Mwanamke anayesadikiwa kuwa mshirikina na kukutwa na mali za wizi
Mali zinazosadikiwa kuwa za wizi zilizokamatwa
Jeshi la Polisi likiondoka na Mali zinazodhaniwa kuwa za wizi
Orodha ya mali iliyokamatwa
JESHI la Polisi Mkoa Mbeya limejikuta likitumia zaidi ya masaa manne kumtafuta mtuhumiwa wa ushirikina bila mafanikio kutokana na mtu huyo kujigeuza Kunguru.
Tukio hilo la ajabu lilitokea juzi kuanzia majira ya saa nne asubuhi ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kusaidiwa na wananchi kumkamata Mwanamke mmoja aliyekuwa amejificha kiushirikina kwa kujigeuza kunguru katika mtaa wa Mapelele kata ya Ilemi jijini Mbeya
Tukio hilo lilitokea baada ya polisi kufika nyumbani kwa mwanamke huyo ambaye anatuhumiwa kumjeruhi vibaya jirani yake aitwaye Anitha Simon kwa kipigo kwa madai ya kumuibia ndala jozi mbili aina ya yeboyebo.
Akizungumza katika eneo la tukio, mtoto wa kaka wa mtuhumiwa ambaye ndiye aliyefanikisha zoezi la kumkamata ,Venance Mwalindile alidai yeye ni chifu katika ukoo wao na kwamba anakerwa na tabia za shangazi yake huyo.
“Nimeamua kufanya hivi kumuumbua shangazi kwani nimekerwa sana na hizi tabia na ndiyo maana nimejitolea kuwasaidia polisi mkamata ili sheria ichukue mkondo wake”alisema Mwalindile.
Hata hivyo Mwalindile alisema kuwa ilikuwa ni kazi ngumu kwake kumkamata mama huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 45 hadi 50 kwani akiwa amejificha chumbani alijibadilisha kuwa kunguru ambapo katika mapambano makali alifanikiwa kumkamata na kumnyonga kunguru huyo ndipo aliporudi katika hali yake ya kawaida na kuwakabidhi Polisi.
Akizungumzia tukio hilo ambalo lilijaza umati wa watu waliokuwa wakishuhudia,Mwenyekiti wa mtaa jirani wa Mwafute Kata ya Ilemi, Charles Kasyupa alisema kuwa wamekuwa na vikao vya mara kwa mara kuhusiana na matukio ya wizi na ugomvi wa mtuhumiwa huyo lakini kumekuwa hakuna mwafaka.
Baada ya kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Polisi walifanya upekuzi katika nyumba yake na kufaninikiwa kuvikuta vitu kadhaa vinavyodhaniwa kuwa ni vya wizi vikiwemo Radio,magodoro,TV,madishi ya kuogea,viti vya Kanisani,mafuta,sukari,spika za Kanisani,nguo mbalimbali na vitu vingine ambavyo idadi na thamani yake haikuweza kufahamika mara moja.
Aidha baada ya kumaliza kupekua nyumba hiyo majira ya saa moja jioni kwa hofu ya usalama wa wananchi waliokuwa na hasira kali Jeshi la Polisi lililazimika kusomba mali zilizokutwa katika Nyumba ya mtuhumiwa.
Jeshi hilo lilitumia gari za Polisi aina ya Land cruser zilirudia mara sita kubeba mali hiyo na kuipeleka Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati kwa ajili ya utambuzi wa mali hiyo wakiwa wameongozana na Mwenyekiti wa mtaa wa Mapelele Jitihada Mwaijulu.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amekiri kukamatwa kwa mwanamke huyo lakini Jeshi lake bado linaendelea na uchunguzi na atatoa ufafanuzi baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tukio hilo.
Via>>Mbeya yetu blog
0 comments:
Post a Comment