MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Friday, 28 February 2014

AHADI YA YANGA: KUFIA UWANJANI KESHO, AL-AHLY KUKIONA CHA MOTO!!

ruvushooting 
Mchezo wa kuwania kuingia hatua ya 16 bora wa Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika kati ya wenyeji timu ya Young Africans dhidi ya timu ya National Al Ahly utafanyika kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam huku tayari tiketi za mchezo huo zikinunuliwa kwa wingi na wapenzi wa soka kwa ujumla.
Young Africans ambao ndio wawakilishi pekee wa mashindano ya kimataifa nchini Tanzania kawa sasa watashuka dimbani kesho kwa lengo moja tu la kuhakikisha historia inaandikwa kwa kuvunja mwiko dhidi ya Waarabu na kuibuka na ushindi katika mchezo huo.
Kikosi cha Mholanzi Hans Van de Pluijm kimekuwa kikiendelea na mazoezi asubuhi na jioni katika Uwanja wa Boko Beach kujiandaa na mchezo huku morali ya wachezaji ikiwa i ya hali ya juu, saikolojia na kimwili wakiwa tayari kwa mechi.
Kuelekea mchezo wa kesho mchezaji pekee ambaye atakosekana ni Rajabu Zahir kutokana na kupata maumivu ya kuchanika nyama za msuli wa paja 
National Al Ahly ambao waliwasili jumatano asubuhi leo jioni majira ya saa 10:00 jioni watafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa tayari kwa kuuzoea kwa mchezo wa kesho kufuatia kufanya mazoezi kwa siku mbili katika shule ya IST Upanga.
Uongozi wa Young Africans umejiandaa na kuhakikisha kila kitu kinakwenda salama kwa upande wa wachezaji, utawala na washabiki watakaojitokeza kushuhudia mchezo huo ulioteka hisia za wapenzi wengi wa soka barani Afrika.
Mechi inatarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na milango ya Uwanja wa Taifa itafunguliwa mapema ili kupunguza msongamano wa watu watakaojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Wapenzi, wanachama na washabiki wa soka kwa ujumla wanaombwa kujitokeza kwa wingi kesho kuja kuipa sapoti timu ya Young Africans kwani ndio timu pekee inayowakilisha nchi na kupeperusha bendera ya Taifa katika mashindano ya kimataifa.

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAPOKEA MSAADA KUTOKA SHIRIKA LINALOSHUGHULIKIA IDADI WATU DUNIANI (UNFPA)

a_03396.png
Mwakilishi Mkaazi wa Shirika linaloshughulikia idadi ya watu Duniani (UNFPA) Mariam Khan akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Afya DK. Mohd Saleh Jidawi vifaa mbali mbali vya mama wajawazito na watoto vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 400 za Kitanzania. Hafla hiyo ilifanyika Wizara ya Afya Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
b_aec01.png




Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Mohd Saleh Jidawi akitoa shukrani kwa baada ya kupokea msaada wa vifaa vya afya vilivyotolewa na Shirika linaloshughulikia idadi ya watu Duniani.
c_46083.png
Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Afya waliohudhuri hafla ya kukabidhiwa vifaa vya Afya vilivyotolewa na Shirika linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA. 

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU MAUAJI YAFANYIKA KWA KISA CHA MAPENZI


Taarifa kutoka Mtwara  Kutoka kwa jeshi la polisi Mkoa wa mtwara ni kuhusu mauaji yaliyotokea huko Mtwara  ambayo chanzo chake kimeelezwa ni wivu wa kimapenzi uliokuwepo kati ya wapenzi hao.
Jeshi la Polisi limesema mauaji hayo yametokea Ligula B kata ya Ligula Tarafa ya Shangani mkoa wa Mtwara,ambayo yanamhusisha Habibu Dastan au Upson Milanzi[26] ambaye anatuhumiwa kumuua mpenzi wake Zuwena Mwapindi[27].
Kifo cha Zuwena kinasemekana ni baada ya kuchomwa na kisu kwenye ziwa  lake la upande wa kushoto,mtuhumiwa baada ya kufanya mauaji hayo alifanikiwa kutoroka lakini kwa ushirikiano wa wananchi na jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo akiwa eneo la Namayakata Tarafa ya Ziwani,Kata ya Nanguluwe,Wilaya ya Mtwara vijijini.
Mtuhumiwa anategemewa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika,MTANDAO HUU Umepata picha za marehemu lakini kutokana na sababu za kimaadili hatutoweza kuziweka hii chini ni picha ya mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi.

