MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Thursday, 26 March 2015

OZIL SASA AITAKA BALLON D’OR


IMG_20150326_082322
Kiungo wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani Mesut Ozil amesema miaka ijayo anaamini atashinda tuzo ya Ballon d’or na jinsi wachambuzi wanavyozidi kumkosoa ndiyo anapata nguvu ya kujituma zaidi.
Mjerumani huyo ameichezea Arsenal mechi 14 tu katika ligi kuu msimu huu kufuatia kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha lakini tangu arudi tena uwanjani amekuwa katika kiwango bora.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea Real Madrid anaonekana kuizoea ligi ya Uingereza tofauti na hapo awali. “Nikiendelea kufanya vizuri, afya yangu ikawa imara basi miaka michache ijayo Ballon d’or itakuwa mikononi mwangu” alisema Ozil. .”Ninajisikia vizuri. Mimi ni mchezaji mkubwa duniani,ninacheza katika klabu kubwa. Pia hii ligi tunatumia nguvu nyingi kuliko kule La Liga kwa hiyo ninazidi kuimarika zaidi kuliko mwanzo ” aliongeza Ozil.
Pia mchezaji huyo amesema kitendo cha kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Scholes kuponda kiwango chake kilimuongezea nguvu ya kupambana na kuongeza kujituma zaidi.
Ozil sasa yupo katika majukumu ya timu ya taifa ya Ujerumani ambao jumapili watashuka dimbani kuwavaa Georgia katika mechi ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya mataifa Ulaya yatakayofanyika mwaka 2016 nchini Ufaransa.

LIONEL MESSI AMPIGA BAO RONALDO KWA UTAJIRI




Lionel Messi ndiye mwanasoka tajiri zaidi duniani baada ya kuingiza karibu pauni milioni moja kwa wiki katika fedha zake za ujira pamoja na alizokuwa akilipwa na wadhamini mbalimbali.



Kutokana na fedha hizo, raia huyo wa Argentina anayekipiga Barcelona alitundika benki hadi kitita cha pauni milioni 47.8.

Katika fedha hizo pauni milioni 26 zilitokana na mshahara tu anaolipwa na Barcelona.
 
Mpinzani au mshindani wa mkubwa Cristiano Ronaldo pauni milioni 39.7.

TOP 10 YA WANASOKA WENYE MKWANJA ZAIDI:
1. Lionel Messi £47.8m
2. Cristiano Ronaldo £39.7m
3. Neymar £26.8m
4. Thiago Silva £20.2m
5. Robin van Persie £18.8m
6. Gareth Bale £17.5m
7. Wayne Rooney £16.5m
8. Zlatan Ibrahimovic £15.8m
9. Sergio Aguero £15.6m
10. Robert Lewandowski £14.8m

Source: France Football Rich List

MOURINHO AWA 1 KWA KUINGIZA MKWANJA MREFU KULIKO MAKOCHA WOTE DUNIAANI

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho ndie yupo juu kwenye Listi ya Mameneja wa Soka wanaevuna fedha nyingi na kwenye 5 Bora pia wamo wenzake wa Ligi Kuu England Arsene Wenger wa Arsenal na Louis van Gaal w Manchester United.
Orodha kamili ni kama ifuatavyo:
1) Jose Mourinho (Chelsea) - £13.2m Kipato kwa Mwaka
2) Carlo Ancelotti (Real Madrid) - £11.4m
3) Pep Guardiola (Bayern Munich) - £11.2m
4) Arsene Wenger (Arsenal) – £8.3m
5) Louis van Gaal (Manchester United) - £7.3m
6) Fabio Capello (Russia) - £6.6m
7) Andre Villas-Boas (Zenit St Petersburg) - £6.25m
8) Sven-Goran Eriksson (Shanghai) - £5.9m
9) Jurgen Klopp (Borussia Dortmund) - £5.3m
10) David Moyes (Real Sociedad) - £5.1m
10) Laurent Blanc (Paris Saint Germain) - £5.1m
10) Rafael Benitez (Napoli) - £5.1m
13) Walter Mazzarri (Alikuwa Inter Milan) - £5m
14) Roberto Di Matteo (Schalke) - £4.4m
15) Luis Enrique (Barcelona) - £4m
15) Luciano Spalletti (Alikuwa Zenit St Petersburg)- £4m
17) Antonio Conte (Italy) - £3.9m
18) Manuel Pellegrini (Manchester City) - £3.8m
19) Brendan Rodgers (Liverpool) - £3.6m
20) Roberto Mancini (Inter Milan) - £3.5m

COPA DEL REY FAINALI NOU CAMP - BARCA NA BILBAO, BAADA REAL KUGOMEA BERNABEU!


COPAdelREYImeamuliwa kuwa Fainali ya Kombe la Mfalme, Copa del Rey, itachezwa Nou Camp, Nyumbani kwa Barcelona, hapo Mei 30 kati ya Athletic Bilbao na Barcelona.
Kawaida Fainali ya Kombe hili huchezwa Uwanja usio wa Timu iliyo Fainali lakini baada ya Real Madrid kugomea kutoa Uwanja wao Santiago Bernabeu ukaanza mvutano wa wapi Fainali hiyo ichezwe.
Kwenye Mkutano wa Shirikisho la Soka la Spain na Klabu hizo mbili, Kura ilitumika na Viwanja vya Sevilla, Vicente Calderon, na Mestalla wa Valencia kubwagwa na kuacha Viwanja vya Barca Nou Camp na San Mames cha Bilbao kwenye kinyang'anyiro.
Hatimae Nou Camp ilipita na hii itakuwa mara ya kwanza kwa Timu iliyo Fainali kucheza Fainali Uwanja wake wa Nyumbani tangu 2002 wakati Deportivo La Coruna walipoifunga Real Madrid Nyumbani kwao Santiago Bernabeu.
Mara ya mwisho kwa Nou Camp kuwa Mwenyeji wa Fainali za Copa del Rey ni 2010.
Ikiwa Barca watatwaa Kombe hili, ambalo wao wanaongoza kwa kulibeba mara nyingi, hii itakuwa mara yao ya 27 wakati Athletic Bilbao wakifuata kwa wingi wa kulitwaa kwa kulichukua mara 23.

EURO 2016: MITANANGE KUENDELEA IJUMAA, COSTA, ROBBEN, RVP NJE!


EURO2016Vita ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, huko Ufaransa Mwakani, inaendelea kunzia Ijumaa hadi Jumanne kwa Mechi za Makundi ambayo yatafikia idadi ya Nusu ya Mechi zake zote.
Mechi 26 zinatarajiwa kuchezwa Wikiendi hii na kumalizika Jumanne kwa Mechi moja ambayo ni kiporo baada ya kuahirishwa hapo awali.
Spain, ambao ni Mabingwa Watetezi, watakuwa kwao Mjini Sevilla kucheza na Ukraine huku wote wakiwa wamefungana katika Nafasi ya Pili ya Kundi C wakiwa Pointi 3 nyuma ya Vinara Slovakia ambao watacheza na Timu ubwete Luxembourg.
Ijumaa, Spain watacheza Mechi yao bila ya Straika wao kutoka Chelsea, Diego Costa, ambae ni Majeruhi, na badala yake Kocha Vicente del Bosque amewaita Mastraika Chipukizi Alvaro Morata na Juanmi.
Siku hiyo hiyo Ijumaa, Harry Kane huenda akacheza Mechi yake ya kwanza kwa England ambao wanacheza na Lithuania Uwanjani Wembley, London wakitaka kuendeleza rekodi yao ya kushinda Mechi zao zote za Kundi E ambalo wanaongoza wakiwa na Pointi 12 zikiwa Pointi 6 zaidi ya Timu zinazowafuatia Slovenia, Switzerland na Lithuania.
Kane, Straika wa Tottenham mwenye Miaka 21, ameifungia Timu yake Bao 29 tangu mwanzoni mwa Msimu ikiwa pamoja na Hetitriki Wikiendi iliyopita walipoichapa Leicester 4-3.
Hiyo hiyo Ijumaa zipo Mechi zingine 3 za Kundi G ambapo Vinara Austria watasafiri kwenda kucheza na Liechtenstein, Sweden watakuwa Ugenini kucheza na Moldova na Russia wako Ugenini huko Monenegro.
Jumamosi, Vinara wa Kundi H Croatia, wanaofungana Pointi na Italy wote wakiwa na 10, watacheza na Norway wakati Itaky wako Ugenini na Bulgaria.
Kocha wa Italy, Antonio Conte, anatarajiwa kuwatumia Wachezaji wapya Watatu ambao ni Mzaliwa wa Brazil anaechezea Sampdoria, Eder, na Mzaliwa wa Argentina anaecheza Palermo, Franco Vazquez pamoja na Kiungo Mirko Valdifiori ambae ana nafasi kubwa kucheza kwa vile Mkongwe wa Juventus Andrea Pirlo ni Majeruhi na Daniele De Rossi hakuitwa.
Kundi A ambalo wamo Netherlands waliofungwa Mechi 2 kati ya 4 za kwanza, watacheza na Turkey Mjini Amsterdam bila ya Mastaa wao Majeruhi Arjen Robben na Robin van Persie wakati Vinara wa Kundi hili, Czech Republic watakuwa Nyumbani kucheza na Latvia, na Iceland, ambao wako Nafasi ya Pili, wako Ugenini huko Kazakhstan.
Israel na Wales, ambao hawajafungwa na wanaoongoza Kundi B, watakutana huko Haifi, wakati Belgium ambao pia wako Kundi hili wako Nyumbani kucheza na Cyprus wakati Bosnia-Herzegovina wako Ugenini kucheza na Andorra wakisaka ushindi wao wa kwanza.
Jumapili, Mabingwa wa Dunia Germany wanasafiri kwenda Tbilisi kucheza na Georgia katika Mechi ya Kundi D ili kufufua Kampeni yao ambayo iko mrama huku Vinara Poland wakiwa Dublin kucheza na Ireland ambao pamoja na Germany na Scotland wapo Pointi 3 nyuma ya Poland.
Scotland wapo kwao Glasgow kucheza na Gibraltar ambayo haipewi nafasi yeyote.
Jumapili hiyo hiyo, Vinara wa Kundi F ambao hawajapoteza Mechi, Romania, wapo kwao kucheza na Faroe Islands wakati Timu ya Pili Northern Ireland watacheza Nyumbani na Finland na Hungary pia wapo Nyumbani kuivaa Greece.
Katika Kundi I, Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, anaweza kuipaisha Nchi yake Portugal kutwaa uongozi wa Kundi wakicheza kwao na Serbia kwa vile Denmark hawachezi.
EURO 2016
Ratiba
**Saa za Bongo
Ijumaa Machi 27
KUNDI C
2345 FYR Macedonia v Belarus
KUNDI C
2345 Slovakia v Luxembourg
KUNDI C
2345 Spain v Ukraine       
KUNDI E
2345 England v Lithuania
KUNDI E
2345 Slovenia v San Marino
KUNDI E
2345 Switzerland v Estonia
KUNDI G
2345 Liechtenstein v Austria
KUNDI G
2345 Moldova v Sweden
KUNDI G
2345 Montenegro vRussia
Jumamosi Machi 28
KUNDI A
1900 Kazakhstan v Iceland
KUNDI A
2100 Czech Republic v Latvia
KUNDI B
2100 Israel v Wales
KUNDI H
2100 Azerbaijan v Malta
KUNDI H
2100 Croatia v Norway
KUNDI H
2345 Bulgaria v Italy
KUNDI A
2345 Netherlands v Turkey
KUNDI B
2345 Andorra         v Bosnia and Herzegovina
KUNDI B
2345 Belgium v Cyprus
Jumapili Machi 29
KUNDI D
2000 Georgia v Germany
KUNDI D
2000 Scotland v Gibraltar
KUNDI F
2000 Northern Ireland v Finland
KUNDI F
2000 Romania v Faroe Islands
KUNDI I
2000 Albania v Armenia
KUNDI I
2245 Portugal v Serbia
KUNDI F
2245 Hungary v Greece
KUNDI D
2245 Republic of Ireland v Poland
Jumanne Machi 31
KUNDI B
2245 Israel v Belgium

Maharamia waziteka meli mbili za Iran


 
     Maharamia wa Somalia wateka nyara Meli mbili za Iran 


 Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia mihadarati na Uhalifu kimesema kuwa maharamia wameteka meli mbili za Iran za kuvua samaki katika ufuo wa Somalia.
Utakeji huo ni wa kwanza kufaulu tangu mwaka 2012.
Ushikaji doria na matumizi ya walinzi wenye silaha umesaidia kupunguza uharamia katika ufuo wa Somalia, ambao awali ulikuwa ukishirikisha zaidi ya meli 200 kwa mwaka.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa wafanyakazi 48 wametekwa nyara katika uharamia huo.
Taarifa hiyo inasema kuwa meli hizo, zilizokuwa zikivua samaki bila kibali katika fuo hizo za Somalia zimepelekwa katika kijiji cha Pwani cha El Huur katikati mwa Somalia.
Ingawa uharamia ulikuwa umepunguka, idadi ya wavuvi haramu imeongezeka.
Uvuvi haramu ndio ulioanzisha mtindo wa kuteka meli Somalia.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa iwapo meli za kigeni zitaendelea kuvua samaki kimagendo katika ufuo wa Somalia, visa vya uharamia navyo vitaongezeka.

Aliyebaka mtawa India akamatwa

Polisi nchini India wamemtia mbaroni mtu aliyedaiwa kubaka mtawa mmoja wa Kanisa Katoliki Magharibi mwa Bengal.
Polisi nchini India wamemtia mbaroni mwanamume mmoja kuhusiana na ubakaji wa mtawa mmoja wa Kanisa Katoliki katika makaazi ya watawa Magharibi mwa Bengal.
Viongozi wa Kikristo nchini India wamekosoa Serikali kwa kuzembea katika kazi yake ya kukabiliana na uhalifu.
Mshukiwa huyo alitiwa mbaroni mnamo Jumatano Usiku mjini Mumbai.
Amesafirishwa hadi Kolkata ili kufanyiwa mahojiano zaidi.

Mshukiwa huyo alitiwa mbaroni mnamo Jumatano Usiku mjini Mumbai.
Yeye ni mtu wa kwanza kutiwa mbaroni kuhusiana na ubakaji huo uliofanyika katika makaazi ya watawa katika Ranaghat majuma mawili yaliyopita.
Washukiwa sita walioshiriki wizi huo wa ubakaji walinaswa katika kamera za CCTV. Kufuatia malalamiko kuwa Serikali hailichukulii swala hilo na umuhimu unaostahili Serikali sasa imekabili kesi hiyo kwa idara ya upelelezi.
Waziri Mkuu Narendra Mondi ameeleza masikitiko yake kuhusiana na shambulio hilo na kutoa zawadi kwa ye yote atakayesaidia kuwatia mbaroni walioshiriki katika uhalifu huo.

kumbe Ndege ya Ujerumani iliangushwa makusudi


Rubani Andreas Lubitz
Rubani wa ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya jumanne alitaka kuiharibu ndege hiyo kulingana na maafisa wa Ufaransa.Kiongozi wa mashtaka katika mji wa Mersaille ,Brice Robin, akizungumza kulingana na habari aliyopata katika kijisanduku cha kunasa sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa ndani ya chumba cha kuendesha ndege pekee.
Rubani huyo kimakusudi aliishusha ndege hiyo kwa kasi huku rubani mwenza akiwa nje ya chumba hicho cha kuendesha ndege.
Bwana Robin amesema kuwa kulikuwa na kimya kikubwa ndani ya chumba hicho wakati rubani mwenza alipojaribu kuingia kwa nguvu.
Hatahivyo abiria walisikika wakipiga nduru kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo,aliongezea.

 

 Mlima wa Alps ambapo ndege ya abiria ya Germanywings ilianguka

Rubani huyo kwa jina Andreas Lubtiz,mwenye umri wa miaka 28, alikuwa hai hadi wakati ndege hiyo ilipoanguka ,kiongozi wa mashtaka alisema.
Ndege hiyo aina ya Airbus 320 iliokuwa ikitoka Barcelona kuelekea Duesseldorf Ujerumani iligonga mlima na kuwauwa abiria wote 144 pamoja na wafanyikazi sita wa ndege baada ya kushuka kwa dakika nane.
"Tunasikia rubani akimuuliza rubani mwenza kuchukua udhibiti wa usukani wa ndege hiyo na vilevile tunasikia sauti ya kiti kikisonga nyuma na mlio wa mlango ukifungwa,bwana Robin aliwaeleza wanahabari.

Matumla Junior kumvaa mchina kesho Wang Xin Hua

 
Kuna msemo usemao “Mtoto wa nyoka ni nyoka” na msemo huu unajidhihirisha katika mpambano kati ya mtoto wa bingwa wa zamani wa dunia wa WBU, Rashid Matumla, Mohamed atakapozichapa na bondia kutoka China, Wang Xiu Hua katika pambano la ubingwa wa WBF la uzani wa Super Bantam siku ya Jumamosi jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Hua tayari amewasili nchini Tanzania na Mohamed amesema amejiandaa vya kutosha kushinda mbele ya mashabiki wa nyumbani.
Kwa mujibu wa waandaaji, mshindi kati ya Matumla Junior na Hua atapata nafasi ya kucheza katika moja ya mapambano ya utangulizi (supporting cards) katika pambano la bondia Floyd Mayweather na Pacquiao litakalochezwa Mei 2 jijini Las Vegas.
Watu kadhaa mashuhuri wanategemewa kuangalia pambano la Matumla Junior na Hua akiwemo bondia wa zamani wa uzito wa juu wa Afrika ya Kusini, Francois Botha, aliyewahi kupingana na bingwa wa zamani, Mike Tyson na Evander Holyfield katika enzi zake.
ngm 1Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassini Abdalla kushoto akisalimiana na bondia Wang Xin Hua kutoka China mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es salaam siku alipo wasili  kwa ajili ya mpambano wake na mohamed Matumla utakaofanyika march 27  kesho katika ukumbi wa diamond jubilee katikati ni Rais wa ngumi za kulipwa nchini PST Emanuel Mlundwa na kulia ni promota wa mpambano uho Jay Msangi Picha na SUPER D BOXING NEWS

Marekani yachapwa 3 -2 na Denmark

 
Mechi kirafiki za kimataifa zilizopigwa usiku wa kuamkia leo ambao Scotland iliwashikisha adabu ndugu za Ireland ya kaskazini baada ya kuwanyuka goli moja kwa bila majibu.
Goli hilo la dakika za lala salama lilifungwa Christopher Berra dakika ya 85 kwa njia ya kichwa baada ya kona iliyochongwa na Matt Ritchie.
Katika mechi nyingine Geogia iliwaadhibu Malta kwa jumla ya mabao 2 - 0 , huku Denmark
Timu ya taifa ya Marekani
ikiwageuza nyanya Marekani baada ya kuwatundika mabao 3 kwa 2.
Kwa upande Ujerumani ilishikwa sharubu na Australia baada ya kutoka sare ya magoli mawili kwa mawili.
Leo kutakuwa na mechi nyingine za kirafiki ambapo Ufaransa wakuwa wenyeji wa Brazil huku Bahrain wakikutana uso kwa uso na Colombia.
Mechi nyingine itakuwa ni kati ya Iran ambao wataumana vikali na Chile.

Tuesday, 24 March 2015

PROF. MUHONGO KUWANIA URAIS 2015


*Wapambe wasema alisurubiwa kwa ajili ya urais
NA GORDON KALULUNGA, MBEYA
WAKATI joto la urais likizidi kupanda ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana na hofu ya baadhi ya majina mazito ya wagombea wa nafasi hiyo kuendelea kujitokeza ikiwa ni pamoja na kujinadi kwa siri, Prof. Sospeter Muhongo, naye amejitosa Katika nafasi kinyang’anyiro hicho, imefahamika.
Kwa mkoa wa Mbeya,  tayari baadhi ya wapambe wake wameanza kazi katika wilaya za Momba, Mbeya Vijijini na Mbeya Mjini huku baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu na waliokuwa katika ngome ya kundi la Edward Lowassa, wanaongoza kazi ya kumnadi kwa wananchi Prof. Muhongo.
Viongozi hao baadhi wameelezwa kuwa walikuwa katika kundi la Vijana wa 4U Movement, linalojinasibu kuwa ni marafiki wa Lowassa.
Mmoja wa wasomi ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema kuwa ameamua kuondoka katika kundi la Lowassa kwasababu mbalimbali ikiwemo kundi hilo kuthamini baadhi ya watu huku wengine hasa wanaofanya kazi kubwa badala ya utapeli kutothaminiwa.
“Hivi karibuni unakumbuka kuwa kulikuwa na kongamano la Vijana wa 4U Movement hapa Mbeya, ni kundi ambalo limeamua kujitafutia fedha kwa migongo ya wengine, jambo ambalo mimi lilinisikitisha na nikaamua kuwaambia hata wakubwa lakini tunapuuzwa” alisema kijana huyo.
Alipoulizwa kuhusu yeye pamoja na wenzake kuamua kumnadai Prof. Muhongo wakati hivi karibuni alijiuzuru kutokana na kashfa ya Escrow, alisema kuwa suala lile mwanasheria Mkuu alisema Bungeni kuwa yeye ndiye anastahili kubeba lawama lakini hakusikilizwa baada ya kubaini kuwa Prof. Muhongo hatakuwa anashikika kwenye Urais hivyo wakaamua kumsulubu baadhi hata bila kujua.
Katika moja ya kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Nsungwe Hotel juzi mjini Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini kati ya wapambe wa kiongozi huyo na vijana wa Bodaboda, vijana hao walielezwa kuwa ni vema wakaanza kuwa na mtazamo chanya wa kumsema vema kiongozi mwenye uaminifu, uadilifu, uzalendo na kuona anataka kutupeleka wapi.
Katika kikao cha wasomi wa vyuo vikuu na wanataaluma kilichofanyika jana katika bustani ya City Pub Jijini Mbeya, wasomi hao wamekubaliana kutompoteza kiongozi huyo huku baadhi wakisifia juhudi zake za kuaminiwa na moja ya Vyuo Vikuu bora kabisa nchini China, The China University of Geosciences (Wuhan), ambacho kwa ushawishi wake kimetoa ufadhili wa masomo katika fani ya Mafuta na Gesi (Oil and Gas Studies) kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu.
“Jumla ya nafasi 22 zitatolewa mwaka huu kwa Watanzania watakaokidhi vigezo, ambapo watapata ufadhili wa masomo hayo kwa asilimia 100 ikiwemo chakula, malazi na gharama za masomo (tuition fee)” alisema mmoja wa kiongozi wa wapambe wa kiongozi huyo mkoani Mbeya.
Prof. Muhongo alipopigiwa simu na mwandish wa habari hizi ili kuthibitisha kama atawania nafasi hiyo ya urais mwaka huu, alisema kuwa, anafahamu taratibu za chama chake hivyo hawezi kukubali au kukataa.
“Mimi nafahamu na kuheshimu taratibu za chama, ukifika wakati chama kikiruhusu kusema nitasema kama nitawania ama la, lakini niseme kuwa ni wakati sasa wa kumpata kiongozi anayeaminika na mwenye uwezo wa kujenga uchumi imara unaotoa fursa kwa kila Mtanzania” alisema Prof. Muhongo.
Aidha alisema yeye amebahatika kukaa karibu na Mwalimu Julius Nyerere na alibahatika kuambiwa nini alikuwa anakusudia kuipeleka Tanzania kwa ajili ya Tanzania itakayoendana na wakati na rasilimali za nchi kuwa tunu kamili za watanzania na siyo kuwa laana.

AJALI HIZI ZITATUA JAMANI KWA SITAILI HIII

  




 Basi hilo baada ya kupata ajali


 Baadhi ya watu wakiwa wamefika kushuhudia ajali hiyo


Basi la morning star linalotka ubaruku-mbeya likiwa limetumbukia katika mfereji baada ya kuacha njia kwa kile kilichoelezwa ni kusapuka tairi la mbele na kupoteza mwelekeo. Jana asubuhi. Watu wawili walifariki dunia akiwamo mtoto wa miezo 9 na mtu mzima mmoja na abiria wengine 23 walijerhiwa vibaya ambapo walipelekwa hospitali ya misheni ya chimala. Wengi wao walivunjika miguu,mikono na kujerhiwa vichwani.



Ajali hiyo ilitokea eneo la itamboleo nje kidogo na mji wa igurusi wakati likielekea Mbeya.

HII NDIO KAZI YA JESHI LA POLISI MOA WA MBEYA

 



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangiakionyesha baadhi ya tunguli zilizokamatwa na jeshi lake.
















    


JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limewakamata watu 15 na kuwafikisha Mahakamani wakituhumiwa kujihusisha na upigaji wa ramli chonganishi ikiwa ni hatua ya kuwasaka waganga wasiokuwa na vibari katika kukomesha maovu yanayotokana na imani za kishirikina.





Hayo yalithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake  ambapo alisema kesi hizo zipo kwenye hatua mbali mbali.





Alisema kuwa katika msako ambao ulianza tangu Machi 6, mwaka huu, Tayari Jeshi hilo limewakamata waganga wa jadi 23 wanaojihusisha na upigaji waramli hizo chonganishi.





Msangi alisema  watuhumiwa 15 walifikishwa mahakamani na  kesi zao zipo katika hatua tofauti  na kwamba watuhumiwa sita  upelelezi bado unaendelea na mtuhumiwa mmoja taratibu zinafanywa ili aweze kufikishwa mahakamani.





Alisema  watuhumiwa walikamatwa katika wilaya tofauti na idadi yao kwenye mabano ambazi ni Wilaya ya Mbeya (7), Chunya(12) , momba(2),Mbozi (01) pamoja na Kyela(01).





Aidha Msangi alisema   baadhi ya zana ambazo wamekamatwa nazo waganga hao ni  pamoja na nyara vza serikali na zana zisizokuwa na nyara zisizokuwa za serikali .





Hata hivyo Kamanda Msangi alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na tabia za kusadiki  imani za ushirikina kwa kupiga ramli ili kutatua matatizo yao kwenye jamii.





Pia alitoa onyo kwa wananchi wanaoshirikiana  kuwaficha waganga wa kienyeji wanaojihusisha na upigaji wa ramli chonganishi ambazo zinadaiwa kuwa chanzo cha uhalifu unaohusiana na imani za kishirikina.


Mwisho.
Picha na Mbeya yetu

VENGU AZUSHIWA KIFO, ORIJINO KOMEDI WAKANUSHA


VENGU 
Taarifa za kufariki dunia kwa Joseph Shamba maarufu kama Vengu, zimekanushwa vikali.

Kuanzia saa 4 asubuhi kumekuwa na taarifa zinazosambaa mitandaoni kwamba Vengu wa kundi la Orijono Komedi amefariki Dunia.
Vengu ameugua kwa takribani miaka mitatu sasa hali yake ikiwa si nzuri.

Meneja wa kundi hilo, Seki David amesema si kweli kuhusiana na taarifa hizo.

“Ni habari zisizo sahihi, Vengu bado ni mgonjwa na ningependa kuwaomba wanaosambaza taarifa hizo kutofanya hivyo,” alisema Seki.

MALAWI KUWASILI ALHAMISI NA TANZANIA YAWASILI JIJINI MWANZA KLWA MAANDALIZI YA MECHI

Malawi6 
Msafara wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) unatarajiwa kuwasili jijini Dar es salaam siku ya alhamis, kabla ya kuunganisha ndege siku ya ijumaa kuelekea jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Taifa Stars siku ya jumapili.
Katika msafara huo utakaokuwa na wachezaji 18 na viongozi 7, kocha mkuu wa The Flames Young Chimodzi amewajumuisha wachezaji nane (8) katika kikosi chake wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.
Wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini ni Limbikani Mzava (Celtic), Harry Nyirenda (Black Leopards), Esau Kanyenda (Polokwane City), na Atusaye Nyondo (University of Pretoria).
Wengine ni Nahodha Joseph Kamwendo (Tp Mazembe – Congo DR), Frank Banda (HBC Songo – Msumbuji), Chimango Kayira (Costal De Sol – Msumbuji) na Gerald Phiri (Caps United – Zimbambwe).

STARS YAWASILI MWANZA

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili salama leo asubuhi jijini Mwanza, tayari kwa maandalizi ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa siku ya jumapili Machi 29, 2015 dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames), mechi itakayochezwa kwenye dimba la Uwanja wa CCM Kirumba.
Kikosi cha Stars kimeondoka kikiwa na wachezaji 18 ambao wameripoti kambini jana, huku kiugo mshambuliaji Mwinyi Kazimoto anayecheza soka la kulipwa nchini Qatar akitarajiwa kuungana na wenzake leo mchana jijini Mwanza.

Wachezaji waliopo kambini jijini Mwanza ni, magolikipa Aishi Manula na Mwadini Ali (Azam FC), walinzi ni Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Aggrey Morris (Azam FC) , Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Haji Mwinyi (KMKM), Hassan Isihaka na Abdi Banda (Simba SC)   Wengine ni Amri Kiemba, Frank Domayo, Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Haroun Chanongo (Stand United), John Bocco (Azam FC), Juma Luizio (Zesco United), Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe).
Mchezaji Mcha Khamis wa Azam FC amejiondoa kikosini kutokana na kuwa majeruhi, huku wachezaji wa Young Africans wakitarajiwa kujiunga na kikosi hicho cha timu ya Taifa mara tu baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya JKT Ruvu siku ya jumatano.