MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Monday, 28 December 2015

ANgali matokeo ya Man United Vs Chelsea, matokeo ya mechi 8 za EPL

Michezo 8 ya Ligi Kuu Uingereza imechezwa leo Jumatatu ya December 28, ikiwa ni muendelezo wa mechi za Ligi Kuu Uingereza, mechi ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa na hisia za mashabiki wengi wa soka, ni mchezo kati ya Man United dhidi ya klabu ya Chelsea iliyomtimua Jose Mourinho hivi karibuni na kumpa kibarua cha muda Guus Hiddink.
2520
Mvuto wa mchezo huu unakuja kufuatia vilabu hivyo viwili kutofanya vizuri kiasi hata,Chelsea kufikia maamuzi ya kumfuta kazi Jose Mourinho, wakati Man United wakiwa wanahusishwa kuwa katika mpango kama huo wa kutaka kumfukuza kocha wake wa kiholanzi Louis van Gaal.
3704
Mchezo huo ambao ulikuwa umeteka hisia za watu wengi umemamlizika kwa sare ya kutofunga, kwa matokeo hayo Man United wanakuwa nafasi ya 6 ikiwa na point 30, wakati klabu ya Chelsea itakuwa nafasi ya 14 baada ya sare hiyo na kufanya itimize jumla ya point 20.
3321
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa December 28
  • Crystal Palace 0-0 Swansea
  • Everton 3-4 Stoke
  • Norwich 2-0 Aston Villa
  • Watford 1-2 Tottenham
  • West Brom 1-0 Newcastle
  • Arsenal 2-0 Bournemouth
  • Man Utd 0-0 Chelsea
  • West Ham 2-1 Southampton

ANGALIA MESSI ALIVYO TWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA DUNIANI

  • Lionel Messi ametangwazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kwenye tuzo za Globe Soccer
  • Barcelona imeshinda tuzo ya klabu bora ya mwaka
  • Tuzo ya Player career imekwenda kwa Andrea Pirlo na Frank Lampard
  • Jorge Mendes amepewa tuzo ya wakala bora wa mwaka
Super Star wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya heshima iliyotolewa na Globe Soccer, Dubai.
Lionel Messi akipokea tuzo yake ya heshima ya mchezaji bora wa mwaka kutoka Globe Soccer, Dubai 
Mabingwa wa La Liga Barcelona ambao walitwaa mataji matatu (treble) msimu uliopita walitangazwa kama klabu bora ya mwaka wakati Josep Maria Bartomeu (Rais wa klabu ya Barcelona) alitangazwa kama rais bora wa klabu wa mwaka.
 
Mshambuliaji huyo wa Argentina, alifanikiwa kupachika mabao 58 na kuisaidia Barcelona kunyanyua ndoo tatu msimu uliopita.
 
Mchezaji mweza wa Pirlo Frank Lampard wanaokipiga kwenye timu ya New York City akipokea tuzo kama ya Andrea PirloWakongwe wanaokipiga kwenye klabu ya New York City Andrea Pirlo na Frank Lampard wao walitwaa tuzo ya heshima kutokana na mchango wao katika soka (Player Career Award).Legend wa Italia Andrea Pirlo akipokea tuzo yake ya heshima baada ya Globe Soccer kutambua mchango wake kwenye soka
 
Jorge Mendez ambaye pia ni wakala wa star wa Real Madrid Cristiano Ronaldo akipokea tuzo ya wakala bora wa mwakaJorge Mendes ambaye pia ni wakala wa super star wa Real Madrid Cristiano Ronaldo yeye alitwaa tuzo ya wakala bora wa mwaka, kocha wa Ubelgiji yeye akatangazwa kama kocha bora wa mwaka.
Wakati huohuo klabu ya Benfica ilitwaa tuzo ya Best Academy of the Year, Ravshan Irmatov alitajwa kama mwamuzi bora wa mwaka .Tuzo 2

Waziri Nape Nnauye akanusha kauli ya Wanaovaa nguo fupi na za kubana kukamatwa

 
Baada ya taarifa kusambaa kuwa Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye ameatangaza kukamatwa kwa watu wanaovaa nguo fupi na zile za kubana mwili wakamatwe, sasa haya ndio maelezo kamili unapaswa kuyafahamu.
nikwamba  waziri Nape amesama taarifa zilizo enea sio sahihi ni watu  labda wana taka kuiharibu wizara nawala hawana mpango huo

UKWELI KUHUSU YANGA KUTANGAZA KUVUNJA MKATABA NA HARUNA NIYONZIMA

Afisa Habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro


Afisa Habari wa klabu ya Yanga Jerry Muro wakati akizungumza na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga juu ya kuvunjwa mkataba kati ya klabu ya Yanga na Haruna Niyonzima
Klau ya Yanga imetangaza kuvunja mkataba na kiungo wake wa kimataifa kutoka nchini Rwanda Haruna Niyonzima kutokana na utovu wa nidhamu ikiwemo kuchelewa kuripoti kambini na kutoipa kipaumbele klabu yake.
Nahodha huyo wa Rwanda alichelewa kurejea kwenye klabu yake mara baada ya kumalizika kwa fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CEFAFA Challenge Cup) iliyofanyika nchini Ethiopia.
Niyonzima ambaye alikuwa akikitumikia kikosi cha timu yake ya taifa aliwasili Dar es Salaam December 16 mwaka huu wakati michuano ya Challenge Cup ilimalizika December 6.
Baada ya kuwasili Niyonzima alitoa utetezi wake kwamba alikuwa akisumbuliwa na majeraha aliyoyapata kwenye michuano ya Challenge kwani alikuwa amefungwa bandage ngumu mguuni. Lakini Yanga ilihitaji uthibitisho wa ripoti ya daktari wake wa timu ya taifa.
December 17, Yanga ilitoa adhabu ya kumsimamisha mchezaji huyo kwa muda usiojulikana huku akiendelea kupokea nusu mshahara kwa muda wote huo aliosimamishwa kwa kipindi kisichojulikana.
Adhabu hiyo ilitangazwa na Katibu mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha baada ya kamati ya mashindano kuazimia adhabu hiyo iwe ni ya awali wakati ikiendelea kujadili ni adhabu gani stahiki itolewe kwa Niyonzima ambaye amejijengea umaarufu mkubwa kwenye soka la Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Leo afisa habari wa Yanga Jerry Muro ametangaza uamuzi uliofikiwa na klabu ya Yanga wa kuvunja mkataba na Niyonzima huku ikimtaka Niyonzima ailipe klabu hiyo zaidi ya dola za kimarekani 71,000 kama fidia inayotokana na mkataba mpya unaomalizika mwaka 2017.

Sunday, 27 December 2015

Muhongo Achoshwa na Umeme wa Bei ya Juu Unaonunuliwa Uganda



Waziri wa wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameuagiza uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Ziwa kuhakikisha wanauingiza mkoa wa Kagera katika Gridi ya Taifa baada ya kubainika nchi inaingia gharama kubwa kununua umeme kutoka Uganda.

Alitoa agizo hilo jana wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Kagera na kusisitiza katika mipango mipya ya Tanesco kwa sasa, ni lazima iondokane na umeme wa gharama kubwa.

Katika ziara hiyo ambayo alikagua mitambo ya kusambaza umeme katika wilaya za Bukoba, Biharamulo na Ngara, Muhongo alisema umeme unaonunuliwa kutoka Uganda wa megawati 5.2 , kila uniti hununuliwa senti nane za Kimarekani.

Aliagiza kwamba kabla ya Tanesco kusaini mkataba mpya na Uganda, wanapaswa kusaini mkataba wa muda wakati wakiendelea kuweka utaratibu wa kuhamishia mkoa wa Kagera kwenye Gridi ya Taifa. Alisema mkoa huo ukiingizwa kwenye gridi, Tanesco itaepuka gharama kubwa za kunununua umeme wa gharama ya juu kutoka nchi hiyo.

Alisema kwa sasa Gridi ya Taifa imefika Nyakanazi, wilayani Biharamulo. “Kwa hiyo hata wilaya nyingine hazina budi kuingizwa katika gridi ili kufanya mkoa uwe na umeme wa uhakika na wa bei nafuu utakaowafanya wananchi kuzalisha kwa kutumia umeme…,” alisema.

Alisema Tanzania lazima iwe na umeme wa uhakika na wa gharama nafuu ndipo itafikia malengo ya nchi ya kipato cha kati. Alisisitiza kuwa, bila umeme, viwanda haviwezi kuzalisha na ajira haziwezi kupatikana. Alisema hakuna nchi yoyote duniani ambayo ina kipato cha kati ambayo watu wa kati hawatumii umeme.

Alisema Tanzania ina asilimia 42 wakati inatakiwa kufikia asilimia 75. “Kwa hiyo Tanesco mtake msitake, lazima umeme uwepo tena wa bei nafuu ili kuwezesha viwanda vyetu viweze kuzalisha kwa wingi na pato letu liweze kupanda zaidi ya mara nne na asiyetaka kasi hiyo ataondoka atuachie kazi zetu,” aliagiza Muhongo.

Wakati huo huo, aliagiza uongozi wa Tanesco wilaya ya Biharamulo kwamba ifikapo Januari 2 mwakani, wawapatie majibu wananchi wa kata ya Nyarukongongo yenye kaya 800 ni lini watapatiwa umeme. Alisema wameshachangia fedha zao na wanahitaji umeme.

Alisisitiza, wakati huu sio wa kusubiri wateja wawafuate maofisa wa Tanesco ofisini bali wao wanapaswa kuwafuata wateja vijijini. Aliwataka Tanesco kuacha tabia ya kuomba fedha Hazina wakati zipo kwa wananchi wanaohitaji kuunganishiwa umeme.

Aidha, ameagiza uongozi wa Tanesco mkoani Kagera kuhakikisha wanafunga umeme katika jengo la Forodha la Rusumo kwa upande wa Tanzania ndani ya wiki moja ijayo na kuepuka hali ya sasa ambayo watumishi wanatumia umeme kutoka Rwanda.

Meneja wa Tanesco wa Kanda ya Ziwa, Aron Maganga alimweleza Waziri Muhongo kuwa ifikapo mwaka 2018, mradi wa Gridi ya Taifa utakuwa umekamilika katika mkoa wa Geita na itakuwa rahisi mkoa wa Kagera kuingizwa kwenye gridi hiyo.

Maganga alisema chini ya mpango wa sasa, shirika limetoa maagizo kwa mameneja wote wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha ifikapo Januari 15 mwakani mita mbovu zote zitarekebishwa na wateja wote wa zamani walioomba kuunganishiwa umeme watakuwa wameunganishiwa umeme.

Waziri aliwataka wananchi hao kuwa ifikapo Janurai 15, matatizo hayo ya kufungiwa umeme na uwapo wa mita mbovu katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera, watoe taarifa kwa wakuu wa wilaya matatizo yao yashughulikiwe.

Waziri Muhongo ametembelea vituo vya kupokea na kusambaza umeme vya kuzalisha umeme vya Kibeta, Biharamulo, Ngara na kukagua jengo la forodha la Rusumo na mradi wa kuzalisha umeme wa maji wa Rusumo.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera, John Mongella kabla ya kuanza ziara ya kukagua miundombinu ya umeme mkoani humo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kushoto) akimsikilizaMhandisi Filbert Mlaki.
Waziri wa nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akikagua moja ya mtambo wa kuzalisha umeme wa Kituo cha Kibeta

Leticia Nyerere Mahututi Nchini Marekani......Apumulia Mashine,

  Familia Yaanza Kujipanga

 

HALI ya afya ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Leticia Nyerere si nzuri.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Leticia amelazwa katika Hospitali ya Doctors Community iliyopo Maryland nchini Marekani.

Chanzo hicho kimeeleza kuwa mwanasiasa huyo amelazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), ingawa haijafahamika anasumbuliwa na tatizo gani.

Tangu juzi usiku, kumekuwapo na taarifa nyingi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zinazodai kuwa Leticia amefariki dunia, jambo ambalo si kweli.

Habari za uhakika ambazo zimepatikana kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ya Nyerere  ni kwamba Leticia yupo hai ingawa anaumwa.

“Hali ya Leticia si nzuri yuko ICU nchini Marekani, kwa muda mrefu sasa amekuwa akiumwa. Tumejaribu kuwasiliana na mmoja wa watoto wake kule Marekani, ametwambia hali si ya kuridhisha kabisa.

“…tunamwombea Mungu ampe  nguvu ili arudi katika hali ya kawaida. Tumeshangazwa na uvumi wa taarifa hizi kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia, jamani hebu tuwe na subiri ya kuwaombea  wenzetu wanapokuwa kwenye matatizo na si kukimbilia kusema fulani kafa,” alisema mwanafamilia huyo.

Leticia aliolewa kisha kutengana na mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere mwaka 1996, ambapo walifanikiwa kupata watoto watatu.

Jana Msemaji wa Familia ya Mageni Msobi, John Shibuda, alikiri kuugua kwa mbunge huyo wa zamani, huku akisita kueleza ugonjwa unaomsumbua.

“Ni kweli Leticia anaumwa na amelazwa Marekani na hali yake si nzuri, kwa sasa tunawasiliana na madaktari pamoja na wanafamilia walioko huko kwa ukaribu zaidi.

“Siwezi kusema ugonjwa kwa sasa kwani suala hilo ni siri kati ya mgonjwa na daktari wake ila sisi kama familia tutaeleza kwa kina wakati utakapofika,” alisema Shibuda.

Julai 27 mwaka huu, Leticia  alitangaza kuihama Chadema  na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akitangaza uamuzi wake, Leticia alisema aliamua kuihama CCM baada ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo wakati huo. Hata hivyo alikiri kuwa alikurupuka katika kufikia uamuzi huo.

“Moyo wangu umekuwa ukisononeka kutokana na kukaa Chadema na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha nje ya nchi, sasa nasema narudi nyumbani kukitumikia chama changu,” alisema.

CCM Yajipanga Kurudia Uchaguzi Zanzibar Huku CUF wasema uchaguzi usirudiwe




KAMATI Maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein imewataka wananchi na wanachama kujiweka tayari na hatimaye kujitokeza katika uchaguzi mkuu wa marudio.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu, wananchi wametakiwa kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio na kuachana na propaganda zinazotolewa na watu wachache kwa lengo la kupotosha ukweli.

“Kikao cha Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar kilichokutana hapa chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar, Dk Shein kimewataka wananchi, wanachama na wafuasi wa CCM kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa marudio ambao tarehe ya kufanyika kwake itatangazwa na taasisi husika,” imesema taarifa hiyo ya Waride.

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25 ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kwa kile alichoeleza ni kuwepo kwa ukiukwaji wa kanuni na sheria za uchaguzi huru wa kidemokrasia.

Katika kikao cha jana kilichohudhuria pia na viongozi kadhaa wa kitaifa akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kilijadili ajenda mbili ikiwemo hali ya kisiasa mara baada ya uchaguzi mkuu kwa upande wa CCM.

Katika taarifa hiyo, chama hicho kimesema kimeridhishwa na mwenendo wa hali ya kisiasa na kimewapongeza wanachama waliojitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Aidha chama kimepongeza na kutoa baraka kwa mazungumzo yanayoendelea ya viongozi wakuu wa kisiasa yakiwa na lengo la kuleta amani ya kudumu. Kamati ya mazungumzo ya hali ya kisiasa Zanzibar yenye lengo la kusaka amani ya kudumu iliyovurugika kutokana na kufutwa kwa uchaguzi mkuu inaundwa na viongozi wastaafu wakiwemo marais, Dk Salmin Amour, Amani Abeid Karume, Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Akizungumza juzi Ikulu, jijini Dar es Salaam, Rais wa Zanzibar, Dk Shein alisema mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na taarifa kamili yatakapofikia tamati. Alipoulizwa kuhusu hatma ya CCM kama uchaguzi mkuu utarudiwa, Waride alisema chama bado kiko imara na hakijatetereka.

