MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Tuesday, 24 March 2015

DANIEL STURRIDGE NA WATOLEWA NJE KATKA TIMU ZAO ZA TAIFA




 

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya England Daniel Sturridge ametolewa katika kikosi cha timu ya taifa baada ya kufanyiwa uchunguzi hapo jana na kugundulika anamaumivu makali juu ya paja.
Mchezaji huyo aliwasili jana katika uwanja wa St.George Park ambapo kikosi hicho cha Roy Hodson kinafanyia mazoezi ili kuonana na madaktari wa timu hiyo ambao baada ya kumfanyia uchunguzi waliona majeraha hayo ambayo aliyapata katika mechi ya juzi waliyofungwa na Manchester United.
Sturridge,25, amekuwa mchezaji wa pili wa Liverpool kutolewa katika kikosi hicho baada ya hapo awali Adam Lallama kutolewa kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya nyama za paja na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo wa Tottenham Hotspurs Ryan Mason ambaye hajawahi kuichezea England hata mechi moja.
Hivyo wachezaji hao watakosa mechi ya kuwania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za mataifa Ulaya 2016 dhidi Lithuania itakayopigwa ijumaa hii kwenye uwanja wa Wembley na ile ya kirafiki dhidi ya Italia kule Turin jumanne ijayo.
Aidha hili ni pigo kwa kocha wa Liverpool Brendan Rodgers ambaye alimkosa Daniel Sturridge kwa muda mrefu mwanzoni mwa msimu huu kutokana na kukaa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha aliyoyapata wakati akiwa na timu ya taifa.
 1090402_heroa

                  Diego Costa wa Hispania

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Hispania Diego Costa ametolewa katika kikosi cha timu ya taifa baada ya madaktari wa timu hiyo kumfanyia uchunguzi na kugundua kuwa anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja.
Imeripotiwa kuwa mshambuliaji huyo aliumia katika mechi ya juzi jumapili ambayo Chelsea iliibuka na ushindi wa 3- 2 dhidi ya Hull City iliyopigwa katika uwanja wa KC.
Taarifa kutoka chama cha soka cha Hispania SFA inasema ” Tumepokea taarifa kutoka kwa daktari wa timu kuwa Costa anamaumivu ya nyama za paja hivyo hataweza kucheza na hivyo atarudishwa katika klabu yake kwa matibabu zaidi “
Hivyo Mchezaji huyo wa zamani wa Atletico Madrid atakosa mechi ya timu ya taifa ya Hispania dhidi ya Ukraine ijumaa hii ambayo ni yakutafuta tiketi ya kucheza fainali za mataifa Ulaya 2016 na ile ya kirafiki dhidi ya uholanzi.


ROBBEN ATAKOSEKANA UWANJANI KWA KUTOCHEZA ZAIDI YA MECH 8

 

26E5AF7E00000578-3006685-image-a-13_1427051152372
Kiungo wa klabu ya Bayern Munich Arjen Robben atakosekana uwanjani kwa muda wa wiki kadhaa baada ya kuumia   katika mechi iliyoisha kwa mabingwa hao wa bundesliga kupokea kichapo cha  2-0 kutoka kwa Borrusia Monchenglabach licha ya kucheza katika uwanjani nyumbani Allianz Arena, inasemekana kiungo huyo atakosa zaidi ya mechi 8

Mholanzi huyo alipata maumivu hayo katika dakika ya 24 ya mchezo baada ya kuchezewa vibaya na beki Tony Jantske na hivyo kutolewa nje akiwa amebebwa kwenye machela.
Hii ni habari mbaya kwa Arjen Robben ambaye amerudi mazoezini hivi karibuni baada ya kuumia katika mechi ya klabu bingwa dhidi ya Shaktar Donetsk Machi 12.

Kocha wa klabu hiyo mhispania Pep Guardiola anakibarua kizito kuziba pengo la winga huyo machachari ambaye anauwezekano mkubwa wa kukosa mechi za robo fainali za klabu bingwa Ulaya dhidi ya FC Porto mwezi ujao.
Aidha Robben,31, atakosa mechi ya timu ya taifa ya uholanzi dhidi ya Uturuki ambayo ni mechi ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya mataifa Ulaya mwaka 2016 na ile ya kirafiki dhidi ya Hispania.

Mabingwa wa netiboli wapatikana visiwani zanzibar





Michuano ya netball ya Afrika ya Mashariki imemalizika Zanzibar huku timu ya MOICT ya Kenya ikitwaa ubingwa kwa upande wa wanawake baada ya kuifunga timu ya NIC ya Uganda kwa mabao 32-29.
NIC ndio walikuwa mabingwa watetezi baada ya kulinyakua kombe hilo mwaka jana katika michuano iliyofanyika Dar es Salaam. Hii ni mara ya pili kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuandaa michuano hiyo mara mbili mfululizo, zamu hii ikiwa ni upande wa Tanzania Zanzibar (visiwani) katika viwanja vya Gymkhana.
Netball, au mpira wa pete ni mchezo ambao kwa miaka mingi umekuwa ukihusisha timu za wanawake pekee, lakini katika kuleta usawa (gender balance) kama ilivyo kwa michezo mingine kama vile mpira wa kikapu (basketball), wavu na mingineyo, mchezo huo katika miaka ya hivi karibuni, umekuwa ukishirikisha timu za wanaume katika kuleta hamasa na ushindani.
Kwa upande wa wanaume, wenyeji Polisi ya Zanzibar waliibuka washindi wa michuano hiyo ya Afrika Mashariki, baada ya kuwafunga wenzao wa JKU (pia ya Zanzibar) kwa mabao 38-34 katika mechi ya vuta nikuvute.
Michuano hiyo hufanyika kila mwaka kwa nchi wanachama kupeana zamu za kuandaa mashindano hayo. Nchi zilizoshiriki ni wenyeji Zanzibar, Kenya, Uganda na Tanzania Bara. Rwanda na Burundi ni sehemu ya jumuiya hiyo ya Afrika ya Mashariki lakini hawana historia kubwa ya kuwa sehemu ya kuwa nchi shiriki.

SKRTEL AFUNGULWA MASHTKA NA FA KWA KUMTIMBA DE GEA!




BAADA ya machungu ya kutandikwa 2-1 kwao Anfield na Mahasimu wao Man United Jumapili na pia Kepteni wao Steven Gerrard kupewa Kadi Nyekundu katika Mechi hiyo hiyo na sasa kufungiwa Mechi 3, balaa kwa Liverpool bado halijaisha kwani sasa FA imemfungulia Mashitaka Sentahafu wao Martin Skrtel kwa kumkanyaga Kipa wa Man United David De Gea katika Mechi hiyo hiyo.
Kwa vile tukio hilo la Skrtel, ambalo lilitokea Dakika za Maheruhi halikuonwa na Refa Martin Atkinson, Kanuni za FA, Chama cha Soka England, zinataka Jopo Huru la Marefa Watatu wa zamani walipitie na ikiwa wote Watatu wataafiki linastahili Kadi Nyekundu basi Mchezaji husika hufunguliwa Mashitaka.
Hayo ndio yaliyomkuta Skrtel, Mchezaji wa Kimataifa wa Slovakia mwenye Miaka 30, ambae amepewa hadi Leo Saa 3 Usiku kujibu Shitaka lake.
Ikiwa atapatikana na hatia, Sentahafu huyo atafungiwa Mechi 3 na atazikosa Mechi 2 za Ligi Kuu England za Aprili 4 huko Emirates na Arsenal na ile ya Anfield na Newcastle hapo Aprili 14 na Marudiano ya FA CUP ya Robo Fainali huko Ewood Park na Blackburn Rovers hapo Aprili 8.
Hizo pia ndizo Mechi ambazo Kepteni Steven Gerrard atazikosa baada ya Kadi Nyekundu kwenye Mechi hiyo hiyo aliyolambwa Sekunde 38 tu tangu aingie Uwanjani kutoka Benchi kwa kumkanyaga kwa kusudi Ander Herrera wa Man United.

Wanasoka wa nje kupunguzwa nchini England

Baadhi ya wachezaji wa kiafrika watakaathirika na sheria hiyo.
Shirikisho la kanda kanda nchini England FA sasa linakusudia kuandaa sheria itakayo kupunguza idadi ya wachezaji kutoka nje ya nchi za Umoja wa Ulaya watakaosajiliwa katika ligi za nchi hiyo.
Mwenyekiti wa shirikisho hilo Greg Dyke asema kwamba ligi kuu ya England ipo kwenye hatari ya kutowasaidia wachezaji raia wa Uingereza kama hatua hazitachukuliwa.
Katika mpango pia itaweka sheria ngumu kwa wachazaji wenye vipaji waliokulia nchini humo.
Mikakati hiyo yote ni ya kuimarisha timu ya taifa ya England ambayo imekuwa haifanyi vizuri kwenye mechi za kimataifa.

:Makavazi ya Tunisia yafunguliwa leo 24 Machi 2015

Hapo jana waziri mkuu wa taifa hilo aliwalaumu maafisa wakuu wa idara za usalama kwa kuzembea kazini
Makavazi ya Bardo nchini Tunisia, yanafunguliwa tena leo Jumanne, juma moja pekee baada ya magaidi kushambulia watalii wa kigeni na kuwauwa 20 kati yao.
Kutakuwa na mkutano wa hadhara kabla ya kufunguliwa tena kwa makavazi hayo ya kitaifa.
Wasanii watawatumbuiza wageni nje ya ukumbi huo unaopendwa na watalii wengi kutoka magharibi kabla ya maafisa kutoa taarifa inayolenga kuthibitisha kuwa magaidi hawataamua maisha ya wenyeji yasalie kuwa ya hofu.
Tangu tukio hilo kumekuwa na hofu kuwa magaidi hao huenda wameangamiza sekta nzima ya utalii ambayo ni kitega uchumi kikubwa cha Tunisia.
Hapo jana waziri mkuu wa taifa hilo aliwalaumu maafisa wakuu wa idara za usalama kwa kuzembea kazini .
Sita kati yao walitupwa nje.Maafisa wa usalama wakishika doria nje ya makavazi hayo ya kitaifa


Waziri huyo mkuu , Habib Essid alisema mikakati imewekwa ilikuimarisha uwezo wa maafisa wa usalama kushirikiana na vitengo vya kijasusi kuzuia mashambulizi zaidi siku za usoni.
Jumba hilo linashehena kubwa zaidi ya sanamu za enzi za warumi.
Wavamizi wawili kati ya watatu waliotekeleza shambulizi hilo walipigwa risasi na kuuawa huku yule aliyesalia akisakwa na maafisa wa kitengo maalum cha kupambana na ugaidi.
Tukio hilo ndilo kubwa zaidi kuwahi kutokea baada ya mapinduzi ya kiongozi wa muda mrefu wa Tunisia Zine al-Abidine Ben Ali mwaka wa 2011.

BREAKING NEWS Ndege ya Ujerumani yaanguka nchini Ufaransa ikiwa na abiria 142 na wahudumu 6


Ndege ya shirika la ndege la Germanwings
Ndege ya abiria inayomilikiwa na shirika la ndege la Germanwing Airbus A320 Imeanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa.
Ndege hiyo ilikuwa imewabeba abiria 142 na wahudumu 6 ikitoka Barcelona Uhispania kuelekea Duesseldorf.
Ndege hiyo inayomilikiwa na shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa chini ya nembo Germanwings imeripotiwa kuanguka karibu na mji wa Digne.
Ndege hiyo ya A320 ilianguka saa tano asubuhi katika Kusini mwa Milima ya Alps.
Viongozi wa Ujerumani na Ufaransa wanaendelea kushauriana kuhusiana na mkasa huo unaowakabilia macho.
Ndege hiyo ya Ujerumani ilianguka katika eneo lisilo na mijengo ambalo halifikiki kwa urahisi nchini Ufaransa Kusini mwa Milima ya Alps.
Ndege kama iliyoanguka
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametaja ajali hiyo kama mkasa na amesema kuwa uwezekano wa kuwapata watu wakiwa hai ni mgumu.
Hali ya hewa katika eneo hilo ilitajwa kuwa nzuri na kituo maalumu cha kukabiliana na mikasa kimetengwa kukabiliana na mkasa huo.
Waziri wa Maswala ya ndani ya nchi uko njiani kuelekea mahali pa ajali hiyo.
Vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kuwa ndege hiyo ilituma ujumbe wa kuwa hatarini kabla ya mawasiliano yake kutoweka .

Monday, 23 March 2015

Hivindivyo Misri, Ethiopia na Sudan zivyopatana

Viongozi wa Ethiopia Misri na Sudan baada ya kutia sahihi mkataba huo
Misri, Ethiopia na Sudan zimetia saini mkataba wa kwanza kuhusu ugavi wa maji katika ya Nile unaopitia mataifa hayo yote matatu.
Mkataba huo unafuatia ujenzi unaoendelea wa bwawa kubwa la ''the Grand Rennissance'' linalojengwa na Ethiopia katika mto Nile.
Ujenzi huo umezua mzozo mkali wa kidiplomasia kati ya Misri na Ethiopia.
Mwandishi wa BBC nchini Ethiopia Emmanuel Igunza na maelezo zaidi.
Viongozi wa mataifa hayo matatu,walikutana jijini Khartoum Sudan kwa sherehe ya kutia saini mkataba huo ambao umetajwa kama hatua ya kwanza katika kutatua mzozo huo.
Bwawa hilo linalotarajiwa kugharimu takriban dola bilioni nne, litakamilishwa mwaka wa 2017 na kuwa moja ya mabwawa kubwa zaidi barani Afrika.
Ethiopia inasema itaisaidia katika kuzalisha nguvu za umeme kwa ajili ya viwanda vyake na pia inatarajia kuuza kawi kwa mataifa jirani.
Lakini akizungumza hii leo, Rais wa Misri Abdel Fattah Al Sisi amesema mkataba huo unashiria nia ya mataifa yote kuleta maelewano kuhusu utumizi wa maji ya mto Nile.
Abdel Fattah Al Sisi alisema “Mradi huu wa bwawa la renaissance linashiria chanzo cha maendeleo kwa mamilioni ya raia wa Ethiopia kwa kuzalisha kawi safi,
lakini kwa ndugu zao wanaoishi katika kingo za mto huohuo wa Nile nchini Misri, na mabo idadi yao ni sawa, inashiria chanzo cha wasiwasi.
Hii ni kwa sababu Nile ndio chanzo chao ha peke cha maji, na hasaa chanzo cha maisha.”
 
 Ethiopia inasema itaisaidia katika kuzalisha nguvu za umeme kwa ajili ya viwanda vyake
Mara kwa mara Misri imepinga mradi huo ikisema huenda bwawa la Rennaissance likapunguza viwango vya maji kwa raia wake.
Hata hivyo Rais wa Sudan Omar al Bashir ametaka mataifa yote matatu kuhakikiha yanazingatia maendeleo lakini pia kutilia maanani maslahi ya nchi zote.
“Tunamini kuwa ushirikiano ndio njia ya pekee ya kuafikia maelewano na utangamano kati ya watu wetu, na kwamba bila ushirikiano, tutapoteza nafasi ya kuwa na masiha bora.
Kwa hivyo tunahitaji kufanya kazi pamoja kujenga mazingira ya ushirikiano na kukariri kwa maslahi ya kitaifa hayageuki na kuwa vikwazo kwa maslahi za kikanda na ujirani mwema.” Alisema rais Bashir
Ethiopia ilianza kubadilisha mkondo wa mto Nile mwezi Mei mwaka wa 2013, ili kujenga bwawa hilo linalotarajiwa kuzalisha megawati 6,000 za umeme litakapokamilika.
Misri kwa upande wake inaamini kuwa ina haki za kihistoria za mto huo kufuatia mikataba ya mwaka 1929 na 1959, inayoipa asilimia 87 ya maji ya mto huo, na pia uwezo wa kupinga miradi yoyote inayojengwa katika mto Nile.

AZAM WASEMA MCHI IJAYO LAZIMA MTU AFE BAADA YA KUCHUA POINT TATU JANA

LIGI KUU VODACOM
RATIBA/MATOKEO
Jumapili Machi 22
Coastal Union 0 Azam FC 1
Ruvu Shooting 0 Simba 3
Tanzania Prisons 0 v Polisi Moro 0
**********************************
Bao la Dakika ya 31 la John Bocco jana huko Mkwakwani Tanga limewapa Azam FC ushindi wa Bao 1-0 na Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Simba imezinduka toka kipigo cha 2-0 toka Mgambo JKT na kuichapa Ruvu Shooting Bao 3-0 zote zikiwa ni Mechi za Ligi Kuu Vodacom.
Bao za Simba  jana    zote zilifungwa Kipindi cha Pili na Ibrahim Hajibu, kwa Penati, Awadh Juma na Elias Maguri.
Yanga bado wako kileleni mwa Ligi wakiwa na Pointi 37 kwa Mechi 18 wakifuata Azam FC wenye Pointi 36 kwa Mechi 18 na kisha Simba waliocheza Mechi 20 na wanwana Pointi 32.
Taarifa kutoka kwa uongozi ya azam umesma mechi ijayo lazima washinde iliweze kujiweka pazuri katka kutetea  kombe la vodacoma msimu huu  .

GERRARD AFEDHEHEKA KADI NYEKUNDU YA SEKUNDE CHACHE TANGU AINGIA UWANJANI!





KEPTENI wa Liverpool Steven Gerrard ameomba radhi kwa kutandikwa Kadi Nyekundu Sekunde 38 tu baada ya kuingia Uwanjani kwenye Mechi iliyochezwa Anfield na Timu yake kutandikwa 2-1 na Manchester United hapo Jumapili.
Gerrard, mwenye Miaka 34 na ambae anahamia huko Marekani kuchezea LA Galaxy mwishoni mwa Msimu, alitolewa nje na Refa Martin Atkinson kwa kumkanyaga kusudi Ander Herrera wa Man United na sasa atakosa Mechi 3 za Liverpool.
Akiongea mara baada ya Mechi hiyo, Gerrard alisema: “Inabidi nikubali, uamuzi ulikuwa sahihi. Nimewaangusha Wachezaji wenzangu na Mashabiki. Nawajibika kwa yote. Hata sijui nini kilitokea labda kukumbwa na Herrera. Sisemi zaidi. Ila nimekuja hapa kuomba radhi.”
Wakati akipewa Kadi Nyekundu, Liverpool ilikuwa nyuma kwa Bao 1-0 na hii pengine ni Mechi yake ya mwisho dhidi ya Mahasimu Man United akiwa amevaa Jezi ya Liverpool Klabu ambayo alianza kuichezea tangu 1998 na kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2005 pamoja na Vikombe vingine 9.
Mechi ambazo atazikosa Gerrard akiwa kwenye Kifungo chake cha Mechi 3 ni ile ya huko Ewood Park dhidi ya Blackburn Rovers ya Marudiano ya Robo Fainali ya FA CUP, Mechi ya Ligi Kuu England huko Emirates na Arsenal na ile ya Anfield na Newcastle hizi zikiwa Mechi kati ya 8 walizobakisha za Ligi.

TEVEZ AIPAISHA JUVE POINTI 17 MBELE KILELENI SERIE A!


















 

Carlos Tevez Leo amefunga Bao 1 na la ushindi na kuipaisha Juventusbkuwa Pointi 17 juu kileleni mwa Serie A walipoifunga Genoa 1-0 ndani ya Juventus Arena Jijini Turin huko Italy.
Hilo ni Goli la Tevez la 24 Msimu huu na Juzi alipiga Bao 2 walipoichapa Borussia Dortmund huko Signal Iduna Park Bao 3-0 na kutinga Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Kwenye Mechi hii na Genoa Tevez, mwenye Miaka 31, alikosa Penati Kipindi cha Pili lakini Juve, wakicheza bila Kiungo wao mahiri Paul Pogba ambae ni majeruhi na atakuwa nje kwa Miezi Miwili, walilinda vyema Bao lao moja.
Sasa Juve wapo nijani kutwaa Taji lao la 20 la Ubingwa wa Italy na hili litakuwa ni la 4 mfululizo.

KALENDA YA FIFA MECHI ZA KIMATAIFA, PATA RATIBA ZILE ZA KIRAFIKI!

 raisi wa fifa Joseph "Sepp" Blatter

 

Hii ni Wiki ya Kalenda ya FIFA ya Mechi za Kimataifa ambazo pia zitachanganyika na za Mashindano rasmi kule ambayo zipo Mechibza Makundi za EURO 2016.
PATA RATIBA BAADHI YA MECHI ZA KIRAFIKI:
**Saa za Bongo
Jumatano Machi 25
Denmark v USA 22:15
Germany v Australia 22:30
Scotland v Northern Ireland 22:45
Alhamisi Machi 26
Bahrain v Colombia 20:00
Iran v Chile 22:00
France v Brazil 23:00
Ijumaa Machi 27
Canada v Guatemala 23:30
Jumamosi Machi 28
Morocco v Uruguay 22:00
El Salvador v Argentina 23:30
Jumapili Machi 29
Mexico v Ecuador 03:30
Brazil v Chile 17:00
France v Denmark 21:45
Jumatatu Machi 30
Colombia v Kuwait 19:00
Qatar v Slovenia 19:00
Macedonia v Australia 22:00
Jumanne Machi 31
Canada v Puerto Rico 02:30
Russia v Kazakhstan 19:00
Switzerland v USA 19:00
Sweden v Iran 20:30
Ukraine v Latvia 21:00
Austria v Bos-Herce 21:15
Luxembourg v Turkey 21:15
Slovakia v Czech Rep. 21:30
Italy v England 21:45
Netherlands v Spain 21:45
Portugal v Cape Verde Islands 22:45
Jumatano Aprili 1
Ecuador v Argentina 03:00
Mexico v Paraguay 03:00