MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday, 10 October 2015

EDWARD LOWASA APATA MAPOKEZI YA NGUVU MJINI TARIME WASEAMA WATAMCHAGUA HIVYO ALIVYO


 
Vijana wa Mjini Tarime wakiongoza mapokezi ya Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, alipowasili mjini Tarime kwa Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 10, 2015. 
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Tarime katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015. 
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, akiwasalimia wananchi wa Mji wa Tarime waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Mh. Vicent Nyerere, akizungumza wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Vijijini kupitia CHADEMA, Mh. John Heche, akihutubia wananchi wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini kupitia CHADEMA, Mh. Ester Matiko akihutubia wananchi wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.

Sehemu ya wananchi wa Mji wa Tarime, walioshiriki Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Tarime Mkoani Mara.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara, Mh. Vicent Nyerere, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Mh. Ester Matimo pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mh. John Heche, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, asikiliza jambo kutoka kwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Mh. Ester Matimo, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Tarime katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba, Tarime Mjini, Mkoani Mara leo Oktoba 10, 2015.




MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 11 OCTOBER 2015

Tembelea blog hii mbeyagreennews usome magazate ya kila siku kama kawaida

SWALA LA JUMA MWAMBUSI KUTUA YANGA, KUJULIKANA KESHO JUMAPILI


Kila kitu kinaenda vizuri kwa Kocha Juma Mwambusi kutua Yanga kumsaidia Hans van Der Pluijm kuifundisha timu hiyo akichukua nafasi ya Charles Mkwasa aliyepata kazi Taifa Stars.


Yanga hadi sasa ina orodha ya makocha kadhaa waliotajwa kumudu kazi iliyokuwa ikifanywa na Mkwasa, lakini taarifa zinasema Mwambusi anayeinoa Mbeya City ndiye mwenye nafasi kubwa ya kupewa dili hilo.

“Pluijm ndiye anayesubiriwa kutoa jibu lake juu ya msaidizi wake na Mwambusi anapewa nafasi kubwa kutokana na uwezo wake hasa jinsi anavyoifunga Simba kila mara,” kilisema chanzo chetu.

Alipotafutwa Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha ili atoe ufafanuzi kuhusu jambo hilo, alisema: “Tuna majina ya makocha wengi na Jumapili (kesho) tutamtangaza aliyekidhi vigezo na Jumatatu ataanza kazi.”

JUMA MWAMBUSI  KOCHA MKUU WA MBEYA CITY
Mwambusi mwenyewe amekuwa mgumu wa kutoa ufafanuzi kuhusu kuhusishwa kwake na Yanga kwani mara kadhaa hapokei simu yake ikidaiwa yupo katika mazungumzo ya kina na viongozi wake.

COUTINHO NA MWENZAKE UONGOZI WA YANGA HAUHUSIKI


UONGOZI wa Yanga SC umesema kwamba beki Mtogo, Vincent Bossou na kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho wote wamesajiliwa kwa mapendekezo ya kocha wao Mkuu, Mholanzi Hans van der Pluijm.
Akizungumza na MTANDAO HUU  jana mjini Dar es Salaam, Katibu wa Yanga SC, Dk. Jonas Tiboroha amesema kwamba wachezaji wote hao ni pendekezo la kocha.
Dk. Tiboroha amesema kwamba wakati klabu inamrejesha Pluijm Januari mwaka huu, alikuta Wabrazil wawili, wote viungo Emerson de Oliveira Neves Roque na Coutinho naye akaamua kuacha mmoja na kubaki na mmoja.
Vincent Bossou (katikati) amecheza mechi moja tu dhidi ya Mbeya City, tena ya kirafiki kwa dakika 45 tangu amesajiliwa Yanga SC Agosti

“Na ndipo aliamua abaki na Coutinho. Na hata katika usajili wa msimu huu, kocha aliafiki aachwe beki Zuttah (Joseph) wa Ghana, ili abaki Coutinho. Sasa kwa nini hamtumii, sisi hatuwezi kumuingilia katika programu zake,”amesema.
Aidha, Katibu huyo amesema kwamba alipoletwa beki Bossou alipelekwa kwenye kambi ya Tukuyu Mbeya kwa majaribio ya wiki mbili na kocha akaridhishwa na uwezo wake na kuagiza asajiliwe.
“Lakini bado uongozi unanyooshewa kidole juu ya usajili wa hawa wachezaji. Mimi nadhani Waandishi wa Habari bora wakamuulize kocha, tena anaweza akawapa sababu nzuri tu,”.
“Sisi tulimuuliza, akasema ana wachezaji wengi na wote wazuri, kila mmoja atacheza wakati ukifika. Akatupa mfano Busungu (Malimi), naye alikuwa anakaa benchi, lakini baada ya kuingia katika mechi na Simba na kufunga bao na kuseti lingine, mechi iliyofuata alianza. Na labda mechi ijayo pia ataanza,”amesema Tiboroha.
Katibu huyo amesema uongozi hauwezi kumuingilia kocha katika upangaji wa timu na hususan wakati ambao timu inacheza vizuri na kushinda.
Andrey Coutinho alikuwa ana wakati mzuri chini ya kocha Mbrazil mwenake, Marcio Maximo kabla ya kuanza kusugua benchi chini ya Mholanzi, Plujm

“Watu watakuona chizi, kuhoji kocha kwa nini hampangi nani wakati timu inashinda kila mechi na kucheza soka ya kuvutia. Mimi nadhani tuwe na subira,”amesema.
Vincent Bossou amecheza mechi moja tu dhidi ya Mbeya City, tena ya kirafiki kwa dakika 45 tangu amesajiliwa Yanga SC Agosti, mwaka huu, wakati Coutinho alikuwa ana wakati mzuri chini ya kocha aliyemsajili, Mbrazil mwenzake, Marcio Maximo kabla ya kuanza kusota benchi chini ya Pluijm.
Winga huyo Mbrazil hadi sasa ameichezea Yanga SC jumla ya mechi 35 na kufunga mabao saba, nyingi akitokea benchi kipindi cha pili mwishoni.  
Yanga SC kwa sasa wanaendelea na mazoezi mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, Oktoba 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
.

Friday, 9 October 2015

PATO LA TAIFA LIMEONGEZA KWA AILIMIA 7.9 HUKU WATANZANIA TUNALIA NJAAA

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) YASEMA 

 Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa za pato la taifa robo ya pili ya mwaka kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2015. Kushoto ni Meneja Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
……………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema pato la taifa limeongezeka kwa asilimia 7.9 huku sekta ya madini na uzalishaji umeme ikifanya kuongezeka kwa pato katika kipindi cha robo mwaka 2015 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2014.

Akizungumza  Dar es Salaam leo asubuhi wakati wakati akitoa taarifa za pato la taifa robo ya pili ya mwaka kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2015, Mkerugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Morrice Oyuke alisema ongezeko hilo la takwimu ni la miezi mitatu ya mwaka huu.

Oyuke alisema ongezeko hilo la pato la taifa linaenda sanjari na matokeo ya thamani ya pato la taifa kwa mwaka huu ambalo lilikuwa ni trilioni 89.0 ambapo  katika robo ya mwaka ni trilioni 45.5 ikilinganishwa na trilioni 39.0 katika mwaka 2014.
Alisema thamani ya pato la taifa ya robo mwaka ya trilioni 45.5 ni kubwa hivyo kusababisha  pato la taifa la mwaka mzima linaweza kukuwa kama uchumi hautotetereka.
“Kama uchumi hautaweza kuguswaguswa na matatizo mingene inaweza ikasababisha pato la taifa la mwaka huu likaongezeka badala ya ile iliyotegemewa hapo mwanzo,”alisema.
Alisema ongezeko hilo la pato la taifa limechangiwa na sekta mbalimbali kufanya vizuri katika kipindi cha robo mwaka.
Alisema sekta ambazo zimeongoza katika kipindi cha robo mwaka ni sekta ya madini,umeme,kilimo na mifugo,viwanda na ujenzi na huduma za kitaalamu.
Alisema sekta ya uzalishaji umemere imekuwa kwa asilimia 18.5 huku bidhaa za viwandani ni asilimia 6.9 madini mawe na kokoto  zimeongezeka asimilia 8.3 limeongezeka kutokana na shghuli za kiuchumi.

