MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Friday, 28 November 2014

SIMBA HATUJASAJILI MCHEZAJI DIRISHA DOGO

Msemaji wa Simba, Hamphrey Nyasio amesema Dar es Salaam leo kuwa klabu hiyo bado haijafanikiwa kunasa saini ya mchezaji hata mmoja hadi sasa.
Lakini, mtandao huu unatambua kwamba licha ya kupewa ofa nono na klabu yake ya sasa Gor Mahia ili aendelee kubaki katika Ligi Kuu ya Kenya (KPL), Sserunkuma ametua jijini Dar es Salaam leo mchana kufanya mazungumzo na uongozi wa Simba kwa lengo la kusajiliwa.
dan
Hata hivyo, uongozi wa juu ya klabu hiyo hautaki kuweka suala hilo hadharini hadi pale mambo yatakapokuwa yamekamilika.
“Kocha mkuu (Mzambia Patrick Phiri) anatarajia kuwasili nchini leo (jana) jioni, (Amissi) Tambwe na (Pierre) Kwizera waliwasili juzi (Jumanne) jioni na wanaendelea vizuri na mazoezi. Hakuna mchezaji mpya ambaye mpaka sasa Simba imefanikiwa kumsajili,” Nyasio amesema.
“(Emmanuel) Okwi na (Joseph) Owino wa=natarajiwa kuwasili nchini kesho,” amesema Nyasio.
Kumekuwa na taarifa zinazodai kwamba Sserunkuma, mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Kenya (KPL), ameshamalizana na Simba huku klabu yake ya sasa Gor Mahia ikitangaza jana kupitia kwa Katibu Mkuu, Chris Omondi kwamba iko katika hatua za mwisho kumwongeza muda wa kuendelea kubaki kwa mabingwa hao wa Kenya.
Kama Simba watashindwa kumalizana naye jijini Dar es Salaam kwa sasa, ni wazi kuwa nyota huyo wa Cranes atarejea Kenya kuongeza muda wa kuendelea kukipiga na Gor Mahia.

PIGO ARSENAL, WILSHERE NJE MIEZI MINNE BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI

KLABU ya Arsenal inakabiliwa na baa la majeruhi, baada ya Jack Wilshere naye kutakiwa kuwa nje kwa miezi minne kufuatia kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu jana.
Na kocha Arsene Wenger atalazimika kuingia sokoni Januari kununua wachezaji ili kupoza maumivu ya tatizo la majeruhi kikosini mwake. 
Wilshere amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu wake wa kushoto baada ya kipigo cha Manchester United cha mabao 2-1 Uwanja wa Emirates Jumamosi iliyopita. Na Nahodha, Mikel Arteta pia anaweza asicheze tena mwaka huu baada ya kuumia Arsenal ikishinda 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund.
Wilshere posted a picture of his ankle in a cast after the operation and insisted he will return soon
Wilshere ameposti picha hii baada ya kufanyiwa upasuaji

Kuuminia kwa Wilshere kunamfanya kocha Arsene Wenger awakose viungo wote watatu tegemeo, Aaron Ramsey, Mathieu Flamini na Tomas Rosicky.
Baada ya upasuaji huo, Wilshere akaposti picha Instagram akiwaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba zoezi limekwenda vizuri.
"Kifundo cha mwishowe kilihitaji upasuaji," ameandika. "Zoezi limekwenda vizuri na asante kwa mkuu James Calder (mpasuaji)!
Wilshere was clearly in pain after the tackle and it is unlikely that he will be back for Arsenal before March
Wilshere akiugulia maumivu baada ya kuumia na anatarajiwa kurejea kikosini Arsenal kabla ya Machi, mwakani

MAYWEATHER KWA MBWEMBWE BANA! SASA ATUPIA PICHA AKIOSHWA NA MREMBO

Bondia ambaye hajawahi kupoteza mchezo, Floyd Mayweather, amezidi kuonyesha mbwembwe zake mtandaoni baada ya kutupia picha akioshwa.

Mayweather ametupia picha hiyo akioshwa na mwanadada mrembo wakati yeye akiwa ametuplia, 

TFF YA SEMA HAKUNA TATIZO MCHEZAJI KUCHEZA TIMU MOJA MARA TATU MSIMU MMOJA

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekiri kufanya makosa kuruhusu kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili kabla ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).

VPL ilisimama kwa wiki saba Novemba 9 baada ya kuchezwa kwa mechi 49 za raundi ya kwanza hadi ya saba kupisha usajili wa dirisha dogo, mashindano ya Kombe la Uhai yanayoshirikisha Timu B za klabu za Ligi Kuu na michuano ya Kombe la Chalenji.
TFF ilifungua dirisha dogo la usajili Novemba 15 na litafungwa Desemba 15 huku mechi za raundi ya nane hadi ya 13 ya mzunguko wa kwanza wa VPL bado hazijachezwa, hivyo kutoa mwanya kwa baadhi ya wachezaji watakaozihama timu zao kipindi hiki cha usajili kucheza mechi tatu dhidi ya timu moja.
bon
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amekiri shirikisho hilo kujisahau katika suala hilo lakini akasisitiza kuwa hakuna tatizo kubwa mchezaji kucheza mechi tatu dhidi ya timu moja.
“Ilikuwa haijawahi kutokea hapa kwetu (Tanzania), tumejifunza kitu lakini mchezaji kucheza mechi tatu dhidi ya timu moja VPL haina tatizo, tatizo kubwa ni mchezaji kusajiliwa na zaidi ya timu mbili msimu mmoja. Hili linakatazwa kikanuni,” amesema Mwesigwa.
Kiungo mkongwe wa Simba Amri Kiemba amejiunga na Azam FC kwa mkopo huku klabu hiyo ya Msimbazi ikiwabana wanalambalamba wasimtumie katika mechi zinazozikutanisha timu hizo mbili msimu huu.
TFF kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Mshindano, Boniface Wambura imepinga vikali uamuzi huo wa Simba kwa kuwa kanuni zinamruhusu mchezaji huyo kukipiga dhidi ya timu iliyomtoa kwa mkopo kwenda timu nyingine, hata hivyo.
Mchezaji wa Ndanda FC aliyecheza dhidi ya Azam FC msimu huu, akisajiliwa Simba atacheza dhidi ya Azam mara tatu katika mechi za msimu mmoja wa ligi kuu, ikiwa ni mfano wa kilichokosewa na TFF kuruhusu dirisha dogo la usajili msimu huu lifunguliwe ilhali mechi za mzunguko wa kwanza bado hazijakamilika.

Thursday, 27 November 2014

FIFA LISTI YA UBORA ZA TIMU DUNIANI: GERMANY YAENDELEA KUWA JUU, TANZANIA YASHUKA 2!


GERMANY-BINGWA2014









FIFA Leo hii imetoa Listi ya Ubora Duniani na Mabingwa wa Dunia Germany wameendelea kushika Namba Moja huku Tanzania ikiporomoka Nafasi 2 na kukamata Nafasi ya 112.
Kulikuwa hamna mabadiliko yeyote ya Timu 7 za juu lakini England, iliyokuwa Nafasi ya 20, imepanda Nafasi 7 na sasa kukamata Nafasi ya 13.
Barani Afrika, Ageria imeendelea kuwa juu kabisa ikiwa Nafasi ya 18 baada kushuka Nafasi 3.
Listi ya Ubora Duniani inayofuata itatolewa Tarehe 18 Desemba 2014.
20 BORA:
1        Germany                
2        Argentina    
3        Colombia     
4        Belgium       
5        Netherlands 
6        Brazil 
7        Portugal                
7        France
9        Spain           
10      Uruguay                 
11      Italy            
12      Switzerland  
13      England                 
14      Chile            
15      Romania                
16      Costa Rica   
17      Czech Republic       
18      Algeria        
19      Croatia        
20      Mexico

MRIDHI WA JAJA EMERSON AANZA MAZOEZI KWA AJILI YA MAJARIBIO NA YANGA SC

Kiungo Mbrazil, Emerson de Oliveira Neves Roque wa pili kulia akiwa mazoezini na wachezaji wenzake, Mbrazl Andrey Coutinho kulia, Hamisi Kiiza Hussein Javu asubuhi ya leo katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, Mabibo, Dar es Salaam. Emerson amewasili jana nchini kwa ajili ya majaribio Yanga SC. 

Kiungo Mbrazil, Emerson Roque leo ameanza kujifua katika kikosi cha Yanga.
Imeelezwa atafanya majaribio kwa wiki mbili, leo imekuwa siku ya kwanza.

Katika mazoezi hayo ya Yanga kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam kulikuwa na ulinzi mkali.

Emerson ambaye inaelezwa atachukua nafasi ya mshambuliaji, Jaja alionekana kama vile amezoeana na wachezaji wengine wa Yanga.


Pamoja naye, kiungo Coutinho na Kocha Marcio Maximo, nao walianza mazoezi yao kwa mara ya kwanza baada ya kurejea nchini, jana.

HII NDIO Kauli ya Bi Maria Nyerere kuhusu Escrow

Mjane wa Hayati Baba wa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, Maria Nyerere, amezungumzia sakata ya ESCROW iliyozungumziwa bungeni mjini Dodoma na kupendekeza ripoti ya mgogoro huo wa IPTL kujadiliwa kwa uwazi ili kupata ufumbuzi na wahusika kuwajibishwa kwa manufaa ya umaa.

GOR MAHIA: SSERUNKUMA HAENDI SIMBA

 
BAADA ya kuenea kwa taarifa kwamba Simba inasaka kwa udi na uvumba saini ya mshambuliaji Mganda Dan Sserunkuma kutoka Gor Mahia, klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Kenya (KPL) imekata mzizi wa fitna kwa kuamua kuongeza muda wa mkataba wa nyota huyo kukipiga nchini humo.
Katibu Mkuu wa Gor Mahia, Chris Omondi amekaririwa leo Jumatano na mtandao wa futaa.com akieleza kuwa wamefungua mlango wa mazungumzo na nyota huyo aliyetwaa kiatu cha mfungaji bora wa KPL msimu huu ili wamwongeze muda wa mkataba wake kubakia katika timu yao.
sere
Omondi amesema Sserunkuma, mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’, ameonesha nia ya kurefusha mkataba wake wa kukipiga na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Kenya.
“Tuko katika mazungumzo naye na ameonesha nia thabiti ya kuendelea kubaki katika timu yetu. Anajua kilichpo mezani na tunajua ni mchezaji muhimu; hivyo hapo ndipo tulipo kwa sasa,” amesema.
Sserunkuma, ambaye alijiunga na Gor Mahia akitokea Klabu ya Nairobi City Stars katikati ya mwaka 2012, alitia kambani mabao 16 msimu huu na kuiwezesha Gor kutetea taji lake la KPL.

BAADA YA KUTUA DAR MAXIMO AMWAGIA SIFA EMERSON MRIDHI WA JAJA

max

Kocha mkuu wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo ameamwagia sifa kiungo mkabaji Emerson De Oliveira Neves Rouqe huku akiutaka uongozi wa Yanga kusaka mechi mbili za kimataifa za kirafiki kabla ya kuivaa Simba Desemba 13 katika mechgi ya Nani Mtani Jembe 2 itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Maximo mara tu baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam leo Jumatano alasiri, amedai Emerson ana uzoefu mkubwa wa mechi za kimataifa na atakuwa msaada mkubwa kwa Yanga kwa vile ni mzuri wa kupandisha mashambulizi na kuilinda timu kushambuliwa.
“Kabla sijarejea Brazil, nilisema Yanga ina washmabuliaji wengi lakini inahitaji viungo wenye uzoefu na wenye nguvu. Emerson ana sifa hizo ndiyo maana nimeamua kuja naye afanye kazi. Kinachofuata atazungumza na uongozi, kisha programu nyingine zitaendelea,” Maximo amesema.
“Jaja nimepata taarifa kwamba ana matatizo ya kifamilia na hataweza kuja tena Tanzania lakini bado sijapata rasmi taarifa kutoka kwake ama wakala wake.”
jaja 1
KUJIPIMA KIMATAIFA
Aidha, kocha huyo wa zamani wa Taifa Stars amesema ameuagiza uongozi wa Yanga kuhakikisha timu yake inapata mechi mbili za kimataifa za kirafiki kabla ya kuikabili Simba katika mechi ya ‘Nani Mtani Jembe 2′.
Emerson, mzaliwa wa Rio de Janeiro, anatarajiwa kuanza majaribio kesho Alhamisi, kabla ya kufanyiwa vipimo vya afya na kusajiliwa kuchukua nafasi ya Jaja, ambaye atakumbukwa kwa mabao yake mawili mazuri aliyofunga wakati Yanga ikiiadhibu Azam FC mabao 3-0 katika mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 14.
Katika mechi 11 ambazo Jaja alipangwa katika Kikosi cha Yanga, alifunga mabao sita, moja katika mechi saba zilizopita za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) na matatu katika mechi za kirafiki pamoja na mawili ya ‘video’ yaliyowapa wanajangwani Ngao ya Jamii.

Monday, 24 November 2014

DOMAYO, KIMWAGA WAREJEA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU


Kiungo Frank Domayo na mshambuliaji Joseph Kimwaga wameondoka nchini kwenda kuendelea na matibabu nchini Afrika Kusini.


Wawili hao wameondoka kwenda kuangalia afya baada ya kuwa wamepata matibabu nchini humo hapo awali.

Nahodha John Bocco, aliwasindikiza vijana hao kabla ya kukwea pika kwenda Afrika Kusini.

Domayo na Kimwaga wanatarajiwa uwanjani raundi ya pili itakapoanza 

AMRI KIEMBA RASMI AZAM, AANZA MAZOEZI CHAMAZI

Igawa kumekuwa na hatua ya majadiliano kati ya Simba na Azam, hatimaye kiungo Amri Kiemba ameanza mazoezi leo.

Kiemba ameanza mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar.

Awali Azam FC ilitaka ipewe kiungo huyo kwa mkopo, lakini Simba ikakataa. nayo ikatangaza dau la dola 15,000 Azam FC ikakataa pia.

Lakini mambo inaonekana yameenda safi na Kiemba rasmi ameanza mazoezi Azam.

Sunday, 23 November 2014

TFF YATOA FURSA WADAU KUCHAGUA JEZI ZA TAIFA STARS!


SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA, TFF, limetoa fursa kwa Wadau kushiriki katika uchaguzi wa Jezi za Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Jezi zilizopendekezwa ni za aina mbili za kutumiwa Mechi za Nyumbani na nyingine ni Jezi za Ugenini na zipo aina kadhaa pamoja na Bukta zake tofauti.
JEZI-TAIFA-STARS
WADAU wanatakiwa watinge Tovuti ya TFF na kupiga Kura zao:

SPURS YAISHINDA 2-1NA LIVERPOOL WACHAPWA BAO 3-1


MATOKEO:
Jumapili Novemba 23
Crystal Palace 3 Liverpool 1        
Hull City 1 Tottenham 2   

Tottenham walitoka nyuma kwa Bao 1 walipocheza ugenini na kuifunga Hull City iliyocheza Mtu 10 Bao 2-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Hull walitangulia kufunga katika Dakika ya 9 kwa Bao la la Shuti la mbali la Jake Livermore.
Lakini Hull City walikatwa maini katika Dakika ya 50 baada ya Kiungo wao Gaston Ramirez kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwa kurudishia alipochezewa Rafu na Jan Vertonghen na huo ukawa mwanya kwa Tottenham kurudi kwenye Mechi.
Harry Kane akaisawazishia Tottenham Dakika ya 61 baada ya Frikiki ya Christian Eriksen kugonga mwamba na kumrudia na alikuwa Christian Eriksen aliewapa ushindi kwa Shuti la Mita 20 katika Dakika ya 90.
Matokeo haya yamewapandisha Tottenham hadi Nafasi ya 10 na kuwaacha Hull wakiwa na ushindi wa Mechi 1 tu katika Mechi 11 zilizopita.
VIKOSI:
Hull City: McGregor; Elmohamady, Dawson, Davies, Robertson; Huddlestone, Livermore; Ben Arfa, Ramírez, Brady; Jelavic
Akiba: Rosenior, Chester, Meyler, Hernandez, Sagbo, Harper, Quinn
Tottenham: Lloris; Dier, Fazio, Vertonghen, Davies; Eriksen, Mason, Dembele, Lamela; Soldado, Kane
Akiba: Chiriches, Lennon, Paulinho, Vorm, Stambouli, Ceballos, Ball

LIVERPOOL HOI, YAPIGWA 3 NA PALACE, NI KIPIGO CHA 3 MFULULIZO!


LIVERPOOL, wakicheza Ugenini huko Selhurst Park Jijini London, waliongoza baada ya Sekunde 90 tu kwa Bao la Rickie Lambert lakini wakajikutwa wakibwagwa chali na kukung’utwa Bao 3-1 na Crystal Palace katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Palace walisawazisha Bao katika Dakika ya 17 kwa Bao la Dwight Gayle alienasa Shuti la Yannick Bolasie lililopiga Posti na kumrudia.
Kipindi cha Pili Dakika ya 78 Joe Ledley aliwapeleka Palace mbele 2-1 na kisha Dakika 3 baadae Frikiki ya Mita 25 ya Mile Jedinak ilitinga na kuwapa Palace Bao lao la 3.
Mechi hii imewaacha Wadau wa Liverpool wakihoji uchezaji wa Nahodha wao Steven Gerrard na Raheem Sterling ambao wameonyesha kufifia mno.
Kipigo hiki cha Leo kinawafanya Liverpool wawe wamechapwa Mechi 3 mfulilizo za Ligi na kushinda Mechi 1 tu kati ya 5 zilizopita na kuwaacha wakiwa Nafasi ya 12 wakiwa Pointi 18 nyuma ya Vinara Chelsea.
Katika Mechi zao 2 zilizopita, Liverpool wametandikwa 2-1 na Chelsea na 1-0 na Newcastle.
VIKOSI:
Crystal Palace: Speroni, Kelly, Dann, Delaney, Ward, Bolasie, Jedinak, Ledley, Puncheon, Chamakh, Gayle
Akiba: Hangeland, Campbell, Zaha, Hennessey, Johnson, McArthur, Bannan.
Liverpool: Mignolet, Manquillo, Lovren, Skrtel, Johnson, Allen, Gerrard, Coutinho, Sterling, Lambert, Lallana
Akiba: Brad Jones, Toure, Moreno, Lucas, Can, Borini, Markovic. 
REFA: Craig Pawson
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumatatu Novemba 24
2300 Aston Villa v Southampton 
Jumamosi Novemba 29
1545 West Brom v Arsenal
1800 Burnley v Aston Villa          
1800 Liverpool v Stoke              
1800 Man Utd v Hull                 
1800 QPR v Leicester                
1800 Swansea v Crystal Palace            
1800 West Ham v Newcastle                
2030 Sunderland v Chelsea                  
Jumapili Novemba 30
1630 Southampton v Man City    
1900 Tottenham v Everton                  
Jumanne Desemba 2
2245 Burnley v Newcastle          
2245 Leicester v Liverpool         
2245 Man Utd v Stoke               
2245 Swansea v QPR                
2300 Crystal Palace v Aston Villa
2300 West Brom v West Ham     
Jumatano Desemba 3
2245 Arsenal v Southampton               
2245 Chelsea v Tottenham         
2245 Everton v Hull         
2245 Sunderland v Man City                
MSIMAMO:
BPL-TEBO-23NOV-B

Saturday, 22 November 2014

LEO ARSENAL v MAN UNITED: WENGER NA WASIWASI WA SANCHEZ! VIKOSI VYATAJWA


MENEJA wa Arsène Wenger ameingiwa na wasiwasi kuhusu Mechi yao ya Ligi Kuu England ya Leo Uwanjani kwao Emirates dhidi ya Manchester United hasa baada ya Mchezaji wake nyota Alexis Sanchez kuchelewa kurudi kutoka kwao Chile.
Sanchez alikuwa kwao huko Marekani ya Kusini kuichezea Nchi yake Chile ambayo Ijumaa iliyopita iliifunga Venezuela 5-0 na yeye kucheza Dakika 85 na kisha Juzi Jumatano walifungwa 2-1 na Uruguay na yeye kucheza Dakika zote 90.
Sanchez alirudi London Alhamisi Usiku baada ya safari ya Masaa 15 ya Ndege kutoka Santiago, Chile na Jana Ijumaa kujiunga Mazoezini na Arsenal.
Wenger amelalamika: “Ni bahati mbaya. Alionekana mchovu na itabidi nimcheki kabla ya Gemu na United. Lakini usimuulize, kwani ukimuuliza mwenyewe atasema yuko fiti!”
TATHMINI ya MECHI:
Arsenal wataingia kwenye Mechi hii ya Jumamosi wakiwa Nafasi ya 6 Pointi 1 tu mbele ya Man United ambayo iko Nafasi ya 7.
Mara ya mwisho Arsenal kuifunga Man United ni Mei Mosi Mwaka 2011 Bao 1-0 Uwanjani Emirates kwenye Mechi ya Ligi na tangu wakati huo wamecheza Mechi 6 na kutoka Sare 2 tu na zote zilizobaki Man United kushinda ukiwemo ushindi wa kishindo wa Bao 8-2 hapo Tarehe 28 Agosti 2012.
WENGER-KOTI
LVG-ZOEZI
JE WAJUA?
-Louis van Gaal ameshamvaa Arsene Wenger na Arsenal yake mara 2.
-Mechi hizo ni za Msimu wa 1999/2000 kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Van Gaal akiwa
Meneja wa Barcelona na kutoka Sare huko Nou Camp na kisha kuichapa Arsenal 4-2 Mjini London.

Man United wanaingia kwenye Mechi hii na Arsenal wakitoka kuifunga Crystal Palace na kabla ya hapo walikwenda Sare na West Bromwich Albion na Chelsea na kufungwa 1-0 na Manchester City huko Etihad Stadium.
Arsenal wao wanatoka kwenye kipigo cha 2-1 mikononi mwa Swansea City na kabla yake waliifunga Sunderland 2-0, kutoka Sare 2-2 na Hull City na kuchapwa 2-0 na Vinara Chelsea.

Uso kwa Uso
Arsenal v Man United
Mechi: 208
-Arsenal Ushindi 73
-Man United 87
-Sare 48
+++++++++++++++++++
Hali za Wacheza
Arsenal watakuwa nae Straika wao Olivier Giroud alievunjika Mguu Mwezi Agosti na huenda akacheza badala ya Danny Welbeck ambae Arsenal walimnunua kutoka Man United hapo Septemba Mosi.
Majeruhi wengine wa Arsenal ambao huenda wakacheza ni pamoja na Mikel Arteta lakini Theo Walcott bado hajawa fiti kwa Mechi na Mezut Ozil bado yuko nje akiuguza Goti lake.
Wachezaji kadhaawa Man United waliokuwa majeruhi wametangazwa kuwa fiti na hao ni pamoja na Angel Di Maria, Kipa David De Gea na Michael Carrick lakini upo wasiwasi kuhusu kucheza kwa Phil Jones, Rafael na Jonny Evans ambao ingawa wamepona majeruhi yao bado wanaonekana si fiti kwa Mechi.
Man United watawakosa Majeruhi Radamel Falcao na Marcos Rojo.
VIKOSI VINATARAJIWA:
Arsenal: Szczesny, Callum Chambers, Mertesacker, Monreal, Gibbs, Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Alexis Sanchez, Cazorla, Danny Welbeck
Man United: David De Gea, Rafael, Phil Jones, Jonny Evans, Luke Shaw, Anders Herrera, Michael Carrick, Angel Di Maria, Juan Mata, Wayne Rooney, Robin van Persie
REFA: Mike Dean
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumamosi Novemba22
1800 Chelsea v West Brom         
1800 Everton v West Ham          
1800 Leicester v Sunderland                 
1800 Man City v Swansea           
1800 Newcastle v QPR               
1800 Stoke v Burnley                 
2030 Arsenal v Man United                  
Jumapili Novemba 23
1630 Crystal Palace v Liverpool   
1900 Hull v Tottenham              
Jumatatu Novemba 24
2300 Aston Villa v Southampton 
MSIMAMO: