Wednesday, 9 March 2016

MCHEZAJI WA ZAMANI ARSENAL ASAINI SUNDERLAND, MASHABIKI ARSENAL WAMTAKA WENGER AAGE KLABUNI!


EBOUEWAKATI Sunderland ikimsaini Beki wa zamani wa Arsenal Emmanuel Eboue, Mashabiki wa Arsenal wamemtaka Meneja wao Arsene Wenger atimke Klabuni hapo.
Eboue, Fulbeki kutoka Ivory Coast mwenye Miaka 32, alikuwa Mchezaji Huru baada ya kuondoka Galatasaray ya Uturuki tangu mwanzoni mwa Msimu.
Akiwa na Galatasaray kuanzia 2011, Eboue alifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Nchi hiyo mara 3 pamoja na Makombe mengine Matano.
Eboue alikuwa na Arsenal kwa Misimu Minane baada ya kutua hapo Mwaka 2004 kutoka Klabu ya Belgium Beveren na kuhamia Galatasaray Mwaka 2011.
Sunderland imempa Eboue, aliekuwa akifanya Mazoezi na Klabu hiyo tangu Februari, Mkataba wa muda mfupi ambao utamalizika mwishoni mwa Msimu.
WENGER-BAIBAI
Huko KC Stadium Jumanne Usiku wakati Arsenal ikiifunga Hull City Bao 4-0 kwenye Mechi ya Marudiano ya Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP na kutinga Robo Fainali ya Kombe hilo ambalo wao ni Mabingwa Watetezi, Mashabiki wa Timu hiyo walifunua na kuanika juu Bango kubwa.
Bango hilo lilisomeka: “Arsene, asante sana kwa kumbukumbu lakini sasa ni wakati wa kusema Kwaheri.”
Kitendo hicho kimeonyesha kuwa baadhi ya Mashabiki wa Arsenal wamemchoka Arsene Wenger ambae hajatwaa Ubingwa wa England tangu 2004 na Msimu huu walianza kwa kuonyesha wamo mbioni lakini tangu 2016 ianze wameporomoka na sasa wapo Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 8 nyuma ya Vinara Leicester City huku Mechi zikibaki 9.
Akihojiwa kuhusu Bango hilo, Wenger alisema: “Hakuna kitu kinanivunja moyo, nafanya kazi yangu. Angalia Historia ya Klabu na utaona sina kitu cha kuogopa!”

0 comments: