MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Friday, 20 November 2015

Licha ya kuto kubali huu ndio msimamo mbaya kwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho …

Kocha wa klabu ya Chelsea ya Uingereza Jose Mourinho bado yupo katika wakati mgumu wa kuhakikisha timu yake inafanya vizuri licha ya kuwa matumaini ya kutetea taji lake la Ligi Kuu Uingereza msimu huu yamepotea kwa kiasi kikubwa, Mourinho kwa sasa anatajwa kuwa hatarini kupoteza kibarua chake kutokana na mwenendo mbovu wa kikosi chake.
November 20 Jose Mourinho amefunguka na kueleza msimamo wake kuhusu dirisha dogo la usajili la mwezi January, wengi huenda wakafikiri kuwa kocha huyo atasajili mwezi January ili kuboresha kikosi chake lakini ana msimamo tofauti kidogo na wengi wanavyofikiria, Mourinho hana mpango wa kumuomba mmiliki wa ChelseaRoman Abramovich kutenga fungu la usajili.
Walsall-vs-Chelsea
“Sitaomba uongozi ufanye chochote katika dirisha la usajili la mwezi January nakiamini kikosi changu, sihitaji klabu itumie fedha kwa ajili ya usajili mwezi January, nafikiri tutacheza vizuri na kupata matokeo, tunaamini mambo mazuri yapo kwa ajili yetu” >>>Jose Mourinho
Klabu ya Chelsea katika dirisha la usajili la mwezi August iliwasajili  PedroAbdul Baba Rahman na Asmir Begovic pamoja na kumchukua kwa mkopo Radamel Falcao lakini hadi sasa imecheza mechi 12 na kupoteza mechi 7, imeshinda 3 na kutoa sare 2 na ipo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza kwa sasa kabla ya Jumamosi ya November 21 kucheza mechi yake ya 13 dhidi ya Norwich City.

kumbe Waziri mkuu kassim majaliwa alisha wahikuwa kocha analessen b ya caf


Healines kwa siku ya November 18 ni juu ya nani atakuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli November 19 kupendekeza jina la waziri mkuu Kassim Majaliwa Kassim ambaye ataapishwa Ijumaa ya November 20 Dodoma.


Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa sio jina geni katika medani za soka, kama unakumbuka vizuri Kassim Majaliwa aliwahi kuwa kocha wa mpira wa miguu na aliwahi kuifundisha klabu ya Singida United, kazi ya ukocha kwa waziri mkuu huyo haikuwa ya kubahatisha bali alikuwa akitambulika rasmi kama kocha mwenye leseni daraja B na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF).


Rais wa TFF Jamal Malinzi akimpongeza Mh Majaliwa

Afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga amezungumzia na kumpongeza Mh Kassim Majaliwa

“Uongozi wa Azam FC na bodi ya uongozi ya Azam FC inampogeza Kassim Majaliwa kwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini kwa wale ambao hawafahamu Mh Majaliwa aliwahi kuwa kocha wa klabu ya Singida United miaka ya nyuma ana leseni B ya ukocha kutoka kwa shirikisho la soka barani Afrika CAF hivyo tumefuraishwa kwa yeye kushika nafasi hiyo” >>> Jafari Idd

JE Unahisi nini ? Kitendo cha ZITTO KABWE Kubaki Bungeni Wakati Wabunge wa Upinzani Wote Wametoka Nje ?

 
JE Unahisi Kitendo cha ZITTO KABWE Kubaki Bungeni Wakati Wabunge wa Upinzani Wote Wametoka Nje Kushinikiza Maalim Seif Atangazwe Mshindi wa Urais Zanzibar?

Magufuli Awaita UKAWA ‘Watoto’.....baada ya kureta fujo Spika Awapa Onyo Kali,


Rais John Magufuli amelaani vikali kitendo cha Wabunge wa Vyama vya Upinzani kuzomea leo bungeni.

Rais Magufuli ameeleza kuwa tabia iliyofanywa na wabunge hao inaonesha jinsi ambavyo hawajakomaa kisiasa na kuwaita watoto huku akimpongeza Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa kuendelea kubaki Bungeni.

“Ndio maana nimempongeza sana Mheshimiwa Zitto. Mheshimiwa zitto umekomaa na naamini hata wana CCM kule Kigoma walikuchagua,”alisema rais Magufuli.

“Mmeona tuna kazi kubwa, bado tuna watoto wengi. Tuendelee kuwavumilia, nadhani na watanzania wameona,” aliongeza.

Aliwataka wabunge wote kusimama pamoja bila kujali itikadi zao za vyama na kuwasisitiza kuwa wanapaswa kuhakikisha kuwa Bunge la 11 linakuwa bunge la kihistoria na kuacha masuala ya kupigana vijembe, kuzomeana na kutoka nje.

Kwa upande wake Spika wa Bunge hilo, Job Ndugai alimuomba radhi rais Magufuli na Shein kwa kile kilichoanywa na wabunge wa Ukawa huku akiahidi kuwa hali hiyo haitajirudia tena.

Ndugai aliwaonya wabunge kuwa kitendo kilichofanywa ni cha aibu hivyo hatawavumilia tena na kwamba wabunge wanaweza kumfanya akawa Spika mpole ama kumfanya awe Spika ‘mbabe’.

“Mnaweza kunifanya nikawa Spika mbabe sana… leo iwe mwisho. Ni kwa sababu wazee hawa walikuwepo. Lakini wazee hao wasipokuwepo, wakifanya tena tabia hii, basi… nisiseme sana,” alisema.
 

Thursday, 19 November 2015

WAtanzania Rais Kikwete Alishindwa Haya, JE John P. Magufuli Ataweza?

 
Rais Magufuli na Jakaya Kikwete
Maisha bora kwa kila mtu ni sera ya CCM, ambayo kiukweli ni nzuri sana na inaleta matumaini kama ikitekelezwa, ila utelezaji wa sera hii unapambana na vikwazo vingi ambavyo sijui rais John Pombe Magufuli ataviweza, maana mtangulizi wake Jakaya Mrisho Kikwete vilimshinda kabisa, vikwazo vikuu vya utekelezaji wa sera hii ya maisha bora kwa kila mtu baadhi ni vifuatavyo:-

1.Watumishi wa serikali, hasa wa halmashauri siyo waaminifu (yaani ni one hundred percent corrupt), kwa sababu kutekeleza sera hii serikali kuu inatuma hela nyingi sana kwenye halimashauri za wilaya ambako watu ndiko walipo ili kutekeleleza miradi mbali ya maendeleo. Kule pesa inakutana na watumishi ambao ni corrupt, wanashambulia hela zote za miradi kwa kujenga mabangaloo, wananunua posh cars kwa hiyo miradi ya maendeleo inakwama automatically na sera ya maisha bora kwa kila mtu nayoinakwama.


2.Watumishi niliowataja hapo juu kwa mujibu wa utaratibu wanasimamiwa na madiwani waliopo katika halimashauri hizo, sasa madiwani hao uwezo wa kuwasimamia vizuri hawana kwa sababu elimu zao wengine ni duni sana, hasa madiwani wa viti maalumu. Katika halmashauri nyingi madiwani hawa ni mizigo tu, kwa hiyo watumishi ambao sio waaminifu wanautumia vizuri mwanya huu kuikwamisha sera ya maisha bora kwa kila mtu, kwa kuwalambisha hela kidogo madiwani hawa halafu wenyewe wanakwapua nyingi.


3.Serikali yenyewe kwa ujumla ni dhaifu, inashindwa kabisa kuwachukulia hatua wabadhirifu hawa inaishia tu kuwahamisha toka halmashauri moja kwenda ingine.


