la 3 na kisha Ruvu Shooting kufunga Bao la Pili kwa Penati iliyopigwa na Jerome Lambele.
Penati hiyo ilitolewa baada ya Singano kuunawa Mpira.
Matokeo haya yameibakiza Simba Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Mbeya City na pia Ruvu Shootinga kubaki Nafasi ya 8.
VIKOSI:
SIMBA: Yaw Berko, Haruna Shamte, Issa Rashid, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Said Ndemla, Amisi Tambwe, Amri Kiemba, Ramadhani Singano
RUVU SHOOTING: Abdallah Rashid, Michael Pius, Mao Bofu, Baraka Jafari, Gedion Sepo, Ali Khan, Hamisi Kisuke, Juma Nade, Elias Maguri, Said Dilunga, Raphael Kyala

MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
18
11
7
0
23
40
2
Yanga SC
17
11
5
1
29
38
3
Mbeya City
20
9
9
2
8
36
4
Simba SC
20
9
8
3
17
35
5
Kagera Sugar
19
6
8
5
1
26
6
Coastal Union
19
5
10
4
5
25
7
Mtibwa Sugar
19
6
7
6
0
25
8
Ruvu Shooting
19
6
7
6
-5
25
9
JKT Ruvu
19
7
1
11
-13
22
10
Prisons FC
17
3
8
6
-3
17
11
Mgambo JKT
19
4
5
10
-17
17
12
JKT Oljoro
20
2
9
9
-15
15
13
Ashanti United
19
3
5
11
-19
14
14
Rhino Rangers
19
2
7
10
-11
13
RATIBA/MATOKEO:
Jumapili Machi 2
Simba 3 Ruvu Shooting 2
Kagera Sugar v JKT Ruvu
Ashanti United v Rhino Rangers
Tanzania Prisons v Mgambo JKT

MAN CITY YANYAKUA UBINGWA WA CAPITAL ONE CUP, 2014

MAN CITY YANYAKUA UBINGWA WA CAPITAL ONE CUP, 2014


city_1_2f29e.jpg

Wachezaji wa Manchester City wakishangilia baada ya kukabidhiwa kikombe hicho. 
city_new_borini_00004.jpg
Na Riziki Mashaka.
Timu ya Manchester City imenyakua ubingwa wa kombe la Capital One baada ya kuitandika Sunderland kwa magoli 3-1 katika dimba la Wembley.
Mshambuliaji wa Sunderland, Fabio Borini alipachika goli mnamo dakika ya 10 na kuiandikia timu hiyo goli la pekee, Sunderland ilikuwa kifua mbele kwa goli 1-0 mpaka kipindi cha kwanza kilipomalizika.
city_new_yaya_3fbdc.jpg
Kiungo wa Man City, Yaya Toure alipopachika goli la kwanza 

Mtanange huo ulichukua sura mpya katika kipindi cha pili baada ya kiungo wa Manchester City, Yaya Toure kusawazisha goli hilo mnamo dakika ya 54, wakati mashabiki wa Man City wakishikwa na butwaa baada ya goli hilo, hali ilizidi kupamba moto kwani Samir Nasri alipachika goli la pili mnamo dakika ya 56 na kuifanya timu hiyo kuwa mbele kwa magoli 2-I.
city_new_nasri_a690b.jpg
Samir Nasri alipokuwa anashangilia baada ya kupachika goli la pili.
Timu hizo zilikuwa zikishambualiana mara kwa mara, na mpaka kufikia dakika ya 69 mshambuali wa Man City, Sergio Aguero alishindwa kuonesha makali yake na hali hiyo ilipelekea kocha wake Manuel Pellegrini kumtoa na kumuingiza kiungo mshambualiaji, Jesus Navas ambaye aliipachikia timu hiyo goli la tatu mnamo dakika ya 89 ya mchezo.
city_new_navas_7337d.jpg
Kiungo wa Man City, Jesus Navas alipokuwa apaichikia timu yake goli la 3. 
city_another_a8e26.jpg
Wachezaji wa Sunderland walipokuwa wanatoka uwanjani baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa.
Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa, Man City ilikuwa kifua mbele kwa jumla ya magoli 3-1, kitendo hicho kiliipelekea timu hiyo kuibuka mabingwa wa kikombe hicho cha Capital One, 2014.
city_new_mashabiki_9af51.jpg
Mashabiki wa Man City walipokuwa wanashangilia ushindi wa timu yao.
city_3_94ac4.jpg
Picha aliyoituma mchezaji wa Man City, Vincet Kompany katika mtandao wake wa Twitter, ni baada ya kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo. 
city_4_91a42.png
Kutoka kushoto ni beki na kapteni wa timu hiyo, Vincet Kompany akiwa amebeba kikombe hicho kwa furaha, kulia ni kocha, Manuel Pellegrini naye akiwa amebeba kikombe hicho cha Capital One kwa mara ya kwanza katika historia yake ya soka la Uingereza.
SUNDERLAND 1 MAN CITY 3
MANCHESTER CITY, chini ya Meneja Manuel Pellegrini, Leo Uwanja wa Wembley Jijini London wametwaa Taji laoCAPITAL_ONE_CUP-BEST la kwanza baada ya kuifunga Sunderland Bao 3-1 na kubeba CAPITAL ONE CUP ambalo ndio Kombe la Ligi Nchini England.
Sunderland walianza vyema kwa kufunga Bao katika Dakika ya 10 Mfungaji akiwa Fabio Borini lakini City walizinduka Kipindi cha Pili na kupiga Bao 3.