“Wapo wanaosema CCM imeyumba, si kweli wala CCM haijapoteza majimbo kwa sababu kura hazikumalizwa kuhesabiwa,” alisema. 
 
Chama cha Wananchi CUF Zanzibar kimesema hakipo tayari kupokea maazimio ya mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa Uchaguzi Mkuu kama yatakuwa yanakwenda kinyume na maamuzi waliofanya wananchi kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 Mwaka huu.

Tamko hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Mipango wa Chama hicho, Omar Ali Shehe katika mahojiano maalum na Nipashe Jumapili juu ya mazungumzo ya kutafuta mufaka wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.

Mazungumzo hayo yanaogozwa na Rais wa Zanzibar DK. Ali Mohamed Shein na kuwashirikisha Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar na Mgombea urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi pamoja na marais wastaafu wa Zanzibar. Alisema CUF kiko tayari kupokea maamuzi na kuyaheshimu kutoka katika Kamati hiyo ya mazungumzo kama yatakuwa yamezingatia maamuzi ya wananchi waliyoyafanya kupitia Uchaguzi Mkuu huo.

Inaaminika kuwa matokeo yaliyofutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) yalikuwa yakimpa ushindi Hamad. “Sisi tunasubiri matokeo ya mazungumzo yao tukiamini kwamba mazungumzo hayo hayatokwenda kinyume na maamuzi waliyofanya wananchi kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu,” alisema Shehe.

Alisema kuwa Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha hakuwa na mamlaka ya kikatiba na kisheria kufuta matokeo ya uchaguzi huo ambao tayari ulikuwa umekamilika kwa asilimia 70 na matokeo ya majimbo 31 yakiwa yametangazwa katika uchaguzi huo.

Shehe alisema siri ya kufutwa kwa matokeo ni baada ya Mwenyekiti kuona CCM wapo katika hatari ya kuanguka katika uchaguzi huo na hakuna sababu nyigine. “Mchezo wa kufuta matokeo kwa sababu tu chama tawala kiko katika hatari ya kuanguka utaendelea kufanyika kama  tukiacha hivi hivi,” alisema.

“Huku ni kuvuruga demokrasia ya nchi yetu.” Alisema miezi miwili sasa imemalizika lakini hakuna mtu yoyote aliyefikishwa Mahakamani kwa kuharibu uchaguzi au Mwenyekiti kuweka vielelezo na ushahidi wa kuharibika kwa uchaguzi huo.

Aidha, alisema msimamo wa Baraza Kuu la CUF ndiyo muongozo wa chama kuwa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar warudi kazini wakamilishe ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi wa awali na kumtangaza mshindi wa uchaguzi huo.

Alisema kuwa hali ya kisiasa ya Zanzibar ipo katika giza kutokana na wananchi kushindwa kufahamu lini watapata viongozi wa kidemokrasia huku wakiendelea kushuhudia kupanda kwa gharama za maisha Visiwani humo.

Hata hivyo alisema kuwa mazungumzo hayo yamesaidia kwa kiasi kikubwa kutuliza hali ya amani na kuondoa hofu wananchi lakini alitaka yakamilike kwa wakati ili wananchi wajue hatia yao ya kupata viongozi.

Aidha alisema kuwa CUF inatambua kuwepo kwa watu wanaotaka kupindisha uchaguzi uliyofanyika Oktoba 25 mwaka huu lakini alisema hawatafanikiwa kutokana na  ripoti za waangalizi wa ndani na nje kuweka wazi kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki Zanzibar.

“Wakati Mwenyekjiti wa ZEC anatangaza kufuta matokeo tayari matokeo katika Majimbo 54 yalikuwa yamekamilika na kubandikwa matokeo na Wagombea kupewa vyeti vyao vya ushindi hoja ya kufuta matokeo Mwenyekiti katoa wapi?” Aliuliza.

“Haiwezekani kufanyika uchaguzi wa marejeo kabla ya uchaguzi wa mwanzo kukamilika Zanzibar, sawa na kusherekea harusi kabla ya ndoa kufanyika.”

