Wednesday, 9 March 2016

Habari Mbaya Kwa Wapaka Poda...Poda Zadaiwa Kusababisha Kansa



Kuna ne.no moja tu linaloweza kusemwa kwa sasa, kuwa tumekwisha, baada ya kubainika kuwa poda iliyotumika kwa miaka mingi nchini, ambayo ni maarufu kama Johnson’s Baby Powder inadaiwa kusababisha kansa ya kizazi inayoleta maafa ikiwemo vifo, Risasi Mchanganyiko lina taarifa kamili.

Taarifa zilizopatikana kupitia mitandao ya internet, zinadai kwamba kampuni inayotengeneza poda hiyo ya Johnson and Johnson ya Marekani, Februari 25, mwaka huu ilihukumiwa kulipa faini ya kiasi cha dola milioni 72 (sawa na shilingi bilioni 144) katika Mahakama ya Missouri kama fidia kwa mwanamke mmoja aliyefariki dunia kwa kansa ya kizazi iliyotokana na matumizi ya vipodozi hivyo.

Familia ya mwanamke huyo, Jacqueline Fox ilitakiwa kulipwa kiasi hicho cha fedha baada ya mahakama kuridhika kuwa ugonjwa na kifo chake kilitokana na matumizi ya vipodozi hivyo kwa zaidi ya miaka 35, akitumia poda pamoja na losheni ya bidhaa hiyo.

Kampuni hiyo ya Johnson & Johnson ilikabiliwa na tuhuma kwamba kwa miongo mingi, kwa lengo la kufanya biashara zaidi, haikuwaonya wateja wake kuwa miongoni mwa viungo vinavyotengeneza bidhaa hiyo, vinasababisha kansa. Zaidi ya kesi 1000 zimefunguliwa huko Missouri na 200 New Jersey, zote zikiilalamikia bidhaa hiyo.

0 comments: