MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday, 20 February 2016

ANGALIA MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA LEO ZA LIGI KUU TANZANIA BARA

Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Simon Msuva (katikati) wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Dar Derby uliopigwa kwenye uwanja wa taifa February 20, 2016
Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Simon Msuva (katikati) wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Dar Derby uliopigwa kwenye uwanja wa taifa February 20, 2016
Yanga imefuta rekodi ya kocha Jackson Mayanja ya ushindi mfululizo baada ya kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Simba mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu hizo kwenye mchezo wa marudiano.
Ushindi huo ni wa pili kwa Yanga dhidi ya Simba ndani ya msimu huu wa 2025-16 baada ya awali kupata ushindi kama huo kwenye mchezo wa raundi ya kwanza.
Beki wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul
Beki wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa Yanga Juma AbdulBeki wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul
Bao la kwanza la Yanga limefungwa na Donald Ngoma dakika ya 39 baada ya Hassan Kessy kutoa pasi fupi kwa golikipa wake Vicent Agban ambayo ilinaswa na mzimbabwe huyo na kuwekwa kambani mapema kipindi cha kwanza.
Yanga walipata bao la pili kutoka kwa nyota wa mchezaji wa zamani wa Simba Amis Tambwe dakika ya 72 kipindi cha pili.
Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano
Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njanoAdbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano
Rekodi unazotakiwa kujua
  • Yanga ndiyo timu ya kwanza kuifunga Simba tangu iwe chini ya kocha Jackson Mayanja tangu kocha huyo atangazwe kuchukua mikoba ya Dylan Kerr.
  • Simba ilikuwa haijafungwa zaidi ya goli moja tangu iwe chini ya Mayanja, Yanga wamekuwa timu ya kwanza kuifunga Simba zaidi ya goli moja baada ya kuifunga bao 2-0.
Raha ya ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba
Raha ya ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya SimbaRaha ya ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba
  • Amis Tambwe ni mchezaji pekee katika msimu huu kuifunga timu yake ya zamani katika mechi mbili ndani ya msimu mmoja.
  • Amis Tambwe, Hamisi Kiiza na Ally Mustafa ni wachezaji ambao leo walikuwa wanacheza dhidi ya timu zao za zamani. Wachezaji hao wamewahi kucheza kwenye vilabu hivyo kwa nyakati tofauti kisha kuhamia kwenye upande pinzani.
  • Yanga inapanda kileleni mwa ligi kwa mara nyingine baada ya kufikisha pointi 46 ikiwa imecheza michezo 19 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 45 baada ya michezo 20.
Mashabiki wa Yanga waksaidia kumshusha shabiki mwenzao aliyepoteza fahamu ili apatiwe huduma ya kwanza
Mashabiki wa Yanga waksaidia kumshusha shabiki mwenzao aliyepoteza fahamu ili apatiwe huduma ya kwanzaMashabiki wa Yanga waksaidia kumshusha shabiki mwenzao aliyepoteza fahamu ili apatiwe huduma ya kwanza
  • Yanga imeshinda kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa taifa baada ya mechi mbili za ugenini. Ilifungwa 2-0 na Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani-Tanga kabla ya kutoka sare ya bao 2-2 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons.
Mashabiki wa Simba wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa jadi Yanga
Mashabiki wa Simba wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa jadi YangaMashabiki wa Simba wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa jadi Yanga
  • Magoli ya mechi ya leo yamedungwa na wachezaji wa kigeni Donald Ngoma (Zimbabwe) na Amis Tambwe (Burundi).
  • Simba imefungwa na Yanga kwenye mechi zote (mbili) za msimu huu (2-0) 26 September, 2015, (2-0) 20 February, 2016.
Nini Kinafuata kwa timu hizo baada ya mchezo wa leo?
Simba itakuwa mwenyeji wa Mbeya City March 6, 2016 kwenye mchezo wao ujao wa VPL kwenye uwanja wa taifa.
Yanga wataialika Mtibwa Sugar kwenye mchezo unaofuata katika liga, mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa taifa February 24, 2016.
Matokeo ya michezo mingine iliyopigwa leo kwenye viwanja mbalimbali
Mgambo JKT 1-1 Tanzania Prisons
Stand United 1-1 JKT Ruvu
Mbeya City 0-3 Azam FC
Toto Africans 1-1 Kagera Sugar

Comments

Kutoka Kampala, mshindi wa kura za Urais Uganda 2016 ametangazwa..


Uganda ilikua kwenye uchaguzi mkuu wa kumchagua Rais na Wabunge juzi ambapo matokeo ya awali yalianza kutolewa kuanzia jana lakini leo matokeo kamili yametolewa naYoweri Museveni ambaye amekuwepo kwenye kiti cha Urais toka mwaka 1986ametangazwa mshindi huku mpinzani wake mkuu ambaye ni Kizza Besigye akikataa matokeo hayo aliyoyaita ya wizi wa kura.
KTN 2
Museveni 2
Rais Museveni alipokutana na Viongozi waangalizi wa uchaguzi Mzee Obasanjo na Banda nyumbani kwa Rais eneo la Rwakitura.

Rais Magufuli Amteua Hebert Mrango kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC

 


 MKUTANO WA MHE. NAPE MOSSES NNAUYE, WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI SANAA NA MICHEZO NA WAANDISHI WA HABARI
 
TAREHE 20/02/2016
-------------
Dondoo Alizozungumza Waziri Nape Nnauye;
Napenda kuwafahamisha kuwa kufuatia Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kumaliza Muda wake, uundwaji wa Bodi Mpya umekamilika. 

Ni vyema kuwafahamisha kuwa katika utaratibu wa kisheria wa kuunda Bodi ya TBC mwenye Mamlaka ya kisheria ya Kumteua Mwenyekiti wa Bodi ni Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania.
 
Napenda kutumia fursa hii kumshukuru sana aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TBC iliyomaliza muda wake, Prof. Mwajabu Possi na wajumbe wake wote kwa kazi waliyoifanya kwa muda wote wa uhai wa bodi hiyo. 

Ninaamini Bodi Mpya itaendeleza yale mazuri yote yaliyofanyika na Baodi iliyopita na kubuni mambo mengine mapya ili kuongeza tija kwa Shirika.
 
Baada ya kutoa maelezo haya ya awali, sasa nichukue fursa hii kuwajulisha yafuatayo;
1.   Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemteua Mhe. Balozi Herbert E. Mrango (pichani) kuwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya TBC. Uteuzi huu unaanza tarehe 19/02/2016 kwa kipindi cha miaka Mitatu.
 
Balozi Mrango kielimu ana shahada ya Uzamili katika uendelezaji wa Mifumo (MSc – Systems Development) aliyoisomea Chuo Kikuu cha Dublin Nchini Uingereza. Aidha amehitimu Shahada ya kwanza ya Takwimu za Kiuchumi katika Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Tanzania.
 
Balozi Mrango alishashika nyadhifa mbalimbali, zikiwemo kuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara  ya Miundombinu Kuanzia Februari, 2011 hadi September, 2013.
 
Nachukua fursa hii kumpongeza Mhe. Balozi Mrango kwa kuaminiwa na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kushika wadhifa huu muhimu. 

Aidha nimhakikishie Mwenyekiti huyu Mpya wa TBC kwamba kwa kuwa Shirika la TBC liko chini ya Wizara yangu, tutampa ushirikiano wa kutosha ili kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika shirika letu la Utangazaji.

2.Kwa mujibu wa Sheria iliyounda TBC, baada ya Mhe. Rais kumteua Mwenyekiti wa Bodi, Waziri mwenye dhamana na shughuli za utangazaji,  anateua Wajumbe sita wa Bodi. 

Katika uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umma, Ofisi ya Msajili wa Hazina ilishatupatia vigezo vya utaalamu wa wajumbe wakati wa uteuzi.

Hivyo basi, mimi Nape Moses Nnauye, nikiwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, kwa kuzingatia vigezo vilivyobainishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kwa kufuata taratibu zingine za kufanya uteuzi, nimewateua wafuatao kuwa wajumbe wa Bodi ya TBC;

(i) Bw. William Steven Kallaghe; Mtaalamu wa Uchumi.  (M.A – Economics; Head of Public Policy: NBC Bank  Tanzania ).

(ii)Bw. Mustapha Kambona Ismail; Mtaalamu wa Sheria. (LLB - UDSM; Associate Director, Litigation & Investment – Bank of Tanzania; Advocate of the High Court of Tanzania).

(iii) Bi. Elimbora Abia Muro; Mtaalamu wa Uhasibu. (CPA, MBA: Senior Internal Auditor, Tanzania Investment Centre).

(iv) Bw. Mick Lutechura Kiliba; Mtaalamu wa Rasilimali watu. (MBA – Public Service Mgt; Director of Management: President’s Office – Public Service Management).

(v) Dkt. Ayub Rioba; Mtaalamu wa Sekta ya Utangazaji na Utangazaji.  (PhD – Mass Communication; Associate Dean: School of Journalism, University of Dar Es Salaam) na

6. Bw. Assah Andrew Mwambene; Mtaalamu wa Sekta ya Habari. ( MSc – Media Research and Analysis; Director of Information: Ministry of Information, Culture, Arts and Sports).

Uteuzi wa wajumbe hawa ni kuanzia tarehe 19/02/2016 kwa muda wa miaka mitatu.

3. Nimalizie kwa kuwapongeza tena wote waliopata uteuzi huu. Tuna matumaini makubwa toka kwao kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa TBC katika tasnia ya Utangazaji katika ulimwengu wa Teknolojia inayobadilika kwa kasi kubwa duniani.

Ni imani yangu kwamba Bodi hii mpya italeta msukumo mpya katika utendaji wa Shirika ili hata watumishi wanaofanya kazi katika shirika hili waendelee kujivunia kuwa ndani ya TBC lakini pia Umma wa Watanzania wajivunie viwango vya utendaji wa Shirika hili.

Friday, 19 February 2016

Matokeo ya awali ya uchaguzi nchini Uganda: Museveni Anaongoza kwa Asilimia 62.03



Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi nchini Uganda yanaonesha kuwa Rais Yoweri Museveni kwa tiketi ya NRM anaongoza akiwa na zaidi ya kura milioni 1.3 sawa na asilimia 62.03.

Anayefuata  ni  Kizza Besigye kwa tiketi ya chama cha FDC asilimia 33.46 huku Waziri Mkuu wa zamani wa Uganda, Amama Mbabazi akionekana kushindwa.

Waziri Nape Nnauye Atengua Uteuzi Wa Katibu Mtendaji Baraza La Michezo Tanzania ( BMT )


Waziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati) akizungumza na waandishi wa Habari leo hii katika ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kutengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mtendaji mkuu wa baraza ilo Bw. Henry Lihaya (wa kwanza kushoto) leo jijini Dar es Salaam kutokana utendaji usiolizisha. Picha na Daudi Manongi.

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ametengua uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo Tanzania Henry Lihaya baada ya kushindwa kutekeleza wajibu wake.

Mhe. Nnauye ametengua uteuzi huo katika ziara yake aliyoifanya leo mapema katika ofisi za BMT kuona miundo mbinu ya ofisi hizo na kujua changamoto walizonazo.

“Baraza likirekebishwa vyama vya michezo navyo vitakuwa mguu sawa na kuleta chachu na maendeleo katika michezo,”alisema Mhe. Nnauye.

Aliongeza kwa kusema kuwa, miaka saba ambayo Lihaya amekuwa Katibu Mtendaji wa Baraza imetosha kwani hakuna mabadiliko yoyote aliyoyafanya katika sekta ya michezo tangu alipoteuliwa mwaka 2009.

Kutokana na utenguzi huo Mhe. Nnauye amemtaka Mwenyekiti wa BMT Dionis Malinzi kupendekeza jina la Katibu Mtendaji mpya wa BMT ambaye anampendekeza kwa mujibu wa sheria ya BMT kifungu cha 5(1) baada ya kupata idhini ya waziri mwenye dhamana.

Vilevile, Mhe. Nnauye amemtaka mwenyekiti kuteua Katibu Mtendaji ambaye atakuwa ni mchapa kazi na mwenye mipango ambayo itaibadilisha BMT na kuleta chachu katika michezo nchini.

Aidha, Mhe. Nnauye amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara ya habari, utamaduni sanaa na michezo kumpangia Lihaya kazi nyingine wizarani.

Wednesday, 17 February 2016

BREAKING NEWS: TCU YAFUTA CHUO KIKUU CHA TIU


Profesa Yunus Mgaya, Katibu Mtendaji wa TCU

IKIWA ni siku 10 kupita baada ya mtandao huu kuripoti mgomo wa walimu katika Chuo cha Kimataifa cha Tanzania (TIU) kilichopo Kimara Stop-Over, Dar es Salaam, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imekifutia leseni chuo hicho.

Walimu hao waligoma kuingia darasani kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kutolipwa malimbikizo ya mishahara yao pamoja na kutopewa mikataba ya kazi.

Taarifa iliyotolewa na Profesa Yunus Mgaya, Katibu Mtendaji wa TCU kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa, chuo hicho kimefutiwa leseni yake kutokana na kushindwa kutimiza masharti yaliyobainishwa kwenye leseni iliyowepewa.

Mgaya ameleza kuwa, chuo hicho kimeanzisha kufundisha programu za astashahada na stashahada bila ithibati ya mamlaka husika na kuongeza TCU haitambui program zinazotolewa na chuo hicho.

Source:Mwanahalisi

Mwanasheria Wa Serikali na Askari Magereza Washikiliwa kwa Kumtorosha Mtuhumiwa Gerezani



Mwanasheria wa Serikali Mkoa wa Katavi pamoja na askari magereza wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuza za kula njama na kisha kumtorosha kwa siku 124 mtuhumiwa wa kesi ya kujaribu kumuua mlemavu wa ngozi (Albino) baada ya kupokea rushwa ya jumla ya Sh3 milioni.

Tukio la kutoroshwa kwa mtuhumiwa huyo linadaiwa kufanyika Oktoba 12 mwaka jana, baada ya kupokea fedha kiasi hicho ambapo Mwanasheria wa serikali mkoani Katavi, Falhati Seif Khatibu(45) alipokea kiasi cha Sh2 milioni na askari Magareza A.287 S/SGT- John Masagula(50) pamoja na A. 5385 SGT Deogratius Katani(50) wakigawana kiasi cha Sh milioni moja.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulifanikiwa kutokana na taarifa za siri kutoka kwa raia wema ambao walidai kuwa kuna mtuhumiwa aliyekuwa anashikiliwa ametoroka kutoka katika gereza la mahabusu la Mpanda lililopo mkoani humo.

Alisema baada ya taarifa hizo ndipo uchunguzi ulipofanyika Januari 19 mwaka huu, na kubaini kuwa mtuhumiwa Alex Manyanza(27) ambaye alikuwa anashikiliwa kwa tuhuza za kujaribu kumuua kwa kumkata kiganja cha mkono mlemavu wa ngozi Limi Luchoma(30), mwanzoni mwa mwaka na kufunguliwa shitaka namba MTO/IR/76/2015 alikuwa ametoroka mahabusu.

Baada ya upelelezi ilibainika kuwa ndugu wa mtuhumiwa huyo ndio waliotekeleza mpango huo na kisha kumtorosha mtuhumiwa na kwenda kumficha katika kijiji cha Kipande kilichopo mkoani Rukwa, na ndipo walipompa fedha hizo mwanasheria mkuu wa serikali ili amuondelee shitaka linalomkabili mtuhumiwa huyo baada ya kufanikiwa kutoroka gerezani.

Alisema mtuhumiwa ni mzoefu kwa vitendo vya kutoroka gerezani kwani kabla ya kufanya tukio hilo alikuwa ametoroka katika gereza la Kalila Nkulunkulu lililopo mkoani humo, ambapo alikuwa anatumikia kifungo cha miaka mitano jela baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la wizi wa mifugo.

Kamishna wa Elimu Awavua Madaraka Wakuu Watatu wa Vituo vya Elimu ya Watu Wazima Dar, Dodoma na Mwanza

 


Kamishna  wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Ufundi, Profesa Eustella Balamsesa amemuagiza Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima, Fedelis Mafumiko kuwavua madaraka Wakuu Watatu (3) wa vituo vya  Elimu ya Watu Wazima kutokana na kukiuka utaratibu wa kuchagua wanafunzi wanaojiunga kidato cha kwanza kuwaingiza katika Mfumo wa Elimu ya Watu Wazima.

Profesa Eustella ameyasema hayo leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam .

Amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakishirikiana na Halmashauri baada ya kuchagua wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wamefanya vizuri wao huchukua wanafunzi waliofeli na kuwapeleka katika shule za serikali wakidai kuwa wanafunzi wamechaguliwa katika chaguo la pili.

Baada ya kuchaguliwa wanafunzi hao wakifika shule wanadaiwa ada wakati serikali imesema elimu  ni  bure, hali inayowachanganya  wazazi.

Wakuu wa vituo waliovuliwa madaraka ni Wotugu Mganda (Dar es Salaam), Senorina Kateule (Dodoma),Steward Ndandu Geita na (Mwanza).

Profesa Eustella amesema kuwa wakufunzi hao wamekuwa wakidandia matokeo ya kidato cha kwanza kwa kufanya upotoshaji kwa wazazi wakati wanafunzi wanaosoma katika elimu ya watu wazima ni hiari kutokana  na sera ya elimu.

Wanafunzi ambao wamechaguliwa kwa mwaka huu wamekuwa wakidai ada ya sh. 80,000 hadi 250,000 na ndipo malalamiko yakaanza kwa wazazi baada ya kudaiwa ada hiyo.

Profesa Eustella, amesema kuwa mmoja wanafunzi katika Mkoa wa Dar es Salaam aliambiwa amefaulu katika chaguo la pili katika shule ya sekondari ya Oasterbay .Baada ya kufika shuleni, mwanafunzi huyo alikuta mambo tofauti kwa kudaiwa ada na kuambiwa awasiliane na Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

Walimu Watatu Wakatwakatwa Mapanga wilaya ya Musoma mkoani , Mara

 

Walimu watatu wa shule ya Secondary Mara iliyopo katika manispaa ya mji wa Musoma Mkoani Mara,Vedastus Rwechungula ,Juma Amos Na Maccelo Ndege, Wamekatwa Mapanga sehemu mbali mbali ya miili yao walipokuwa wakirejea shuleni hapo Usiku wa Saa Nne toka matembezini.

Wakizungumza wakiwa wamelazwa katika hospital ya Rufaa ya Musoma,Walimu hao wamesema kuwa Vitendo vya Uhalifu jirani na Shule hiyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara kutokana na vibaka waliopo katika eneo hilo kuwakata watu kwa mapanga.
 

Wakurugenzi Wanne wa Halmashauri Mkoani Kagera,Mtwara,Geita na Tunduma Wasimamishwa Kazi

 


WAZIRI nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne  kwa  tuhuma  za  kuwahonga wakaguzi wa fedha  kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa  Hesabu za  serikali (CAG) ili wapewe hati  safi huku Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi .

Wakurugenzi  waliosimamishwa  kazi  ni   Elizabeth Chitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera, Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara  na  Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.
 
Pia,Waziri Simbachawene   amemsimamisha kazi  mkurugenzi Halmashauri ya  Tunduma Mkoani  Mbeya Bi Halima Ajali  ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kuwatumia watoto wake katika shuguli za halmashauri na kuwalipa posho na kusababisha upotevu wa mapato.
 
Aidha, Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini,CAG  waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe  hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo mchana Jijini Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika  baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wizara yake
 
Akibainisha makosa ya kila mkurugenzi,Waziri Simbachawene amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu  alimwagiza  mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni tatu kwa maafisa wa  ofisi ya CAG kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo  huku akijua ni kosa kisheria. Watumishi wa  wa ofisi ya CAG  waliopokea pesa hizo ni Stevin Buawa,John Elias pamoja na Kilembi Mkole
 
Katika Halmashauri ya Nanyumbu, Simbachawene amesema  kuwa  tarehe 26 Juni 2015, mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa walimkabidhi fedha Milioni 3 na laki tano  afisa wa ofisi ya  CAG  kwa lengo la kutoa hati safi
 
Waziri Simbachawene amesema mwezi Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmashauri  ya  Mbogwe mkoani Geita Abdalla Mfaume na mweka hazina wake waliwapatia milioni 16  maafisa wakaguzi wa ofisi ya CAG  ili wafiche ufisadi walioubaini
 
Amesema katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ikiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadh

Wema Sepetu na Idris Sultan Wathibitisha kuharibika…Kwa ujauzito wake

Hii ni post aliyoiandika Mwigizaji Wema Sepetu saa kadhaa baada ya Baba Watoto mshindi wa Big Brother Africa Idris Sultan kuthibitisha kwamba ujauzito huo wa mapacha umeharibika.

Ni kweli, na imeniuma sana lakini kwenye hatua maishani mwangu naweza kusema Alhamdulillah kwa kila kitu, Alhamdulillah kwa wote wanaojua uchungu nilio nao na wameonyesha moyo wa kibinadamu, nawashukuru kwa upendo wenu.. MNANIPA NGUVU.
wema
Alhamdulillah kwa wote wanaojua uchungu nilionao na wamefurahia kwasababu zao binafsi. Nawashukuru kwa uwepo wenu, MNANIPA UJASIRI, Alhamdulillah kwa siku ya kesho Ilimradi nina pumziSITACHOKA KUJARIBU TENA.
Wema 2
Hata ukikosa, ukakosa, ukokosa eeeeeeh…sema ASANTE, KWELI YEYE NI MUNGU…. alimalizia kuandika Wema Sepetu

Tuesday, 16 February 2016

NACTA YAKANUSHA KUTANGAZWA KWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE2015

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2015 

Baraza la Mitihani la Tanzania limekuwa likipigiwa simu na watu mbalimbali wakiomba ufafanuzi kuhusu taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetangaza kuwa matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2015 yamezuiwa kwa muda hadi tarehe 08/03/2016. Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watahiniwa na umma kwa ujumla kuwa taarifa hizo ni za UONGO na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki. Hivyo, Baraza linaomba umma kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa Wizara haijasitisha utoaji wa matokeo hayo.  o. Matokeo yatatangazwa mara tu mchakato utakapokamilika.

 Imetolewa na, AFISA HABARI NA UHUSIANO

Monday, 15 February 2016

Samatta ameanza kukutana na changamoto za kazi ndani ya Belgium

Striker Mbwana Samatta ameanza kukutana na changamoto za kazi ndani ya Belgium ambapo anaishi huko na kucheza kwenye ligi kuu.


Samatta akiwa anajiandaa kwenda kufanya mazoezi amekutana na barafu(snow) za kutosha kitu ambacho yeye hajazoea. Kwenye maisha ya soka amecheza Tanzania na Congo ambapo hali ya hewa ni joto lakini maisha mapya ya Beilgium ni baridi na snow kama pica zinavyoonyesha hapa.

Mapokezi ya Diamond, Familia yake na Team yake Mjini KISUMU

   

Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platinum siku ya jana akiwa na Zari  na Tiffah pamoja na team yake ya wasafi walitua mjini Kisumu nchini Kenya, na hizi ni baadhi ya picha za mapokezi yake hapo jana pamoja na ‘sound check’ aliyoifanya mapema leo kwa ajili ya show itakayofanyika leo mjini humo.


Saturday, 13 February 2016

Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally Aruhusiwa kutoka hospitali....Aitaka Serikali iboreshe hospitali za ndani

 

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir, ameitaka Serikali iweke mikakati thabiti ya kuzipa uwezo hospitali za ndani ili kupunguza gharama kwa Watanzania wengi kwenda kutafuta matibabu nje ya nchi. 

Mufti aliyasema hayo jana muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alikokuwa amelazwa kwa takribani wiki moja akipatiwa matibabu. 

Alisema kuna haja ya hospitali kubwa kama Muhimbili kuangaliwa kwa jicho la tatu ili iweze kutoa huduma za kimataifa, hilo litawezekana endapo kutakuwa na vitendea kazi vya kutosha na madaktari kufanya kazi katika mazingira mazuri. 

Mufti alisema kwa kufanya hivyo Watanzania watarudisha imani kwa hospitali za nyumbani na madaktari wake, tofauti na hali ilivyokuwa miaka ya karibuni ambapo wengi walikuwa wakikimbilia nje ya nchi kwa ajili ya kutafuta matibabu. 

“Binafsi nilikuwa siamini kama naweza kutibiwa hapa nchini, tayari nilishakata tiketi kwa ajili ya kwenda nje ya nchi lakini nashukuru Mungu siku moja kabla ya safari nilihakikishiwa kwamba naweza kupata matibabu hapa. 

“Niwasihi Watanzania wenzangu kuamini kwamba Tanzania nayo tuna madaktari bingwa wengi ambao wanafanya kazi nzuri, muhimu kwa Serikali ni kuwaboreshea mazingira ya kufanya kazi,”alisema Sheikh Zubeir 
Kwa upande wake Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu alisema ni matarajio ya Serikali kuona viongozi wote wanatibiwa hospitali za nyumbani, jambo litakalowashawishi Watanzania wengine kuamini huduma zinazotolewa. 

Alisema kwa viongozi wakubwa kama Mufti kutibiwa nchini kumewasukuma kuongeza vifaa na huduma bora zaidi, ili kuifanya Muhimbili kuwa miongoni mwa taasisi zinazoheshimika. 

“Kama Mufti ametibiwa hapa nyumbani kuna sababu gani ya kupeleka watu nje, kwa sasa tumepata hamasa ya kuongeza vitendea kazi na huduma, ili Muhimbili iendelee kuheshimika na ivuke mipaka itoe huduma ndani na nje ya nchi,” alisema Mwalimu 
Akitoa salamu za Bakwata Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Suleiman Said Lolila alimshukuru Rais John Magufuli kwa kufanikisha matibabu ya Mufti. 

“Madaktari wamefanya kazi kubwa tuna kila sababu ya kushukuru kwa hilo na Watanzania wote kwa ujumla kwa dua zao hatimaye leo Mufti ameruhusiwa kurudi nyumbani,” alisema Lolila 
 Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akimualika Mufti Mkuu Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally kuongea na wanahabari katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya madaktari kumruhusu kurejea nyumbani baada ya afya yake kuimarika.
 

Mgombea wa Urais Marekani Donald Trump Aitukana Tena Africa..Adai lazima Itawaliwe Tena na Mkoloni..

.

Donald Trump: “There Is No Shortcut To Maturity, Africa Should Be Recolonized”

American business mogul Donald Trump has said that Africa needs to be recolonized. This time around he has directed his anger to African leaders who according to Trump, have failed to exercise leadership and are keeping their people in worse conditions.

Speaking yesterday in Nebraska, Trump said that Africans are slaves living like slaves in their own land yet they claim they are independent.

Trump was responding to a question by a South African journalist on whether he thinks African leaders were right to seek mass withdrawal from the Hague based International Criminal Court.

“It is shameful for African leaders to seek exit from ICC. In my view, these leaders want to have all the freedom to oppress their poor people without anyone asking them a question. I think there is no shortcut to maturity and in my view, Africa should be recolonized because Africans are still under slavery. Look at how those African leaders change constitutions in their favour so that they can be live presidents.

They are all greedy and do not care about the common people” Said Trump
“When I saw them gang up against ICC yet they can’t even find an amicable solution for the ongoing quandary in Burundi, I thought to myself these people lack discipline and humane heart. They can’t lead by example. The only thing they are interested in is accumulating wealth from poor tax payers. Before they think of exiting from ICC, they should first restore peace in Burundi and other war-tone countries rather than gathering like hyenas with the aim of finishing the poor people” Added Trump.

Mwaka huu wa kazi tu....Uongozi Wa Hospitali ya Rufaa Mbeya yapewa siku 60 Kununua Mashine ya CT Scan

   


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Khamis Kigwangalla amewapa siku 60 viongozi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya (MRH) wawe kununua mashine ya CT-scan.

Dk Kigwangalla alitoa agizo hilo juzi jioni, baada ya kuwasili jijini Mbeya ghafla na kwenda moja kwa moja kwenye hospitali hiyo na kupokea taarifa iliyoeleza pia kwamba ni ya kanda, lakini haijawahi kupata mashine za CT scan.

Kukosekana kwa CT-scan kumesababisha wagonjwa kwenda Dar es Salaam au watumie mashine ya mtu binafsi iliyofungwa jijini hapa miaka miwili iliyopita.

“Haingii akilini mtu binafsi hapahapa Mbeya anamiliki CT-scan, lakini hospitali kubwa kama hii imekosa,”alisema.

Dk Kigwangalla alishangazwa zaidi aliposikia kuwa mapato ya hospitali hiyo ni zaidi ya Sh500 milioni kwa mwezi.

“Sasa nawapa siku 60 nataka kuona mashine hiyo imefungwa, vinginevyo mtakuwa mmeshindwa kazi, nitakula sahani moja na nyie viongozi,” alisema.

Aliwataka watumishi wa hospitali hiyo kuwa na mawazo chanya kwa maendeleo na kutoa mfano wa CT-scan nzuri na ya kisasa kama ile iliyonunuliwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN) inauzwa Sh3 bilioni jambo ambalo wanaweza kulitekeleza badala ya kusubiri Serikali iwapelekee.

Awali, Mkuu wa Kitengo cha Maabara cha hospitali hiyo, Abednago Mwakila alisema mbali ya kukosa mashine hiyo kwa miaka yote, nyingine zilizopelekwa hapo hazifanyi kazi baada ya kuharibika na hawajui mafundi wanapatikana wapi.

Alitoa mfano wa mashine ya kuangalia mgando wa damu aliyodai ni kifaa muhimu, lakini haifanyi kazi kwa zaidi ya miaka minne kutokana na kukosekana kwa fundi.

Baada ya kuelezwa hivyo, Dk Kigwangala aliuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuorodhesha mashine ambazo hazifanyi kazi na kumpelekea ofisini aweze kufanya utafiti na kubaini watu walioingia mkataba na Serikali wapeleke mashine hizo.

Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Idsory Thomas alisema agizo lililotolewa na Dk Kigwangalla litatelekezwa kwa wakati.