Rooney amesuasua kusaini mkataba mpya
Old Trafford na ilidaiwa kwamba alikuwa anajiandaa kuondoka mwishoni mwa
msimu kwa ajili ya kupata changamoto mpya ya soka nje ya Man United.
Mkataba wa Rooney unatarajiwa
kumalizika mwishoni mwa msimu ujao Juni 2015 na kulikuwa na wasiwasi
kwamba staa huyo wa zamani wa Everton alikuwa anataka kuondoka bure
mwishoni mwa msimu ujao hili apate fedha nyingi zaidi.
Hata hivyo, kocha David
Moyes amefanikiwa kumshawishi nyota huyo kubaki lakini kwa gharama za
kumlipa mshahara wa Pauni 300,000 (Sh.750 milioni) kwa wiki ambao
unaweza kuwa wa mwisho kwake klabuni hapo.
Wakati huohuo, licha kumnasa kiungo
mchezeshaji wa Chelsea, Juan Mata na kufanikiwa kumbakiza Rooney, Moyes
amekumbana na pigo baada ya kiungo wa Juventus aliyekuwa anamwinda,
Arturo Vidal kusisitiza kwamba atabaki klabuni hapo.
Moyes ameshasafiri mpaka Italia kwa
ajili ya kumwangalia nyota huyo wa kimataifa wa Chile ambaye yupo katika
kiwango cha juu na alikuwa anataka kumchukua katika kikosi chake kwa
ajili ya kukitia makali na kukirudisha katika ushindani.
Moyes atalazimika kuongeza juhudi zake kwa kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos ambaye anaweza kuuzwa. Chanzo: mwanaspoti
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE
Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE
Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE
Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE
Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu
MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE
Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu
Saturday, 1 February 2014
KALLSTROM: MPYA ARSENAL MAJERUHI KABLA KUANZA KUCHEZA!
MCHEZAJI MPYA wa Arsenal, Kim Kallstrom, atakuwa nje kwa muda baada kugundulika ameumia Mgongo.
Kallstrom, Miaka 31, inadaiwa aliumia
Mazoezini Jumanne huko Abu Dhabi, UAE, wakati alipokuwa na Klabu yake
Spartak Moscow na aliwaeleza Arsenal matatizo yake hapo Jana alipotua
London kwa upimwaji Afya lakini Vipimo vya MRI havikuonyesha tatizo
lakini Kipimo cha CT kilionyesha lipo tatizo kwenye Mgongo wake.
Inadaiwa Wenger alijulishwa taarifa hizi
lakini ikaamuliwa wakamilishe Usajili wake hiyo Jana ambayo ndio
ilikuwa Siku ya mwisho ya Uhamisho wa Wachezaji kwenye Dirisha la
Uhamisho la Januari.
Inakisiwa Kallstrom atazikosa Mechi 6 za
Arsenal ambazo ni dhidi ya Crystal Palace, Liverpool, mara mbili,
Manchester United, Bayern Munich na Sunderland.
Kallstrom, Raia wa Sweden aliewahi kuichezea Lyon ya France, ndie Mchezaji pekee
aliesainiwa na Arsenal kwenye Dirisha la
Uhamisho la Januari na amesainiwa kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu ili
kuziba pengo la Viungo Majeruhi Aaron Ramsey na Jack Wilshere pamoja na
Mathieu Flamini ambae amefungiwa Mechi 3 baada Kadi Nyekundu.
Mchezaji huyo sasa anatarajiwa kurudi
kwao Sweden kisha kwenda Urusi na baadae kurudi London kuendelea na
Matibabu akiwa na Arsenal.
LA LIGA: BARCA YAPIGWA NA VALENCIA BAO 3-2 KWAO NOU CAMP
>>JUMAPILI: ATLETICO AU REAL KUTWAA UONGOZI?!
LA LIGA sasa ni mshikemshike kweli baada
ya Leo Valencia kufanya kweli Uwanjani Nou Camp na kuichapa Barcelona
Bao 3-2 na kuwaweka Mabingwa hao kwenye njia panda maana Jumapili
Atletico Madrid au Real Madrid zina nafasi kubwa kuwapiku uongozi wa
Ligi.
