Cristiano Ronaldo amerudi tena kwenye headlines baada ya weekend kufunga goli nne peke yake katika ushindi wa goli 7-1 dhidi ya klabu ya Celta Vigo, goli hizo hizo alizofunga Ronaldo hakuzichukulia poa kocha wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane.
Zidane ambaye amejiunga na timu A ya Real Madrid kuchukua nafasi ya Raphael Benitez, amezungumza na kusisitiza kwa mara nyingine tena kuwa Real Madridwanahitaji kuendelea kumbakiza kikosini Cristiano Ronaldo ambaye alikuwa akihusishwa kutaka kuhama.
Baada ya Ronaldo kufunga goli nne peke yake dhidi ya Celta Vigo, anakuwa mchezaji wa kwanza Ulaya kufunga jumla ya goli 350 akiwa na klabu moja kwa muda mfupi. Hii sio mara ya kwanza Zidane anazungumza kuhusu kauli za kumuhitaji Ronaldo, kitu ambacho kinahisiwa kuwa huenda akawa ana mipango ya kuondoka.
0 comments:
Post a Comment