Alisema wakati Mwenyekiti Jecha anafuta matokeo hayo katika meza yake majimbo tisa yalikuwa yanamsubili kutangaza matokeo baada ya uhakiki kukamilika na kubakia Majimbo 14 ya Wilaya tatu za Kisiwani Pemba.

Aidha alisema kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo alivunja kanuni na sheria kutokana na kitendo cha ZEC kuhakiki matokeo ya Urais mara mbili wakati tayari kazi kama hiyo ilikuwa imefanyika katika Majimbo na kumalizika na kumalizika  salama kabla ya kufutwa kwa matokeo hayo.

“Mwenyekiti arudi kazini atangaze marokeo na mshindi wa urais wa Zanzibar uchaguzi wa marudio hatutaki kusikia Zanzibar,” alisema Shehe.

Jecha alisema aliamua kufuta matokeo ya uchaguzi huo baada ya kutawaliwa na vitendo vya udaganyifu ikiwemo idadi ya wapiga kura kuzidi katika baadhi ya vituo kinyume na idadi ya watu waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura Visiwani humo.

Kocha Louis Van Gaal asema ni heri nijiuzulu kuwa meneja wa klabu hii kuliko kusubiria nifukuzwe






























Kocha Louis Van Gaal wa Manchester United ya nchini England amesema ni heri ajiuzulu kuwa meneja wa klabu hiyo kuliko kusubiria afukuzwe kwani ni dhihaka kwake na kwamba itachafua career yake ya maisha yake ya soka kama kocha.
Presha imezidi kuwa juu kwa mwalimu huyo wa mpira mara baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Stoke City huku akionekana kukalia kuti kavu klabuni hapo kutokana na matokeo hayo ambapo ni kipigo cha nne mfululizo na mchezo wa 14 bila ushindi.
Wiki iliyopita tetesi zilisambaa zikimtaja kocha huyo kuwa katimuliwa kazi, kitu ambacho kilimkasirisha Van Gaal ambaye alijinasibu kurudisha ari ya ushindi katika kikosi chake kabla ya kufungwa tena, huku akitakiwa kupambana tena na Chelsea katika uwanja wa Stamford Bridge.
Akiongea mara baada ya kumalizika mchezo dhidi ya Stoke City, kocha huyo alisema atajiuzulu Kama atapoteza tena mchezo wa Jumatatu hii dhidi ya Chelsea, ambao utakuwa ni mchezo wa tano mfululizo.
Kocha huyo kwasasa amekua katika wakati mgumu zaidi na inatia shaka kuona kama anapata sapoti ya uongozi na wadhamini wa klabu mara baada ya matokeo ya weekend iliyopita.