MSIMAMO-Timu za Juu:
| NA | TIMU | P | W | D | L | F | A | GD | PTS |
| 1 | FC Barcelona | 22 | 17 | 3 | 2 | 59 | 16 | 43 | 54 |
| 2 | Atletico de Madrid | 21 | 17 | 3 | 1 | 52 | 14 | 38 | 54 |
| 3 | Real Madrid CF | 21 | 17 | 2 | 2 | 60 | 21 | 39 | 53 |
| 4 | Athletic de Bilbao | 21 | 13 | 3 | 5 | 41 | 27 | 14 | 42 |
Barca
walitangulia kufunga Bao katika Dakika ya 7 Mfungaji akiwa Alexis
Sanchez na Valencia kujibu na kupiga Bao mbili katika Dakika ya 44
lililofungwa na Parejo na Dakika 4 baadae kupitia Pablo Piatti.
Barca walisawazisha kwa Penati ya Lionel
Messi na hilo ni Bao lake la kwanza baada kutofunga katika Mechi 3
lakini Paco Alcácer, katika Dakika ya 59, aliipigia Valencia Bao la 3 na
kuwapa ushindi.
Barca walimaliza wakiwa Mtu 10 baada
Jordi Alba kupewa Kadi ya Njano ya pili kwenye Dakika ya 78 na kutolewa
nje kwa Kadi Nyekundu.
Ukiiondoa Real Madrid, Valencia imekuwa
Timu ya kwanza kuondoka Nou Camp bila kufungwa tangu Oktoba 2011 Sevilla
ilipopata Sare ya 0-0.
Matokeo haya yameiacha Barca uongozini
ikiwa Pointi 54, sawa na Atletico Madrid, lakini Atletico wana Mechi
moja mkononi ambayo watacheza Nyumbani kesho Jumapili na Real Sociedad
wakati Real Madrid, walio Pointi 1 nyuma ya Barca na Atletico, pia
watacheza Jumapili Ugenini na Athletic Bilbao.
Atletico na Real zina nafasi nzuri kuitungua Barca toka kileleni.
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Ijumaa Januari 31
Granada CF 1 Celta de Vigo 2
Jumamosi Februari 1
FC Barcelona 2 Valencia 3
Levante v Rayo Vallecano
Getafe CF v Real Valladolid
Malaga CF v Sevilla FC
Jumapili Februari 2
Elche CF v UD Almeria
Real Betis v RCD Espanyol
Atletico de Madrid v Real Sociedad
Athletic de Bilbao v Real Madrid CF
Jumatatu Februari 3
Villarreal CF v Osasuna
UVCCM MKOA WA MBEYA WAMTAKA JOHN SAMWEL MALECELA ASINGILIE MASWALA YA VIJANA NDANI YA CCM
| Edward Kakwale toka Momba |
YUSUF MANJI AWAWAKIA WANOOMUANDAMA SEIF MAGARI
Dar
es Salaam. Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amewaonya
wanachama na mashabiki wa timu hiyo wanaotishia maisha Mwenyekiti wa
Kamati ya mashindano ya imataifa wa klabu hiyo, Seif “Magari” Ahmed kuwa
sheria kali zitachukuliwa dhidi yao.
Katika
taarifa yake aliyoitoa jana, Manji amesema kuwa si suala jema kwa
wanachama kumuhusisha Seif na matokeo ya timu hiyo ambayo kwa sasa
imeshinda mechi moja na kutoka sare mechi moja katika mzunguko wa pili
wa Ligi kuu ya Tanzania Bara.
Manji
amesema kuwa madai kuwa Seif siyo mwanachama halali wa Yanga hayana
msingi wowote na kuyaita madai hayo kuwa ni ya uzushi na yanaenezwa na
maadui zao ambao hawaitakii Yanga mema.
Alisema kuwa hivi karibuni kumekuwa na madai ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu, taarifa za hujuma ndani ya timu ambazo zimewahusisha uongozi na baadhi ya wanachama jambo ambalo si la kweli.
Alifafanua kuwa ni haki kwa kwa nia njema kwa wanachama kuhoji mwenendo wa timu yao pale wanapoona-hairidhishi
na ni wajibu wa wanachama kuchanganua mawazo merna na mabaya na siyo
kumuhisha mtu kwa moja kwa moja kutokana na mtazamo hasi walionao.
“Ushindi au mwenendo mzuri wa timu unatokana na viwango vizuri, nidhamu na ushirikiano wa wahusika wote, wachezaji,
walimu, viongozi, wanachama na wapenzi kwa ujumla. Uongozi ulikutana na
wachezaji, walimu, baadhi ya wanachama na wapenzi na kuyazungumzia na
kukubaliana kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa wahusika wote na
kuchukua hatua ya kubadilisha benchi la ufundi,” alisema Manji.
Aliongeza
kwa kusema kuwa uongozi ulifika mbali zaid kwa kutoa adhabu na onyo
kali kwa baadhi ya wachezaji walionyesha utovu wa nidhamu kwa kipindi
kilichopita na kusikitishwa kuona kuwa baadhi ya wadau kwa kutumia
vyombo vya habari wanachochea na kutengeneza uhasama ambao kwa kweli
haupo ama kwa faida zao binafsi, au kwa kutumiwa na watu ambao hawana nia njema kwa klabu.
Manji
pia aliwaomba wadau wote wanamichezo na hasa wahariri wa michezo
kudhibiti matumizi mabaya ya watu au vyombo vya habari yanayochangia
sana kuzorotesha michezo nchini.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA JUMUIYA YA ISTIQAAMA DAR.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akuhutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa
Jumuiya ya Istiqaama, uliofanyika katika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar
es Salaam, leo Feb 01, 2014. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwasili kwenye Ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kufungua rasmi Mkutano
Mkuu wa Jumuiya ya Istiqaama, leo Feb 01, 2014. Picha na OMR
Baadhi ya Wanachama wa Jumuiya ya Istiqaama, wakimsikiliza Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakati alipokuwa akihutubia kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Jumuiya hiyo
leo katika Ukumbi wa Karimjee. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum,
baada ya kufungua rasmi Mkuu wa Jumuiya hiyo leo katika Ukumbi wa
Karimjee. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum,
baada ya kufungua rasmi Mkuu wa Jumuiya hiyo leo katika Ukumbi wa
Karimjee. Picha na OMR
Picha ya pamoja baada ya kufunguliwa mkutano huo.
MWENYEKITI WA CCM DR. JAKAYA KIKWETE AWASILI SALAMA MBEYA KWA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akishuka kwenye
ndege mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Songwe mkoani Mbeya mara baada ya kuwasili rasmi mkoani humo tayari kwa
kuongoza maadhimisho ya Miaka 37 ya Chama cha Mapinduzi yanayofanyika
kesho kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ambapo amepokelewa na
viongozi mbalimbali wa kitaifa wa Chama na Serikali pamoja na wananchi
waliojitokeza katika mapokezi hayo.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na
Ushirika Mh. Godfrey Zambi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa
Songwe.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati ni Mkuu wa mkoa wa
Mbeya Mh. Abas Kandoro na Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman
Sigalla kushoto.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na
Marck Mwandosya Waziri asiyekuwa na Wizara maalum, katikati ni Mkuu wa
Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla na kushoto ni Dr. Harrison Mwakyembe
Waziri wa Uchukuzi.
Mwenyekiti wa Cma Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Kamnda wa Polisi mkoa wa Mbeya SACP AHMED Z. MSANGI .
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr.Jakaya Kikwete akipokea heshima
kutoka kwa kikosi cha vijana wa Chipukizi mkoa wa Mbeya mara baada ya
kuwasili uwanja wa ndege wa Songwe kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi na kutoka kushoto ni
Dr. Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi, Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.
Abas Kandoro, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula, Mkuu wa
Wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman Sigalla na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr.Jakaya Kikwete akivishwa skafu na
vijana wa chipukizi mkoa wa Mbeya mara baada ya kuwasili mkoani humo
kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa serikali na chama.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na viongozi na wabunge
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na vijana wa UVCCM.
Mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi CCM Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa katika kikao
cha ndani na viongozi wa CCM mkoa wa Mbeya kutoka kulia ni Katibu Mkuu
wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti
Bara na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh. Godfrey Zambi
wajumbe wa harmashauri kuu mkoa wa Mbeya wakiwa katika kikao hicho.
Mary
Mwanjelwa Mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Mbeya akisalimiana na
makada wa chama hicho kushoto ni Kada wa CCM Richard Kasesela.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya
Mbeya Mh. Dr. Norman Sigalla wakati aliookuwa akizungumza jambo naye
katikati ni Kada wa CCM Bw. Mwakipesile na kuliani Mkuu wa mkoa wa Mbeya
Mh. Abas Kandoro.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Kamnda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP AHMED Z. MSANGI wakati wa mapokezi hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na viongozi wanawake wa mkoa wa Mbeya.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwa msisitizo na Dr.
Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi wakati wa mapokezi hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na viongozi wanawake wa mkoa wa Mbeya.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwa msisitizo na Dr.
Harrison Mwakyembe Waziri wa Uchukuzi wakati wa mapokezi hayo.
Ndege ya Rais Jakaya Kikwete ikiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe mkoani Mbeya



















