MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Wednesday, 2 July 2014

KOCHA MBEYA CITY FC AHITAJI CHANGAMOTO MPYA BAADA YA KUPATA `NONDOZ` YA CAF



 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhlOC7m3kmSBnmfpQqwG94xB5pbfv-sBx0mIBSw06yo3geW7VAkr1HUdbo4u0bk-5sBXGg3PjeWTB4fXkoch-fYifB3LIL6-1JHcZpapeXqJNG8JfaiX4Wq0WblL4CrWyRtNKaHcHDhOA/s1600/mb.jpg
Juma Mwambusi (wa kwanza kushoto) akiwa na Maka Mwalwisyi (wa pili kushoto) kwenye moja ya mechi ya Mbeya City fc katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.



ALIYEKUWA kocha msaidizi wa Mbeya City fc, Maka Mwalwisyi amedhamiria kupata changamoto mpya katika kazi yake ya ukocha baada ya kuamua kuachana na klabu hiyo kutokana na  mkataba wake kumalizika.

Akizungumza na MTANDAO HUU, Maka amesisitiza kuwa mara baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumalizika tangu mei 30, aliamua kuhudhuria kozi ya CAF ya leseni B, hivyo anaona kuna haja ya kuachana na kazi ya kuwa kocha msaidizi wa Juma Mwambusi.

“Baada ya mkataba wangu kumalizika kulikuwa na kozi ya leseni B ya CAF ambayo ilikuwa inaendelea jijini Dar es salaam, nimehudhuria ile kozi, mwisho wa siku nilipomaliza nikatafakari na kuona kwamba kidogo nahitaji changamoto baada ya kuwa na daraja B”. Alisema Maka.

“Na nahitaji kuwa na timu yangu ambayo itanipa changamoto kama mwalimu wa daraja B, kocha Mwambusi ana falsafa yake na mimi nina falsafa yangu, kwa hiyo nahitaji falsafa yangu ionekane na sio kuwa chini ya kocha Mwambusi”. Aliongeza Maka.

Maka aliyesaidiana na Mwambusi kuifikisha Mbeya City katika nafasi ya tatu msimu uliopita alifafanua kuwa  hana tatizo na kiongozi yeyote wala mtu yeyote yule bali ameamua mwenyewe kuondoka katika klabu hiyo kwani anataka kuonyesha falsafa yake.

kwa sasa mwalimu huyo mwenye daraja B hajapata klabu yoyote ya kuinoa hapa nchini na amesema imekuwa ngumu kupata timu kwani watu walikuwa wanajua bado yupo Mbeya city.

Maka ni muumini mkubwa wa soka la vijana na hata vijana wengi wanaocheza kikosi cha pili cha Mbeya City walitokea katika akademi yake ya FOYSA.
Mbali na kutoa wachezaji hao, pia alitoa wachezaji mbalimbali wanaocheza timu tofauti tofauti za ligi kuu soka Tanzania bara.
 
Na Frank Momanyi, Dar es salaam

Imechapishwa Julai 2, 2014, saa 3:45 alasiri
 

LUIS SUAREZ SAFARI YAIVA KUJIUNGA FC BARCELONA MSIMU UJAO

article-2677164-1F43D0D600000578-630_634x347Anaondoka? Liverpool na Barcelona wanatarajia kuanza mazungumzo juu ya kuuziana Luis Suarez.
KLABU za Liverpool na Barcelona zinatarajia kuanza kufanya mazungumzo juu ya bei ya awali ya paundi milioni 80 ili kuuziana mshambuliaji mweye matatizo kwa sasa, Muurguay, Luis Suarez.
Mtandao wa michezo wa Sportsmail unafahamu kuwa maofisa wa Liverpool, akiwemo mkurugenzi mtendaji, Ian Ayre, wamekubali kukutana na mkurugenzi wa michezo wa FC Barcelona, Raul Sanllehi,  mjini London ili kujadiliana thamani ya mchezaji huyo mwenye miaka 27.
Barcelona wanatazamiwa kutoa paundi milioni 60 kwa kuzingatia kuwa Suarez amefungiwa miezi minne kucheza soka baada ya kumng`ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini.
Liverpool hawapo tayari kushusha bei ya Suarez, lakini wanataka kumhusisha mshambuliaji wa Barcelona Alexis Sanchez kama sehemu ya makubaliano hayo.
 

MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA USONI NA MTOTO WAKE

DSC00268TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 02.07.2014.
• MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA USONI NA MTOTO WAKE.
• WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA POMBE HARMU YA MOSHI [GONGO]
• JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI MALAWI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA.
 KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA MARTHA KYANDO (73) MKAZI WA KIJIJI CHA IBUNGILA AMEUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA USONI KISHA KUNYONGWA SHINGO NA MTOTO WAKE AITWAE KISWIGO ANGANISYE (33) MKAZI WA KIJIJI CHA IBUNGILA WILAYANI RUNGWE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.07.2014 MAJIRA YA SAA 00:30 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA MPUNGUTI, KIJIJI CHA IBUNGILA, KATA YA MALINDO, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. AIDHA INADAIWA KUWA KABLA YA KUUAWA MAREHEMU PIA ALIBAKWA.
INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO NI BAADA YA MTUHUMIWA AMBAYE INASEMEKANA ANA MATATIZO YA AKILI KUCHUKIA BAADA YA MAREHEMU KUMPIKIA MAGIMBI BADALA YA UGALI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO KWA KOSA LA KUPATIKANA NA POMBE HARMU YA MOSHI. WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA NA 1. EMANUEL SAKALA (21) MKAZI WA MWANJELWA, 2. SHABAN ZUBERI (23) MKAZI WA MWANJELWA 3. JAMES ANDREW (24) MKAZI WA MAKUNGULU 4. MIKIDADI MWALUGOYA (25) MKAZI WA MWANJELWA 5. SADIKI HUSSEIN (24) MKAZI WA JUAKALI.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA WAKIWA NA GONGO UJAZO WA LITA 5 KATIKA MSAKO ULIOFANYWA KATIKA ENEO LA BENKI – MWANJELWA, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJINI MBEYA MNAMO TAREHE 01.07.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI MALAWI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. WAHAMIAJI HAO HARAMU NI PAMOJA NA 1. THOMAS JUMA (29) NA 2. BONIFACE CHITETE (29).
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 01.07.2014 MAJIRA YA SAA 23:15 USIKU KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA KATIKA ENEO LA KYELA- KATI, KATA YA KYELA-KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MUFTI ATEGUA KITENDAWILI CHA UONGOZI ARUSHA NA KUWEKA WAZI KILA KITU

MUFTI
Na  Mahmoud Ahmad, Arusha
MUFTI  Shekh  Mkuu wa Tanzania, Issa Bin Shaaban Simba, jana ameondoa sitofahamu ya muda mrefu kuhusu uongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa, uliopo Bondeni Manispaa ya Arusha na Masjid Quba, kwa kuwataja viongozi wanaostahili kuwepo madarakani.
Kabla ya kuwataja viongozi hao, alisema kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na uongozi wa bakwata katika ngazi za juu za Mkoa, ambao umesababishwa na ukaidi wa makusudi wa baadhi ya watu kukiuka utaratibu wa katiba ya BAKWATA  juu ya upatikanaji uongozi katika ngazi hizo.
Alisema hali hiyo imesababisha kuw ana makundi mawili ya uongozi katika ngazi ya Mkoa, Wilaya ya Arusha, Msikiti Mkuu wa Ijumaa Arusha Mjini na Masjid Quba, jambo linalokwamisha maendeleo ya Uislamu Mkoani Arusha.
Mufti Shekh Simba alisema kutokana na hali hiyo amelazimika kufanya ziara Mkoani Arusha na kukutana na viongozi wa serikali,viongozi wa BAKWATA wa makundi yote yanayokinzana.
Alifafanua upatikanaji wa viongozi  katika ngazi  Msikiti chini ya uongozi wa Mtaa, Wilaya, Mkoa na taifa kuwa ni lazima kufuata katiba ya Bakwata ya mwaka 199 toleo la mwaka 2008, Ibara ya 10 ya katiba inayozungumzia muundo wa Bakwata ili kutekeleza mipango na shughuli
zake.
Aidha alisema katika sheria hiyo inasema kuna aina mbili za uongozi katika ngazi zote, ambazo ni wale wa kuchaguliwa na kuteuliwa.
Alisema kutokana na utaratibu huo sheria hiyo ilikiukwa na viongozi waliopo madarakani ambao Nipashe, ilipata majina yao ambayo ni  Ahmed Issa Mtea,Abas Ramadhani,Yusuph Mohamed,Abdul Azizi Shaban, Masud Hussein,Shaban Juma,Hussein Ijunje,Abdallah Hanafi, Mbaraka Mtonyi, Hassan Waziri na Amini Mussa na hawastahili kuwa viongozi tena.
Hata hivyo Mufti Shekh Simba, aliwataja wanaostahili kuwepo madarakani katika Ofisi ya Mkoa ni Sheikh wa Mkoa, Shaban Juma Abdallah, Kaimu Katibu wa Mkoa, Ustadhi Abdallah Masoud na Mwenyekiti wa halmashauri Ustadhi Mohamed Juma Marawi.
Katika baraza la Masheikh Mkoa ni Sheikh Mwinshehe Mwinyimgeni,Sheikh Nassib Idd Nassib, Sheikh Hussein Said Ijunje,Sheikh Abdallah Hanafi Simba na Sheikh Abdulrahman Salum.
Aliwataja wajumbe wanostahili kuwepo kwenye Halmashauri ya Mkoa ni Hassan Waziri Salum, Said Rashid Golugwa,Athuman Amir Yunus,Seif Juma Banka,Athuman Juma Luwuchu. Mohamed Kidange Laizer, Salim Rajab
Majaaliwa na Rashid Kilavo Msuya.
Ofisi ya Wilaya ni Sheikh abdulrahaman Salum,Ustadhi Mbaraka Musa Mtonyi na ustadhi Mohamed Juma Marawi.
Katika Baraza la Masheikh Wilaya ni Sheikh Shaaban Maarouf,Omar Omar Mgaza, Ayoub Hussein Juma na Hassan Abdallah Mlali.
Aliwataja wajumbe wa halmashauri ya Wilaya ambao wote ni Ustadhi, Ramadhan Abdulrahaman, Mbega Hussin Mbega, Abdallah Yahya Mgongo, Ahamed Mgwasa Twarbushi,Khamis  Abdllah Mwalimu,Kiruwa Selemani Kiruwa,Mashaka Abdallahh Said, Wally Juma Laizer, Ibrahim Said Munga na Abdi Nassoro.
Wajumbe wa Mamlaka ya Msikiti Mkuu wa ijumaa Arusha Mjini aliwataja kuwa ni Sheikh Shaaban Juma ambaye ni Imamu na mwenyekiti wa mamlaka,ust. Juma Khamis ni Katibu,Ali Mkuruzi ni Muhazini,Faraji Swai ni Mjumbe, Hassan Magire,Idd Mussa,Said Diria, Ally Idd. Muhamed Ngeseyan, Sheha Mussa, Ahmed Omar, Sheikh Rajab Hassan Kiungiza na
Jawahir Shaha, Maulid Rashid, Rashid Kawapani na Hassan Salum Kikao.
Wengine ni Wazee watano wasuluhishi wa migogoro Msikitini ni Muhammad Abdulrahaman, Ibrahim Said Munga,Kassim Mamboleo,Jaafar Wally na Hussein Bakar.
Viongozi wa Msikiti wa Masjid Quba  uliopo mtaa wa Levolosi, aliwataja viongozi wao ni Sheikh Hassan Waziri ambaye ni Imamu na mwenyekiti wa Msikiti, katibu wa msikiti Abubakar Sharif, Mweka hazina Chohan Jumbe na wajumbe ni Ally Shaaban Majeshi, Said Mwinyi,Hassan Msalu,Ghulam Mohamed, Athuman Ndosi,Ramadhan Mdoe,Issa Anzuwani, Hamza Khamis Amiri, Idris Ngido na Yusuph Abdi Ngome.
“Kwa mujibu wa Katiba ya bakwata ya mwaka 199 toleo la mwaka 2008, natamka viongozi halali wa bakwata Mkoa wa Arusha, Wilaya ya Arusha, mamlaka ya msikiti Mkuu wa ijumaa Mjini Arusha na Masjid Quba ni hao nilioorodhesha katika orodha hii niliyosoma,”alisema na kusimama kuondoka.
Naye Mwenyekiti  wa  Msikiti Mkuu Ijumaa, Abdul  Azizi baada ya Mufti kuzungumza na kutaja majina ya viongozi wanaotakiwa kuepo madarakani, alizungumza na waandishi wa habari na kusema Mufti Sheikh Simba amekosea kutaja orodha hiyo wakati suala la uongozi lipo Mahakamani.
“Ila sisi tutaendelea kuongoza Msikitini hadi hapo Mahakama itakapoamua na si vinginevyo, lakini naomba waumini wa dini hii ya Kiislamu wawe wavumilivu mpaka Mahakama itakapoamua, ila alichofanya Mufti Sheikh Simba ni sawa na kuleta vita Arusha,”alisema.

TRA YAMUA KUDHIBITI KAZI ZA WASANII NCHINI TANZANIA

wasanii 

Mamlaka ya Mapato nchini imeanzisha mfumo wa kutoa stempu kwa kazi za wasanii ili kudhibiti unyonywaji wa kazi  hizo unaofanywa na baadhi ya wasambazaji na wazalishaji feki hivyo kuwafanya wasanii wanufaike na kazi zao pamoja na kulipa kodi kwa serikali.
Akizungumza na Wasanii wa muziki na filamu jijini Arusha ,Afisa elimu kwa mlipakodi TRA,Frank Mwaselela amesema kuwa mfumo huo tayari umerasimishwa kisheria na baada ya kutoa elimu kwa wasambazaji na wasanii hakuna kazi yeyote itakayoruhusiwa kuuzwa pasipo kuwa na stempu.
Afisa huyo amesema kuwa mfumo huo utawasaidia wasanii kutoibiwa kazi zao  na pia kazi zao kuwa na ulinzio wa kisheria baada ya kupitia taratibu sahihi ambazo ni kuzisajili baraza la sanaa (BASATA) Na pia kwa baraza linalohusika na haki miliki (COSOTA).
Naye Afisa  Kodi  Msafiri Mbibo kutoka makao makuu ya TRA amesema kuwa mfumo huo wa stempu umeanza mwaka jana   utasaidia kuondoa wimbi kubwa la wizi na uharibifu wa kazi za sanaa .
“Mpango huu utasaidia kuhakikisha kuwa wasanii kuwa mikataba inayozingatia  haki za wasanii,tayari tuimeshaanza kufanya operesheni kuwakamata wanaouza kazi zisizo na stempu na kuharibu mashione mkoa wa Dar tutaelekea mikoani pia” Alisema Afisa huyo
Katibu wa Chama cha Wauzaji wa kazi za wasanii jijini hapa James Male amesema kuwa jitahada zinazofanywa na TRA na Serikali ni nzuri na ameiomba mamlaka hiyo kuzitazama kazi walizonunua miaka ya nyuma kabla ya kuanzishwa kwa mfumo wa stempu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii mkoani Arusha ,Kassim Digega ameipongeza mamlaka hiyo kwa kuonyesha nia ya dhati ya kulinda kazi zao ili waweze kunufaika na kulinufaisha taifa kwa kulipa kodi.
 
 Na Mahmoud Ahmad,Arusha.
 

Balozi wa Libya nchini Tanzania ajiua kwa kujipiga risasi soma hapa

Balozi wa Libya nchini Tanzania amejiua kwa kujipiga risasi kichwani.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam , John Solombi anasema kuwa balozi huyo kwa jina Ismail Nwairat, alijipiga risasi Jumanne usiku na kufariki akiwa anapokea matibabu hospitalini.
Msemaji wa serikali ya Tanzania Arthur Mwambene amethibitisha taarifa hiyo kuwa balozi huyo alijiua ndani ya makao ya ubalozi wa Libya mjini Dar es Salaam Jumanne usiku.
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde endelea kutembelea mtandao huu

JUMUIYA YA KIISLAMU YA MUZDALIFAT WATOA SADAKA YA RAMADHANI ZANZIBAR

DSC_0688Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat wakishirikiana na Taasisi ya WEFA kutoka Ujarumani wakitoa Sadaka ya Unga, Mchele, Sukari, na Mafuta ya kupikia kwa watu mbalimbali kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika kijiji cha Kilimani Tazari Mkoa wa Kaskani Unguja. DSC_0705Mmoja kati ya Wazee wa kijiji cha Kilimani Tazari akipokea Sadaka iliotolewa na Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat wakishirikiana na Taasisi ya WEFA kutoka Ujarumani kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Zanzibar.
DSC_0688Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat wakishirikiana na Taasisi ya WEFA kutoka Ujarumani wakitoa Sadaka ya Unga, Mchele, Sukari, na Mafuta ya kupikia kwa watu mbalimbali kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani katika kijiji cha Kilimani Tazari Mkoa wa Kaskani Unguja. DSC_0705Mmoja kati ya Wazee wa kijiji cha Kilimani Tazari akipokea Sadaka iliotolewa na Jumuiya ya Kiislamu ya Muzdalifat wakishirikiana na Taasisi ya WEFA kutoka Ujarumani kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

MAVAZI YA HIJABU (Niqab )ni haramu nchini Ufaransa


Mahakama ya haki za binadamu barani Ulaya imeamrisha kuendelea kutekelezwa hukumu ya kupiga marufuku vazi la hijab linalofunika uso mzima nchini Ufaransa.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na nne raia wa Ufaransa ambaye alidai kuwa marufuku hiyo inakiuka haki zake za kuabudu na kujieleza.
Mahakama hiyo hata hivyo imesisitiza kuwa Ufaransa inayo haki ya kuhifadhi utangamano na usawa katika jamii kwa kuweka marufuku hiyo.
Sheria hiyo iliwekwa nchini Ufaransa miaka minne iliyopitana tangu hapo Ubelgiji imeiga.

Rais Kagame azungumzia uhusiano kati ya Rwanda na Tanzania ATOA YAKE YAMOYONI SOMA HAPA

Kagame: Tanzania ni ndugu zetu na hakuna wa kuwatenga ndugu hawa!


Akiongea na waandishi habari leo amesema Tanzania ni ndugu wala haitaji kufanya ziara Tanzania kubembeleza udungu.
Amesema matatizo ya wanyarwanda yanafanana sana na ya wantazania hivyo haoni haja ya kuhasimiana ndugu wanaofanana na wenye matatizo yanayofanana. Hata hivyo ameonya kwamba Rwanda itapambana na yoyote anayeshirikiana na FDRL.

Amesema dunia hii ni ya ajabu maana inawasikiliza na kuwatunza wauaji alafu inalazimisha maridhiano. "Inawezekana tuna sauti ndogo, hatusikiki lakini nawaakikishia hatutaridhiana na wauaji zaidi ya kupambana nao na marafiki zao" alisema.


Rais Kagame azungumzia uhusiano kati ya Rwanda na Tanzania

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kwamba Rwanda na Tanzania ni mataifa ndugu na yataendelea kuwa ndugu kwa sababu yanachangia udugu huo.

Rais Paul Kagame wa Rwanda
Rais Paul Kagame ameyasema hayo mjini Kigali kwenye kikao na waandishi wa habari.Nchi za Rwanda na Tanzania zilikabiliwa na wakati mgumu kuanzia mwaka jana kutokana na kutofautiana kuhusu kundi la waasi wa kihutu la FDLR linaloendesha mambo yake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo dhidi ya utawala mjini Kigali.
Mwandishi wetu Sylivanus Kalemera kutoka Kigali ana ripoti

RUVU SHOOTING YANASA `BUNDUKI` KUFANYA MAKUBWA MSIMU UJAO!

DSCN1347-FILEminimizer 
Mkenya, Tom Alex Olaba anaendelea na mkakati wake wa kusuka kikosi chake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kushika kasi mwezi agosti mwaka huu.

BAADA ya kuingia kambini mapema kabisa, klabu ya wapiga kwata wa Ruvu Shooting yenye maskani yake mabatini, Mlandizi, mkoani Pwani imeendelea kujiimarisha kwa kufanya usajili wa wachezaji wapya kwa mujibu wa mapendekezo ya kocha mkuu, Mkenya, Tom Alex Olaba.
Afisa habari kwa klabu hiyo, mwenye maneno mengi, Masau Bwire ameuambia mtandao huu kuwa klabu hiyo imefanikiwa kuwanasa wanandinga watano wenye uzoefu wa hali ya juu katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara kwa lengo la kumaliza katika nafasi nzuri msimu ujao.
Masau alisema klabu hiyo inafuata taratibu zote za uongozi na haifanyi mambo kiholelaholela kama zinavyofanya klabu zingine zinazoshiriki ligi kuu hususani Simba na Yanga. 

Na Frank Momanyi, Dar es salaam
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ATEMBELEA BANDA LA KAMPUNI YA P.I.L KATIKA MAONYESHO YA (TANTRADE) SABASABA

  KAMPUNI YA PROPERTY INTELNATIONAL LIMITED YATEMBELEWA NA PINDA

1w 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Miengo Pinda akiwasili kwenye banda la Kampuni ya Property Itnernational Limited ya jijini Dar es salaam wakati alipotembelea banda hilo Katika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa (TANTRADE) kwenye viwanja vya Mwalimu J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es salaam, Ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kampuni hiyo inayojihusisha na miradi mikubwa ya upimaji na uuzaji wa viwanja vilivyopimwa kitaalamu maeneo mbalimbali nchini. kulia aliyeongozana naye ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda. 2w 
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akimsikiliza Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Property International Limited Bw. A. Haleem wakati akitoa maelezo kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na kampuni hiyo nchini wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya 38 ya TANTRADE katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar essalaam. 3w 
Kutoka kulia ni Wakuu wa kampuni hiyo Mkurugenzi Mohamed Mahfoudh, Abdu Thabit , Hashim Thabit na Masoud Saeed Alawi wakimsubiri Mh. waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati alipotembelea bada lao. 4 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda wa pili kutoka kushoto akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati akitoa maelezo kuhusu shughuli za kampuni hiyo Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara na katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Property International Limited Bw. Bw. A. Haleem na kutoka kulia ni Mkurugenzi wa TANTRRADE Bi. Anna Bulondo na Mkurugenzi wa kampuni ya Property International Limited Mohamed Mahfoudh, 5w 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiagana na wakuu wa kampuni hiyo mara baada ya kutembelea banda lao kwenye maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa TANTRADE kwenye viwanja vya Sabasaba barabara ya Kirwa leo.

Ajali ya ndege yawauwa wanne Kenya

Ajali ya ndege Nairobi
Shughuli za uokozi zikiendelea baada ya ndege ya mizigo kuanguka jijini Nairobi
Watu wanne akiwemo Rubani wa ndege moja ya mizigo, wamefari dunia baada ya ndege walimokuwemo kuanguka mapema leo asubuhi katika eneo la Utawala- Embakasi jijini Nairobi.
Kwa mjibu wa shirika la msalaba mwekundu Nchini Kenya, ndege hiyo ilianguka dakika chache tu baada ya kupaa kutoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.
Ndege hiyo ya mizigo ilikuwa imebeba SHEHENA ya Miraa ama milungi kuelekea Mogadishu Nchini Somalia.
Barabara ya Estern Bypass jijini Nairobi imefungwa kwa muda huku msongamano mkubwa wa magari ukishuhudiwa.

 

Israeli yaapa kuiadhibu Hamas


Viongozi wa Israeli
Benjamini Netanyahu(kushoto) na Shimon Peres(kulia)
Kikao cha baraza la mawaziri cha usalama kimekaa kwa mara ya pili nchini Israel tangu miili ya vijana watatu wa Israeli ipatikane katika eneo la West Bank hapo jana.
Kabla ya kuingia kwenye kikao hicho, waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu, aliapa tena kuwasaka wale waliowauwa vijana hao na kukabiliana na kundi la wanamgambo wa Palestina la Hamas, analolilaumu kuhusika na mauaji hayo.
"kwanza kuwafuata wale wote waliohusika katika utekeji nyara . Yeyote aliyehusika na mauaji ataadhibiwa ipasavyo. Hatutapumzika wala kutulia hadi tumpate mhusika wa mwisho na haijalishi ni wapi watajalibu kujificha'', alieleza Netanyahu.
Kundi la Hamas limekana kuhusika na mauaji hayo. Tarifa zaidi zinasema kuwa mawaziri wa Israeli walikuwa na hoja tofauti juu ya kuchukuliwa kwa hatua yoyote walipokutana jana.
Miili ya vijana watatu imezikwa katika eneo la kati la Israeli, ambapo maelfu ya raia wa Israeli walihudhuria , akiwemo Bwana Netanyahu na rais wa Israeli , Shimon Peres.

Algeria ; Ramadhan haikutugharimu

Kipa wa Algeria ;Hatukushindwa kwa sababu ya mfungo wa ramadhan.
Kipa wa Algeria Rais M’Bolhi amekanusha madai wachezahi wao walishindwa na Ujerumani kutokana na wao kuwa wadhaifu kwa kufunga saumu.
M’Bolhi ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo ambayo Algeria walishindwa mabao 2-1 na Ujerumani katika muda wa ziada anasisitiza kuwa Saumu hakikuchangia kwao Kushindwa.
M’Bolhi anasema kuwa wachezaji hao wamekwisha zoea kucheza hata wakiwa kwenye mfungo na hivyo haipaswi kutolewa kama sababu .
''Tulishindwa katika mechi hiyo mabao mawili bas,
Hatukushindwa kwa sababu ya mfungo wa ramadhan.
Wajua Ramadhana si swala la jumuiya hilo la swala la mtu binafsi na mola wake''alisema MBolhi.
Kabla ya mechi hiyo kulikuwa na ubishi baada ya kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic kukataa kuulizwa maswali kuhusiana na mfungo wa ramadhan ambao ulikuwa umeanza jumamosi .
Halilhodzic alikataa kufichua idadi ya wachezaji wake ambao wanafunga mfungo wa Ramadhan kabla ya mechi .
Halilhodzic, mwenye umri wa miaka 61, alikataa kujibu swali ikiwa wachezaji wake watafunga Ramadhan au la wakati wakicheza.
Hatukushindwa kwa sababu ya mfungo wa ramadhan.
Kulingana na dini ya Kislamu ,Saumu (Ramadhan) ni nguzo muhimu ya dini na ifikapo wakati wa ramadhan kila mtu mwenye umri wa baleghe hujinyima chakula kuanzia alfajiri hadi magharibi .
Hiyo inaamisha kuw wachezaji wa Algeria hawakuwa wamekula chochote hadi baada ya kipindi cha pili cha mechi hiyo ndipo waliporuhusiwa na dini kunywa na kisha kula .
Kufuatia ushindi huo Ujerumani ilifuzu kwa robo fainali ya kombe la dunia ambapo watakutana na Ufaransa ijumaa ijayo.

KOMBE LA DUNIA:Ubeljiji wachapa mtu 2-1 Marekani

Mfungaji bao la Ubeljiji Lukaku
Mabao ya muda wa ziada ya Kevin de Bruyne na mchezaji wa akiba Romelu Lukaku yaliwezesha Ubeljiji kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la dunia timu hiyo ilipoilaza Marekani mabao 2-1 huku Salvador Brazil.
Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Ubeljiji kufuzu kwa hatua hiyo ya robo fainali baada ya kipindi cha miaka 28 .
Kipa wa marekani Tim Howard alitajwa kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo kufuatia mchezo mzuri aliodhihirisha kwa kuokoa mikwaju tele kutoka kwa vijana wa Marc Wilmots .
Tineja mshambulizi wa Lille mzaliwa wa Kenya Divock Origi alianza katika mechi hii badala yake Lukaku na alichangia katika mashambulizi ya lango la Marekani kwa ushirikiano na Jan Vertonghen na De Bruyne.
Hata hivyo kocha Jurgen Klinsmann alilazimika kufanya mabadiliko baada ya Fabian Johnson, kujeruhiwa na nafasi yake ikachukuliwa na DeAndre Yedlin.
Marekani pia walipoteza nafasi nyingi ya kushinda mechi hiyo Chris Wondolowski alipopiga nje pasi yake Jermain Jones.
Timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu kufikia mwisho wa muda wa kawaida matokeo yakiwa ni 0-0 .
Lakini punde baada ya kuanza kwa muda wa ziada De Bruyne alichonga mkwaju wa Lukaku na kumwacha Howard ameduwaa.
Ubeljiji itachuana na Argentina
Lukaku mwenyewe aliihakikishia ubeljiji tiketi ya robo fainali alipofunga bao la pili kunako dakika ya 15 ya kipindi cha ziada na kutokea hapo Ubeljiji wakarejea nyuma kulinda ngome yao.
Labda hatua hiyo haikuwa nzuri sana kwani iliiruhusu Marekani kushambulia lango lao kila walipopata mpira .
Juhudi zao vijana wa Klinsmann zilizaa matunda Green alipofuma kimiani pasi ya Michael Bradley na kuipa marekani matumaini ya kufufua kampeini yao .
Marekani iliendeleza wimbi baada ya wimbi la mashambulizi wakitafuta bao la kusawazisha lakini wapi muda ulikuwa umekwisha na hivyo sasa wakalazimika kuyaaga mashindano hayo.
Ubeljiji sasa watachuana na Argentina jumamosi ya tarehe 5 julai katika mechi ya Robo fainali kwa mara ya kwanza katika miaka 28.

Tuesday, 1 July 2014

KOMBE LA DUNIA:Argentina ya piga mtu 1-0 yatinga Robo fainali Switzerland watupwa/

KOMBE LA DUNIA: DI MARIA AFUNGA BAO DAKIKA 118, ARGENTINA IPO ROBO FAINALI!

ARGENTINA-DI_MARIA-BAO-USHINDIBAO la Dakika ya 118 la Angel Di Maria limewapa Argentina ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Switzerland kwenye Mechi ya Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia huko Brazil na kuwaingiza Robo Fainali.
Licha ya kutawala, Argentina walishindwa kuipenya Switzerland na Gemu kumalizika 0-0 baada Dakika 90 na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30.ARGENTINA-SWISS
Ndipo kwenye Dakika ya 118 Lionel Messi alikokota Mpira vizuri na kumpasia Angel Di Maria, Fowadi wa Real Madrd, ambae alifunga Bao safi la ushindi.
Mara baada ya Bao hilo, Uswisi mara mbili walipata nafasi kupitia Beki wao Blerim Dzemali aliepiga Kichwa na Mpira kupiga Posti na nafasi nyingine kupiga nje.
Kwenye Robo Fainali hapo Jumamosi, Argentina watacheza na Belgium au USA ambazo zinakutana kwenye Mechi ya Raundi ya Pili baadae Usiku huu.
VIKOSI:
ARGENTINA: Romero, Federico Fernandez, Zabaleta, Garay, Rojo, Gago, Mascherano, Di Maria, Higuain, Messi, Lavezzi.
Akiba: Orion, Campagnaro, Biglia, Perez, Maxi Rodriguez, Augusto Fernandez, Demichelis, Palacio, Alvarez, Aguero, Andujar, Basanta.
SWITZERLAND: Benaglio, Lichtsteiner, Schar, Djourou, Rodriguez, Inler, Behrami, Xhaka, Shaqiri, Mehmedi, Drmic.
Akiba: Sommer, Ziegler, Senderos, von Bergen, Lang, Barnetta, Seferovic, Stocker, Dzemaili, Fernandes, Gavranovic, Burki.
Refa: Jonas Eriksson (Sweden)
KOMBE LA DUNIA
RAUNDI YA PILI YA MTOANO
**Saa za Bongo
JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
49
Brazil 1 Chile 1, Penati 3-2
Mineirão
Belo Horizonte
2300
50
Colombia 2 Uruguay 0
Maracanã
Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
51
Netherlands 2 Mexico 1
Castelao
Fortaleza
2300
52
Costa Rica 1 Greece 1, Penati 5-3
Pernambuco
Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
53
France 2 Nigeria 0
Nacional
Brasilia
2300
54
Germany 2 Algeria 1
Beira-Rio
Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
55
Argentina 0 Switzerland 0 [Dak 120, 1-0]
Corinthians
Sao Paulo
2300
56
Belgium v USA
Fonte Nova
Salvador






ROBO FAINALI
IJUMAA, JULAI 4, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
France v Germany [57]
ROBO FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

2300
Brazil v Colombia [58]
ROBO FAINALI
Estadio Castelão, Fortaleza

JUMAMOSI, JULAI 5, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

1900
Argentina v Mshindi 56 [59]
ROBO FAINALI
Nacional, Brasilia

2300
Netherlands v Costa Rica [60]
ROBO FAINALI
Arena Fonte Nova, Savador

NUSU FAINALI
JUMANNE, JULAI 8, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi 57 v Mshindi 58 [61]
NUSU FAINALI
Estadio Mineirão, Belo Horizonte

JUMATANO, JULAI 9, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Mshindi 59 Mshindi 60 [62]
NUSU FAINALI
Arena Corinthians, Sao Paulo

MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2300
Aliefungwa 61 v Aliefungwa 62
MSHINDI WA 3
Nacional, Brasilia

FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014

SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA

2200
Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62
FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro








Watu wazidi kuawaua mpaka sasa watu18 wauawa katika mlipuko nchini Nigeria


Uharibifu uliotokea baada ya shambulizi
Takriban watu 18 wameripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea sokoni mjini Maiduguri Kaskazini mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa gari lililokuwa limebeba mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.
Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kufanya shambulio hilo.
Tukio hili linakuja huku ripoti ya hivi karibuni ya jeshi la Nigeria ikisema kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi la wapiganaji la Boko Haram.
Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambilizi ya mara kwa mara licha ya operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji hao
Mwandishi wa BBC Habiba Adamu toka mji mkuu wa Nigeria Abuja aliyetembeela eneo hilo anasema kuna utata wa idadi ya waliouawa katika shambulio hilo kwani wakati wengine wakisema waliouawa ni watano wengine wanasema huenda idadi ya waliouawa ikawa ni zaidi ya hiyo iliyotolewa.

Abiria Wanalipa nauli ya daladala kwa kutumia kadi ye kielektroniki nchini kenya

 
Serikali nchini Kenya imeanzisha mfumo mpya wa kulipia nauli ya usafiri.
Katika mfumo huo unaoidhinishwa taratibu, badala ya kulipa kwa pesa taslimu, abiria analipa kwa kutumia kadi ye kielektroniki wanapoabiri matatu au kwa jina jingine daladala.
Mfumo huu mpya una maana kwamba serikali inaweza kuwatoza kodi wafanyabiashara, wa sekta hiyo, inayokadiriwa kuwa na faida ya dola bilioni 2 na nusu kwa mwaka.
Lakini wakosoaji wanasema watu wengi hawajnunua kadi hizo na hawaelewi jinsi zinavyofanya kazi.

Haya ndiyo Maisha ya watu wa mwambao wa ziwa Tanganyika( angalia)

Vijana na watoto wakioga kandokando ya ziwa Tanganyika eneo la Kijiji cha Karema Wilayani Mpanda Mkoani Katavi hali hiyo ni hatari kwa afya ya watoto na akina mama hao ambao ndio wathirika zaidi na hali hii juhudi zaidi zinahitajika kuwaokoa na hali hiyo kuhakikisha jamii hii ya mambao na wao wanapata maji safi ya bomba kwa matumizi ya kunywa kuoga na kupikia.

Na Kibada Kibada Katavi Maisha ya wakazi wa mwambao wa ziwa Tanganyika yanaendelea kama wanavyoonekana wakazi hao wakijishughulisha na shughuliza za kutafuata maisha ya yao ya kila siku bila kujali athari wanayoweza kuipata hasa kupata mlipuko wa magonjwa yanayoweza kusababishwa na matumizi ya maji machafu kama maji ya ziwani kwa kutumia maji hayo kwa kunywa kuoga na shughuli nyingine za kimaisha.
???????????????????????????????

AFARIKI HOSPITAL AKIPEWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00207
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA RAHABU KIHANIKU (60) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.343 CMQ AINA YA HONDA ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA NDULA MWASANGAJA (32) MKAZI WA MTAA WA BAGAMOYO –TUKUYU.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI KATIKA KIJIJI CHA KIKOTA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO MTOTO ANGEL OSWARD (02) MKAZI WA KIKOTA ALIYEKUWA AMEBEBWA NA MAREHEMU AMEVUNJIKA MGUU WA KUSHOTO NA AMELAZWA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA – TUKUYU. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA MAENEO YENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA AJALI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIUME, MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 19-20 AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA 22:14 USIKU KATIKA MTAA WA MBILINYI – SAE, KATA YA ILOMBA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.

TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SABA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA BHANGI. WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA NA 1. JELY EVARIST (24) MKAZI WA MWANJELWA 2. STAFORD NGENZI (21) MKAZI WA MWANJELWA, 3. ALAN AGUSTINO (23) MKAZI WA ILEMI 4. ASIFIWE ABSOLOM (22) MKAZI WA JUA KALI 5. DATI SAMWEL (24) MKAZI WA MWANJELWA 6. MWAKISYE NAZARETH (23) MKAZI WA MWANJELWA NA 7. MICHAEL EZEKIEL (40) MKAZI WA NZOVWE.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MAENEO TOFAUTI JIJINI MBEYA WAKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA GRAM 429. MSAKO ULIFANYIKA KATIKA MAENEO YA JUA KALI, MAKUNGULU NA MAJENGO MAPYA, KATA ZA ILEMI NA NZOVWE, TARAFA ZA SISIMBA NA IYUNGA MNAMO TAREHE 30.06.2014 MAJIRA YA SAA 23:30. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA WAUZAJI WA BHANGI.
TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA WATU AU MTANDAO WA WATU WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI NA USAMBAZAJI WA DAWA ZA KULEVYA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.