AZAM WA PUNGUZA GEPU LA POINT KWA YANGA JUMATANO AZAM FC NA MTIBWA

Shomari Kapombe akipongezwa na wachezaji wanzake wa Azam FC baada ya kuifungia timu yao bao la pili
Shomari Kapombe akipongezwa na wachezaji wanzake wa Azam FC baada ya kuifungia timu yao bao la pili
Magoli kutoka kwa Kipre Tchetche na Shomari Kapombe yameipa Azam ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es Salaam.
Kipre Tchetche aliifungia Azam bao la kuongoza dakika ya 11 kipindi cha kwanza bao ambalo lilidumu kwa muda wote wa kipindi cha kwanza.
Salum Kanoni (kulia) akichuana na Kipre Tchetche
Salum Kanoni (kulia) akichuana na Kipre Tchetche
Baada ya kupata bao hilo Azam walijikuta wakibanwa vilivyo na Kagera Sugar ambao walimiliki mchezo kwa asilimia nyingi na kutengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kukwamisha mipira wavuni.
Wakati dakika za kipindi cha kwanza zinakaribia kumalizika, Kagera Sugar walipata mkwaju wa penati baada ya beki wa Azam kuunawa mpira kwenye eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo kuamuru lipigwe tuta. Beki wa zamani wa Simba SC Salumu Kanoni akapiga penati hiyo lakini ikaokolewa na mlinda mlango wa Azam FC Aishi Manula.
Shomari Kapombe (kushoto) akimtoka beki wa Kagera Sugar
Shomari Kapombe (kushoto) akimtoka beki wa Kagera Sugar
Kipindi cha pili bado Azam walikuwa kwenye wakati mgumu kwasababu walizidi kubanwa na Kagera Sugar kwa muda mwingi wa kipindi cha pili lakini bado tatizo la kushindwa kuzitumia nafasi zilizopatika kupachika mabao liliendelea kuwaandama.
Dakika ya 78 Shomari Kapombe akazima matumaini ya Kagera Sugar kupata japo pointi moja ugenini baada ya kumzidi mbio beki wa Kagera Sugar Juma Jabu na kutupia mpira kambani kuipa Azam FC bao la pili na la ushindi kwenye mchezo huo.
Kwenye mchezo huo Kagera Sugar watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nyingi za wazi walizotengeneza baada ya kufanikiwa kuwashika Azam kwa muda mwingi wa mchezo.
Juma Jabu akiondosha mpira kwenye hatari mbele ya Kipre Tchetche
Juma Jabu akiondosha mpira kwenye hatari mbele ya Kipre Tchetche
Azam FC imefikisha pointi 32 pointi moja nyuma ya vinara wa VPL Yanga SC ambao wanapointi 33 wakiwa mbele kwa mchezo mmoja kwani wao wameshacheza michezo 13 hadi sasa.
Kagera Sugar wao bado wapo kwenye nafasi ya 15 wakiwa na pointi tisa nafasi moja mbele ya African Sports ya Tanga ambayo inaburuza mkia ikiwa na pointi nne tu baada ya kushuka dimbani mara 12.

 

CCM MKOA WA IRINGA YATAJA WASALITI 102, YUPO MWENYEKITI CCM MKOA NA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA





KAMATI ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa imetangaza majina ya makada wake 102, wakiwemo vigogo wa chama hicho mkoani hapa, wanaotuhumiwa kukisaliti na kukihujumu chama wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Wasaliti hao wametangazwa jana na Katibu Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk Yahaya Msigwa ikiwa ni wiki moja tu tangu vijana wa chama hicho waifungie kwa zaidi ya saa mbili  kamati hiyo, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza, katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa, mjini Iringa.

Vijana hao zaidi ya 50 wanaotarajiwa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Manispaa ya Iringa, Kaunda Mwaipyana, waliifungia kamati hiyo wakishinikiza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu ajiuzulu kwa madai ya kukisaliti chama hicho katika uchaguzi wa Jimbo la Iringa Mjini.

Msambatavangu mwenyewe amenukuliwa mara kadhaa akikanusha tuhuma hizo huku akidai kwamba zinasukwa na vigogo wenzake wa chama hicho mkoani hapo ili kulinda maslai yao na kuficha ukweli halisi wa sababu zilizopelekea wapoteze jimbo hilo na kata 14 kati ya 18 kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akizungumza na wanahabari jana, Msambatavangu ambaye alikiri jina lake kuwemo katika orodha ya makada wa CCM wanaotuhumiwa kukisaliti chama hicho iliyopokelewa na kamati aliyoiongoza yeye mwenyewe alisema pamoja na kwamba tuhuma hizo dhidi yake hazina ukweli yupo tayari kuhojiwa na kutoa utetezi wake katika vikao vitakavyofanya kazi hiyo.

“Najua na wanajua kwamba tuhuma hizo dhidi yangu hazina ukweli wowote na ikithibitika ni za kweli nitajiuzulu vinginevyo niwahakikishie wana CCM mkoani hapa kwamba nitawania tena nafasi hii ya uenyekiti katika uchaguzi ujao kwasababu sifa ninazo,” alisema.

Akizungumza na wanahabari, Dk Msigwa alisema taarifa iliyopokelewa katika kamati hiyo inaonesha Iringa Mjini inaongoza kwa kuwa na wasaliti wengi, ikiwa na jumla ya wasaliti 32.

Pamoja na kukataa kutaja majina ya wasaliti hao kwa madai kwamba watajulikana watapoanza kuitwa kwenye vikao vya maadili vya ngazi mbalimbali za chama hicho mkoani hapa, alijikuta akilazimika kuwataja vigogo wawili waliohusishwa katika tuhuma hizo Iringa Mjini baada ya wanahabari kumbana kwa maswali.

Mbali na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa kutajwa rasmi katika orodha ya watuhumiwa hao, Dk Msigwa alimtaja kigogo mwingine aliyepo katika orodha hiyo kuwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa anayewakilisha Manispaa ya Iringa, Mahamudu Madenge.

Katika mchakato wa chama hicho wa kumpata mgombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini uliofanyika Agosti mwaka huu, Msambatavangu na Madenge walikuwa ni miongoni mwa wana CCM 13 waliojitosa kuwania nafasi hiyo ambayo mshindi wake alikuwa Frederick Mwakalebela.

Wakati Mwakalebela alishinda kura hizo za maoni kwa kupata kura 4,388, Msambatavangu alikuwa mshindi wa pili kwa kupata kura 2,077  na Madenge alikuwa wa tano kwa kupata kura 423, nyuma ya Dk Yahaya Msigwa aliyepata kura 1,097 na Dk Augustine Mahiga ambaye Rais Dk John Magufuli amemteua kuwa mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje, aliyepata kura 745.

Kama tuhuma hizo zilivyokanushwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa; Madenge naye amekanusha kuhusika na tuhuma hizo akisema; “Baada ya kushindwa kura za maoni nilirudi kijijini kwangu Image wilayani Kilolo na kufanya kampeni za kata ya Image na za jimbo la Kilolo ambako CCM na wagombea wake walipata ushindi mkubwa.”

Madenge alisema mbali na Kilolo, aliombwa pia kufanya kampeni katika majimbo ya uchaguzi ya wilaya ya Mufindi ambako pia CCM ilipata ushindi mnono.

“Naomba waniache kwasababu wanajua mimi nilishindwa vibaya kura za maoni kwa kupata kura 423 tu; kura ambazo hata kama ningewaambia walionipigia wakawapigie hao Chadema zisingeathiri matokeo hayo,” alisema.

Katika uchaguzi, huo Mchungaji Peter Msigwa wa Chadema alichaguliwa kuongoza jimbo hilo baada ya kupata kura 43,154 dhidi ya kura 32,406 za Frederick Mwakalebela wa CCM.

Akitaja orodha ya wasaliti wengine, Dk Msigwa alisema katika majimbo ya wilaya ya Mufindi kuna wasaliti 26 wakiwemo watumishi wanne halmashauri hiyo ambao hata hivyo hawakutajwa majina.

Kwa upande wa wilaya ya Kilolo, alisema taarifa waliyopokea inaonesha kuna wasaliti 23, huku Jimbo la Kalenga ikiwataja wasaliti saba na jimbo la Isimani wasaliti 14 wakiwemo watumishi wanne.

Alisema katika kuzishughulikia tuhuma hizo, watuhumiwa hao wataitwa kwenye vikao vya maadili vya ngazi mbalimbal ili wapate fursa ya kujitetea na watakaothibitika kutenda makosa hayo watachukuliwa hatua kwa kuzingatia kanuni, taratibu na Katiba ya chama.

“Wale ambao maamuzi dhidi yao hayawezi kufanywa na vikao vya ngazi ya kata, wilaya na mkoa, taarifa zao zitapelekwa taifani na tuombe vikao hivyo vya taifa vitende haki kwa kuzingatia ushahidi na mapendekezo yatakayotolewa na vikao vyetu ili kushughulikia tatizo hili la usaliti,” alisema.

Wakati huo huo, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Elisha Mwampashi ambaye pia ni Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa amekanusha uvumi unaonezwa na baadhi ya wa CCM kwamba chama hicho kilitumia zaidi ya Sh Milioni 600 kwa ajili ya uchaguzi wa jimbo la Iringa Mjini.

“Sio kweli hata kidogo, hatukuwa na fedha hizo, na nataka mjue CCM ilizingatia sana sheria ya gharama za uchaguzi wakati  tukifanya kampeni. Niwashukuru CCM Makao Makuu, Mkoa na wana CCM na wapenzi wetu kwa jinsi walivyojitolea katika kampeni hizo,” alisema.

Chanzo; frankleonard blog