MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday, 9 April 2016

VIDEO: Skendo ya wanajeshi wa JWTZ Congo, yazungumziwa na makao makuu


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) chini ya Umoja wa Mataifa limekuwa likitekeleza majukumu ya ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa takribani miaka mitatu. Siku kadhaa zilizopita ziliripotiwa taarifa za kulituhumu jeshi hilo kuhusika na unyanyasaji wa kijinsia unaodaiwa kufanywa kwa wananchi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
April 08 2016 kutoka makao makuu ya Jeshi hilo wametoa taarifa za kusikitishwa na tuhuma hizo na hapa Afisa Habari wa Jeshi hilo James Macheta, ameyazungumza haya….>>>’Jeshi letu haliwezi kupuuza taarifa hizo, hivyo limeanza kuchukua hatua za kiuchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo ingawa rekodi za majukumu ya ulinzi wa amani zilizokwishafanywa na jeshi letu zinaonyesha hakukuwa na tuhuma kama hizo’.
UNAWEZA KUANGALIA TAARIFA NZIMA ILIYOTOKA MAKAO MAKUU YA JWTZ KWENYE VIDEO HII HAPA CHINI

Samatta apiga bao la 3 baada ya timu yake kuibuka kwa ushindi wa 4-0

  
Headlines za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kuzidi kufanya vizuri zinazidi kuongezeka kila kukicha ndani ya Ligi Kuu Ubelgiji akiichezea klabu ya KRC Genk.
Samatta amerudi kwenye headlines baada ya kocha wa klabu ya KRC Genk kumpa nafasi ya kucheza mechi dhidi ya KV OostendeKRC Genk imeibuka na ushindi wa goli 4-0, lakini kama kawaida Mbwana Samatta alifunga goli la tatu la Genk dakika ya 77 baada ya kuingia dakika ya 77 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis. nakumbuka samata anavaa jezi namba 77
Goli la Samatta lilifungwa baada ya Samatta kutumia vyema pasi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Neeskens Kebano. Goli hilo linakuwa goli la tatu kwa Samatta toka ajiunge na klabu ya KRC Genk.
Video ya goli la Samatta

Friday, 8 April 2016

Ridhiwani Kikwete Akana kufanya biashara na Kampuni Ya Lugumi Inayotuhumiwa na Jeshi la Polisi



Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekanusha taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Lugumi, inayodaiwa kupewa zabuni ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole kwenye vituo vya Polisi.

Ridhiwani ametajwa katika habari hizo kuwa ni mmiliki wa kampuni ya Lugumi pamoja na wamiliki wengine ambao ni Said Lugumi na aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema.

Ridhiwani ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema yeye hahusiki na kampuni yoyote ya Lugumi ingawa wana urafiki wa kawaida na mmiliki wa kampuni hiyo.

“Kwanza kabisa mimi si mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo, hilo ni jambo la msingi kabisa watu waelewe na sijawahi kufanya biashara yoyote na Lugumi. Said Lugumi ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo tunafahamiana naye na ni rafiki yangu,” alisema Ridhiwani.

Ridhiwani alisisitiza kuwa hana uhusiano wa kibiashara na mtu huyo na kwamba hafahamu ni kwa nini amehusishwa na kampuni ya Lugumi.

“Hapa ni watu tu wanaamua kuingiza tu maneno yao, haya maghorofa ninayotajwa kumiliki Dar es Salaam hata sijawahi kutembelea ujenzi wake, wameamua kuniingiza, Lugumi nafahamiana naye binafsi tu lakini wananiingiza,” alisema Ridhiwani.

Alisema jambo hilo bado liko ndani ya Kamati ya Bunge na baadae ameliona kwenye magazeti ya juzi kuwa Jeshi la Polisi litatoa taarifa yao, hivyo asingependa kulizungumzia kwa undani.

Hivi karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilitoa siku saba kwa Jeshi la Polisi nchini kupeleka mkataba walioingia baina yao na Kampuni ya Lugumi.

Kamati hiyo ilipokutana na Jeshi hilo kupitia taarifa ya hesabu zao za mwaka 2013/14 zilizokaguliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Aeshi Hilaly alisema jeshi hilo mwaka 2011 liliingia mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya kufunga mashine za kuchukua alama za vidole katika vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima ambavyo viko 108.

Alisema mkataba huo ulikuwa wa Sh bilioni 37 pamoja na kodi na kwamba hadi sasa kampuni hiyo imeshapewa asilimia 99 ya fedha zote ili hali vituo vilivyofungwa mashine hizo ni 14 tu, kati ya vituo vyote 108.

Ridhiwani alisema angependa jamii ifahamu kuwa hana uhusiano na kampuni hiyo kwa kuwa hafahamu kabisa hata malipo yaliyofanywa kati ya Serikali na kampuni ya Lugumi anasikia tu kama ambavyo watu wengine wamesikia.

Wachina kizimbani kwa kukwepa kulipa kodi


Raia wawili wa China, Ma Jun na Huifang Ma leo wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashtaka mawili likiwamo la kushindwa kutumia  Mashine ya Kodi za Kielektroniki (EFDs) katika biashara zao.

Jun na Ma, ambao wote ni  wafanyabiashara na wakazi wa Mtaa wa Narung’ombe eneo la Kariakoo wanakabiliwa na kushindwa kutumia mashine za EFDs pamoja na kushindwa kujisajili katika kodi ya ongezeko la Thamani(Vat) wakati wakijua kufanya hivyo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo, mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Jun hakuwepo mahakamani hapo kwa madai kuwa yupo nje ya nchi na upande wa mashtaka umeiomba Mahakama kutoa hati kwa ajili ya kumkamata mshtakiwa huyo.

Akisoma hati ya mashtaka, mbele ya Hakimu Mkazi Mwanadamizi Mfawidhi wa mahakama hiyo Said Mkasiwa, Wakili kutoka Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), Cherubin Chuwa alidai kuwa washtakiwa kwa pamoja walitenda  makossa hayo Machi 23,mwaka huu.

Chuwa alidai siku hiyo ya tukio, washtakiwa hao ambao wanamiliki Kampuni ya HM Textile  Co Ltd  Iliyopo  block 54 katika kiwanja namba 6 kilichopo mtaa wa Agrey  eneo la Kariakoo, walishindwa kutumia  mashine za EFDs kwa ajili ya kutoa risiti kwa wateja wao ambao walikuwa wanafanya manunuzi mbalimbali katika duka hilo ambalo linauza mapazia na nguo mbalimbali, huku wakijua kuwa ni kosa kisheria.

Mwandesha Mashtaka huyo aliendelea kudai kuwa, katika shitaka la pili ambalo pia linawakabili washtakiwa wote, inadaiwa kuwa muda na siku hiyo  hiyo katika duka hilo, washtakiwa walishindwa kujisajili katika kodi ya ongezeko la Thamani(Vat) wakati wakijua kufanya hivyo kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Chuwa alidai washtakiwa hao walishindwa kujisajili katika Kodi ya Ongezeko la Thamani(Vat) ambayo ni kinyume cha sheria , na kwamba mashtaka hayo yamefunguliwa kupitia sheria za TRA.

Hata hivyo mshtakiwa wa  pili, Huifang  alikiri shtaka la kwanza huku shtaka la pili akikana kuhusika.

Kutokana na hatua hiyo wakili Chuwa alisema dhamana ya mshtakiwa huyo iko wazi ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kila kutoka taasisi inayotambuliwa kisheria watasaini bondi ya Sh 3milioni na kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafiria.

Mshtakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi April 21, mwaka huu.

