Tuesday, 1 March 2016

Rosemary Odinga: Nilikosea, Olduvai Gorge iko TANZANIA

  •  
Image caption'Nilikosea, nawaomba radhi watanzania' ,Rosemary Odinga
Mwanawe aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary, amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya ilhali liko Tanzania.
''Bonde la Oldupai ama Olduvai liko Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa nikihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New York Marekani(International Young Leaders Assembly).
''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''.
''Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile eneo la Kajiado.
Image caption''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''.
Nisemeje ,,nawaombeni radhi Watanzania.
Olduvai Gorge iko salama wala haijanyakuliwa na kenya
'Katika ile hali ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika mashariki ndio kitovu cha ubinadamu'' alisema bi Odinga kupitia mtandao wake wa Instagram.
Tamko lake kuhusiana na bonde hilo la Olduvai (Oldupai) lililoko Tanzania lilihusiana na mada ya siku hiyo.
Image caption'Katika ile hali ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika mashariki ndio kitovu cha ubinadamu'' alisema bi Odinga
Olduvai ndiko kulikopatikana vifaa vilivyotumika na watangulizi wa binadamu yapata miaka milioni moja na laki sita iliyopita (milioni 1.6)
Bi Rosemary aliomba radhi baada ya kuzomewa na maelfu ya watu kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook Instagram na Twitter wakidai aliwapotosha hadhira yake na haswa ulimwengu kwa kusema eti Olduvai ipo Kenya.
Mbunge Zitto Kabwe alikuwa amechangia mada kwa kusema kuwa Tanzania sharti izinadi vivutio vyake vya kitalii ilikuzima dhana potovu.
Aidha alidai kuwa watu wanafikiria kuwa mlima kilimanjaro uko Kenya ilahali ukweli halisi upo Tanzania sawa na mwanamuziki nyota Diamond Platnumz ambaye ni Mtanzania.

0 comments: