MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Friday, 9 October 2015

WENGER ASEMA BRENDAN RODGER AMEONEWA..ALISTAHILI MUDA ZAIDI

Wenger alisema ,”Tusisahau kwamba Liverpool haijakua bingwa kwa miaka mingi sana. Wameshinda mataji 18 tu kwenye championship. Walikuja karibu sana kushinda kwenye miaka 2 iliyopita kitu ambacho ni kizuri ukiangalia historia yao.Sasa sijui kwanini wamefanya haya maamuzi kwa sasa, ni vigumu sana kwangu mimi kuelewa.”
“Nimeshangazwa sana na nimejiskia vibaya, nadhani unavyopoteza kazi ya maisha yako ni vigumu wakati mgumu sana na zaidi ya hapo ni ndani ya mechi 8 tu.”

KWA NAMNA HII SOKA LA BONGO HALITA SONGA MBELE ANGALIA KILICHO TOKEA KIKIKOSI CHA TOTO AFRIKAN

Wachezaji wa Toto Africans wamegomea kufanya mzoezi kutokana na madai mbalimbali ya fedha wanayoidai klabuni hapo.


Habari za ndani ya klabu hiyo baada ya kufanyika ufuatiliaji zinaeleza kuwa baadhi ya wachezaji waIisema mgomo huo unatokana na madai ya fedha za usajili, mishahara, posho za safari na za michezo yao ya nje ya mkoa.

Alipoulizwa juu ya hilo, Makamu Mwenyekiti wa Toto, Waziri Gao, alisema: “Kweli wamegoma wakidai maslahi yao mbalimbali lakini uongozi unalifanyia kazi.”

Alisema kiasi ambacho wanachodai wachezaji hao kinafika shilingi milioni 12, alisema kuwa kama fedha hizo hazitapatikana basi huo ndiyo utakuwa mwisho wao kwa kuwa hawana njia nyingine ya kupata fedha.

Rais Kikwete kupewa tuzo ya heshima na Taswa na wanamichezo jumatatu ijayo


Televisheni ya Azam TV, nao wamejitokeza kudhamini sherehe ya kumuaga Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete iliyoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa).

Sherehe hizo zimepangwa kufanyika Jumatatu ijayo kwenye Ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Mweyekiti wa Taswa, Juma Pindo amesema kuwa Azam TV, wamedhamini sehemu ya zawadi za ving’amuzi vya Televisheni hiyo vitakavyotolewa kwa wanamichezo bora 10 waliofanya vizuri katika kipindi chake.
Sherehe hizo zitakazopambwa na burudani mbalimbali wakati wa sherehe hiyo ambayo zaidi ni maalum kumshukuru Kikwete ambaye alionyesha uanamichezo wakati wa kipindi chake cha uongozi.

Tuesday, 6 October 2015

SPUTANZA YA AHIDI KUMSAIDIA JUMA NYOSO WA MBEYA CITY KWA ATHABU ALIYO PEWA

Beki wa Mbeya City, Juma Nyosso amepiga hodi kwenye Chama cha Wachezaji Tanzania (Sputanza) na kuomba kutetewa rasmi.


Nyosso anataka TFF kuangalia upya adhabu yake ya kutocheza kwa miaka miwili pamoja na Sh milioni mbili ikiwa ni baada ya kumshika makalio mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco.

Mwenyekiti wa Sputanza, Mussa Kisoki ambaye mwanzo waliitetea adhabu hiyo, amebadilika na kusema sasa watamtetea Nyosso.

"Hii ndiyo kazi yetu, kweli adhabu tuliiunga mkono lakini hatuwezi kukataa kumtetea mchezaji hasa kama tunaona mambo hayajakaa vizuri," alisema Kisoki.

Kisoki amesema wameona kama kuna tatizo katika hizo katika uamuzi wa jambo hilo na sasa wanataka TFF ipitie upya, 

pia ,ameongeza kuwa mpira nikazi yake  nandiyo anayo itegemea katika maisha hivyo inaweza kumuathiri pakubwa

LICHA YA STARS YAKAM KUIVAA MALAWI KESHO MKWASA APEWA MKATABA WA KUDUMU RASIMI

starsprs


Charles Boniface Mkwasa amepewa mkataba wa kudumu kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na kumalizika  Machi 31, 2017.
TFF Imefikia makubaliano hayo na kocha Mkwasa baada ya kurudhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi cha timu ya Taifa, ambapo mpaka sasa ameweza kuingoza Stars katika sare ya michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria.
Kufuatia kusaini mkataba huo, Mkwasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.
 Naye kocha Mkwassa ameeleza kufurahishwa na makubaliano haya na ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha kiwango cha Timu ya Taifa kinapanda.
Aidha Kocha Mkwassa ametoa wito kwa wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.
starsmalawiKocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Malawi kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.
Mkwasa amesema kikosi chake kipo kaika hali nzuri baada ya kufanya mazoezi ya mwisho leo asubuhi ambapo wachezaji wote wapo katika hali nzuri wakiwemo wachezaji wawili Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu kutoka klabu ya TP Mazembe ya Congo DR.
“Tunatambua umuhimu wa mchezo wa kesho, wachezaji wana ari na morali ya hali ya juu, kikubwa tunawaomba watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutu sapoti katika mchezo huo wa kesho” Alisema Mkwasa.
Kwa upande wa kocha msaidizi wa Malawi (The Flames), Ramadhan Nsanzurwimo amesema wanaiheshimu Tanzania, wanatambua kesho kutakua na mchezo mzuri, na wao kama Malawi wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo.

FAHAUMU KUHUSU SWALA TANZANIA KUANZA UCHIMBAJI MAFUTA KILOMBERO MKOANI MOROGORO



Na Mwandish Wetu
……………………………………………..
Kampuni ya mafuta na gesi ya Swala Tanzania plc inapenda kutaarifu kwamba imechagua eneo kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha mafuta na utafutaji kwa mwaka 2016 ambao utafanyika kwenye eneo tarajiwa la Kito kwenye leseni ya Kilosa- Kilombero.
Akifafanua kuhusu kuanza kwa uchimbaji huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Swala, David Mestres Ridge alisema kuwa tafsiri ya marudio ya 2013 na 2014 ya takwimu za mirindimo zimesababisha kuboreshwa kwa uelewa wa eneo tarajiwa la Kito, huku akiongeza kuwa tathmini za mirindimo zilizopo zimebainisha kuwepo umbo la ziada kwenye ufa unaopakana na bonde hilo la Kito lilopo upande wa magharibi mwa bonde la Kilombero. 
“Tafsiri mpya za takwimu kwenye bonde la Kito zimeonesha kuongezeka kidogo kwa ukubwa muundo wa ramani iliyotengenezwa awali wakati mapitio ya awali ya muundo huo wa ziada yameiwezesha kampuni kukubaliana na hazina iliyopo kwenye bonde la Kilombero.
Ridge alisema, “Mapitio ya kiufundi kwa Bonde la Kilombero yanaonesha matarajio ya Kito yatakuwa makubwa na yametoa vidokezo vya matumaini vya kuwepo rasilimali muhimu ndani ya bonde hilo. Kampuni ya Swala ipo kwenye mchakato wa kumalizia tathmini ya athari za mazingira (EIA) kwenye maeneo yaliyoteuliwa kwa ajili ya uchimbaji na pia kutafuta wakandarasi wa uchimbaji kwa ajili ya kisima cha utafutaji mafuta cha Kito kwa mwaka 2016.

DKT. HOSEAH AZINDUA JENGO LA OFISI YA TAKUKURU JIJINI MBEYA

  


Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya ambapo amesema kuwa Taasisi  hiyo imeweza kufanikiwa  kupambana na rushwa kwa kiasi kikubwa  ambapo jumla  kesi kubwa za rushwa 1,993 kuanzia mwaka 2004-2015 zimeweza kufunguliwa ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 81 ikilinganishwa na kesi 384 zilizokuwepo miaka 10 ilioyopita (1995-2004)  .
 Amesema ,ongezeko hilo la kesi kubwa limetokana na jitihada za Taasisi hiyo katika kupambana na kuzuia rushwa nchini hasa katika kipindi cha serikali ya awamu ya nne, chini ya rais Jakaya Kikwete.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akitoa salama za mkoa wa mbeya katika hafla ya uzinduzi wa jengo la Takukuru Mkoa wa Mbeya .

Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mbeya xavery Mhyella akatoa taarifa ya Takukuru Mkoa wa Mbeya mbele ya Mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo imehudhuriwa na  Mkurugenzi wa Mkuu  Takukuru  nchini Dkt, Edward Hosea Octobar 5 mwaka huu..

Mkaguzi Mkuu wa Kanda Takukuru Ndugu Joice Shundi akizungumza katika hafla hiyo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Wende wakitoa burudani za ngoma za asili katika uzinduzi huo wa jengo la ofisi mpya ya Takukuru Mkoa wa Mbeya .



Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa dini waliohudhuria hafla hiyo ya uzinduzi wa jengo zilizopo eneo la forest ya zamani karibu na Mahakama kuu jijini Mbeya.






Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akizindua rasmi jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya Octoba 5 mwaka huu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali na taasisi binafsi mkoani humo amabapo jengo hilo limetumia kiasi cha shilingi bilioni 1.2 hadi kukamilika kwakwe.

Muonekano wa jengo la ofisi Mpya za TAKUKURU Mkoa wa Mbeya zilizopo foresti ya zamani karibu na Mahakama kuu jijini hapa.

Viongozi wa kimila waliohudhuria sherehe hizo.


Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah  akipanda mti katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akishiriki zoezi la upandaji mti
 katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya.




Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akisimikwa kuwa chifu wa kabila la wasafwa katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya.



Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah pili kushoto  na mkuu wa mkoa wa Mbeya Abas Kandoro kushoto katika picha ya pamoja na viongozi Dini katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya.




Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akipokea zawadi kutoka kwa wafanyakazi wa TAKUKURU (Cofee Table) katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya
Afisa Elimu  kwa Umma TAKUKURU Mkoa wa Mbeya Ndugu Sala Chodota akitoa ufafanuzi kwa vilabu vya wanafunzi walio hudhuria sherehe hizo za uzinduzi wa jengo jipya za ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya .
Picha na Emanuel Madafa ,Jamiimojablog Mbeya