MAGOLI:
Man City 3
-Yaya Touré Dakika ya 55
-Nasri 56
-Jesús Navas 90
Sunderland 1
-Borini Dakika ya 10

Bao la kwanza la City lilifungwa na Yaya Toure kwa kigongo cha Mita 30 na Dakika moja baadae Nasri akaipa City Bao la Pili.
Bao la Tatu la City lilifungwa na Jesus Navas alieingizwa Dakika ya 58 kumbadili Sergio Aguero.
VIKOSI:
Man City: Pantilimon, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov, Nasri, Toure, Fernandinho, Silva, Dzeko, Aguero
Akiba: Hart, Lescott, Milner, Negredo, Javi Garcia, Jesus Navas, Clichy.
Sunderland: Mannone, Bardsley, Brown, O'Shea, Alonso, Ki, Larsson, Cattermole, Colback, Johnson, Borini
Akiba: Gardner, Fletcher, Celustka, Giaccherini, Vergini, Scocco, Ustari.
Refa: Martin Atkinson

 

' TUMEANZA BUNGE MAALUM LA KATIBA MPYA KWA KUSHINDWA'

 
bunge_a54c8.jpg
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba amesema mwanzo wao umekuwa mbaya, kutokana na wengi wao kuwa na misimamo ya vyama na makundi yaliyowapeleka kwenye Bunge hilo.
Bunge hilo linaendelea kujadili na kurekebisha Rasimu ya Kanuni, zitakazotumika kuongoza mijadala ya kuboresha Rasimu ya Pili ya Katiba iliyoandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ili kupata Rasimu ya Mwisho ya Katiba Mpya, ambayo itakubaliwa au kukataliwa wananchi kwa kuipigia kura ya maoni.
"Siyo siri kwamba kilicho nyuma ya pazia ya ubishi uliyoibuka kwenye semina iliyolenga kurekebisha Rasimu ya Kanuni ni wengi wetu kuingia bungeni tukiwa na misimamo ya vyama au vikundi vilivyotutuma, mfumo wa kura za wazi ni wenye lengo la kudhibiti wajumbe wasikiuke maagizo waliyopewa na waliowaagiza," anaeleza Cheyo
Anasema misimamo haikutolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) peke yake bali vyama vyote vya siasa na kijamii vimejiwekea misimamo ambayo wajumbe walioingia bungeni, wameagizwa kuijengea hoja na kuisimamia, kuhakikisha inazingatiwa katika Katiba mpya ijayo.
Tofauti iliyopo kati ya CCM na vingine inatajwa na Cheyo kwamba ni kuwa na idadi kubwa ya wajumbe wa Bunge hilo, pia chama hicho kinaelezwa na mjumbe huyo kuwa ni chenye itikadi ya kuwa na misimamo na kuweka mbinu madhubuti za kuwasimamia walioagizwa kuitekeleza, kuhakikisha hawatendi kinyume.
"Tukirejesha fikra zetu nyuma, hatutakosa kumbukumbu juu ya kilichotokea enzi za Mwalimu Nyerere (Hayati Baba wa Taifa) wakati wakijadiliana na kuamua kuhamishia makao makuu ya nchi mjini Dodoma, ilifika wakati akasema, "Asiyetaka anyooshe mkono juu." Ingawa kulikuwa na wasiyotaka lakini tulibaki kimya bila kidole hata kimoja kunyooshwa," anaeleza Cheyo
Cheyo anasema ili mabishano yanayoendelea bungeni hususan kwenye hoja ya aina gani ya kura itumike; kati ya siri au ya wazi ni lazima wajumbe wote "wavue" tofauti zao, kwa kubaki na wadhifa mmoja tu wa ujumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na hivyo wawe na jukumu la kuboresha Rasimu ya Pili, ambayo itakayowasilishwa kwao na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Anahimiza wajumbe kuitikia wito wa Rais Jakaya Kikwete, unaowataka kuweka kando misimamo yao na kwamba ikiwa hilo halitatokea, misimamo ya vyama vya siasa na makundi ya kijamii itawafikisha hatua ya kutoka nje ya vikao vya Bunge pale mijadala itakapowadia na kupamba moto.
