Saturday, 5 March 2016

Mtanzania Single Mtambalike, Ashinda Tuzo ya Filamu Bora Ya Kiswahili, Afrika!.


Star wa Bongo Movie wa Kitanzania, Single Mtanzania, Single Mtambalike, "Richie Rich", meshinda tuzo ya filamu bora ya Kiswahili katika tuzo za filamu za Afrika huko Nigeria usiku huu.

Richie ameshinda kupitia filamu yake ya Kitendawili aliyocheza na Mona Lisa na kutengenezwa na kampuni ya Proin, ameshinda katika kipengele cha ‘Best Indigenous Language Movie/TV Series/ Swahili.’

Kwenye tuzo hizo, waigizaji Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Single ‘Richie’ Mtambalike na Yvonne ‘Monalisa’ Cherry wanawania Tuzo.

Lulu alitajwa kuwania tuzo hizo kwenye kipengele cha Best Movie – East Africa kupitia filamu yake ya Mapenzi ya Mungu pamoja na Monalisa kupitia Daddy’s Wedding.

JF pia ipo ukumbini hapo ikiwakilishwa na mwana jf Le Mutuz, hope soon ataripoti.

Mwanamuziki wa Tanzania, Ali Kiba atatumbuiza katika tuzo hizo.

Tuzo hizo kubwa za filamu Afrika, zitaoneshwa live kupitia channel ya Africa Magic na Maisha Magic East kwenye DSTV.

My Take.
Sisi wengine huwa hatuangalii bongo movies kwa sababu ya mambo ya hovyo hovyo na ujinga ujinga mwingi, lakini kitendo cha movi za kibongo kuanza kushinda tuzo za kimataifa, labda kutaturudishia attention yetu kurudi kutazama Bongo Movies, tangu alipofariki Kanumba, kwa wengine wetu, alikufa na Bongo Movie, landa sasa Kanumba kapata mrithi, hivyo kupandisha tena chati ya bongo movies!.

Hongera Richie Rich!.

0 comments: