MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Tuesday, 1 July 2014

Israel yaapa kulipiza kisasi dhidi ya kikundi cha wapiganaji wa Hamas


Benyamin Netanyahu,waziri mkuu wa Israel

Israel imeapa kulipiza kisasi dhidi ya kikundi cha wapiganaji wa Hamas wa Kipalestina wanaosemekana kuwateka na kuwaua vijana watatu katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa mto Jordan.
Miili ya vijana hao Naftali Frenkel, Gilad Shaar na Eyal Yifrach ilionekana Jumatatu jioni, baada ya kupotea kwa zaidi ya wiki mbili.
Waziri Mkuu wa Israel, Benyamin Netanyahu amesema: "Hamas wanahusika na Hamas watalipa." Hamas wanakanusha kuhusika na tukio hilo.
Israel imefanya mashambulio ya anga zaidi ya 30 katika Ukanda wa Gaza usiku kucha.
Miili ya vijana watatu waliotekwa na kuuawa ilipatikana karibu na mji wa Halhul
Mashambulio hayo yamekuja ikiwa ni kujibu mashambulio 18 ya maroketi kutoka Gaza tangu Jumapili usiku, limesema jeshi la Israel.
Majeshi ya Israel pia yamesambaa katika mji wa Palestina wa Halhul. Miili ilipatikana chini ya kifusi cha miamba karibu na mji huo. Afisa mmoja wa Israel anasema inaonekana kuwa vijana hao watatu waliuawa kwa kupigwa risasi mara baada ya kutekwa kwao.
Israel imewataja watuhumiwa wawili wa utekaji wa vijana hao kuwa ni Ayoub al-Kawasma na Abu Aisheh. Jeshi la Israel limesema lilitegua milipuko iliyokuwa imetegwa wakati wa kuzivamia nyumba za watuhumiwa hao.
Askari wa Israel walitegua milipuko katika nyumba za watuhumiwa wawili wa Hamas. Picha zimeonyesha uharibifu mkubwa uliofanyika katika nyumba ya Abu Aisheh.
Mpalestina mmoja pia aliuawa baada ya kuwarushia kilipuzi wanajeshi wa Israel waliokuwa katika operesheni katika mji wa Jenin ulioko magharibi mwa mto Jordan, mapema Jumanne, limesema jeshi la Israel.

Mlipuko waua watu watano nchini Nigeria angalia hapa

Boko Haram wamekuwa wakifanya mashambilizi ya mara kwa mara licha ya operesheni ya kijeshi dhidi ya wapiganaji hao
Takriban watu watano wameripotiwa kuuawa katika mlipuko uliotokea sokoni Maiduguri kaskazini mwa Nigeria.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa gari lililokuwa limebeba mkaa lilipuliwa na bomu linalodhaniwa liliwekwa ndani ya gari hilo.
Hadi sasa hakuna kundi lolote la kigaidi lililokiri kuandaa shambulio hilo.
Tukio hili linakuja huku ripoti ya hivi karibuni ya jeshi la Nigeria ikisema kuwa limeshambulia moja ya ngome za kundi la wapiganaji la Boko Haram.
Mwandishi wa BBC Habiba Adamu toka mji mkuu wa Nigeria Abuja aliyetembeela eneo hilo anasema kuna utata wa idadi ya waliouawa katika shambulio hilo kwani wakati wengine wakisema waliouawa ni watano wengine wanasema huenda idadi ya waliouawa ikawa ni zaidi ya hiyo iliyotolewa.

Cameroon yadaiwa kupanga mechi kati yao na Brazil

Shirikisho la FIFA linataka uchunguzi uwe wazi
Maafisa wa Cameroon watapelelezwa kutokana na madai kwamba saba kati ya wachezaji wa timu ya taifa hilo walihusika katika kupanga mechi katika Kombe la Dunia linaloendelea nchini Brazil.
Kamati ya maadili ya shirikisho la kandanda la taifa hilo litachunguza shutuma za "udanganyifu" wa "wachezaji saba wabaya" katika mechi zao tatu za makundi.
Madai hayo yametolewa na gazeti moja la kijerumani na mtu aliyehukumiwa kwa kuhusika na kupanga mechi nchini Singapore.
Cameroon ilipoteza mechi zote za kundi A, ikiwemo ile waliolazwa na Croatia kwa mabao 4-0.
Mchezaji wa 'The Indomitable Lions' Alex Song, alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumgota Mario Mandzukic mgongoni katika mechi hiyo, huku wachezaji wenzake Benoit Assou-Ekotto na Benjamin Moukandjo wakizozana baadaye katika mechi hiyo.
Ripoti kutoka katika shirikisho la kandanda la Cameroon lilisema: "Madai yaliyotolewa majuzi kuhusu udanganyifu katika mechi tatu za mwanzo za Cameroon katika Kombe la Dunia la 2014, hasa kati ya Cameroon na Croatia, na vile vile 'kuwepo na wacheza saba wabaya katika timu yetu ya taifa' hayaambatani na maadili na kanuni zinazopendekezwa na usimamizi wetu, pamoja na kanuni za Fifa na maadili ya taifa letu.
"Tuna nia kuu ya kutumia mbinu zote zinazostahili ili kutatua swala hili linalosumbua kwa muda mfupi iwezekanavyo."
'FIFA yataka uchunguzi wa wazi'
Fifa haikusema iwapo ilikuwa ikichunguza swala hilo au la, kwani bodi hiyo inayosimamia kandanda ulimwenguni "ilitaka uchunguzi uwe wazi".
Wachezaji wa Cameroon wakichapana katika mechi yao uwanjani
Hata hivyo, iliongezea kuwa: "kwa ujumla, uadilifu katika mchezo huu ndio swala linalopewa kipaumbele na Fifa, kwa hivyo, tunatilia madai yoyote kuhusu udanganyifu maanani sana."
'Mgogoro wa marupurupu'
Matayarisho ya Cameroon kabla ya michezo hiyo nchini Brazil yalitatizika baada ya wachezaji kukataa kupanda ndege kuelekea Brazil hadi wakati mgogoro uliohusiana na wachezaji hao kulipwa marupurupu yao ulipotatuliwa.
Maelewano ya fedha hatimaye yalifikiwa na shirikisho la kandanda la Cameroon, Fecafoot, lakini safari ya kikosi hicho kuelekea Brazil ilikuwa imecheleweshwa kwa takriban siku nzima.
Walianza michezo hiyo kwa kushindwa kwa bao 1-0 na Mexico kabla ya kulazwa na Croatia na wenyeji Brazil waliowafunga mabao 4-1.
"Wachezaji kadhaa walikosa nidhamu, na ndio sababu tumefungwa mabao manne," mkufunzi wa Cameroon Volker Finke aliambia gazeti la kifaransa la L'Equipe baada ya kushindwa na Croatia.
"Ninajua ni vigumu kucheza na wachezaji kumi, lakini hilo si sababu ya kupoteza katika mkondo huu.
"Mechi ilikuwa sawa hadi tulipoonyeshwa kadi nyekundu. Wacroatia walifanya vizuri mbele ya lango lakini Cameroon pia ilikuwa na nafasi ya kufunga.
"Tabia ya wachezaji kadhaa kwa kweli sio nzuri. Hata tulipokuwa bado na wachezaji 11 kila upande, haikuwa ya kupendeza."

angalia Kituo cha Boko Haram chashambuliwa



Jeshi la Nigeria limesema kuwa limekishambulia kituo cha ujasusi cha wapiganaji wa Boko Haram kinachodaiwa kuhusika na utekaji wa wasichana zaidi ya 200 nchini humo.
Hata hivyo taarifa za jeshi hilo zinasema kuwa kiongozi wa kituo hicho cha Boko Haram Babuji Ya'ari amekamatwa.
Ya'ari pamoja na kutuhumiwa kuhusika katika utekaji wa wasichana hao lakini pia alihusika katika mauaji ya kiongozi wa kijadi wa Gwoza, imebainisha taarifa ya serikali.
Jishi hilo pia limegundua kuwa Ya'ari aliyekuwa mfanya biashara alikuwa akijifanya ni mwanaharakati katika kutokomeza kundi la Boko Haram ili kupata nafasi ya kuchunguza harakati za jeshi la Nigeria na mipango dhidi ya kundi hilo la kigaidi.
Anatuhumiwa kuhusika katika maandalizi ya mashambulio kadhaa likiwemo lile lililotokea Maiduguri na makao makuu ya mji wa Borno mwaka 2011.

Sarkozy akamatwa ,kuhojiwa na polisi kuhusu fedha za uchaguzi


Nicolas Sarkozy, rais wa zamani wa Ufaransa

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anashikiliwa akihojiwa kutokana na tuhuma za kufanya ushawishi kuhusu kesi inayochunguzwa ya matumizi mabaya ya fedha katika uchaguzi uliopita.
Bwana Sarkozy anashikiliwa Nanterre, karibu na mji mkuu Paris, katika tukio la aina yake dhidi ya rais huyo wa zamani wa Ufaransa.

Mwanasheria wa Bwana Sarkozy, alihojiwa Jumatatu kuhusu tuhuma za kutafuta taarifa za ndani kuhusu kesi inayomkabili kiongozi huyo wa zamani.
Hali ya sasa hivi inaonekana pigo katika jaribio la Bwana Sarkozy kuwania kiti cha urais mwaka 2017.
Wachunguzi wanajaribu kutafuta iwapo Bwana Sarkozy, mwenye umri wa miaka 59, ambaye alikuwa rais wa Ufaransa kutoka mwaka 2007 hadi 2012, aliahidi kumpa wadhifa mkubwa jaji wa Monaco, Gilbert Azibert, ikiwa ni shukrani ya kupatiwa taarifa kuhusu uchunguzi unaofanyika dhidi kuhusu fedha aliyoitumia katika kampeni ya uchaguzi.
Wanachunguza madai kwamba Bwana Sarkozy alionywa simu yake ilikuwa inadukuliwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa fedha zilizotumika katika kampeni.
Bwana Azibert, mmoja wa majaji waandamizi katika mahakama ya rufaa, aliitwa kuhojiwa Jumatatu. Jaji mwingine Patrick Sassoust, naye pia alihojiwa, kama ilivyokuwa kwa mwanasheria wa Bwana Sarkozy, Thierry

MBEYA: KITUO KIPYA CHA MABASI NANE NANE CHAZINDULIWA LEO INGAWA BADO KINA MAPUNGUFU.



 Mabasi yakiwa yamepaki katika kituo kipya cha mabasi Nanenane

 Hili eneo ambalo kuna Manyasi ni eneo ambalo limetengwa maalum kwa ajili ya kuweka sehemu ya abiria kungojea usafiri au walio na wageni kungojea watu wao lakini hakuna kilicho jengwa , hali inayosababisha usumbufu mkubwa.

 Baadhi ya Abiria na watu wanaongoja ndugu zao wakiwa wamekaa katika  manyasi huku wakiwa hawana eneo maalum la wao kukaa, jambo ambalo linasababisha wapigwe na jua pia Mvua ikinyesha hakuna pa kujihifadhi.

 Madereva na makonda wakiwa katika eneo hilo jipya la kituo cha basi





 Abiria wakiwa wamekaa tuu bila mpangilio

Biashara zinaendelea

Swali linakuja hapa kwa Halmashauri ya Jiji, Je wakati kituo hiki cha basi kinazinduliwa hamkuona kuwa kunatakiwa kuwe na sehemu ya mapumziko? Wananchi wanaomba muwawekee eneo la mapumziko kulipo kuendelea kukaa katika majani ambayo hata hivyo yatakuwa mavumbi siku chache zijazo

Mapigano mapya yaripotiwa Iraq


Mapigano mapya yameripotiwa kati ya kundi la Jihad la Sunni na majeshi ya serikali katika mji wa Tikrit nchini Iraqi.
Watu walioshuhudia mapigano hayo wameona vumbi la milipuko ya mapigano hayo na kwamba makazi ya Rais wa zamani Saddam Hussein yameshambuliwa pia.
Hata hivyo kuna taarifa kwamba waasi hao wananshikilia baadhi ya ngome za kijeshi katika mapambano hayo.
Tikrit ni mji ambao umekuwa ukishikiliwa na wanajeshi wa Isis tangu 11mwaka huu ambapo walifanikiwa kujiimarisha Kaskazini na magharibi mwa Iraq.
Rais wa Marekan Barack Obama ametangaza kupelekwa kiasi cha wanajeshi 200 kuimarisha usalama wa ubalozi wake mjini Baghdad.
Bunge la Iraqi linatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza kuzngumzia hali hiyo tangu kufanyika kwa uchaguzi mwezi April.
Waziri mkuu wa Iraq Nouri Maliki ana nia ya kuwania kipindi cha tatu cha uongozi wake japo kuwa waangalizi wa kimataifa wanamhusisha na machafuko ya sasa na kuona kwamba hafai kugombea tena.
Kikosi cha wanajeshi 750 wa mMarekani kipo nchini Iraq kukabiliana na wapiganaji hao.

TAASISI YA FARIDAS FOUNDATION YAZINDULIWA

 Farida A. Sekimonyo Mkurugenzi wa Faridas Foundation Akiomba Sala ya  Uzinduzi Rasmi katika uzinduzi wa taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wake uliofanyika kwenye hoteli ya Blue Pear jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Mshehereshaji wa Shughuli ya uziinduzi wa Faridas Foundation Taji Liundi
 Elias Masaki katibu mkuu ‘CHAWATA’ na pia Mweka Hazina Shirikisho la watu wenye ulemavu akichangia  mawazo kuhusiana na jinsi Farida Foundation Inavyofanya kazi zake kwa Jamii
 Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia maada mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika uzinduzi wa Faridas Foundation
Kassim  Kibwe Katibu wa “SHIVYAWATA” Temeke na Mwenyekiti wa Albino  akichangia maada Iliyokuwa ikiendelea katika uzinduzi wa Faridas foundation
Wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini Uzinduzi wa Faridas Foundation
Afisa Miradi wa Faridas Foundation Bw.Lumanus  akijadiliana Jambo Na Mkurugenzi Wa Faridas Foundation Bi Farida A.Sekimonyo
 Wasanii walemavu wajulikanao kama Mabaga Fresh waliojitokeza kutumbuiza kwenye uzinduzi wa Faridas Foundation wakifurahia mada zilizokuwa zinatolewa
 Kikundi  cha Mabaga Fresh Wakitoa Burudani kwenye uzinduzi wa Faridas Foundation

HANS POPPE: F.O.S. NI UKUTA WA CHUMA, SIMBA SC SASA WAPINZANI WATAISIKIA HANS POPPE: F.O.S. NI UKUTA WA CHUMA, SIMBA SC SASA WAPINZANI WATAISIKIA KWENYE BOMBA


MWENYEKITI wa Friends Of Simba (F.O.S.), Zacharia Hans Poppe amesema umoja wao ni sawa na ukuta wa chuma, maana yake wapinzani wa Simba SC katika soka ya Tanzania sasa wasitarajie mteremko kwa klabu hiyo. Kwa miaka mitatu sasa Simba SC haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na pia haijashiriki michuano ya Afrika. Lakini baada ya kigogo wa F.O.S., Evans Elieza Aveva kuchaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa klabu hiyo Jumapili, Simba SC inatarajiwa kurejesha makali yake.
Mwenyekiti wa F.O.S., Zacharia Hans Poppe amesema Simba SC sasa itacheza mpira
Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Poppe amesema kwamba Friends Of Simba ni ukuta wa chuma. “Lango la Simba SC sasa liko salama, Friends Of Simba ni beki imara, haipitiki, sawa na ukuta wa chuma, sasa tunakwenda kucheza mpira, nawaomba wana Simba SC wote waliojitenga kwa sababu ya matokeo mabaya, warudi uwanjani timu yao ikicheza, watafurahi,”amesema. Poppe amesema uongozi uliopita wa Alhaj Ismail Aden Rage haukuwa na ushirikiano, uliwagawa wanachama na akiwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji alijitahidi kumshauri Mwenyekiti wake, lakini hakusikilizwa. “Nilitumia muda wangu mwingi kumshauri Rage, lakini hakunisikiliza. Friends tulikuwa tunachangishana fedha, nampelekea Rage akafanyie shughuli za klabu. Baadaye yeye anakwenda kusema, ni fedha za klabu. Wewe unadhani waliotoa fedha zao watajisikiaje? Basi, Friends wakaanza kujitenga na huo ndiyo ukawa mwanzo wa Simba SC kufanya vibaya, sababu hamasa ilipotea na wachezaji wakatumbukiwa nyongo. Mishahara ikawa inachelewa, mfumo mzima wa malipo ya wachezaji ukawa haueleweki, timu ikawa ipo ipo tu. Lakini sasa tuna uongozi ambao utasikiliza ushauri na kuufanyia kazi. Uongozi ambao utaifanya Simba  SC kuwa ya wana Simba wote,”amesema Hans Poppe. Poppe amesema anafahamu kuna ushindani mkali hivi sasa katika Ligi Kuu kutoka kwa mabingwa, Azam FC, wapinzani wao wa jadi, Yanga SC walioshika nafasi ya pili na hata Mbeya City, waliomaliza nafasi ya tatu, lakini wao (F.O.S.) watatumia uwezo na uzoefu wao kuicheza Ligi wamalize juu ya timu zote hizo.
 Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

YUSSUF BAKHRESA ANATUBANIA JOHN BOCCO, FREE STATE STARS WALALAMIKA


 
KLABU ya Free State Stars ya hapa imesema imekuwa ikimtaka sana mshambuliaji wa Azam FC, John Raphael Bocco, lakini wanasikia hawawezi kumpata kwa sababu mchezaji huyo ni kipenzi cha mmoja Wakurugenzi wa timu yake Tanzania, Yussuf Bakhresa.  Meneja Mkuu wa Free State, Rantsi Mokoena ambaye ni mtoto wa mmiliki wa timu, Mike Makoena amesema kwamba wamejaribu mara kadhaa kutaka kumhamishia Bocco Afrika Kusini, lakini inashindikana.
Yussuf Bakhresa analalamikiwa na Free State Stars kuwabania John Bocco
“Bocco ni mshambuliaji wa kiwango cha kidunia, Azam inakali mafanikio yake. Kama anakuja hapa, akicheza kidogo tu mtamsikia yuko Ulaya. Ila tumekata tamaa, tunasikia yule ni kipenzi cha mtoto wa mwenye timu (Yussuf), anamlea vizuri naye ameridhika na maisha ya pale,”amesema Rantsi.  Kwa upande wake, mtoto mwingine wa mwenye timu hiyo, Kootso Mokoena ambaye ni Meneja wa timu amesema Tanzania ina wachezaji wazuri ambao amekuwa akiwaona mara kadhaa. “Nimekuwa nikiwaona wachezaji wa Tanzania mara kadhaa, wakati fulani nilikuja Dar es Salaam mkiwa mnacheza na Msumbiji mkafungwa 1-0, kuna mchezaji nilimpenda pia, lakini nilipotaka kumchukua ikaibuka mizengwe, nikaacha,”.
John Bocco anatakiwa sana Free State ya Afrika Kusini
“Ngassa (Mrisho) nilimuona Uganda mwaka juzi (kwenye Kombe la Challenge). Nilimpenda tangu hapo, wakati wote nimekuwa nikimfuatilia bila mafanikio, na sasa tunajaribu kwa mara ya mwisho,”amesema Kootsi.  Free State Stars leo itatuma ofa ya nyongeza kidogo katika kujaribu kumnunua Ngassa, baada ya klabu yake, Yanga SC kukataa ofa ya awali ya dola za Kimarekani 80,000 zaidi ya Sh. Milioni 130, ikitaka dola 150,000 zaidi ya Sh. Milioni 240. Ngassa tayari yuko hapa Bethlehem akifanya mazoezi na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, iliyomuajiri kocha wa zamani wa Yanga SC, Mbelgiji, Tom Saintfiet na mwenyewe ameonyesha dhamira ya kubaki. Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Nteze John Lungu aliwahi kuchezea Free State mwaka 1997 wakati bado inaitwa Qwa Qwa Stars kabla ya kununuliwa na familia ya Makoena mwaka 2003. Wachezaji kadhaa wakubwa wamepitia katika klabu hiyo akiwemo Bunene Ngaduane wa DRC, Jonathan Mensah wa Ghana, Kennedy Mweene wa Zambia, John Tlale na Siphiwe Tshabalala wote wa Afrika Kusini na ambao pia wapo Bafana Bafana.
 Na Mahmoud Zubeiry, BETHLEHEM