Cheyo anabainisha kuwa haafiki utaratibu wa 'wengi wape' katika kupitisha hoja na hatimaye Rasimu ya Mwisho ya Katiba, akisema; "Hili ni suala nyeti lisilohitaji kufanyiwa mzaha hata kidogo. Kupitisha hoja kwa mtindo wa wengi wape, tutapitisha kwa wingi wetu sawa lakini tunapitisha nini? Hapo ndipo patakapoibuka mabishano ambayo yatatufikisha mahala pa kutoka na aibu," anaeleza cheyo
Anaasa wajumbe wenzake kukumbuka kuwa tangu mchakato wa kutafuta Katiba Mpya nchini uanze, fedha nyingi za wananchi zimetumika na kwamba kushindwa kwao kutekeleza kwa ufanisi jukumu lililo mbele yao, kutasababishia taifa hasara ambayo bila shaka hawataweza kusamehewa na vizazi vya sasa na vijavyo.
"Tanga kuna kijiji niliona kwenye TV, wanachota maji ya kutumia kutoka kwenye kijiji kingine, wakitembea kwa miguu mwendo mrefu tena ndani ya maji. Ni bora fedha zilizotumika katika mchakato huu zingetumika kutatua kero za wananchi kama hizo. Ninachomaanisha hapa ni wajumbe tuone umuhimu wa kazi iliyo mbele yetu," anaeleza Isack Cheyo
Pamoja na kuweka kando itikadi na tofauti zao, ili kumaliza suala la kura ya siri au wazi ipigwe, Cheyo anasema ni vyema wajumbe wakafanya uamuzi kwa kuchagua baadhi ya wajumbe watakaowakilisha makundi yote yaliyomo kwenye kikao kitakachojadiliana na kuamua cha kufuata; akisema ni vigumu ndani ya kundi la watu zaidi ya 600, kufikia muafaka wa suala hilo.
Lugha za kukera bungeni
Cheyo anasema mtu yeyote anayesema ovyo tena hadharani huku akiwa mwenye umri wa utu uzima, ni ishara kwamba, hakudhibitiwa kitabia tangu akiwa katika umri mdogo; "Usipodhibitiwa kitabia ukiwa mtoto, utasema ovyo mpaka uzeeni mwako na hilo ndilo tunaloshuhudia bungeni."
Anasema ikitokea wakaamua kufuatilia historia ya malezi ya wanaotumia lugha chafu kwenye vikao vya Bunge, itathibitika kuwa anayoeleza ni kweli tupu na kwamba watu hao wanatia dosari hadhi ya taifa na kuwa mfano mbaya kwa watoto ambao wanafuatilia vipindi vya vikao vya Bunge, vinavyotangazwa moja kwa moja kwenye vituo vya televisheni na redio.
"Jana ilifika wakati nikatamani kuwaomba waeleze ikiwa wanapenda sana vijembe, waruhusu tuite vikundi vya taarabu bungeni, vitumbuize ili vitoe vijembe vilivyowekwa kitaalamu zaidi, na hapo ikumbukwe ni vikao vya kurekebisha rasimu ya kanuni, je tukianza mijadala itakuwaje? Inabidi ifike wakati tubadilike," anaeleza Isack Cheyo.
Chanzo:Mwananchi

HUYU NDIO MTOTO ALIYE BURUZWA NYUMA YA PIKIPIKI NA BABA YAKE KISA HAJAENDA SHULE.


Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.



Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya sa tatu asubuhi katika moja ya mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo alikataa kwenda shule kitendo ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.

 mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa lengo la kumkamata baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.

  Baada ya kumkamata na kumtia kumtia mikononi mwao walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo Ihayabuyaga kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.
Akizungumzia tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea mtuhumiwa huyo Abel Richard amesema tukio hilo liliwafanya wananchi kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga.

Amesema mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Geita baada ya katibu huyo kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo na kuwatuma askari kwake kumchukua haraka kwa usalama wake.

Afisa upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa upelelezi

HUYU NDIO MSICHANA ALIYEONGOZA MATOKEO YA KIDATO MWAKA 2013

Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano ‘exclusively’ na Robina Nicholaus, msichana aliyeshika nafasi ya kwanza/ aliyeongoza kitaifa (Tanzania One) kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2013.
 
Robina, mwenyeji wa wilaya ya Bunda mkoa wa Mara ambaye alikuwa anasoma katika shule ya wasichana ya Marian, akiwa na ndoto ya kuwa daktari wa watoto amejibu maswali kumi muhimu na majibu yake yanaweza kuchukuliwa kama mfano wa kuigwa kwa wanafunzi walioko shuleni ambao wanakumbwa na changamoto kadhaa, na wazazi wanaowapeleka watoto wao shule.
Ulifanya nini ghafla ulipopata taarifa kuwa umekuwa wa kwanza Tanzania nzima, na je, ulitegemea?
 Nilipopata matokeo kwamba nimekuwa wa kwanza, kwanza nilifurahi sana na kilichobaki zaidi ilikuwa ni kumshukuru Mungu kwa sababu yeye ndiye kayawezesha yote. Nilihisi kama kupaa vile…nilifurahi sana halafu my mom alikuwa pale… alikuwa analia akaniinfluence na mimi machozi yatoke, I was very happy yaani. Sikutegemea kuwa wa kwanza lakini nilikua na uhakika wa kufanya vizuri kwa sababu niliplan kufanya vizuri.
Kama msichana ulifanya nini kuzivuka changamoto za kimasomo na kufanikisha kwa kiasi kikubwa? 
Safari ya taaluma ni ndefu ndio, kwenye safari ya masomo kuna changamoto za hapa na pale, ambapo mara nyingi wasichana waga tunafanya maamuzi ambayo sio sahihi. Lakini kwangu mimi nimeweka interest yangu sana kwa wazazi. Kwa hiyo nilikuwa open kwa wazazi na kuwaomba ushauri wa hapa na pale nifanye nini. Na katika vyote nilivyokuwa nafanya ni kufanya kile kitu ambacho hakiwezi kusubiria kwanza ambacho ni masomo. Kwa hiyo naweka juhudi pale ili ukishafanya kila mtu ajue kwamba umefanya.


Ilikuwa mbaya sana kwenye kusoma hasa form three ambapo nilianza kushuka and all that. Kwa hiyo wazazi pamoja na walimu pia walikaa na kuweza kunisaidia na mimi mwenyewe nilikuwa tayari kusikia ushauri wao na kuweza kusoma kwa bidii zaidi ili niweze kupata ile nafasi yangu niliyokuwa naipata toka nianze.

Nini kilichofanya ushuke kimasomo wakati huo?
 

 Kilichofanya nishuke ni ile kupoteza malengo na juhudi zangu, na pia kuona kwamba vitu vinaanza kuwa vigumu halafu kuweka hiyo kwenye akili kwamba hicho ni kigumu siwezi kukifanya. Lakini nilipoamua kuweka juhudi na kuona kwamba ni vitu vya kawaida kwamba navyozidi kukua na vitu vinazidi kuwa vigumu na natakiwa nitafute njia ya kuvi-overcome, ndo hivyo nikaweza kufanikiwa.

Ratiba yako ya siku ulipokuwa shule kwa ujumla wake ilikuwa vipi na muda gani ulikuwa unajisomea?

