MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Friday, 9 October 2015

PATO LA TAIFA LIMEONGEZA KWA AILIMIA 7.9 HUKU WATANZANIA TUNALIA NJAAA

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) YASEMA 

 Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Morrice Oyuke (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa za pato la taifa robo ya pili ya mwaka kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2015. Kushoto ni Meneja Takwimu za Pato la Taifa, Daniel Masolwa.
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
 Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
……………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
OFISI ya Taifa ya Takwimu imesema pato la taifa limeongezeka kwa asilimia 7.9 huku sekta ya madini na uzalishaji umeme ikifanya kuongezeka kwa pato katika kipindi cha robo mwaka 2015 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka 2014.

Akizungumza  Dar es Salaam leo asubuhi wakati wakati akitoa taarifa za pato la taifa robo ya pili ya mwaka kuanzia mwezi Aprili hadi Juni 2015, Mkerugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Morrice Oyuke alisema ongezeko hilo la takwimu ni la miezi mitatu ya mwaka huu.

Oyuke alisema ongezeko hilo la pato la taifa linaenda sanjari na matokeo ya thamani ya pato la taifa kwa mwaka huu ambalo lilikuwa ni trilioni 89.0 ambapo  katika robo ya mwaka ni trilioni 45.5 ikilinganishwa na trilioni 39.0 katika mwaka 2014.
Alisema thamani ya pato la taifa ya robo mwaka ya trilioni 45.5 ni kubwa hivyo kusababisha  pato la taifa la mwaka mzima linaweza kukuwa kama uchumi hautotetereka.
“Kama uchumi hautaweza kuguswaguswa na matatizo mingene inaweza ikasababisha pato la taifa la mwaka huu likaongezeka badala ya ile iliyotegemewa hapo mwanzo,”alisema.
Alisema ongezeko hilo la pato la taifa limechangiwa na sekta mbalimbali kufanya vizuri katika kipindi cha robo mwaka.
Alisema sekta ambazo zimeongoza katika kipindi cha robo mwaka ni sekta ya madini,umeme,kilimo na mifugo,viwanda na ujenzi na huduma za kitaalamu.
Alisema sekta ya uzalishaji umemere imekuwa kwa asilimia 18.5 huku bidhaa za viwandani ni asilimia 6.9 madini mawe na kokoto  zimeongezeka asimilia 8.3 limeongezeka kutokana na shghuli za kiuchumi.

“Kutokana na taarifa hii ya pato la taifa kwa robo mwaka taarifa hizi zitumike katika kupanga na kurekebisha sera mbalimbali za maendeleo ya nchi,” alisema.

STARS WAWASILI SALAMA LILONGWE, NA SASA WAKO SAFARINI KWA BASI KWENDA BLANTYRE

   

Wachezaji wa Taifa Stars wakitremka kwenye ndege baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu, mjini Lilongwe, Malawi muda huu tayari kwa safari ya barabara ya saa tatu kuelekea Blantyire kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya wenyeji Jumapili mchujo wa awali kuwania kupangwa kwenye makundi ya kugombea tiketi ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi. Tanzania ilishinda 2-0 mchezo wa kwanza
Sasa safari inaanza upyaa kwa saa tatu kuelekea Blantyre
Vijana wanaonekana wako vizuri kuelekea mchezo huo wa Jumapili

MASHABIKI WA MBEYA CTY MATAWI KUKUTANA KESHO KWAJIRI YA MAANDALI NA SIMBA FC


IMG_0505
KIKAO cha mashabiki wa timu ya Mbeya city Fc kutoka umoja wa matawi yote yaliyopo jijini mbeya na maeneo jirani wanatarajia kufanya kikao kesho jioni kwenye hotel ya Appleline, ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Simba uliopangwa kuchezwa mwishoni mwa juma lijalo kwenye uwanja wa Sokoine.
Muda mfupi uliopita katibu mkuu wa umoja huo Thimoth Mwalongo amesema kuwa kikao hicho cha kesho licha ya kuwa na ajenda nyingi lakini kubwa zaidi itakuwa ni mikakati ya kuhakikisha City inaibuka na ushindi kwa mara nyingine mbele ya timu hiyo ya Msimbazi.
“Ni kikao muhimu, kwa sababu kitakuwa na mambo mengi ya kujadili na kujadiliwa lakini kubwa zaidi ni mikakati kuhakikisha tunawashikisha adabu Simba kwa mara nyingine, naomba mashabiki wenzangu wajitokeze kwa wingi ili tuweke mipango sawa tukiwa na nguvu moja kama ambavyo imekuwa kwenye nyakati zilizopita” alisema.
Akiendelea zaidi Katibu huyo wa umoja wa mashabiki aliweka wazi kuwa bado wanaimani kubwa na kikosi cha timu yao licha ya matokeo mabaya kwenye michezo kadhaa iliyopita na wanauhakika City itakuwa sehemu ya timu nne za juu kwenye msimamo wa ligi ya msimu huu.
“Ni kweli tumeanza vibaya lakini hatuna shaka, imani ya kila mmoja wetu hapa timu yetu itakuwa sehemu ya timu nne za juu mwisho wa msimu, tumekuwa na kawaida ya kuanza vibaya lakini tunamaliza vizuri ingawa mwaka huu kuna utoafauti kidogo kwenye kikosi hasa ukizingatia ugeni wa wachezaji wengi lakini imani kwa timu yetu ni kubwa sana” alimaliza.
IMG_3093


