>>SPURS KUANZA NA BORUSSIA DORTMUND!
ALHAMISI Usiku huko Anfield, Mahasimu wakubwa wa England, Liverpool na Manchester United, watapambana kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI.
Hii ni Mechi ya 195 kwa Klabu hizi kupambana lakini hii itakuwa ni mara ya kwanza kwao kupambana kwenye Mashindano ya UEFA Barani Ulaya.
Licha ya Kombe hilo kudharauliwa na Wadau na kutukuzwa UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, lakini kwa Klabu hizi ambazo zipo Nafasi za 6, Man United, na ya 7, Liverpool, kwenye Ligi Kuu England na hivyo kupunguza nafasi zao za kucheza UCL Msimu ujao, kulitwaa Kombe hili kutawapa fursa ya kucheza UCL Msimu ujao.
Uso kwa Uso
-Hii ni mara ya kwanza kwa Klabu hizi kukutana kwenye Mashindano ya UEFA.
-Liverpool na Man United zimekutana mara 166 kwenye Ligi na Man United kushinda mara 67 na Liverpool mara 55
-Kwenye Vikombe huko England wamecheza mara 18 huku Man United wakiongoza kwa kushinda mara 11 na Liverpool mara 7
-Katika Mechi 4 zilizopita, Man United wameshinda mara zote chini ya Meneja wao Louis van Gaal
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Liverpool: Mignolet; Flanagan, Lovren, Touré, Clyne; Henderson, Can, Milner; Coutinho, Sturridge, Firmino.
Majeruhi: Gomez, Ings, Lucas, Rossiter
Manchester United: De Gea; Darmian, Smalling, Blind, Rojo; Carrick, Schneiderlin, Mata, Herrera, Memphis; Martial.
Majeruhi: Keane, Rooney, Shaw, Young
REFA: Carlos Velasco Carballo (Spain)
EUROPA LEAGUE - Raundi ya Mtoano ya Timu 16
**Saa za Bongo
2100 FC Shakhtar Donetsk v RSC Anderlecht
2100 FC Basel 1893 v Sevilla FC
2100 Borussia Dortmund v Tottenham Hotspur
2100 Fenerbahce v SC Braga
2305 Villarreal CF v Bayer 04 Leverkusen
2305 Athletic Club v Valencia CF
2305 Liverpool v Manchester United
2305 Sparta Prague v Lazio
**Marudiano Alhamisi Machi 17
KALENDA
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Kwanza: 10 Machi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswisi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswisi
0 comments:
Post a Comment