MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Thursday, 29 August 2013

TAARIFA RASMI YA KURUDISHWA KWA URUSHWAJI WA MATANGAZO YA RADIO IMANI FM NA NEEMA FM

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUREJESHWA KWA URUSHAJI MATANGAZO RADIO IMAAN FM NA KWA NEEMA FM RADIO


1.0 Utangulizi:

Mnamo tarehe 26/02/2013 Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa uamuzi wa kuvifungia vituo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kukiuka Sheria na Kanuni za Utangazaji.

Kamati ya Maudhui iliuita uongozi wa vituo hivyo tarehe 11/02/2013 na tarehe 14/02/2013 ili kujitetea na vyote vilikiri kosa. Baada ya kutafakari utetezi wa Radio Imaan na Radio ya Kwa Neema FM na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Utangazaji, Kamati iliamua kutoa adhabu kwa vituo vyote viliwi kama ifuatavyo:-

a)   Vituo vyote vilipewa  onyo pamoja na kufungiwa kurusha matangazo kwa kipindi cha miezi sita kuanzia
tarehe 26/02/2013;

b)  Vituo vyote vilitakiwa kuithibitishia Mamlaka ya Mawasiliano na Kamati ya Maudhui kwa maandishi kuwa hawatarejea kutenda kosa la aina hiyo au linalofanana na hilo. Ikiwa vitarudia Kamati ya Maudhui haitasita kuvifutia leseni zao za utangazaji.

2.0 Kutekeleza adhabu na hatua zilizochukuliwa na vituo hivyo na Mamlaka ya Mawasiliano:   

Baada ya Uamuzi huo kusomwa, vituo vyote viwili vilianza kutekeleza adhabu mara moja kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Mamlaka ya Mawasiliano ilipokea barua ya udhibitisho wa kutofanya kosa tena yaani “Commitment letter” pamoja na sera ya uhariri (Editorial Policy) na ratiba ya vipindi kutoka kwa vituo vyote viwili.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilifanya ukaguzi kwa vituo vyote viwili ili kujiridhisha na kuzipitia sera za uhariri pamoja na mwongozo wa vipindi kabla ya kuvifungulia.

3.0 Kurejeshwa kwa Matangazo

Kamati ya Maudhui iliandika barua tarehe 27/08/2013 kuhusu kuvifungulia vituo hivyo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kutumikia adhabu kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Vituo hivi vimeanza kurusha matangazo yake kuanzia leo tarehe 28/08/2013 baada ya muda wa adhabu kuisha.

Kamati ya Maudhui inapenda kutumia fursa hii kuvionya vyombo vya habari vya utangazaji vya redio na televisheni kuwa makini katika kutekeleza masharti ya leseni pamoja na kufuata Sheria na Kanuni za Utangazaji. Kamati ya Maudhui haitasita kutoa adhabu kali au kuvifungia vituo vitakavyokiuka Masharti ya leseni, Sheria pamoja na Kanuni za Utangazaji au hata kuvifutia leseni zao.

Kamati ya Maudhui inatoa wito kwa vyombo vya habari vya utangazaji kuzingatia Sheria, Kanuni na Masharti ya leseni ilikuboresha Sekta ya Utangazaji na kudumisha amani nchini.

Eng. Margaret Munyagi
Mwenyekiti,
Kamati ya Maudhui Ya TCRA,
S.L.P. 474,
DAR ES SALAAM.
28/08/2013

----

KUHUSU KAMATI YA MAUDHUI:

1.1. Kamati ya Maudhui ni kamati iliyoundwa kwa mujibu wa sehemu ya IV kifungu cha 26 (1) cha Sheria Namba 12 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, na marekebisho yake katika kifungu 173 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) Mwaka 2010

Kwa mujibu wa sheria, majukumu na kazi za Kamati ya Maudhui ni pamoja na:-

(a) Kumshauri Waziri wa Sekta kuhusiana na Sera ya Utangazaji nchini;
(b) Kushughulikia malalamiko kutoka kwa watangazaji na watumiaji wa huduma za utangazaji nchini;
(c) Kusimamia na kuhakikisha kuwa kanuni za utangazaji zinafuatwa.
(d) Kusimamia na kufuatilia maudhui ya vituo vya utangazaji.

1.2. Kamati hii ilianza kazi zake Oktoba 2012 baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (MB) tarehe 4 Desemba, 2012.

1.3. Kamati ya Maudhui inaundwa na wajumbe watano. Wanne ni wateuliwa wa Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Utangazaji na Mwenyekiti ambaye huchaguliwa miongoni mwa wajumbe wa Bodi ya TCRA. Muundo huo umetolewa na sehemu ya 26 (2) ya Sheria ya TCRA ya Mwaka 2003.