Asubuhi nilikuwa naamka mapema kabla ya time table ya shule haijaanza kwa sababu tunatakiwa tuamke mapema kwenda misa kwenye saa kumi na moja hivi. Kwa hiyo naamkaga kwenye saa tisa najiandaa naenda darasani kwa sababu siwezi kusoma usiku kwa sababu usiku nakuwa nimechoka, kwa hiyo my extra time inakuwa asubuhi ambako I’m still fresh. 
Nasoma then ikifika muda wa misa naenda kusali. Nikitoka kusali kuna kazi ndogo ndogo za kufanya kujiandaa na time table ya school and all that. And my free time ile mchana nikitoka darasani kuanzia saa nane, nakuwa nimepanga nini natakiwa nifanye, ni somo gani natakiwa kulisoma at that time ambapo ni saa nane mpaka saa kumi na nusu. Ambapo ni muda wa concentration, kama kuna kitu ambacho sijaelewa naenda kuwafuata waalimu kwa sababu wanakuwa wapo at that time. And kuna some free time kama ile break time, ni kuanzia saa nne na dakika 40 mpaka saa tano na robo, pale hauwezi kusema unatake breakfast all the time, unatake breakfast for a short time halafu nyingine inabaki unaweza kufanya maswali matano ya physics. Yaani every little time ambayo unaweza kuipata, you don’t let it go to waste tu, una-utilize.
Marafiki ulionao wanaweza kusaidia kukupandisha au kukushusha. Wewe ulikuwa na marafiki wa aina gani? 
Marafiki wangu nimewachagua kwa category..yeah (anacheka), ikifika muda wa kusoma nakuwa na mtu ambaye najua atanisaidia, kwa hiyo nilikuwa na rafiki yangu anaitwa Sarafina amekuwa wa nne. Alikuwa ananiinfluence sana kusoma, huyo ni wakati wa kusoma, kwenye academics namfata yeye.

Ikifika wakati wa social siwezi kumfata sarafina kwa sababu she is not that social, yeye yuko kama mimi we are not that social, kwa hiyo ninaye social friend. Pia ikifika muda wa kuspend, I have an economical friend. Ambaye I’m sure nikikaa nae nikiwa naspend siwezi kwenda beyond my budget. Kwamba siwezi kufulia. Kwamba we are all in the same status, same friends, yeah.
Ni kitu gani kilikuwa kinakuboa sana shuleni na kukunyima furaha muda mwingine?
Kitu ambacho kilikuwa kinaniboa sana, ikifika wakati ambapo kwa mfano watu wachache kwenye darasa wamefanya kosa halafu sasa mnakuwa included as a whole class halafu mnapata adhabu. Hiyo adhabu directly itaharibu time table yangu ya kusoma. Kwa hiyo badala ya kusoma nafikiria ningekuwa nasoma physics, I’m either slashing an area..yaani hiyo ilikuwa inaniboa sana yaani.
Ulishawahi kuitwa ‘Msongo’ au majina kama hayo? Ulikuwa unaichukuliaje na je, ilikutenga na marafiki zako? 
Yeah, msongo…kauzu. Yeah mimi naipenda hivyo kwa sababu nafanya nachotakiwa kufanya ambacho ni kusoma. Hiyo haikunitenganisha na marafiki zangu. 

Vuta taswira, je, ingetokea ukapata division Zero na kuwa wa mwisho Tanzania nzima ungefanyaje? Na unawashauri nini waliofeli kwa kiasi hicho?
Kama ningepata zero, kwanza ningefikiria…na ningekuwa very disappointed kweli, lakini pia ningefikiria kuhusu kujipa second chance, ningeenda kusoma tena. 
Kwa waliofeli ningependa kuwashauri wasikate tamaa hata kidogo and wajipe second chance. Kwa wengine pia ambao wana vipaji vyao wanaweza kuviendeleza. But pia kwa kuwa elimu ni muhimu..ku-reseat pia ingekuwa ana option.
Robina Nicholaus ni msichana wa aina gani?

Robina ni mtu mkimya lakini mcheshi pia. Nisingependa nikae na mtu halafu nikawa kimya just because ni mkimya... I will try kuchekesha, and of course I’m funny anyway.

ANGALIA MATOKEO.RATIBA NA MSMAMO WA LIGI KUU YA ENGLAND BPL BAADA YALIVERPOOL YAKWEA NAFASI YA PILI!


MATOKEO:BPL2013LOGO
Jumamosi Machi 1
Everton 1 West Ham 0
Fulham 1 Chelsea 3
Hull 1 Newcastle 4
Stoke 1 Arsenal 0
Southampton 0 Liverpool 3

Wakicheza Uwanja wa Saint Mary, Liverpool wameichapa Southampton Bao 3-0 na kukwea hadi Nafasi ya Pili kutoka Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England.
Bao za Liverpool zilifungwa na Luis Suarez, Dakika ya 16, Raheem Sterling Dakika ya 58 na Penati ya Dakika za Majeruhi ya Steven Gerrard baada ya Suarez kuangushwa na Jose Fonte.
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumapili Machi 2
1930 Aston Villa v Norwich
1930 Swansea v Crystal Palace
1930 Tottenham v Cardiff

MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Chelsea
28
30
63
2
Liverpool
28
38
59
3
Arsenal
28
24
59
4
Man City
26
42
57
5
Tottenham
27
3
50
6
Everton
27
11
48
7
Man Utd
27
12
45
8
Newcastle
28
-2
43
9
Southampton
29
1
39
10
West Ham
28
-4
31
11
Hull
28
-5
30
12
Stoke
28
-14
30
13
Swansea
27
-4
28
14
Aston Villa
27
-10
28
15
Norwich
27
-19
28
16
Crystal Palace
26
-18
26
17
West Brom
27
-8
25
18
Sunderland
26
-16
24
19
Cardiff
27
-29
22
20
Fulham
28
-34
21
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Machi 8
1545 West Brom v Man United
1800 Cardiff v Fulham
1800 Crystal Palace v Southampton
1800 Norwich v Stoke
1800 West Ham v Hull
2030 Chelsea v Tottenham

HUYU NDIYE ALEN HALILOVIC - MRITHI WA MESSI NDANI YA FC BARCELONA - AZITOSA SPURS NA MAN UNITED AENDA CAM NOU


Baada ya miezi kadhaa ya tetesi juu ya atma yake itakuwa wai, kinda la klabu ya Dinamo Zagreb mwenye miaka 17 Alen Halilovic hatimaye ameamua timu ya kujiunga na kucheza soka na uamuzi aliochukua ni habari mbaya kwa vilabu vya Arsenal, Man United na Tottenham.

Badala ya kuchagua kujiunga na vilabu hivyo kutoka EPL, usiku wa jana kiungo huyo kinda wa timu ya taifa ya Croatia aliandika kupitia akaunti ya instagram na kuthibitisha kwamba anajiunga na klabu bingwa ya Spain FC Barcelona.

Halilovic, ambaye ni kiungo mshambuliaji amekuwa akifuatiliwa na vilabu vingi vya bara la ulaya kutokana na kipaji kikubwa alichokionyesha kiasi cha kuitwa 'New Messi'

Kupitia akaunti yake ya Instagram aliandika: Thanks Dinamo Zagreb for everything!!My first club and biggest love!!Now is time to move on to Barcelona 

Halilovic anategemewa kujiunga na Barcelona mwishoni mwa msimu huu na ataanza kuitumikia Barcelona B.
  ANGALIA UWEZO WAKE JE? ANASTAHILI KUTWA MESSI MPYA !!!

ANGLIA PICHA 7 KUHUSU MAUAJI YALIYOTOKEA KWENYE KITUO CHA TRENI NCHINI CHINA

 
1 
Taarifa iliyosambaa kwenye mitandao mbalimbali inasema kuwa kuna kundi la watu waliokuwa na visu limewashambulia na kuua watu 28 huku zaidi ya 100 wakijeruhiwa katika kituo cha treni kilichopo mjini Kunming nchini China.
6 
Mashahidi wa tukio hilo wamesema kuwa washambuliaji hao walivalia nguo nyeusi na kuwavamia abiria waliokuwa wakingojea treni na kuwakatakata huku wengine wakiwadunga visu wale hasa walioshindwa kukimbia kwa kasi.
3 
Polisi wamefanikiwa kuwauwa washambuliaji watano kati ya kumi waliofanya shambulio hilo,Shirika la habari la Xhinua limewalaumu watu wanaopigania kujitenga katika mkoa wa Shinjiang kwa tukio hilo,ulinzi bado umeimarishwa eneo la tukio.
2
4
5
7

HATIMAYE SIMBA YASHINDA MECHI YAKE DHIDI RUVUSHOOTING KWA BAO 3-2 LEO

 Simba mpyaHatimaye baada ya vipigo vitatu na sare mbili klabu ya Simba leo imepata ushindi katika mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Vodacom.
Mchezo wa uliochezwa katika dimba la uwanja wa taifa baina ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting umeisha kwa matokeo ya 3-2.
Alikuwa yule yule bwana Amis Tambwe ambaye alianza kufungua kitabu cha mabao kwa upande wa Simba mwanzoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya kuongeza la pili mwishoni mwa kipindi cha pili. Mpaka mpira unaenda mapumziko Simba walikuwa mbele kwa mabao mawili kwa nunge.
Kipindi cha Ruvu Shooting walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika 70, dakika mbili baadae Haruna Chanongo akaongeza bao la 3 kwa Simba. Dakika ya 83 Ruvu wakafunga bao la pili kwa penati baada ya beki Joseph Owino kuunawa mpira kwenye boksi la penati. Ruvu waliendelea kulisakama lango la Simba lakini bahati haikuwa yao na mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalikuwa 3-2 – Simba wakitoka na ushindi.