Mrema Amuomba Rais Magufuli Atimize Ahadi yake ya Kumpa KAZI Kama Alimwahidi Wakati wa Kampeni



Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) taifa, Augustine Mrema amemuunga mkono Rais John Mgufuli kwa kasi yake ya kupambana na ufisadi na kumuomba ampe kazi ili amsaidie kutekeleza jukumu hilo.

Mrema alimuomba Rais Magufuli atambue uzoefu wake kwa kukumbuka jinsi alivyopambana na mafisadi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu.

Huku akieleza CV yake hiyo, Mrema alimkumbusha Rais kuhusu ahadi aliyompa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka jana, ya kumpa kazi katika Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa atashinda na kuwa Rais.

Akizungumza na waandishi wa habari kijijini kwake Kiraracha mkoani Kilimanjaro, Mrema alisema kuwa anasikitishwa na ukimya wa Rais Magufuli kwa sababu aliamini kuwa angetekeleza ahadi hiyo ya kumpa kazi muda mfupi baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri, jambo ambalo hadi sasa hajalifanya.

Alisema, alikutana na Rais Magufuli mwaka jana katika kampeni jimboni Vunjo kwenye eneo la Njia Panda lililopo ndani ya mji mdogo wa Himo na kuambatana naye kwenye mkutano wa hadhara, ambapo alimwombea kura kwa wafuasi wake na kuahidiwa ajira.

“Katika kampeni, Dk Magufuli alifika kwenye mkutano wangu nikamwombea kura kwa kuwaambia watu wangu wamchague kwa kuwa ni mchapakazi na mwadilifu. Aliahidi kunipatia kazi katika Serikali na sasa namkumbusha na kumuuliza mbona yupo kimya?” Mrema alieleza na kuhoji.

Alipoulizwa ni kazi gani inayomfaa katika Serikali ya Magufuli, alisema yeye alishawahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu hivyo yuko tayari kufanya kazi yoyote itakayomfaa ila alitamani zaidi kupangwa sehemu nyeti ili amsaidie kutumbua majipu.

Mrema alimpongeza Rais Magufuli kwa jitihada binafsi za kutumbua majipu anazozifanya na alijigamba kuwa yeye ndio mwenye uzoefu wa kupambana na mafisadi kutokana na rekodi yake nzuri ya kipindi cha Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.

Katika hatua nyingine, Mrema alikanusha taarifa ya kuhongwa fedha ili kufuta kesi ya kupinga matokeo aliyoifungua dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo, James Mbatia.

Alisema, taarifa hizo ni za kupuuzwa kwa sababu zinalenga kumpaka matope kwa wananchi wake wa Vunjo.

Mrema alieleza kuwa walifikia maridhiano ya pamoja kuhusu kuondoa kesi hiyo mahakamani na kwamba, hilo lilifanywa kwa kuzingatia maslahi ya wananchi. 

Pamoja na hayo, alikiri kumlipa Mbatia Sh mil 40 ikiwa ni sehemu ya kupunguza gharama alizotumia katika kesi hiyo, ikiwemo malipo ya mawakili wake.

Najuta Kuachana na Mke Wangu wa kwanza – Gardiner


Mtangazaji wa Clouds FM, Gardiner G Habash amesema miongoni mwa vitu anavyojutia katika maisha yake ni kuachana na mke wa kwanza aliyezaa naye mtoto wa kike, Karen, ambaye kwa sasa yupo mwaka wa pili chuoni.
GARDNER43

Akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV, Gardiner alisema kutokana na kubadilisha kazi ya awali na kuwa mfanyabiashara kipindi anaishi Mwanza, alijikuta akiiweka kwenye mawe ndoa yake kwa kukosa muda nayo.
“Yale mazingira niliyokutana nayo Mwanza ya kibiashara yalisababisha nikaachana na mke wangu wa kwanza, ni kitu ambacho najuta,”alisema staa huyo. “Nisije nikasema sana mwisho nikalia hapa bure,” alisisitiza.
Amesema mke wake huyo kwa sasa aliolewa japo wana mawasiliano mazuri sababu ya mtoto wao. Kuhusu kama anajuta kuachana na Lady Jaydee, Gardiner alisema: Siwezi kusema najuta kwamba alitokea kwenye maisha yangu na siwezi kusema kwamba najuta tuliachana. Lakini ninachoweza kusema tu kwamba kwa suala la Jaydee ni suala ambalo nilichagua sana lisiwe ni jambo ambalo nalizungumzia au kulitolea comment kwasababu yule ni public figure unaposema kitu kuhusu yeye tafsiri zinakuwa ni tofauti na vile unavyotarajia.”
“Kwahiyo sina majuto yoyote, na sina aina yoyote ya chuki au uadui na nategemea hata yeye atakuwa anafeel the same,” alisisitiza.
Alidai kuwa yeye na Lady Jaydee hawana mawasiliano ya aina yoyote kwa sasa na mara ya mwisho walikutana kipindi wanakamilisha taratibu za talaka.
Kwa upande mwingine Gardiner amedai kuwa maisha aliyonayo sasa ni ya furaha tele. Mtangazaji huyo amejiunga tena na Clouds FM akitokea EFM.
Bongo5

 

Maalim Seif Sharrif Hamad Kutoa Mwelekeo Wake Kisiasa Kesho

 


Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad kesho ataelezea mwelekeo wake kisiasa, ikiwamo kufafanua kiundani uamuzi wa chama hicho kususia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

Mgombea huyo wa urais Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana ataeleza mambo hayo ikiwa imepita takribani wiki moja tangu Baraza Kuu la chama hicho kutoa msimamo wake wa kutomtambua Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein pamoja na wawakilishi na madiwani.

CUF kilisusia kushiriki uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20 mwaka huu baada ya Oktoba 28 mwaka jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya urais, uwakilishi na udiwani, akisema kulikuwapo na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi.

Habari kutoka ndani ya chama hicho zinaarifu kuwa mkutano wa kiongozi huyo utakuwa wa kwanza kwake, tangu kumalizika kwa uchaguzi wa marudio na ataeleza mambo muhimu yatakayotoa picha halisi ya mwelekeo wake na CUF.

“Katika mkutano uliopita tamko lilikuwa la Baraza Kuu ila keshokutwa (kesho) Maalim Seif atazungumza kama Katibu Mkuu na aliyekuwa mgombea urais. Kuna masuala mengi atayaeleza kwa kina, hasa hili la uamuzi wa CUF kususia uchaguzi,” zilieleza taarifa hizo.

“Atazungumzia kwa kina uchaguzi ulivyokuwa na kujibu maswali ya watu wa kada mbalimbali waliokuwa wakihoji nini hatima ya CUF, baada ya kususia uchaguzi na hivyo kupoteza nafasi za uwakilishi.”

Rais Magufuli Kaeleza Kwanini Hapendi Sana Kusafiri Nje ya Nchi

Tunajua Rais Magufuli amekuwepo nchini Rwanda kwa ziara ya siku mbili kuanzia April 6 2016 mpaka April 7 jioni aliporudi Tanzania, kwenye moja ya maongezi yake mbele ya Wananchi wa Rwanda ameongea pia kuhusu kwanini hapendi kusafiri nje ya nchi na toka achaguliwe October 2015, amesafiri nje ya nchi kwa mara ya kwanza April 2016.
‘Nataka niwaeleze ndugu zangu, mimi sipendi sana kusafiri kwasababu ninapenda kubana matumizi… nimealikwa sehemu nyingi nimealikwa Ulaya lakini na sehemu nyingine bado sijaenda, nilipoalikwa na Muheshimiwa Kagame nimekuja na ninataka niwaeleze ndugu zangu wa Rwanda hii ndio safari yangu ya kwanza kutoka nje ya Tanzania‘ – Rais Magufuli.

Riyama Awapa Makavu Wanaoponda Mahusianio Yake na Kijana Huyu

Msanii wa filamu nchini Riyama Ally ambaye siku za karibuni ametolewa mahali na msanii wa muziki wa kizazi kipya Leo Mysterio amevunja ukimya kwa watu ambao wamekuwa wakisema kuwa anatoka na dogodogo huyo.

Riyama amesema kuwa wanataka atoke na mzee ndiyo wamuone kuwa ana heshima.

Kupitia kipindi cha eNEWS kinachorushwa na EATV Riyama amesema kuwa Leo Mystereo ndiyo furaha yake, na ujio wake katikia maisha yake umemuongezea changamoto kwenye maisha yake na kumfanya awe na furaha muda wote.
” Watu wanatakiwa wajue penzi haliingiliwi wewe ukicheka au ukinuna mimi hainisaidii kwani mimi natafuta furaha yangu na huyu ndiye furaha yangu, wewe unataka mimi niondoe furaha yangu nitaipata wapi. Unataka niwe na babu wa miaka mingapi ili uone Riyama ana heshima huyo babu unayetaka niwe naye asiponiheshimu pia mtasema. Jamani binadamu kweli maneno yapo kwa ajili ya kusema ila inabidi tuwe tunachagua vitu vya kusema” alisema Riyama Ally.

Riyama alisema kuwa wapo baadhi ya watu wamekuwa wakiongea vibaya sana juu ya mahusiano yake lakini amewataka kutambua kuwa wao wamependana na wana mipango na wameridhiana wao hivyo kuwatenganisha kwa maneno si jambo jepesi.

Masanja Mkandamizaji na Wenzako..Vengu Yupo Wapi na Anaendeleaje Kiafya?

Leo Nimesoma Makala moja katika Gazeti fulani wakimuongelea Msanii Vengu Ambae alikuwa Original Comedy kabla ya kuanza kuugua Mwaka 2009 kiasi cha kupelekwa India kupata matibabu, Gazeti hilo wamesimulia jinsi walivyofanya juhudi za kumtafuta kijana huyo ili kujua anaendeleaje baada ya miaka mitano sasa ya ukimya..lakini bila mafanikio hawakuweza kupata lolote la maana kuhusu alipo ama afya yake.....

Masanja na Wenzako wa Original Comedy sisi Washabiki wa Vengu tunataka kujua alipo na hali ya yake kiafya kwa sasa...Tumemmiss.......

Waziri Ummy Mwalimu azindua Duka la Dawa la MSD Kanda ya Mbeya


0f5c4672-9fd5-4bcf-87cc-9862e000a1c2

Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amefanya uzinduzi wa duka la dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kwa Kanda ya Mbeya.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri Mwalimu amesema uzinduzi wa duka hilo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na serikali ya Rais Magufuli kuwatia wananchi huduma bora na kwa gharama nafuu.
“Neema hii imekuja kwa kipindi cha Rais Magufuli, sasa amekidhi matakwa na shauku ya wananchi wa Mbeya kwa kuwapa duka la dawa,
“Sera ya huduma ya afya inataka wananchi wachangie isipokuwa wazee, watoto na wajawazito na kupitia duka hili wananchi wataweza kupata dawa kwa gharama nafuu,” amesema Mhe. Mwalimu.
Duka hilo la dawa la Kanda ya Mbeya limetumia Shilingi Milioni 13 kwa ukarabati wa jingo na vifaa vyake.
0f5c4672-9fd5-4bcf-87cc-9862e000a1c2
Mh.Ummy Mwalimu akionesha moja ya dawa inayouzwa dukani hapo kwa shilingi 7,000 ambapo kwenye maduka binafsi inauzwa shilingi 25,000,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurine Bwanakunu na kulia ni Mfamasia wa duka hilo, Cornel Mkeng'e
2ff7c78a-1555-486b-93f6-19118e784a78
Mfamasia wa Duka la Dawa, Cornel Mkeng'e akitoa maelezo kwa Mh.Ummy Mwalimu mara baada ya kuzindua duka hilo
7a1d5446-ae11-4b37-946b-337d47d8e85c
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiangalia jinsi ya ufungashaji wa dawa kwenye ghala jipya la Kanda ya Mbeya.ghala hilo limelozinduliwa leo jijini Mbeya
18f8ebf2-a48e-4f8d-ae8a-99ce5c23f6ac
Duka la Dawa la Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Kanda ya Mbeya ambalo litahudumia mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi.
e38d5120-d82d-496e-85f2-e82f53d9dcbb
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akipata maelezo jinsi ya utunzaji dawa kwenye ghala hilo.

Angalia Mabula Alivyo mbwaga Ezekiel Wenje Kesi Ya Ubunge Jijini Mwaza Leo

 

Mbunge wa jimbo la Nyamagama,jijini Mwanza pichani akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi wa jimbo hilo na Mahakama kuu ya jijini Mwanza dhidi ya aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha CHADEMA,Mh.Ezekiel Wenje.
****
EZEKIEL Wenje, mbunge wa zamani wa Jimbo la Nyamagana, Mwanza ameshindwa kwenye kesi aliyoifungua katika Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga dhidi ya Stanslaus Mabula.

  

Mahakama hiyo leo imempa ushindi Mabula (CCM) baada ya kujiridhisha kuwa, upande wa madai hauna ushahidi unaokidhi, kuithibitishia mahakama.

Wenje alifungua kesi hiyo akipinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo mwaka jana yaliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kumpa ushindi Mabula.

Katika kesi hiyo namba tatu ya mwaka 2015, ambayo ilionekana kugusa hisia za wakazi wa Nyamagana imehudhuriwa na idadi kubwa ya wafuasi wa upinzani na CCM.

Akitupilia mbali shauri hilo leo Kakusulo Sambo, Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga amesema kuwa, amefikia hatua hiyo baada ya upande wa mpeleka maombi kuiomba mahakama kuifunga kesi hiyo.

Amesema upande wa mpeleka maombi, ulidai kwamba kutokana na ombi lao la kupokelewa kwa fomu namba 21B kukataliwa kortini hapo, ulidai hakuna umuhimu wa kuendelea kwa kesi hiyo.

Jaji Sambo amesema, upande wa mpeleka maombi, licha ya kupewa muda wa siku 10 kupeleka fomu namba 21B lakini hawakufanya hivyo.

Amesema, pamoja na kuchelewa kupeleka fomu hiyo pia walipopewa muda wa kujieleza katika ombi lao la kuiomba mahakama kupokea fomu hizo, hawakueleza sababu za msingi.

Hata hivyo amesema baada ya kuwasilishwa kwa ombi hilo kortini, mahakama ilikaa na kutafakari kwa kina juu ya ombi hilo ambapo imeamua kutupilia mbali kesi hiyo.

“Mleta maombi aliomba kufunga kesi mahakamani na mahakama sasa imepitia ombi lao, hivyo na kuona kesi hii haina msingi wowote ule na tunakubaliana nao,” amesema Jaji Sambo.

Hata hivyo wakati shauri hilo likitupiliwa mbali kortini hapo, Wenje pamoja na wakili wake, Deya Outa hakuwepo mahakamani hapo bila taarifa yoyote.

Rais Magufuli Amteua Bwana G. Byakanwa Kuwa Mkuu Wa Wilaya Ya Hai .


 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Gelasius Gaspar Byakanwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.

Taarifa iliyotolewa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 08 April, 2016. Bw. Byakanwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Antony Mtaka aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.

Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Byakanwa alikuwa Katibu wa Rais Msaidizi Mwandamizi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
08 Aprili, 2016

Taarifa rasimi Kutoka JWTZ Kuhusu Wanajensi wa Tz Kutuhumiwa na Unyanyasi wa Kingono Congo




Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa kwa taarifa zinazo lituhumu JWTZ kuhusu unyanyasaji wa kijinsia unaodaiwa kufanywa na Wanajeshi wetu kwa Wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

JWTZ chini ya Umoja wa Mataifa (MUNUSCO) limekuwa likitekeleza majukumu ya Ulinzi wa amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo takribani miaka mitatu sasa.Katika muda ambao JWTZ limekuwa nchini Congo hapakuwepo na tuhuma kama hizo.

Aidha, JWTZ limetekeleza na limeendelea kutekeleza majukumu kama hayo katika nchi mbalimbali duniani kama vile Msumbiji, Liberia, Visiwa vya Comoro (Anjouan), Lebanon, Sudan katika jimbo la Darfur na sehemu nyingi kama hizo.

Katika kutekeleza majukumu hayo JWTZ limeyatekeleza kwa nidhamu na weledi wa hali ya juu.JWTZ limekuwa moja ya majeshi mengi yanayofanya vizuri na kutoa mchango mkubwa katika Ulinzi wa amani katika nchi ambazo limetekeleza majukumu hayo.

Hivi karibuni kumezuka tuhuma nchini Congo kuhusu Wanajeshi wa JWTZ kuwanyayasa kijinsia wananchi wa Congo. 

Kimsingi JWTZ haliwezi kupuuzia taarifa hizo, hivyo limeanza kuchukuwa hatua za kiuchunguzi ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo ingawa rekodi za majukumu ya ulinzi wa amani zilizokwisha fanywa na JWTZ sehemu mbalimbali zinaonesha kuwa hakukuwa na tuhuma kama hizo.

Kufuatia tuhuma hizo, JWTZ kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa unafanya uchunguzi wa kina ili kujiridhisha na ukweli wake. JWTZ halitasita kuchukua hatua kali kwa watakaobainika katika tuhuma hizo.

JWTZ bado lipo imara na linaendelea kutekeleza majukumu yake nchini Congo kwa kufuata sheria na taratibu za Umoja wa Mataifa.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Simu: 0784-477638/0756-716085
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk

Bosi wa Zamani wa TRA Harry Kitillya, na wenzake Wanyimwa Dhaana hazarani leo


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imepuuza ombi la dhamana ya kesi inayowakabili Harry Kitillya, Shose Sinare na Sioi Solomoni ambapo wamerejeshwa rumande.

Kitillya, alikuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); Sinare, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano na Uwekezaji katika Benki ya Stanbic na Sioi Solomoni, Mwanasheria wa Benki ya Stanbic.

Dhamana yao imesikilizwa mbele ya Amilis Mchaura, Hakimu Mkazi Kisutu ambapo mawakili wa pande zote mbili waliwasilisha hoja zao.

Dk. Lingo Tenga ndiye aliyeongoza jopo la mawakili upande wa watetezi ambapo upande wa serikali umesimamiwa na Oswadi Tibabyekonya, Wakili Mkuu wa Serikali Mahakama ya Kisutu.

Upande wa utetezi uliomba mahakama kubatilisha mashitaka ya utakatishaji pesa haramu uliosababisha watuhumiwa hao kukosa dhamana. Tibabyekonya ameieleza mahakama kuwa, shitaka la utakatishaji fedha halina dhamana.

Upande wa utetezi ulifanya mapitio ya kesi mbalimbali zinazofanana na kesi hizo ikiwemo kesi namba 314 ya mwaka 2015 kwenye Mahakama ya Rufaa ya Mwanza iliyokuwa ikimkabili Kigunda Francis aliyeshitakiwa kwa kosa kama hilo lakini alipewa dhamana.

Christopher Msigwa, wakili wa serikali amesema kuwa kesi hiyo haina dhamana kwa sababu, kosa hilo linaathiri uchumi wa taifa.

Washitakiwa wamekosa dhamana na wamerudishwa rumande hadi tarehe 22 Aprili mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.