PIGO KWA MANCHESTER CITY KWENYE MECHI Vs UNITED BAADA AGUERO KUPATA MAJERAHA

October 25 Manchester City watakua na mechi muhimu dhidi ya Manchester united. Hadi sasa Manchester city imepata pigo kwa mchezaji wao muhimu Kun Aguero baada ya kupata jeraha akiwa anacheza na timu yake ya taifa.

Aguero alishidwa kuendelea na mechi na kutolewa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Tevez. Kila mtu anajua Aguero ni mchezaji muhimu sana kwa Man city ambapo wiki iliyopita aliweza kufunga magoli 5 peke yake.
Ripoti zaidi kuhusu jeraha la Aguero inasemekana kwamba alitokwa machozi kwa maumivu makali akiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kutolewa alivyotolewa uwanjani. Jeraha hilo inasemekana kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mechi hiyo muhimu. Ikumbukwe pia Aguero alipata jeraha kwenye EPL wiki kadhaa zilizopita
2D3841AD00000578-0-image-a-1_1444398952186

WENGER ASEMA BRENDAN RODGER AMEONEWA..ALISTAHILI MUDA ZAIDI

Wenger alisema ,”Tusisahau kwamba Liverpool haijakua bingwa kwa miaka mingi sana. Wameshinda mataji 18 tu kwenye championship. Walikuja karibu sana kushinda kwenye miaka 2 iliyopita kitu ambacho ni kizuri ukiangalia historia yao.Sasa sijui kwanini wamefanya haya maamuzi kwa sasa, ni vigumu sana kwangu mimi kuelewa.”
“Nimeshangazwa sana na nimejiskia vibaya, nadhani unavyopoteza kazi ya maisha yako ni vigumu wakati mgumu sana na zaidi ya hapo ni ndani ya mechi 8 tu.”

KWA NAMNA HII SOKA LA BONGO HALITA SONGA MBELE ANGALIA KILICHO TOKEA KIKIKOSI CHA TOTO AFRIKAN

Wachezaji wa Toto Africans wamegomea kufanya mzoezi kutokana na madai mbalimbali ya fedha wanayoidai klabuni hapo.


Habari za ndani ya klabu hiyo baada ya kufanyika ufuatiliaji zinaeleza kuwa baadhi ya wachezaji waIisema mgomo huo unatokana na madai ya fedha za usajili, mishahara, posho za safari na za michezo yao ya nje ya mkoa.

Alipoulizwa juu ya hilo, Makamu Mwenyekiti wa Toto, Waziri Gao, alisema: “Kweli wamegoma wakidai maslahi yao mbalimbali lakini uongozi unalifanyia kazi.”

Alisema kiasi ambacho wanachodai wachezaji hao kinafika shilingi milioni 12, alisema kuwa kama fedha hizo hazitapatikana basi huo ndiyo utakuwa mwisho wao kwa kuwa hawana njia nyingine ya kupata fedha.

Rais Kikwete kupewa tuzo ya heshima na Taswa na wanamichezo jumatatu ijayo


Televisheni ya Azam TV, nao wamejitokeza kudhamini sherehe ya kumuaga Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete iliyoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa).

Sherehe hizo zimepangwa kufanyika Jumatatu ijayo kwenye Ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Mweyekiti wa Taswa, Juma Pindo amesema kuwa Azam TV, wamedhamini sehemu ya zawadi za ving’amuzi vya Televisheni hiyo vitakavyotolewa kwa wanamichezo bora 10 waliofanya vizuri katika kipindi chake.
Sherehe hizo zitakazopambwa na burudani mbalimbali wakati wa sherehe hiyo ambayo zaidi ni maalum kumshukuru Kikwete ambaye alionyesha uanamichezo wakati wa kipindi chake cha uongozi.