KOMBE LA DUNIA: Algeria 1-2 Ujerumani


Wafungaji mabao ya Ujerumani Mesut Ozil na Andre Schurrle
Mechi imekamilika . Ujerumani 2-1 Algeria .
Ujerumani sasa itachuana na Ufaransa katika robo fainali ya kombe la dunia katika uwanja wa Marakana.
Afrika sasa haina mwakilishi katika robo fainali ya kombe la dunia la mwaka wa 2014 baada ya wawakilishi wenza wa bara la Afrika katika mkondo wa pili Nigeria kushindwa mabao mawili kwa nunge na Ufaransa katika mechi iliyotangulia .
Kufutatia ushindi huu wa Ujerumani ni dhahiri sasa kuwa timu zote zilizoongoza baada ya mechi za makundi ndizo zilizofuzu kwa robo fainali ya kombe la dunia .
Ufaransa itakabiliana na Ujerumani siku ya ijumaa katika uwanja wa Maracana saa moja usiku saa za Afrika Mashariki.
Mechi itatangulia ile kati ya weneyeji Brazil na Colombia.
Jumamosi ijayo Uholanzi itakuwa na kibarua kiguimu dhidi ya Costa Rica
30:00+01 GOOOOOAL Ujerumani 2-1 Algeria Djabau
30:00 Ujerumani imefuzu kwa robo fainali
30:00 Ujerumani 2-0 Algeria Mesut Ozil
Ujerumani 1-0 Algeria 20''
17:50 Kipa wa Ujerumani Nuer anaudaka bila wasiwasi.
16:30 FREEKICK kuelekea upande wa Ujerumani na mpira unapigwa na Ibrahimi
15:30 Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi kama kile cha kwanza lakini wanaofanya mashambulizi sasa ni Algeria .
15:00 Ikiwa mechi hii itaisha ikiwa hivi,basi inaonesha kuwa timu zote zilizoshinda makundi yao ndizo zilizoshinda mechi za mkondo wa pili.
15:00+01 Kipindi cha kwanza cha muda wa ziada kimekamilika Ujerumani 1-0 Algeria
15:00+01 Algeria wanaonekana kukubali hatima ya mechi hii
15:00 Kipindi cha kwanza kimekamilika .
13:40 Moustafa anajaribu kupenya safu ya ulinzi ya ujerumani lakini wapi
12:50 Mpira unatolewa nje na Aissa Mandi
11:00 KONA kuelekea lango la Ujerumani
02:50 André Schürrle''02 ET anaifungia Ujerumani bao lao la kwanza
02:00 GOOOOOOOAL Ujerumani 1-0 Algeria
ETRATIME
90:00+4 Mechi imekamilika Algeria 0-0 Ujerumani .Mechi hii sasa itaamuliwa katika muda wa zaida
89:00 Ujerumani inaendelea na mashambulizi lakini Algeria inahimili mikiki yao.
86:00Freekick kuelekea lango la Algeria nje tu ya eneo
Muller anakosa nafasi ya wazi
85:14
85:00 Muller anakosa fursa ya wazi
Nuer analazimika kuisadia safu yake ya ulinzi
74:30 Slimani anamjaribu Nuer kuitoka mbali lakini wapi ,Boateng anazuia duh!
71:48 Freekick baada ya Muller kuangushwa nje ya eneo
70:00 Kipa wa Ujerumani anafanya kazi ya ziada kuzuia shambulizi la Algeria.
Kipa wa Algeria anafanya kazi ya ziada
65:00
61:40 Kona kuelekea lango la Algeria ,Inapigwa na Kroos na shambulizi linazimwa .
60:00 Ujerumani 0-0 Algeria ''60
58:02 Nipe nikupe katikati ya uwanja lakini ujerumani wakionesha ukakamavu wao
Ujerumani 0-0 Algeria 62''
54:50 Shambulizi linazimwa baada ya kipa wa Algeria Rais kuutema
54:20 Kona kuelekea lango la Algeria
52:13 Andre Schurrle anapoteza nafasi nzuri mbele ya lango la Algeria .
48:41 Ujerumani wanaonekana wamechochewa kushambulia lango la Algeria
Algeria 0-0 Ujerumani 55
47:30 Kona kuelekea lango la Algeria .
46:30 Ujerumani 0-0 Algeria
46:00Kipindi cha pili kimeanza tena.
45:00+1 kipindi cha kwanza kimekamilika timu zote zikiwa hazijapata bao lolote
Kroos akishambulia Rais Mbolhi
45:10 Freekick Kuelekea lango la Ujerumani
44:50 Toni Kroos anatuma kombora lakini nje .
44:50 Algeria 0-0 Ujerumani
jaribio lingine katika lango la Algeria
41:15
37:00 Kipa wa Algeria anautema mpira mbele ya lango ,,,Nusura Muller atume kombora lakini unatoka nje na ni Goal Kick kuelekea lango la Ujerumani
36:00 Algeria wanawadhibiti Wajerumani hatua kwa hatua katika mechi hii
33:00 Leohart Frasha Lavendar matumaini ya mende kubeba kabati..,hahaha
33:00 Frank Mshana wa Tz anasema Ubinafsi ndio unatuangusha
31:10 Free kick kuelekea lango la Ujerumani nje ya eneo
30:00 Ujerumani 0-0 Algeria
Boateng na mpira !
28:30
24:45 Muller na Boateng wanashirikiana kumpokonya Soudani mpira .
23:50 Inazimwa kwa kicha na sasa imemfikia Ozil na Ujerumani wanapanga shambulizi lengine
22:30 Ujerumani inapata KONA
Slimani anapoteza nafasi nyengine alikuwa ameotea
20:45 Mechi inavyoendelea inaonesha timu zote zimetoshana nguvu
17:50 Zidane na slimani wanapoteza nafasi nyengine ya wazi mbele ya lango la Ujerumani
16:20 OFFSIDE Bao la Algeria linakataliwa kwa kuwa Slimani alikuwa keshaotea .
15:30 Ujerumani 0-0 Algeria
Mashabiki wa Algeria
12:40
10:30 Algeria Inashambulia lango laUjerumani ikibainika kuwa Slimani anamshinda kwa kasi Per Mertesacker .
08:40 Algeria wanageuza ulizni kuwa shambulizi linalomlazimu kipa wa Ujerumani kuondoka langoni ili kuzuia mashambulizi Islam Slimani
07:43 Shambulizi kuelekea upande wa Algeria .
02;50 Offside ya kwanza kuelekea upande wa Algeria .
01 Mpira unaanza uwanjani Porto Alegre
Algeria inabeba matumaini ya Afrika inapochuana na Ujerumani katik mechi ya mwisho ya mkondo wa 16 bora.
Wimbo wa taifa unachezwa
Algeria inabeba matumaini ya Afrika inapochuana na Ujerumani katik mechi ya mwisho ya mkondo wa 16 bora.
Mshindi atachuana na Ufaransa ambayo iliizima Nigeria 2-0
Mara ya mwisho Algeria iliilaza ujerumani Magharibi mabao 2-1
Algeria inakabiliana na Ujerumani.
Hii ni Mara ya kwanza kwa Algeria kuchuana na Ujerumani tangu mwaka wa 1982