Majina ya wajumbe ni kama ifuatavyo:-

i. Mhandisi Margareth Munyagi -Mwenyekiti
ii. Bwana Walter Bgoya -Makamu Mwenyekiti
iii. Bwana Abdul Ngarawa -Mjumbe
iv. Bwana Joseph Mapunda -Mjumbe
v. Bwana Yusuf Nzowa -Mjumbe

Source
Kwa hisani ya wavutiblog

UVCCM YA PONGEZA KK YA CCM TAIFA KUMVUA UAWANA CHAMA MANSOOR HIMIDI

JUMUIYA ya UVCCM wilaya ya Dimani, imeunga mkono uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM uliotolewa Dodoma wa kumvua uanachama aliyekuwa Mwakilishi wa jimbo la Kiembe Samaki, Mansoor Yussuf Himid.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa UVCCM wilaya hiyo,Yussuf Ramadhan imeelezea kuwa umoja huo umepata faraja na imani kubwa kuona chama chao kikichukua na kufuata mkondo wa kinidhamu kukabiliana vurugu zilizokuwa zikifanywa na Mwakilishi huyo.

Alisema uamuzi huo usiishie kwa Mansoor pekee bali wanataka kila Mwakilishi, Mbunge na kiongozi yeyote wa CCM anaekwenda kinyume na sera za chama hicho achukuliwe hatua.

Alisema bado kuna Wawakilishi wengine wanaotoa matamko ya kukikebehi na kukikejeli chama huku kauli na misimamo yao ikiwa haina tofauti na ile ya upinzani.

Alisema umefika wakati kwa CCM kuwachukulia hatua za kimaadili Wawakilishi na Wabunge ambao mchana ni wana CCM na usiku hugeuka na kuwa maadui na wasaliti.

Imeandikwa na Mwandishi wa ZanziNews.com


 

Wednesday, 28 August 2013

MBUNGE WA JIMBO LA RUNGWE MAGHARIBI, PROFESA DAVID MWAKYUSA ACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 40

  KWA AJILI YA UJENZI WA KANISA LA SABATO LA SWEBO- NTOKELA WILAYANI RUNGWE.

Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa akizungumza na waumini wa kanisa la Wasabato wa Swebo Ntokela kuashiria ufunguzi wa harambee ya ujenzi wa kanisa.

Mgeni rasmi Profesa Mwakyusa akiwa meza kuu pamoja na viongozi wa Kanisa la Sabato siku ya harambee.
Kwaya ya Kanisa hilo ikitumbuiza kanisa hapo siku hiyo ya harambee.
Katibu mkuu wa kanisa la Sabato Jimbo la Nyanda za juu kusini Mchungaji Steven Letter akisoma neno la Mungu kuashiria ufunguzi wa Harambee hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa na waumini wakifuatilia kwa makini zoezi la Harambee lililokuwa likiendelea kanisani hapo.
Award Mpandila akisimamia zoezi la uchangiaji wa harambee lilipokuwa likiendelea.

Mwonekano wa jengo la kanisa hilo lilipoishia na kulazimu kufanya harambee ili kumalizia ujenzi wake.

Profesa David Mwakyusa Waziri wa Afya wa Zamani  na Mbunge wa sasa wa Jimbo la Rungwe Magharibi(CCM) amefanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Milion 40 katika harambee ya uchangiaji ujenzi wa kanisa la Sabato la Swebo lililopo Ntokela Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Katika Harambee hiyo  Profesa Mwakyusa ambaye alikuwa Mgeni rasmi, kabla ya kuanza kwa zoezi hilo aliwasihi waumini  wa kanisa hilo kuacha tabia ya kunung’unika pale wanapojitoa kwa ajili ya kusaidia shughuli mbali mbali za kikanisa ambazo zinafanywa na makanisa hayo  ili kusaidia jamii.

Imeelezwa kuwa baadhi ya waumini wamekuwa na moyo wa kujitolea pindi misaada mbali mbali inapohitajika katika makanisa, badala yake huanza kuumia  katika mioyo yao kwa kile walichotoa kwa kuona wametoa kiasi kingi.

Prof. Mwakyusa alisema  kama waumini wameamua kujitoa kwa ajili ya shughuli  za kanisa  hawana budi kunung’unika ndani ya nafsi zao kwani kazi ya mungu ni kujitolea si busara muumini kutoa msaada halafu ujutie baadaye.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi  mmoja wa wajumbe wa kamati  ya maandalizi  ya harambee hiyo  Bw.Awadi Mpandila  alisema kuwa lengo la kuanzisha ujenzi huo wa kanisa kulitokana na wingi wa waumini katika  kanisa hilo ambao wanafikia 835.

Award alisema kuwa ujenzi huo ulianza  mwaka 2002 na kiasi cha fedha kilichotumika mpaka sasa ni mil.279 na zinazohitajika ili kuweza kukamilisha jengo
hilo ni sh. Mil.90.

Mbali na kukamilika kwa Harambee hiyo Mpandila anatoa wito kwa wadau na marafiki wa karibu ambao walipewa kadi za mwaliko lakini walikwama kufika kuendelea kuchangia kutokana na fedha zilizopatikana kutokidhi kiwango.

Alisema fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kupaua na kumalizia jengo la kanisa hilo ambalo hatua za ujenzi wa awali umekamilika hivyo Wadau na marafiki wamekumbushwa kumtolea Mungu kupitia ujenzi wa kanisa hilo.

Hata hivyo katika harambee hiyo jumla ya sh. Mil.46 zilipatikana huku fedha iliyochangwa papo kwa papo ni sh. Mil.23 huku ahadi zikiwa mil.23 .

Aidha katika harambee hiyo ,Prof. Mwakyusa alichangia zaidi ya mil.2 pamoja na familia yake.

  Habari kwa hisani ya Mbeya yetublog

KAULI ZA JAJI MUTUNGI NA TENDWA BAADA YA KUAPISWA MSAJILI WA VYMA VYA SIASA

Picture: Mutundi-Kikwete-Tendwa
 
Msajili mpya wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amesema kazi iliyoo mbele yake ni ngumu, hivyo ameomba apewe miezi mitatu aifahamu kwanza ofisi kabla ya kuueleza umma matarajio yake, ikiwa ni pamoja na namna atakavyoshughulikia changamoto zote zinazoikabili ofisi aliyokabidhiwa kuisimamia.

Jaji Mutungi alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi na wa habari, muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, Ikulu, jijini Dar es Salaam juzi: “Mimi bado ni mgeni, nipeni muda niifahamu ofisi, najua kazi ni ngumu,” alisema Jaji Mutungi.

Alisema ugumu wa kazi katika ofisi hiyo, unatokana na matarajio ya jamii kwake kuwa makubwa, hivyo mategemo yake ni kupata ushirikiano kutoka kwa wadau, wakiwamo waandishi wa habari ili kufanikiwa kuzikabili changamoto hizo.

Hata hivyo, aliwahakikishia Watanzania kuwa kazi yake katika ofisi hiyo itakuwa ni kutenda haki tupu kama fani yake ya Uanasheria inavyomtaka atende: “Subirini nikiingia ofisini. Nipeni miezi mitatu,” alisema Jaji Mutungi.

Naye Msajili mstaafu wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ambaye alihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Jaji 
Mutungi jana, aliwataka Watanzania kumsaidia msajili huyo mpya kutenda mambo yote anayotarajia kuyafanya, kama vile kukuza demokrasia, ambayo alisema ndiyo msingi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.

Hata hivyo, Tendwa alisema kustaafu kwake siyo mwisho wa maisha, bali ni mwanzo wa maisha mengine mapya: “Ninawaaga Watanzania, ambao walikuwa wananiamini katika demokrasia. Mtu akikupiga madongo, usimrudishie atakuja kujuta,” alisema Tendwa na kuongeza: “Ukiona watu wengi wanakupigia makofi, jiulize je, wananipenda au wananipaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Kama hawakutaki shukuru.”

Alisema anachojivunia katika kipindi chake cha miaka 13 cha uongozi wa ofisi hiyo, pamoja na mambo mengine, ni kusimamia utitiri wa vyama, ambavyo vingi vimekuwa vikiishi kwa migongano, lakini akafanikiwa kuviweka sawa.

Tendwa aliteuliwa aliteuliwa kushika wadhifa huo Aprili 27, 2001 akichukua nafasi ya George Liundi.

Wengine waliohudhuria hafla ya kuapishwa kwa Jaji Mutungi jana, ni Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman; Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. Wengine ni Msajili Mkuu wa Mahakama, Ignas Kitusi; Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Hussein Katanga; pamoja na viongozi wakuu wa vyama vya siasa nchini. 

Jaji Mutungi aliteuliwa na Rais Kikwete kushika nafasi hiyo Agosti 2, mwaka huu. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Tendwa, ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria. Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

--- Habari ya maandishi imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la NIPASHE na picha kutoka IKULU.

 

KAGAME AKATA MGUU NCHINI TANZANIA "WABUNGE WA RWANDA WASYSIA KIKAO CHA BUNGE LA EALA"


 

Rais wa Rwanda, Paul Kagame
RAIS Paul Kagame wa Rwanda, sasa hayupo tayari kukanyaga ardhi ya Tanzania kutokana na kile kinachoonekana kuwa ni mgogoro wa kidiplomasia unaoendelea kati yake na Rais Jakaya Kikwete. MTANZANIA Jumatano limedokezwa.

Wakati hayo yakifikia hapo, kikao cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA), linakoketi mjini Arusha kilivunjika baada ya Spika wa bunge hilo, Magreth Zziwa, kugongana kauli na Mbunge mmoja wa Rwanda jambo lililosababisha wabunge wote wa Rwanda kususia kikao na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge.

Mwenendo wa hayo yaliyojitokeza jana katika Bunge la Afrika Mashariki hadi kikao kuvunjika, msingi wake ni mgogoro unaowagusa wakuu hao wawili wa dola.

Habari zilizolifikia gazeti hili toka katika vyanzo vyake mbalimbali vilivyo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, lakini pia katika vikao vya Bunge hilo la Afrika Mashariki vinavyoendelea jijini Arusha zinaeleza kuwa, Rais Kagame hata kama ataalikwa kuja nchini leo, hatakuja. 

Chanzo Mtanzania
 Jumatano, Agosti 28, 2013  
Na Waandishi Wetu

Tuesday, 27 August 2013

CHUJI AKATWA MSHAHARA KWA KUCHELEWA MAZOEZINI

 
Sh 50,000 imeondolewa katika mshahara wa kiungo nyota wa Yanga, Athumani Idd ‘Chuji’.

Kocha Mkuu, Ernie Brandts ndiye aliyepitisha uamuzi huo baada ya Chuji kuchelewa mazoezi ya jana.




Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Yanga kilieleza kwamba Chuji alijitahidi kujitetea baada ya kuchelewa nusu saa, lakini kocha huyo akasisitiza akatwe.


“Kocha alisema ni lazima akatwe mshahara kwa kuwa ilikuwa ni uamuzi aliousisitiza kwamba lazima kila mchezaji awahi.


“Chuji alijitetea kuwa ni majeruhi, lakini kocha akamuambia alijuaje hawezi kucheza na hiyo ni kazi ya dokta, hivyo akasisitiza tena lazima akatwe,” kilifafanya chanzo.



Brandts amepitisha adhabu ya wachezaji kukatwa fedha katika mshahara wao kila wanapochelewa mazoezini ikiwa ni sehemu ya kudumisha nidhamu katika kikosi chake.


chanzo salehjembeblog 

KAMATI KUU YA CCM YA BATILISHWA KUFUKUZWA KWA MADIWANI KAGERA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imejadili na kutolea maamuzi pamoja na mambo mengine suala la Madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera.

Katika maamuzi yake, Kamati Kuu imebatilisha uamuzi uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM ya Mkoa wa Kagera Agosti 13, 2013 wa kuwafukuza uanachama Madiwani hao.

Hivyo Madiwani hao wanane ni wanachama halali wa CCM.

Kamati Kuu imetoa uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera haikuzingatia Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2012 Ibara ya 93 (15). Ibara hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni:-

“Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na 
Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, isipokuwa kwa suala la kumvua uanachama au uongozi Diwani lisifanyike hadi Kamati Kuu imearifiwa na kutoa maelekezo”.

Aidha, Kamati Kuu imewaonya Madiwani wa CCM wa Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba Mjini na Meya kwa kusababisha kukosekana kwa utulivu, mshikamano na amani katika Manispaa na Chama.

Kamati Kuu pia imeitaka Serikali kufanya ukaguzi wa haraka wa mambo yanayolalamikiwa dhidi ya Meya ili ukweli ujulikane na hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za Mitaa.

Wakati tuhuma hizo dhidi ya Meya zikichunguzwa; Kamati Kuu inawataka Madiwani wa CCM  kurejesha utulivu kwenye Manispaa na Chama kwa ujumla ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi wa Bukoba.

Imetolewa na:-

Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM
ITIKADI NA UENEZI
27/08/2013
Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity

 

MAJABU YA MWAKA 2013:WANAFUNZI WOTE DARASANI WAFELI MTIHANI WA SEKONDARI



Wanafunzi wote walifeli mtihani wa kujiunga na chuo kikuu cha Liberia

Kwa mara ya kwanza katika historia ya Liberia, wanafunzi wote wamefeli mtihani wao wa mwisho wa sekondari na hivyo kumaanisha kuwa hakuna hata mmoja ambaye atafuzu kuingia chuo kikuu.
Waziri wa elimu wa Liberia amesema ameshinda kufahamu ni kwa nini hakuna wanafunzi hao wamefeli kiasi hicho.

Zaidi ya wanafunzi elfu ishirini na watano walianguka mtihani huo ambao ungewapa fursa ya kujiunga na chuo kikuu cha Liberia ambacho ni moja ya vyuo vikuu vinavyoendesha na serikali.

Lakini wasimamizi wa chuo hicho wameiambia BBC kuwa wanafunzi hao hawakuwa makini na ufahamu mzuri wa lugha ya Kiingereza ambayo ilitumiwa kuwatahini.
Taifa la Liberia linaendelea kujinasua kutokana na athari za mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyomalizika zaidi ya miaka kumi iliyopita.

Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, amekiri kuwa mfumo wa elimu nchini humo bado ungali duni na unahitaji marekebisho ya dharura.
Mwandishi wa BBC mjini Monrovia, anasema shule nyingi nchini humo havina vifaa vya kimsingi na waalimu waliohitimu.

Lakini hii ni mara ya kwanza katika historia ya taifa hilo kwa wanafunzi wote kufeli mtihani huo licha ya kulipa ada ya usajili ya dola ishirini na tano.

Chuo hicho kikuu ambacho kina idadi kubwa ya wanafunzi hakitakuwa na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wakati muhula mpya utakapoanza mwezi ujao.

Lakini wanafunzi wengi wanasema hawajaamini matokeo ya mtihani huo na waziri wa Elimu Etmonia David-Tarpeh, ameiambia BBC kuwa anatarajia kukutana na wasimamizi wa chuo hicho ili kujadili suala hilo.

WANAJESHI WA UN WASOMBWA NA MAJI DARFUR NCHINI SUDANI



Wanajeshi wa kutunza amani wa UN nchini Sudan.
Wanajeshi wanne wa kutunza amani wa Umoja katika eneo la Darfur nchini Sudan hawajulikani waliko baada ya kusombwa na mafuriko.
Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa, Rania AbdulRahman, amesema kuwa wanajshi hao walikuwa wakisindikiza msafara wa magari ya kutoa misaada, wakati waliposombwa na maji.

Afisa huyo amesema kuwa wanajeshi wengine wawili walipatikana wakiwa hai na kundi la uokoaji
Shirika la Umoja wa Mataifa wa Afya Duniani WHO, limesema kuwa zaidi ya watu laki tatu nchini Sudan, wameathiriwa na mafuriko na zaidi ya watu hamsini wamefariki mwezi huu.

Shirika hilo limesema kuwa eneo linalokaribia mji mkuu wa Khartoum ndilo limeathirika zaidi na mafuriko hayo ambayo ndiyo mabaya zaidi kuwahi kukumba eneo hilo kwa zaidi ya miaka ishirini na mitano iliyopita.

Wanajeshi wakwama kwenye mto

Kikosi cha Umoja wa Mataifa na kile cha Muungano wa Afrika katika eneo hilo la Darfur, UNAMID, ndilo kubwa zaidi duniani na lina zaidi ya wanajeshi elfu ishirini.

Mafuriko nchini Sudan

Wanajeshi hao wa kutunza amani walikuwa wakielekea eneo la Misterei, takriban kilomita hamsini, Kusini Magharibi mwa mji mkuu wa eneo hilo Geneina, na msafara wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, wakati msafara wao uliposomba na mafuriko.

Msemaji wa WFP Amor Almagro amethibitisha kuwa wafanyakazi wa shirika hilo la WFP waliokuwa kwenye msafara huo, watano kati yao raia wa Sudan na wawili wa mataifa ya Kigeni wako salama.
Umoja wa Mataifa haujatoa majina au uraia wa wanajeshi hao ambao hawajulikani waliko.

Mwaka uliopita, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, alilieleza baraza la usalama la Umoja huo kuwa wanajeshi watatu kutoka Tanzania walizama majini baada ya gari lao la kijeshi, kukwama katika mto mmoja nchini Sudan.
Katibu huyo mkuu vile vile alilieleza baraza hilo kuwa kikosi chake nchini Sudan kinakabiliwa na upungufu wa vifaa vya kutosha na vya kisasa, hali ambayo inaadhiriwa juhudi zao za kutunza amani katika eneo hilo la Darfur.

Wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa, wako katika eneo hilo la Darfur, kujaribu kumaliza mzozo uliodumu kwa miongo kadhaa kati ya wanajeshi wa serikali na waasi.
Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa zaidi ya watu laki tatu wameuawa kwenye mzozo huo wa Darfur.

NDUGU YAKE NA FREEMAN MBOWE AJIUNGA NA CCM KUTOKA CHADEMA

Picture
L-R: Grace Mbowe, Hassan Mtenga

DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea CHADEMA, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.

Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika CHADEMA, siyo kwa sababu ya familia.

Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.

Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai CHADEMA wanafanya propaganda za 
kuwadanganya wananchi.

Alisema itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya kifamilia, hivyo kwake siyo ajabu kuondoka CHADEMA, kwani kila mtu ana utashi wake wa kisiasa.

“Nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,”alisema Mbowe.

Alisema, “kuwapo kwangu CHADEMA siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia.”

“Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.
Picture: Grace Mbowe, Hassan Mtenga
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Hassan Mtenga kushoto akimkabidhi yadi ya CCM, Grace Mbowe, baada ya kutoka CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.
Aliviasa vyama vya siasa, kuwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi, yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa ushirikiano.

Awali, akipokea kadi ya CHADEMA, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.

Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi sasa amepokea wanachama 530.

Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo kitovu cha upinzani bali CHADEMA ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya CCM.

Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea. c  
chanzo kwa hisani za HabariLeo

 

HIGUAIN APATA AJALI NCHINI ITALIA, ASHONWA NYUZI KUMI

Mshambuliaji wa Napoli ya Italia, Gonzalo Higuaín ya boti na kulazimika kushonwa nyuzi kumi tu baada ya kufikishwa hospitali.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo na kuripotiwa na gazeti moja la Italia zimeeleza, Higuain raia wa Argentina aliumia wakati akiendesha boti iliyogonga mwamba katika kisiwa cha Capri, nchini Italia.


Capri ni kisiwa ambacho watalii wengi hupenda kwenda kupumzika na Higuain alikuwa katika mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na Seria A.

 Imeelezwa aliteleza na kuangukia kwenye mawe hali iliyomsababishia majeruhi hayo na baada ya kufikishwa hospitali na hali yake inaendelea vizuri.
 Daktari katika Hospitali ya Capilupi, Mauro Ingrosso amethibitisha kuumia kwa Higuain na kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.

 “Ni kweli na tumemshona nyuzi kumi, kati ya hizo nane ni upande wa shavu na mbili chini ya kidevu lakini anaendelea vizuri sana,” alisema.

 Higuain amejiunga na timu hiyo ya Italia akitokea Real Madrid ya Hispania na huu ni msimu wake wa kwanza.

PSG YAONYESHA JEURI YA FEDHA, YATENGA EURO MILIONI 40 KUMSAJILI PEDRO WA BARCA

Matajiri wa Ufaransa, PSG wamezidi kuonyesha jeuri ya fedha baada ya kuibuka na kuweka mezani dau kubwa la euro milioni 40 wakitaka kumsajili Pedro wa Barcelona.

Dau hilo kubwa na la kushtukiza na uongozi wa PSG umetangaza dakika chache zilizopita kwamba unataka kumsajili Pedro.


Bado Barcelona haijasema lolote kuhusiana na ofa hiyo ambayo kabla haikuwa imetegemewa kwamba PSG wangeitangaza katika hatua za mwisho za usajili.

MESSI AKATAA KUCHEZA BARCELONA, ATAKA 100%




Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi amesema anaweza kucheza katika mechi inayofuatia ya timu yake hiyo lakini hatafanya hivyo.

Messi raia wa Argentina amesema atarudi katika kikosi hicho hadi pale atakapoamini yuko fiti kwa asilimia mia.

 
Awali ilionekana huenda alikuwa amejerea katika hali yake ya kawaida, lakini baadaye akasisitiza asingependa kubahatisha.

“Mpira ni maisha yangu, natamani kucheza kila wakati. Ninaamini sasa ni vizuri nikawa mvumilivu na kusubiri hadi pale nitakapokuwa fiti kabisa,” alisema.

Messi aliumia katika mechi ya kwanza ya Super Cup dhidi ya Atletico Madrid na timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.

JENGO LA "SAMAKI SAMAKI" MBEZI LAUNGUA MOTO MUDA MFUPI ULIO PITA

Taarifa zilizopatika muda mfupi uiopita inapasha kuwa kiota cha starehe cha Samaki Samaki tawi la Africana huko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kimeteketea kwa moto ambao chanzo chake halisi hakijajulikana bado.

Timu ya mafundi wa DAWASCO wanaokarabati na kuhamisha bomba la maji walikuwa katika eneo hilo.

Hizi ni picha zilizotumwa mitandaoni za kilichotokea kabla ya zimamoto kufika na kuanza juhudi za kuzima moto huo usisababishe madhara zaidi.

Hizi ni picha zilizotumwa mitandaoni za kilichotokea kabla ya zimamoto kufika na kuanza juhudi za kuzima moto huo usisababishe madhara zaidi.

 

CHUO KIKUU CHAWEKA UTARATIBU WA KUVAA KOFIA ILI KUZUIA WANAFUNZI KUIBIA MAJIBU

Wakufunzi katika chuo kimoja huko nchini Thailand wamelazimika kufuta utaratibu wa wanachuo kuvaa kofia zilizoundwa kwa makaratasi katika vyumba vya mitihani ili kuzuia wasichunguliane mitihani na majibu.

Picha mbili zilizowekwa kwenye ukurasa wa Facebook (sasa hivi zimeondolewa), zilionesha namna wanafunzi hao walivyokuwa katika moja ya vyumba vya mtihani. Watu waliotoa maoni mbalimbali walipinga vikali na hata kulaani uvaaji kofia hizo.

Mmoja wa wahadhiri wa chuo hicho aliyehojiwa na chombo kimoja cha habari kuhusu utaratibu huo, alisema kuwa ni mbinu waliyokuja nayo wanachuo wenyewe walipoulizwa ni kwa namna gani wanadhani wanaweza kujilinda wenyewe dhidi ya kuibia majibu ya mitihani, na asiliani haukuwa utaratibu wa chuo. Mhadhiri huyo akasema kwa kuwa picha hizo zimeibua gumzo na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wahadhiri wa chuo  hicho, wamelazimika kufuta utaratibu huo na kuwaomba wanachuo watunge mbinu mpya.

Baadhi ya wachuo walihuzunika kwa mbinu yao kupokelewa vibaya, tofauti na walivyoifurahia wao.
Picture
Hii nipicha ya wanafunzi wa Kasetsart University wakifanya mtihani  (picha na: odditycentral.com)

Picture 
habari kwa hisania ya The NPR.

 

MWANAMKE MWINGINE WA KITANZANIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA DUBAI AIRPORT

Picture: Tanzanian Woman caught with drugs in Dubai
Photo of a woman caught with Dhs3 million of drugs (photo: Yahoo! News)
A cross-post from Yahoo! News — A woman caught with Dhs3 million of drugs in her suitcase claims she was unwittingly being used as a mule by her husband, Dubai Police said.

The Tanzanian woman was arrested at Dubai International Airport in transit to her home country from Brzail. She claims her husband arranged for her to go on a three-month trip to Brazil so that she could unwind.

However, she told officers that while on holiday, a friend of her husband asked her to take some bags back to Tanzania. She was arrested in Dubai after officers at theairport became suspicious of her behavior. They found 3kg of cocaine in herluggage, worth Dhs3 million.

“She claimed that her husband got her in trouble as he offered her a relaxing trip to Brazil and she went for three months. Her husband’s friend asked her to deliver the bags to her husband in Tanzania,” an official in anti-narcotics said. The suspect has been referred to public prosecution.

ANGARIA ORODHA YA WALIO KAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA 2009--2013

Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa amenukuliwa kutoa orodha ya waliokamatwa wakisafirisha dawa za kulevya kutoka mwaka 2009 hadi Mei, 2013.

“Tumewakamata ‘mapapa’ (wauza unga wadogo) wengi sana na tunahakikisha kwamba ‘nyangumi’ (wauza unga vigogo)  nao hawachomoki. Mara nyingi vigogo wamekuwa wakiwalisha kiapo kibaya vijana wanaowabebesha unga kwamba  ikitokea wakakamatwa wasiwataje lakini nao tunawabana kitaalam mpaka wanawataja, kwa sasa bado tunaendelea kuwadaka,” amenukuliwa kusema Kamanda Nzowa.

Orodha hii inabainisha kiasi na aina ya madawa waliyokamatwa nayo katika mabano.

Steven  Gwaza, (heroin gramu 825.7), Rebecca Wairimu Mwangi (heroin gram 1,800), Khatibu Bakari Khatibu, Khalid Salim Maunga, (cocaine gramu 1,007.4), Dhoulkefly  Awadh, (cocaine gramu 893.58), Abdallah Pashua Kipevu (heroin gramu 31,000), Diaka Brama Kaba (heroin gramu 31,000), huyu alikamatwa akiwa na Ndjane Abubakar, Sylivia Kaaya Namirembe, Farid Kisuule, Robinson Dumba Teise na Ismail Mugabi.

Wengine ni Rashid Salim Mohamed, (cocaine gramu 1,374.32), Mini Thabo Hamza (cocaine gramu 1,595.74), Hamis Mohamed Mtou (cocaine gramu 850), Kwako Sarfo, Mnigeria (cocaine gramu 1,1951.80), Mustapha Musa (cocaine gramu 286), alikuwa na Aman Saidfadhil Daruweshi na Afshin  Jalal.

Kamanda Nzowa akaendelea kuwaanika, Jack Vuyo, (heroin gramu 42,000) huyu alikuwa na Anastazia Elizabeth Cloete. Simon Eugenio Fadu (cocaine gramu 8,000), Assad  Aziz, (heroin gramu 50,000), alikuwa na
Isamil Shebe Ismail, Rashid Salim na Majed Gholamghader.

Wengine kwenye orodha hiyo ni, Anna  Jamaniste Mboya, (cocaine gramu 1,140), Fredy William Chonde (heroin gramu 175,000),  Kambi Zuber, Abdul Ghan na Shahbaz Malik, Livinus Malik (Wapakistani) (cocaine gramu 804.7), Chukwudu  Denis Okechukwu, Paulo Ekechukwu na Hycenth Stan (Wanigeria) (cocaine gramu 81,000).

Aidha wapo, Shoaib S.O. Mohammed, Fedro Alfredo Chongo, (cocaine gramu 1,530), Kadiria  Said Kimaro (heroin gramu 1,365.91),  Abdallah Rajab Mwalimu (cocaine gramu 716.5), Mwiteka Godfrey Mwandemele (cocaine gramu 1,112),  Abbas Kondo Gede (cocaine gramu 1,112), Mwanaidi  Ramadhan Mfundo (cocaiane gramu 5,000), alikuwa na Sarah David Munuo,  Antony  Karanja, Benny Ngare,  Almasi Hamis Said, Yahya Haroun Ibrahim, Aisha Said Kungwi, Rajab Juma Mzome na John  William Mwakalasya.

Wengine ni Ally Mirzai Pirbakhshi (cocaine gramu 97,000) alikuwa na Aziz Juma Kizingiti, Said Mashaka Mrisho, Abdulahman  Mtumwa na Hamidu Kitwana Karimu.

Ramadhan Athuman (heroin gramu 3,000) alikuwa na Rashid Mohammed, Ally Mohammed Kichaa na Issa Abdulahman. Rashid  Ally Mtopea (heroin gramu 12,000) alikuwa na Idd Adam Mwaduga, Nurdin Adam. Maurine Amatus Lyumba, John  Adams Igwenma  wa (Mnaijeria) (cocaine gramu 830.19).

Upendo Mohammed Cheusi, Abdallah Omar Salum (cannabis sativa gramu 1,000) alikuwa na Cosmos Chukwumezie, Ifeanyi  Malven Kalu Oko (Wanaijeria)  (heroin gramu 3,185.38), Allan Duller (cocaine gramu 3,882.92), Alberto Mendes kutoka Ghana, (gramu 1,277.10 za heroin).

Wengine ni Joseph Chukwumeka Nwabunwanne (Mnaijeria), (gramu 1,245.96 za heroin) Kwaku Safo Brobbey Mghana (gramu 13,781.78 za heroin), Princewill Ejike Mnigeria (gramu 981.12 za heroin), Mary Mvula (Mzambia) (gramu 391.51 za cocaine), Waziri Shaban Mizongi, (gramu 2,013 za heroin) akiwa na Santos Joseph Mpondela, Kelvin Kelven Mwazeni.

Wengine ni Emmanuela Adom, (Mghana) (gramu 9,838.1 za cocaine), Asha Omary Ramadhan, (gramu 1.56), Mariam Mohammed Said, (gramu 9,857.54 za bangi) akiwa na Abdullatif A. Fundikira.

Aliendelea kuwataja Marceline Koivogui, Mghana (gramu 1,073.82 za heroin), Edwin Cheleh Swen Mliberia (gramu 1,509.35 za heroin),  akiwa na Benjamin Obioma Onuorah  wa Nigeria, Sofia Seif Kingazi, (gramu 3,379.54 za cocaine), Josephine Mumbi Waithera Mkenya (gramu 3,249.82 za cocaine), Iddi Juma Mfaume,( gramu 563.25 za heroine), Amina Kassim Ramadhani,( gramu 1,980.11 za heroine) na Vivian Edigin Mnigeria ( gramu 797.56 za cocaine), Hadija Tambwe,( gramu 33,507.04 Za cannabis), Sasha Farhan na Mnyeke Sativa, na Mychel Andriand Takahindangeng (Muindonesia), ( gramu 3,932.44 za cocaine).

Wengine ni Kristina Biskavevskaja Mluthenia (gramu 4,000 za cocaine), Stephen Basil Ojiofor Mnigeri (gramu 1,173 za cocaine), Judith Marko Kusekwa, (gramu 1,793 za heroin), Khamis Said Bakari, (gramu 1,793 za heroin).

Kundi la mwisho ni Tabia Omary au Neema Omary (gramu 994.97 za  heroin), Masesa au Habiba Andrew Joseph, (gramu 1,037.9 za heroin).

 

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA MH MUTUNGI APASHWA LASMI JANA IKULU

Picture
Rais Jakaya M. Kikwete akimwapisha Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi Ikulu jijini Dar es Salaam leo. (picha: Ikulu)

 Chanzo habarihi kwa hisani ya Ikulu blog

TANROADS WAANZA MKOANI MBEYA BOMOABOMOA BARABARA YA MBEYA CHUNYA

wakazi wa isanga mbeya waingia kiwewe kuvunjiwa nyumba zao

Baadhi ya  ya wakazi wa Isanga Mbeya wakiwa hawaamini kinachotokea




 

 






 





 








Picha kwa hisani ya mbeya yetublog