Tuesday, 6 October 2015

SPUTANZA YA AHIDI KUMSAIDIA JUMA NYOSO WA MBEYA CITY KWA ATHABU ALIYO PEWA

Beki wa Mbeya City, Juma Nyosso amepiga hodi kwenye Chama cha Wachezaji Tanzania (Sputanza) na kuomba kutetewa rasmi.


Nyosso anataka TFF kuangalia upya adhabu yake ya kutocheza kwa miaka miwili pamoja na Sh milioni mbili ikiwa ni baada ya kumshika makalio mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco.

Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kisoki ambaye mwanzo waliitetea adhabu hiyo, amebadilika na kusema sasa watamtetea Nyosso.

"Hii ndiyo kazi yetu, kweli adhabu tuliiunga mkono lakini hatuwezi kukataa kumtetea mchezaji hasa kama tunaona mambo hayajakaa vizuri," alisema Kisoki.

Kisoki amesema wameona kama kuna tatizo katika hizo katika uamuzi wa jambo hilo na sasa wanataka TFF ipitie upya, 

pia ,ameongeza kuwa mpira nikazi yake  nandiyo anayo itegemea katika maisha hivyo inaweza kumuathiri pakubwa

LICHA YA STARS YAKAM KUIVAA MALAWI KESHO MKWASA APEWA MKATABA WA KUDUMU RASIMI

starsprs


Charles Boniface Mkwasa amepewa mkataba wa kudumu kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na kumalizika  Machi 31, 2017.
TFF Imefikia makubaliano hayo na kocha Mkwasa baada ya kurudhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi cha timu ya Taifa, ambapo mpaka sasa ameweza kuingoza Stars katika sare ya michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria.
Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.
 Naye kocha Mkwassa ameeleza kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha kiwango cha Timu ya Taifa kinapanda.
Aidha Kocha Mkwassa ametoa wito kwa wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.
starsmalawiKocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Malawi kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.
Mkwasa amesema kikosi chake kipo kaika hali nzuri baada ya kufanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi ambapo wachezaji wote wapo katika hali nzuri wakiwemo wachezaji wawili Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kutoka klabu ya TP Mazembe ya Congo DR.
“Tunatambua umuhimu wa mchezo wa kesho, wachezaji wana ari na morali ya hali ya juu, kikubwa tunawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutu sapoti katika mchezo huo wa kesho” Alisema Mkwasa.
Kwa upande wa kocha msaidizi wa Malawi (The Flames), Ramadhan Nsanzurwimo amesema wanaiheshimu Tanzania, wanatambua kesho kutakua na mchezo mzuri, na wao kama Malawi wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo.

FAHAUMU KUHUSU SWALA TANZANIA KUANZA UCHIMBAJI MAFUTA KILOMBERO MKOANI MOROGORO



Na Mwandish Wetu
……………………………………………..
Kampuni ya mafuta na gesi ya Swala Tanzania plc inapenda kutaarifu kwamba imechagua eneo kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha mafuta na utafutaji kwa mwaka 2016 ambao utafanyika kwenye eneo tarajiwa la Kito kwenye leseni ya Kilosa- Kilombero.
Akifafanua kuhusu kuanza kwa uchimbaji huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Swala, David Mestres Ridge alisema kuwa tafsiri ya marudio ya 2013 na 2014 ya takwimu za mirindimo zimesababisha kuboreshwa kwa uelewa wa eneo tarajiwa la Kito, huku akiongeza kuwa tathmini za mirindimo zilizopo zimebainisha kuwepo umbo la ziada kwenye ufa unaopakana na bonde hilo la Kito lilopo upande wa magharibi mwa bonde la Kilombero. 
“Tafsiri mpya za takwimu kwenye bonde la Kito zimeonesha kuongezeka kidogo kwa ukubwa muundo wa ramani iliyotengenezwa awali wakati mapitio ya awali ya muundo huo wa ziada yameiwezesha kampuni kukubaliana na hazina iliyopo kwenye bonde la Kilombero.
Ridge alisema, “Mapitio ya kiufundi kwa Bonde la Kilombero yanaonesha matarajio ya Kito yatakuwa makubwa na yametoa vidokezo vya matumaini vya kuwepo rasilimali muhimu ndani ya bonde hilo. Kampuni ya Swala ipo kwenye mchakato wa kumalizia tathmini ya athari za mazingira (EIA) kwenye maeneo yaliyoteuliwa kwa ajili ya uchimbaji na pia kutafuta wakandarasi wa uchimbaji kwa ajili ya kisima cha utafutaji mafuta cha Kito kwa mwaka 2016.