“Kutokana na taarifa hii ya pato la taifa kwa robo mwaka taarifa hizi zitumike katika kupanga na kurekebisha sera mbalimbali za maendeleo ya nchi,” alisema.

STARS WAWASILI SALAMA LILONGWE, NA SASA WAKO SAFARINI KWA BASI KWENDA BLANTYRE

   

Wachezaji wa Taifa Stars wakitremka kwenye ndege baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu, mjini Lilongwe, Malawi muda huu tayari kwa safari ya barabara ya saa tatu kuelekea Blantyire kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji Jumapili mchujo wa awali kuwania kupangwa kwenye makundi ya kugombea tiketi ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi. Tanzania ilishinda 2-0 mchezo wa kwanza
Sasa safari inaanza upyaa kwa saa tatu kuelekea Blantyre
Vijana wanaonekana wako vizuri kuelekea mchezo huo wa Jumapili

MASHABIKI WA MBEYA CTY MATAWI KUKUTANA KESHO KWAJIRI YA MAANDALI NA SIMBA FC


IMG_0505
KIKAO cha mashabiki wa timu ya Mbeya city Fc kutoka umoja wa matawi yote yaliyopo jijini mbeya na maeneo jirani wanatarajia kufanya kikao kesho jioni kwenye hotel ya Appleline, ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma lijalo kwenye uwanja wa Sokoine.
Muda mfupi uliopita katibu mkuu wa umoja huo Thimoth Mwalongo amesema kuwa kikao hicho cha kesho licha ya kuwa na ajenda nyingi lakini kubwa zaidi itakuwa ni mikakati ya kuhakikisha City inaibuka na ushindi kwa mara nyingine mbele ya timu hiyo ya Msimbazi.
“Ni kikao muhimu, kwa sababu kitakuwa na mambo mengi ya kujadili na kujadiliwa lakini kubwa zaidi ni mikakati kuhakikisha tunawashikisha adabu Simba kwa mara nyingine, naomba mashabiki wenzangu wajitokeze kwa wingi ili tuweke mipango sawa tukiwa na nguvu moja kama ambavyo imekuwa kwenye nyakati zilizopita” alisema.
Akiendelea zaidi Katibu huyo wa umoja wa mashabiki aliweka wazi kuwa bado wanaimani kubwa na kikosi cha timu yao licha ya matokeo mabaya kwenye michezo kadhaa iliyopita na wanauhakika City itakuwa sehemu ya timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi ya msimu huu.
“Ni kweli tumeanza vibaya lakini hatuna shaka, imani ya kila mmoja wetu hapa timu yetu itakuwa sehemu ya timu nne za juu mwisho wa msimu, tumekuwa na kawaida ya kuanza vibaya lakini tunamaliza vizuri ingawa mwaka huu kuna utoafauti kidogo kwenye kikosi hasa ukizingatia ugeni wa wachezaji wengi lakini imani kwa timu yetu ni kubwa sana” alimaliza.
IMG_3093


PIGO KWA MANCHESTER CITY KWENYE MECHI Vs UNITED BAADA AGUERO KUPATA MAJERAHA

October 25 Manchester City watakua na mechi muhimu dhidi ya Manchester united. Hadi sasa Manchester city imepata pigo kwa mchezaji wao muhimu Kun Aguero baada ya kupata jeraha akiwa anacheza na timu yake ya taifa.

Aguero alishidwa kuendelea na mechi na kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Tevez. Kila mtu anajua Aguero ni mchezaji muhimu sana kwa Man city ambapo wiki iliyopita aliweza kufunga magoli 5 peke yake.
Ripoti zaidi kuhusu jeraha la Aguero inasemekana kwamba alitokwa machozi kwa maumivu makali akiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kutolewa alivyotolewa uwanjani. Jeraha hilo inasemekana kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mechi hiyo muhimu. Ikumbukwe pia Aguero alipata jeraha kwenye EPL wiki kadhaa zilizopita
2D3841AD00000578-0-image-a-1_1444398952186