Israel yasema Hamas iliwauwa vijana wake


Vijana wa Israel waliopatika awakiwa wameuawa
Msemaji wa jeshi la Israel amesema kuwa miili hiyo ilikuwa chini ya miamba iliopo kwenye mji wa west Bank wa Hebron.
Israel imepeleka vikosi vyake katika kijiji cha Palestina cha Hal-hul.
Katika kikao cha dharura cha mawaziri ,waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema vijana hao walitekwa na kuuawa katika mauji aliyosema yamefanywa na wanyama.
Netanyahu amelilaumu kundi la Wapalestina la Hamas, na akaahidi kulipiza kisasi.
Benjamini Netanyahu
Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu
Hamas imekana kuhusika na mauaji hayo kupitia mshauri rasmi wa rais wa Palestina Mahmoud Abbas -Abdallah Abdallah
Mwandishi wa BBC aliyeko mashariki ya kati anasema milio ya mashambulizi ya ndege za Israeli imesikika kote katika ukanda wa Gaza .
Kulikuwa na tetesi kuwa Israeli ingeileng maeneo ya Hamas baada ya kikao chake cha mawaziri cha usalama .
Mji wa Gaza umesalia kuwa ngome kuu ya Hamas na ofisi zake katika eneo hilo zimekuwa zikivamiwa katika kipindi cha zaidi ya wiki mbili na nusu.
vifo vya karibu wapalestina watano vimeripotiwa na mamia ya wapalestina wamekamatwa.

Kituo cha Boko Haram chashambuliwa


Jeshi la Nigeria limesema kuwa limekishambulia kituo cha ujasusi cha wapiganaji wa Boko Haram kinachodaiwa kuhusika na utekaji wa wasichana zaidi ya 200 nchini humo.
Hata hivyo taarifa za jeshi hilo zinasema kuwa kiongozi wa kituo hicho cha Boko Haram Babuji Ya'ari amekamatwa.
Ya'ari pamoja na kutuhumiwa kuhusika katika utekaji wa wasichana hao lakini pia alihusika katika mauaji ya kiongozi wa kijadi wa Gwoza, imebainisha taarifa ya serikali.
Jishi hilo pia limegundua kuwa Ya'ari aliyekuwa mfanya biashara alikuwa akijifanya ni mwanaharakati katika kutokomeza kundi la Boko Haram ili kupata nafasi ya kuchunguza harakati za jeshi la Nigeria na mipango dhidi ya kundi hilo la kigaidi.
Anatuhumiwa kuhusika katika maandalizi ya mashambulio kadhaa likiwemo lile lililotokea Maiduguri na makao makuu ya mji wa Borno mwaka 2011.