4.Idara ya usalama wa taifa(TISS) nayo imezorota sana, kule wanawaona kabisa watumishi ambao siyo waaminifu wanavyofanya wananunua magari mawili mawili na kujenga nyumba kali ndani ya mwaka mmoja tu wa kuajiriwa lakini hawapeleki habari kunakohusika, wanashughulika na mambo yasiyokuwa na tija kama kufuatilia mikutano ya CHADEMA.

Mh. John Pombe Magufuli akiweza kuyadhibiti hayo hapo juu, basi maisha bora kwa kila mtu inawezekana.

By laurent Msembeyu/JF

Kyela yalipuka kwa vifijo baada ya Mwakyembe kukosa Uwaziri mkuu


Picha sio Halisi
Kyela mjini imelipuka kwa shangwe baada ya kusikia mbunge wao hajachaguliwa kuwa waziri mkuu.
Mwakyembe alitumia gia ya kutumwa na Magufuli ili apewe uwaziri mkuu ili kushinda kura ya maoni CCM baada ya kubebwa na viongozi wa chama hapo wilayani kwa ahadi za kumpa Mwenyekiti ukuu wa wilaya akiwa waziri mkuu.

Kwenye uchaguzi mkuu aliendeleza uongo wake kwa kuwaambia wananchi katumwa na Magufuli na Kyela itapata waziri mkuu. Mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na mkuu wa polisi wakatumia nguvu kulazimisha ushindi. Kesi ya ushindi wake iko mahakamani Mbeya. Inasemekana mkuu wa wilaya aliahidiwa cheo cha mkuu wa mkoa.

Mwakyembe ameingia kwenye mgogoro mkubwa na vijana wilayani hapa baada ya kutumia visasi kuifungia redio ya Kyela fm ambayo inamilikiwa na mpinzani wake kisiasa na ambayo inasikilizwa sana na wakazi wa Kyela. Pia vijana waliokuwa wanapinga ushindi wake walipigwa vibaya na polisi na wengine mpaka kupewa vilema.

Mwakyembe ambaye wilayani Kyela kapoteza umaarufu kabisa baada ya utendaji wake kuwa mbovu mno. Ana sifa kubwa kitaifa wakati wilayani kwake kashindwa kutatua hata matatizo madogo. Siku hizi kapachikwa jina la Nkurunziza baada ya kuona anang'ang'ania kubaki madarakani.

chanzo kitenge blog

Mama Amchoma Mwanaye Kwa Maji Moto Baada ya Kumtuhumu Ameiba Nyama Jikoni

 
 Polisi mkoa wa Mara inamshikilia mwananke mmoja (jina tunalo) mkazi wa Bweri Manispaa ya Musoma kwa kosa la kumchoma mtoto wake mwenye miaka minne, kwa maji ya moto, mikono yote miwili baada ya kumtuhumu kuwa ameiba nyama jikoni.

Mama huyo alikamatwa Novemba 14 saa nne asubuhi katika eneo la Morembe kata ya Bweri mjini Musoma baada ya Polisi kufika nyumbani kwake kumkamata kwa kosa jingine la kumkatakata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili Kabula Rubeni (32) akimtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, ACP Alex Philip Kallangi alidai kuwa siku ya tukio hilo la kumchoma moto mtoto huyo, mama yake mzazi alikuwa amepika nyama jikoni na baadaye alikwenda kuchota maji.

Kamanda Kallangi alidai baada ya mama huyo kurudi alimkuta mwanaye anakula nyama ndipo alishikwa na hasira na kuanza kumchapa sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha akachukua mikono yote miwili na kumchoma kwa maji ya moto.

Baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama, mama huyo alianza kumtibu mtoto huyo kwa siri hapo nyumbani kwa dawa za kienyeji bila majirani kufahamu kilichokuwa kikiendelea nyumbani kwa mama huyo.

Kamanda Kallangi alieleza kuwa kilichosababisha kufahamika kwa taarifa hizo, ni baada ya Kabula aliyekuwa ameshambuliwa kwa mapanga na mwanamke huyo kwenda polisi kutoa taarifa ya kushambuliwa.

Kallangi alieleza kwamba polisi walipofika nyumbani kwake ndipo walipewa taarifa za mtoto huyo kujeruhiwa kwa kuchomwa moto. Kutokana na tukio hilo polisi hao, kwa kushirikiana na maofisa ustawi wa jamii na kituo cha ushauri cha Jipe Moyo walimchukua mtoto huyo na kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara kwa matibabu na kisha kupelekwa Jipe Moyo anakoishi hadi sasa kwa uangalizi zaidi.

Kallangi alisema mtuhumiwa huyo yupo kituoni na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni kujibu mashtaka yanayomkabili.

Ofisa Ustawi wa Jamii Musoma, Vedastus George aliwataka wazazi na walezi kuzuia hasira zao pale watoto wanapowakosea na hata wanapowaadhibu wawe makini ili waziwaumize kama alivyofanyiwa mtoto huyo.

Watanzania Waishio Uingereza Wameandamana Kutokana na Mgogoro Unaoendelea ZANZIBAR

 

Leo muda wa 10:00 Kulikuwa na maandamano  London, downing street, madhumuni ni kuishukuru serikali ya UK kwa juhudi ulio chukua juu ya mkwamo wa kisiasa zanzibar, na pia kuomba ichukue hatua zaidi ili wazanzibari na watanzania kwa ujumla tupatiwe haki yetu ya msingi tulio fanya tarehe 25 October 2015.








Waziri Mkuu Mteule Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa kuapishwa Leo Saa Nne

 


Sherehe za kumuapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu Mteule zitafanyika katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Novemba, 2015 kuanzia saa 4.00 Asubuhi.
 

Sherehe hizo zinafanyika siku moja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha jina lake kwa kura nyingi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia uteuzi uliofanywa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 

Kwa mujibu wa ratiba ya sherehe hizo, Wageni waalikwa wote wanapaswa kuwasili katika Ikulu ya Chamwino kuanzia majira ya saa mbili asubuhi. 

Sherehe hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Marais Wastaafu, Mawaziri Wakuu wastaafu na waheshimiwa wabunge. 
Imetolewa na Idara ya Habari MAELEZO 
19 Novemba, 2015

Ukawa Wazua Hofu, bungeni dodoma Polisi Wajipanga Kuwakabiri

 


Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umezua hofu kubwa bungeni kutokana na hali ya kutangaza msimamo wao wa kutokukubaliana na Rais John Magufuli kulihutubia Bunge.

Jana umoja huo ulitangaza rasmi kwamba umemwandikia spika barua ya kuhoji uhalali wa Rais kulihutubua bunge wakati uchaguzi wa Zanzibar umefutwa na kulifanya taifa la Zanzibar kutokuwa na rais.

Hali hiyo imeifanya serikali kuwa na hofu kubwa ambayo inaonekana kuwatesa viongozi wa CCM siku ya leo iwapo msimamo wao utaendelea kuwa huo.

Ili kuonesha kuwa hofu ni kubwa leo kuanzia asubuhi, maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma hususani katika maeneo ya bunge kulikuwepo na magari ya polisi ya maji ya kuwasha.

Mbali na magari ya polisi yenye maji ya kuwasha yakiwa yameegeshwa katika maeneo mbalimbali ya bunge, magari mengine ya jeshi la polisi yalionekana kurandaranda huku yakiwa yamesheheni askari.

Hali hiyo imetafsiriwa na baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma kuwa ni njia pekee ya kuwatishia watanzania kutokana na tangazo la Ukawa la kutomtaka Rais John Magufuli kulihutubia Bunge.

Lipumba Amtahadharisha Rais Magufuli Kuhusu Dr. Shein Kuhudhuria Bungeni Leo



Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amemtaka Rais John Magufuli kuishauri Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar kabla ya kuhutubia bunge leo jioni, .
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam Prof. Lipumba alisema, ZEC imebakiza kuhakiki majimbo 14 ambapo haitachukua saa tatu katika kupitia majimbo hayo na kumtangaza mshindi

Profesa Lipumba alisema kuwa uchaguzi huo ulifutwa baada ya kushindwa kwa dhahiri mgombea wa kiti hicho kupitia Chama cha Mapinduzi CCM ndipo hapo vyombo vya dola vikamshinikiza ambapo mwenyekiti watume hiyo alichukua hatua ya kuvunja katiba kwa kufuta uchaguzi huo

Prof. Lipumba amesema kuwa, hulka ya Chama Cha Mapinduuzi (CCM) kuingilia na kuvuruga matokeo sio mara ya kwanza na kwamba walianza mwaka 1995 akitoa mfano Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kuwa aliiandikia barua tume kufuta uchaguzi na agizo hilo kutekelezwa.

Katika  hatua  nyingine, Lipumba  alimtaka  Rais Magufuli kuandaa bajeti upya ambayo ni halisia na inatekelezeka badala ya kutegemea ya mwaka 2015/16 ambayo haiwezi kutekelezeka.

UKAWA Watahadharishwa Kutofanya VURUGU Leo Bungeni Wakati Rais Magufuli Akihutubia

 

Wabunge wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa wameonywa kutofanya jambo lolote litakaloashiria kuvuruga Bunge wakati Rais John Magufuli atakapolihutubia leo jioni.

Akiongea jana mjini Dodoma, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye alisema kuwa Wabunge hao wa Ukawa wanapaswa kufahamu kuwa kitendo chochote watakachofanya kwa lengo la kuvuruga hotuba hiyo ni kinyume cha sheria na taratibu za Bunge na kwamba hawatavumiliwa.

Nape alionesha kuwashangaa wabunge hao kudai kuwa hawamtambui Rais Magufuli ili hali wanashiriki katika shughuli zote za Bunge ikiwa ni pamoja na kumpigia kura Waziri Mkuu ambaye ameteuliwa na Rais huyohuyo wanaedai hawamtambui.

Naye Mbunge wa jimbo la Nzega, Dkt Khamis Kigwangala alisema kuwa wabunge wa Ukawa wana haki ya kuingia Bungeni na kukaa kwa utulivu au kutoka nje endapo hawatakuwa tayari kusikiliza hotuba hiyo lakini sio kuvuruga hali ya amani ili watanzania wasipate nafasi ya kumsikiliza Rais.

“Hawawezi kuwanyima haki watanzania kumsikiliza Rais wetu akiwa anatoa dira ya uelekeo wa Taifa letu,” alisema Khamis Kingwangala.

Wabunge wa Ukawa juzi walifanya mkutano na vyombo vya habari na kueleza kuwa hawatakubali kumuona Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein akiingia katika Bunge hilo leo kwa kuwa kipindi chake cha urais Zanzibar kimekwisha.
 
Walisisisitiza kuwa watafanya ‘jambo’ ambalo hata hivyo hawakulitaja. Wabunge hao pia walisema kuwa wamemuandikiabarua Spika wa Bunge kuhoji uhalali wa hotuba ya Rais wakati Zanzibar bado haijampata Rais mpya.

KURASA ZA MAGAZETI LEO NOVEMBA 19 ALHAMISI HEAD LINE


DSC02461 DSC02463 DSC02464 DSC02465 DSC02466 DSC02468 DSC02469 DSC02470 DSC02471 DSC02472 DSC02473 DSC02474 DSC02475DSC02476 DSC02477 DSC02479 DSC02480 DSC02481 DSC02482 DSC02483 DSC02484 DSC02485 DSC02486 DSC02487 DSC02488 DSC02489 DSC02490DSC02491 DSC02492 DSC02493 DSC02494 DSC02495 DSC02496 DSC02497 DSC02498 DSC02499 DSC02500 DSC02501 DSC02502 DSC02503 DSC02505 DSC02506DSC02507