BENKI YA DUNIA YAISIMAMISHIA UGANDA MSAADA WA DOLA MILION 90

 
S_77135.png
Benki ya dunia imesitisha mkopo wa dola milioni 90 kwa Uganda wa kuimarisha sekta ya afya kufuatia kupitishwa kwa sheria inayoharamisha ushoga na kutoa adhabu kali kwa watakaopatikana na hatia
Hatua hiyo ya benki ya dunia haikutarajiwa na wengi kwani taasisi hiyo mara nyingi hujiepusha kuingilia masuala ya ndani ya kisiasa ya nchi wanachama au kuhusiana na masuala kama haki za mashoga, kuepuka kuzishurutisha nchi wanachame wake 188.
Hata hivyo msemaji wa benki hiyo David Theis amesema katika barua pepe kuwa wamesitisha mradi huo wa kuboresha sekta ya afya ya Uganda hadi watakapoufanyia tathmini na kuhakikisha malengo yake ya maendeleo hayataathiriwa na sheria hiyo mpya ya kuharamisha ushoga.
Rais wa benki hiyo Jim Yong Kim amewatumia wafanyakazi wake barua akisema benki ya dunia inapinga ubaguzi na itawalinda wafanyakazi wake wote na kuongeza kupitishwa kwa sheria hiyo ya Uganda sio nchi ya kwanza kufanya hivyo kwani ushoga umeharamishwa katika nchi 83 na zaidi ya nyingine 100 zinawabagua wanawake.
Mkopo ulikuwa uimarishe sekta ya afya
Licha ya kusimamishwa kwa mkopo huo wa dola milioni 90,benki ya dunia bado ina miradi mingine nchini Uganda ya kiasi cha dola bilioni 1.56. Mkopo huo ulitarajiwa kuidhinishwa hapo jana na ulipaswa kuangazia miradi ya kuboresha afya ya uzazi,afya ya watoto wachanga na uzazi wa mpango
Kutiwa saini kwa sheria hiyo ya kuharamisha ushoga Uganda na Rais Yoweri Museveni mapema wiki hii kumeibua shutuma kali kutoka kwa nchi za magharibi na mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Norway,Denmark na Uholanzi zimetangaza kuwa zitasitisha misaada kwa serikali ya Uganda kutokana na sheria hiyo na nchi nyingine wafadhili ikiwemo Marekani pia zimetishia kusitisha misaada na kutafakari upya uhusiano kati yao na Uganda.
Ghadhabu hiyo ya nchi za magharibi kuhusu kuharamishwa kwa ushoga ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha gerezani kwa watakaokutikana na hatia imeporomosha thamani ya shilingi ya Uganda na kusababisha Benki nchini humo kuingilia kati kwa siku mbili mfululizo
Kutiwa saini kwa sheria hiyo ya kuharamisha ushoga Uganda na Rais Yoweri Museveni mapema wiki hii kumeibua shutuma kali kutoka kwa nchi za magharibi na mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Norway,Denmark na Uholanzi zimetangaza kuwa zitasitisha misaada kwa serikali ya Uganda kutokana na sheria hiyo na nchi nyingine wafadhili ikiwemo Marekani pia zimetishia kusitisha misaada na kutafakari upya uhusiano kati yao na Uganda.
Ghadhabu hiyo ya nchi za magharibi kuhusu kuharamishwa kwa ushoga ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha gerezani kwa watakaokutikana na hatia imeporomosha thamani ya shilingi ya Uganda na kusababisha Benki nchini humo kuingilia kati kwa siku mbili mfululizo
Serikali ya Uganda haina wasiwasi
Hata hivyo msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo amesema Uganda inaweza kujiendeleza bila ya misaada kutoka nchi za magharibi na kuongeza Uganda haina wasiwasi na hatua hizo kwani ni wakati kwa Afrika kupinga ukoloni, utumwa na ubabe kutoka magharibi.
Mwanaharakati ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kuwatetea mashoga nchini Uganda Frank Mugisha alikutana na maafisa wa ngazi ya juu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani mjini Washington hapo jana kuomba usaidizi utakaowalinda mashoga.
Ofisi ya kutetea haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa umelaani kuchapishwa kwa majina ya watu wanaodaiwa kuwa mashoga nchini Uganda katika gazeti moja la udaku nchini humo na kuonya hatua hiyo inakiuka haki ya kuwa na faragha na kuonyesha wazi kuwa maisha ya mashoga yamo hatarini.
Kiongozi wa upinzani Uganda Kizza Besigye ameishutumu serikali kwa kutumia suala hilo kuwahadaa raia wa nchi hiyo ili wasiangalie masuala muhimu kama ufisadi au kuwepo kwa jeshi la Uganda Sudan Kusini

HAYA NDIO MANENO YA PNC KUHUSU KILICHOTOKEA KATI YAKE NA OSTAZ JUMA NAMUSOMA

 
pnc 
Usiku wa kuamkia February 26 uliingia kwenye headline kwenye mitandao ya kijamii na hii ni baada ya kusambaa kwa video na picha zinazomuonyesha Pancras Ndaki Charles au Pnc kupiga magoti mbele ya Ostaz Juma Namusoma kama kumuomba msamaha wa kurudi kwenye kundi.
Picha hizo zimeibua mambo mengi sana na baadhi ya wasanii na wadau wakubwa wakidai kuwa Ostaz Juma Namusoma kamdharirisha Pnc,miongoni mwa wasanii walioonekana kukerwa zaidi na kitendo hicho ni pamoja na member wa zamani wa kundi hilo Kitale na wadau wengine kama Adam  Juma,Suma Mnazaleth,Said Fela na wengine wengi.
31 
Hii ni nafasi naomba tuitumie kumsikiliza Pnc mwenyewe akielezea hali hiyo>>’‘Kuomba samahani hiki kitu sijaona kama ni kitu kibaya kwangu hata kupiga goti kumuomba samahani- kwa sababu hata baba yangu siku zote nilipokuwa nikimkosea yaani ilikua kawaida yangu,baba bana nisamehe yaani kwa kwa upande wetu ni heshima tu nimechukulia’
‘Kwa sababu  mwenyewe anadai yeye hajazijichapisha yeye zile picha,tulikuwa wengi kifupi sijajua siwezi kumlaumu nikasema ostaz umechapisha inshu zangu, kikubwa kuhusu haya mambo mi napotezea naangalia mambo yangu’
‘Unajua ostaz wanamchukulia kama kaka yangu wakinipigia simu ndugu zangu wananilaumu wewe umemfanya nini ostaz,tumeshaongea na ostaz kinachofuata sasa hivi ni kuingia studio na kufanya kazi zangu kama kawaida’.

ANGALIA KUHUSU AJALI YA BUSI KUGONGA TRENI LEO FEBRUARY 28 SINGIDA


bunda2

Hii ni Taarifa kutoka Mkoani Singida ambapo Habari zilizotoka zinahusisha ajali iliyohusisha  Basi la Bunda Bus lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Mwanza asubuhi ya February 28  limegongana na Treni Eneo la Manyoni mkoani Singida.
bunda3

Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana ingawa inawezekana  ni sababu ya Bus hilo kuingia njia ya treni,mpaka sasa idadi kamili ya majeruhi na waliopoteza maisha bado haijatangazwa,MTANDAO HUU  bado inafatilia chanzo cha ajali hii.
bunda4

bunda5

bunda1

RAISI KIKWETE AKUTANA NA MEYA WA MJI WA VALLEJO

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya sanamu ndogo ya mji wa Vallejo toka kwa  Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea  Ikulu  jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis alipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha na  Meya wa Mji wa Vallejo nchini Marekani Mstahiki Osby Davis na ujumbe wake walipomtembelea  Ikulu  jijini Dar es salaam Alhamisi Februari 27, 2014. Meya Davis yuko nchini na ujumbe wa wafanyabiashara 15 kutoka Vallejo wakiwa katika ziara ya kutafuta fursa za uwekezaji na ushirikiano. Mji wa Vallejo ni mji dada na wa Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.


TAARIFA YA TUME: RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO JIMBONI CHALINZE


Tume ya taifa ya uchaguzi imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo wa jimbo la CHALINZE, mtakumbuka kuwa jimbo hilo limekuwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo bwana Said Bwanamdogo kufariki dunia tarehe 22 Januari 2014 kwenye hospitali ya MOI jijini Dar es Salaam.
 
Ratiba ya uchaguzi kwenye jimbo hilo iko kama ifuatavyo:-
  1. Uteuzi wa wagombea - Tarehe 12 Machi 2014
  2. Kampeni na Uchaguzi - Tarehe 13 Machi 2014
  3. Siku ya Uchaguzi - Tarehe 6 April, 2014
Tarehe ya wagombea ubunge kuchukua Fomu za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi ni kuanzia tarehe 03 Machi, 2014 hadi tarehe 12 Machi, 2014 (siku ya uteuzi) kabla ya saa 10:00 Alasiri.
 
Wagombea wanatakiwa kuwasilisha fomu za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi siku ya uteuzi si zaisi ya saa 10:00 Alasiri.

KAYA ZAIDI YA 5000 ZA MANISPAA YA IRINGA KUFIKIWA NA MAJI SAFI NA SALAAMA

 
????????Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Kulia) akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Wataalam hao waliongozwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Watatu Kulia mwenye koti jeusi) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Wapili Kulia). ????????Viongozi wa msafara wa wataalam wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Bibi Florence Mwanri (Kushoto) na Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla, Prof. Longinus Rutasitara (Kulia) wakitaka ufafanuzi juu ya maendeleo ya mradi. ????????Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (Kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa hiyo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. ????????Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William (aliyenyanyua mkono) akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya tanki la kuhifadhia maji kwa ajili ya mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa. ????????Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto wa Uwanja wa Ndege wa Iringa (Nduli) ambao ni wanufaika wa mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ya Iringa , Bw. Ranier Nyimbo (Mwenye Fulana nyeusi) akitoa maelekezo wakati wa ukaguzi uliofanywa na wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango kwenye uwanja huo. ????????Baadhi ya wanavijiji wa Nduli na Kigonzile kutoka manispaa ya Iringa wakichota maji katika bomba pekee linalopatikana katika mpaka wa vijiji hivyo. Adha hii itaisha mwezi Juni mwaka huu mara baada ya kukamilika  kwa mradi wa maji unaolenga kuzifikia zaidi ya kaya 5000 za manispaa ikiwemo wanavijiji hawa. ????????Mhandisi wa maji wa Manispaa ya Iringa, Taphali Ngwada (Watatu Kulia) akiwaonesha wataalam kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango moja ya mabomba yatakayotumika kusambaza maji.
PICHA NA SAIDI A. MKABAKULI
………………………………………………………………………………………..
Katika kukamilisha ahadi na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 – 2016), Serikali imejidhatiti kuwafikishia maji safi na salama wakazi wa zaidi ya kaya 5000 za Manispaa ya Iringa kufikia katikati ya mwaka huu wa fedha.
Hayo yalibainishwa na Naibu Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri wakati wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayodhaminiwa na serikali na wafadhili.
Bibi Mwanri alisema kuwa katika kutimiza Mpango wa huo wa Maendeleo Serikali inawekea mkazo katika Kuendeleza adhma yake ya utekelezaji wa miradi ya maji iliyoibuliwa katika Programu ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) hasa katika maeneo sugu yenye upungufu wa maji hasa maeneo ya vijijini ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuuendelea kuimarisha usimamizi vyanzo vya maji.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Kaimu Mhandisi wa maji wa Mkoa wa Iringa, Mhandisi Kingazi William alisema kuwa kupitia Mpango huo wa Maendeleo wa Miaka Mitano zaidi ya vijiji 10 vya mkoa wa Iringa vitanufaika na miradi hiyo ya maji ambayo inagharimu zaidi ya milioni 600.
Maji ni eneo mojawapo la kipaumbele la kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano unaoratibiwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Maeneo mengine
ya vipaumbele yaliyoainishwa katika mpango ni pamoja na: miundombinu ya usafiri, nishati; kilimo; viwanda; maendeleo ya rasilimali watu; na huduma za jamii.

CAF CHAMPIONZ LIGI: MABINGWA AL AHLY HICHI NDICHO WANACHOJIVUNIA KUMFUNGA YANGA KESHO JUMAMOSI!

 AhlyTaarifa kutoka timu ya AL-AHLY imesema wanjivunia kuweka  rekodi nzuri katika kombe hili pia wanachezaji wazuri wenye kiwango wamesma jumamosi hii rasma wapigwe soma zaidi
MABINGWA WA AFRIKA, Al Ahly, Jumamosi wanaanza kampeni yao ya kutetea Taji lao wakitaka kulitwaa kwa mara ya 3 mfululizo huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwa kupambana na Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI.
Al Ahly ndio Klabu inayotamba Barani Afrika kwa kutwaa Ubingwa wake mara 8 lakini safari hii watapata upinzani mkali toka kwa Yanga ambao waliweka rekodi ya kupiga Bao nyingi kwenye Mashindano haya Msimu huu baada ya kuwafumua Komorozine ya Comoro Jumla ya Bao 12-2 katika Mechi mbili kikiwemo kipigo cha 7-0 katika Mechi ya kwanza.
Msimu huu, Al Ahly wamerudi kwenye Ligi ya kwao kutetea Taji lao la Mwaka 2011 baada ya Ligi hiyo kusimamishwa kutokana na vurugu Nchini Misri lakini hivi sasa wapo Nafasi ya 4 baada kufungwa Mechi 3 katika Mechi 9 za Ligi.
Mechi nyingine za mvuto za Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI ni ile ya Gor Mahia ya Kenya na Espérance Sportive de Tunis ya Tunisia ambayo ilifika Nusu Fainali Msimu uliopita.
Timu nyingine iliyofika Nusu Fainali Msimu uliopita ni Coton Sport ya Cameroun ambao wataanza Ugenini na Flambeau de l’Est ya Burundi.
TP Mazembe, Timu ya Congo DR inayowika Barani Afrika na ambayo inao Mastaa wawili wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, wao wataanza Ugenini na Les Astres de Douala ya Cameroon.
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Kwanza
Jumamosi Machi 1
Dynamos – Zimbabwe v AS Vita Club - Congo, DR
Young Africans – Tanzania v Al Ahly - Egypt
AC Leopards de Dolisie – Congo v Primeiro de Agosto - Angola
Flambeau de l’Est – Burundi v Coton Sport FC - Cameroon
Nkana FC – Zambia v Kampala City Council FC - Uganda
Gor Mahia – Kenya v Espérance Sportive de Tunis - Tunisia
Al Zamalek – Egypt v Kabuscorp - Angola
Kaizer Chiefs - South Africa v Liga Muculmana de Maputo – Mozambique
Stade Malien de Bamako – Mali v  Al-Hilal - Sudan
Jumamosi Machi 2
Enyimba International FC – Nigeria v AS Bamako - Mali
Entente Sportive de Sétif - Algeria         v ASFA-Yennenga - Burkina Faso
Berekum Chelsea – Ghana v Al Ahli - Benghazi - Libya
Les Astres de Douala - Cameroon v TP Mazembe - Congo, DR
The Barrack Y.C.II – Liberia v Sewe Sport - Ivory Coast
Horoya Athlétique Club – Guinea v Raja Club Athletic - Morocco

JAPANI KUTOSITISHA MISAADA YAKE NCHINI UGANDA

 
museven_akisaini_mswada_wa_kupinga_ushoga_e2e42.jpgNa Fadhy Mtanga
IKIWA ni siku chache tu tokea rais wa Uganda, Yoweri Museveni kutia saini sheria inayoharamisha ushoga nchini Uganda, serikali ya Japan imesema haitositisha misaada yake kwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Kauli hiyo imetolewa jana na balozi wa Japan nchini Uganda, Junzo Fujita. Fujita aliyasema hayo baada ya kuweka saini makubaliano yatakayoziwezesha jamii za mashariki na kaskazini ya Uganda kunufaika na msaada unaofikia kiasi cha dola za Kimarekani 203,183 kupitia mpango wa Grant Assistance for Grassroots Projects.

"Jambo hili (sheria dhidi ya ushoga) na misaada ni vitu tofauti. Kwa mtazamo wangu, watu wanaathirika na wanahitaji maji safi. Hatuwezi kufumba macho yetu eti kwa sababu ya jambo hilo (sheria dhidi ya ushoga)." Alisema Fujita.

Hata hivyo, balozi huyo alikiri wazi kuwa namna Japan inavyolichukulia suala la ushoga inatofautiana kidogo na nchi zingine wahisani kama Marekani na Uingereza. Akakubali kuwa kutiwa saini kwa sheria hiyo nchini Uganda kumechochea hasira kwa jumuiya ya nchi wahisani.

Lakini, Fujita akaweka wazi msimamo wa Japan akisema, "Tunawasiliana na serikali yetu nyumbani kuhusiana na hili – ili tufahamu kama tunapaswa kuungana na nchi wahisani zingine ama la."

Akasema kuwa nchi zote ikiwemo Uganda, zinawajibika kutii matakwa ya mikataba ya kimataifa ya haki za kibinadamu ambayo imeiridhia.

Wahisani wakasirishwa
Nchi wahisani zimeonesha kukasirishwa na hatua hiyo ya serikali ya Uganda. Kwa mujibu wa sheria mpya dhidi ya ushoga iliyotiwa saini na Yoweri Museveni siku ya Jumatatu jijini Entebbe, kosa la mapenzi ya jinsia moja litamfanya mtuhumiwa anayepatikana na hatia hiyo kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Waziri wa Fedha wa Sweden, Anders Borg ameionya Uganda kuwa hatua hiyo itaiathiri Uganda kiuchumi. Aliyasema hayo Jumanne wiki hii akiwa nchini Uganda kama sehemu ya ziara yake kwa nchi za Afrika Mashariki kwa madhumuni ya kupitia ukuaji wa uchumi katika eneo hilo.

"Sasa tunapitia upya mipango yetu ya usaidizi kwa Uganda na ni wazi tutalizingatia hili." Alisema Borg. Akaongeza kuwa tayari amekwishaifikisha hoja yake kwa Waziri wa Fedha wa Uganda, Maria Kiwanuka na Waziri Mkuu, Amama Mbabazi. Mkutano wake wa mawaziri hao waandamizi wa serikali ya Uganda ulifuatia mkutano wake na wanaharakati wa ushoga nchini humo.

Wakati hayo yakijiri, tayari Waziri wa Masuala ya Kigeni wa Marekani, John Kerry ametoa taarifa maalumu kuwa serikali yake inapitia upya uhusiano wake na Uganda ili kuondoa misaada yake kufuatia kusainiwa kwa sheria hiyo ambayo Marekani inasema ni ya kinyanyasaji yenye kukandamiza haki za kibinadamu.

Vile vile, nchi za Norway, Denmark na Uholanzi zimesimamisha rasmi misaada yake kwenye bajeti ya Uganda siku hiyo hiyo ya Jumatatu mara tu Yoweri Museveni alipotia saini sheria hiyo.

Uingereza nayo imeonesha nia ya kuacha kuisaidia Uganda huku Umoja wa Mataifa nao ukieleza wazi kuudhiwa na sheria hiyo. Katibu Mkuu Ban Ki-moon anapigia chapuo kufutwa haraka kwa sheria hiyo.

HIVI NDIVYO TFF NA POULSEN WALIVYO KUBALIANA KUVUNJA MKATABA

 
images_1edf8.jpg
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.
Uamuzi huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.
Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.
Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
Akizungumzia benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya Tanzania.
Amesema kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.
Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.
Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba.
Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union).
Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.
TWIGA STARS IMEWIVA, SHEPOLOPOLO YATUA
Wakati Zambia (Shepolopolo) imewasili leo mchana (Februari 27 mwaka huu), Twiga Stars imesema mazoezi yamewaingia barabara tayari kwa mechi dhidi ya Wazambia hao itakayochezwa kesho (Februari 28 mwaka huu).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itafanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni, na hakutakuwa na kiingilio.
Wakizungumzia mechi hiyo, Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage na nahodha wa timu hiyo Sophia Mwasikili wamesema kikosi chao kimewiva kwa ajili ya mpambano huo baada ya kufanyia kazi upungufu uliojitokeza katika mechi ya kwanza.
Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14 mwaka huu jijini Lusaka kwa mabao 2-1, na inahitaji ushindi ili iweze kusonga mbele kwenye michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika Oktoba mwaka huu nchini Namibia.
Iwapo Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Zambia katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa moja na Azam Tv itacheza raundi ya mwisho na Zimbabwe.
Msafara wa Shepolopolo una watu 26 ambapo wachezaji ni Anita Mulenga, Annie Kibanji, Carol Howes, Debora Chisanga, Emelda Musonda, Esther Mukwasa, Grace Zulu, Hazel Nali, Hellen Mubanga, Lweendo Chisamu, Meya Banda, Mirriam Katamanda, Misozi Zulu, Mupopo Kabange, Noria Sosala, Rachel Lungu na Susan Banda.
Viongozi ni Maclean Daka, Charles Bwale, Kaluba Kangwa, Enala Phiri, Cornelia Chazura, James Nyimbili, Besa Chibwe, Dorothy Sampa na Kabungo Katongo.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)