MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Saturday, 1 February 2014

MAJANGA YANAENDELEA MAN UNITED, YAPIGWA NA STOKE CITY 2-1

>>EVERTON YASHINDA, SPURS YABANWA!

>>JUMAPILI: ARSENAL v PALACE, WBA v LIVERPOOL!
MATOKEO:
Jumamosi Februari 1
Newcastle 0 Sunderland 3
West Ham 2 Swansea 0
Cardiff 2 Norwich 1
Everton 2 Aston Villa 1
Fulham 0 Southampton 3
Hull 1 Tottenham 1
Stoke 2 Man Utd 1

STOKE CITY 2 MAN UNITED 1
 
Bao mbili za Charlie Adam zimewapa Stoke ushindi wao wa kwanza kwenye Ligi tangu Mwaka 1984 dhidi ya Man United walipoichapa 2-1 Uwanjani Britannica.
Man United, wakianza Mechi kwa kuwachezesha kwa pamoja kwa mara ya kwanza Juan Mata, Robin van Persie na Wayne Rooney, walipata pigo kwa kuwapoteza Msentahafu wao wawili Jony Evans na Phil Jones walioumia Kipindi cha Kwanza tu, na bahati ilizidi kuwa mbaya kwao baada ya Frikiki ya Adams kumbabatiza Michael Carrick na kutinga wavuni.
Baada Kipindi cha Pili kuanza, Van Persie aliisawazishia Man United lakini Shuti la Mita 25 la Adams liliwapa ushindi Stoke.
 

CARDIFF CITY 2 NORWICH CITY 1
Cardiff walitoka nyuma na kuichapa Norwich Bao 2-1 na kujinasua toka mkiani na kumpa Pointi za kwanza Meneja Ole Gunnar Solskjaer.
Robert Snodgrass aliipa Norwich Bao la kuongoza lakini Mchezaji mpya wa Mkopo kutoka Man United, Wilfried Zaha, alitoa pasi safi kwa Craig Bellamy na kisha mpya mwingine, Kenwyne Jones, kuwapa ushindi kwa kufunga Bao la Pili.
 
EVERTON 2 ASTON VILLA 1
Everton walitoka nyuma kwa Bao 1 na kuifunga Villa Bao 2-1 kwa Bao za Naismith na Mirallas na Bao la Villa kufungwa na Bacuna.
 

FULHAM 0 SOUTHAMPTON 3
Bao 3 za Kipindi cha Pili za Lallana, Lambert na Rodriguez, zimewapa ushindi Southampton wa Bao 3-0 walipoichapa Fulham iliyokuwa kwao Craven Cottage na kuitupa mkiani mwa Ligi.
 
HULL CITY 1 TOTTENHAM 1
Hull na Tottenham zilitoka Sare ya Bao 1-1 baada ya Paulinho kuisawazishia Tottenham Bao wakati Hull walipotangulia kwa Bao la Long.
 
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumapili Februari 2
16:30 West Brom v Liverpool
19:00 Arsenal v Crystal Palace
Jumatatu Februari 3
23:00 Man City v Chelsea
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Man City 23 42 53
2 Arsenal 23 24 52
3 Chelsea 23 23 50
4 Liverpool 23 29 46
5 Everton 24 12 45
6 Tottenham 24 -1 44
7 Man Utd 24 10 40
8 Newcastle 24 1 37
9 Southampton 24 7 35
10 Aston Villa 24 -7 27
11 Stoke 24 -14 25
12 Swansea 24 -6 24
13 Hull 24 -7 24
14 Sunderland 24 -11 24
15 Norwich 24 -18 24
16 Crystal Palace 23 -16 23
17 West Brom 23 -6 22
18 West Ham 24 -9 22
19 Cardiff 24 -22 21
20 Fulham 24 -31 19

REKODI YA MAN CITY ETIHAD NCHINI ENGLAND TISHIO ULAYA

 
article-2434736-166DD583000005DC-121 634x3861 20ac8
TUTATOKA? Hili ni swali la makocha wengi barani Ulaya wanaopeleka timu zao kwenda kumenyana na Manchester City kwenye uwanja wao wa Etihad. Hawa jamaa balaa sana kwenye uwanja wao msimu huu. 
Kwenye mechi 11 za Ligi Kuu England walizocheza uwanjani hapo msimu huu wamefunga mabao 42.
Kocha Jose Mourinho, Jumatatu atasafari na kikosi chake cha Chelsea kwenda uwanjani hapo, lakini tayari ana wasiwasi wa kupigwa tano au sita.
Arsenal, Tottenham na West Ham kila moja zilifungwa mabao sita zilipokwenda Etihad msimu huu, Norwich City ilipigwa saba na Manchester United ilikung'utwa mabao manne.
Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, CSKA Moscow na Viktoria Plzen zilikubali kuruhusu mabao tisa kwenye nyavu zao zilipoifuata Manchester City nyumbani. Etihad si mahali pazuri kabisa kwa wapinzani msimu huu. Mourinho atapaweza?
Vinara hao wa Ligi Kuu England wanaonolewa na Manuel Pellegrini walianza msimu kwa kusuasua baada ya kupokea vichapo kutoka kwa Cardiff City, Aston Villa, Chelsea na Sunderland na pia kutoka sare dhidi ya Stoke na Southampton, lakini rekodi ya kwenye uwanja wao wa nyumbani inatisha.
Nani ataweza kuwadhibiti? Chelsea itakwenda
uwanjani hapo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mchezo wao wa mzunguko wa kwanza, lakini hilo linaweza kuwa baya zaidi kama Pellegrini atahitaji kulipa kisasi.

Manchester City itamkosa straika wake, Sergio Aguero, lakini bado wana mastraika wengine hatari zaidi, Alvaro Negredo, Stevan Jovetic, Eden Dzeko, ambao wote ni hatari sana. Pellegrini watu wake muhimu kikosini anapocheza mechi kubwa ni Vincent Kompany, Samir Nasri, David Silva, Yaya Toure, Fernandinho, Gael Clichy na Zabaleta. Chanzo: mwanaspoti

MERSON ASEMA NA KUDAI KUWA CHELSEA ITAIFUNGA MAN CITY

 

RTO1 c5d0e
NI wababe. Wanatembeza vichapo vinene kila wanapocheza na timu kubwa. Matokeo huwa ni 6-3, 5-1, 4-1. Hawa ni Manchester City. Jumatatu usiku watakuwa katika uwanja wao wa nyumbani Etihad kukipiga na wababe wenzao, Chelsea. 
Lakini 'mwendawazimu' mmoja ametabiri kwamba katika pambano hilo, Chelsea itaibuka mbabe mbele ya Manchester City, tena katika uwanja wa ugenini na kila shabiki atashangaa.
Kiungo wa zamani wa Arsenal, Paul Merson amedai kwamba ana kila sababu ya kuamini kuwa Chelsea itaichapa Manchester City katika pambano hilo la Jumatatu usiku na kukomesha ubabe wao unaozidi kushika kasi katika miezi ya karibuni.
"Ukweli ni kwamba Chelsea hawatakwenda Etihad kwa ajili ya kujihami. Manchester City hawatakuwa na Sergio Aguero na wanapomkosa wanakuwa timu tofauti kabisa. Wawili waliopo mbele, Edin Dzeko na Alvaro Negredo watapambana vilivyo na John Terry na Gary Cahill. Wale hawawezi kushuka chini na kusumbua kama Aguero anavyofanya," alisema Merson.
"Kama wakicheza kama ninavyofikiri, sioni jinsi gani Chelsea itapoteza mechi hii. Kama wakienda kwa ajili ya kujilinda Man City watatengeneza nafasi nyingi. Lakini mara kadhaa nimeiona Man City wakiwa wazembe katika ulinzi," aliongeza Merson.
"Crystal Palace, Cardiff na hata
Watford wamekwenda pale na kutengeneza nafasi na wangeweza kushinda mechi. Katika mechi kubwa huwa wanapambana zaidi na itavutia kuona nini kitatokea wakati watakapocheza na moja kati ya timu kubwa Ligi Kuu England kwa sasa kama Chelsea ambayo ina mastaa wa kuweza kuwashtukiza."

Katika hali ya kushangaza, Merson ametabiri kwamba pambano la leo Jumamosi kati ya Stoke City na Manchester United litaisha kwa sare licha ya Man United kupata nguvu kwa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Juan Mata.
"Bado kuna kazi kubwa ya kufanya Manchester United. Wana Robin van Persie, Wayne Rooney na Juan Mata katika timu yao kwa sasa, lakini sehemu ya ulinzi haijabadilika na hata kiungo kipo hivyo hivyo kwa hiyo nadhani Stoke haitapoteza mechi hii," aliongeza Merson huku akizitabiria ushindi Arsenal na Liverpool ambazo zinacheza na Crystal Palace na West Brom. Chanzo: mwanaspoti

LIGI KUU ENGLAND: SUNDERLAND YAITWANGA NEWCASTLE! 3-0 ANGALIA MATOKEO YA MECHI ZINGINE



>>KEVIN NOLAN AIPA USHINDI WEST HAM!!
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 1
Newcastle 0 Sunderland 3
West Ham 2 Swansea 0
18:00 Cardiff v Norwich
18:00 Everton v Aston Villa
18:00 Fulham v Southampton
18:00 Hull v Tottenham
18:00 Stoke v Man Utd

NEWCASTLE 0 SUNDERLAND 3
BPL2013LOGOKwenyei Dabi ya maeneo ya Tyne-Wear ambayo ni ya 150, Sunderland wameichapa Newcastle Bao 3-0 Uwanjani Saint James Park na hii ni mara ya pili mfululizo Msimu huu kuifunga na hii ni ni mara ya kwanza kufanya hivyo tangu 1967.
Msimu huu, katika Mechi ya kwanza chini ya Gus Poyet kama Meneja mpya, Sunderland waliichapa Newcastle Bao 2-1.
Katika Mechi ya Leo, Fabio Borini ndie alianza kuifungia Sunderland kwa Penati katika Dakika ya 19 baada ya Anita kumuangusha Bardsley.
Bao nyingine za Sunderland zilifungwa na Adam Johnson, Dakika ya 23 na Colback katika Dakika ya 80.
Ushindi huu umeipandisha Sunderland hadi Nafasi ya 12.


WEST HAM 2 SWANSEA CITY 0
Straika wa West Ham Andy Carroll alitengeneza Bao mbili na zote kufungwa na Kevin Nolan lakini alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu ambayo wengi wanahisi haikustahili.
Carroll alipewa Kadi hiyo katika Dakika ya 59 baada kumgusa Chico Flores na mkono wakati wote walipoanguka chini.
Licha ya kucheza Mtu 10, West Ham walijikaza na kulinda Bao zao.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumapili Februari 2
16:30 West Brom v Liverpool
19:00 Arsenal v Crystal Palace
Jumatatu Februari 3
23:00 Man City v Chelsea
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
F
F
GD
PTS
1
Man City
23
17
2
4
68
26
42
53
2
Arsenal
23
16
4
3
45
21
24
52
3
Chelsea
23
15
5
3
43
20
23
50
4
Liverpool
23
14
4
5
57
28
29
46
5
Tottenham
23
13
4
6
30
31
-1
43
6
Everton
23
11
9
3
35
24
11
42
7
Man United
23
12
4
7
38
27
11
40
8
Newcastle
24
11
4
9
32
31
1
37
9
Southampton
23
8
8
7
31
27
4
32
10
Aston Villa
23
7
6
10
26
32
-6
27
11
Swansea
24
6
6
12
29
35
-6
24
12
Sunderland
24
6
6
12
25
36
-11
24
13
Norwich
23
6
6
11
18
35
-17
24
14
Hull
23
6
5
12
22
29
-7
23
15
Crystal Palace
23
7
2
14
15
31
-16
23
16
West Brom
23
4
10
9
27
33
-6
22
17
West Ham
24
5
7
12
24
33
-9
22
18
Stoke
23
5
7
11
22
37
-15
22
19
Fulham
23
6
1
16
22
50
-28
19
20
Cardiff
23
4
6
13
17
40
-23
18

SIMBA SC YAFUFUA MATUMAINI YA UBINGWA, YAILIPUA OLJORO 4-0

Nyamazeni; Tambwe akishangilia bao lake la pili leo
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
SIMBA SC imefufua matumaini ya ubingwa, baada ya leo kuifunga JKT Oljoro ya Arusha mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya Simba SC itemize pointi 30 baada ya kucheza mechi 15, ikiwa nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City pointi 31, Yanga SC pointi 32 na Azam FC pointi 33 kileleni. 
Hadi mapumziko tayari Wekundu wa Msimbazi walikuwa mbele kwa mabao 3-0, matatu akifunga Mrundi Amisi Tambwe na moja kiungo mzalendo, Jonas Mkude.

Mabao yote hayo yalitokana na pasi na kiungo machachari wa pembeni wa timu hiyo, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ ambaye kwa hakika alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa. 
Jonas Mkude alifunga kwa shuti kali la umbali wa mita 20 baada ya kuletewa kwenye himaya yake moja kwa moja mpira wa kona uliopigwa na Messi.
Wachezaji wa Oljoro walijazana kwenye lango lao kumlinda kipa wao Mohamed Ali, lakini Messi akautoa nje kabisa mpira alipokuwa Mkude, ambaye aliunganisha moja kwa moja kwa shuti kali.

La kwanza; Jonas Mkude kulia akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza Tambwe akipongezwa na Awadh Juma kulia na Donald Mosoti kushoto Haroun Chanongo akimuacha chini beki wa JKT Oljoro
Tambwe alifunga bao lake la kwanza leo na la pili kwa Simba SC dakika ya 22 akiunganisha krosi nzuri ya Messi wakati la tatu, alifunga dakika ya 28 baada ya kupata pasi ya kutanguliziwa kutoka kwa winga huyo machachari anayetumia vyema mguu wake wa kushoto.
Kipindi cha pili, Simba SC walirudi na moto wao na kufanikiwa kupata bao la nne dakika ya 52 mfungaji Tambwe tena, safari hii akiunganisha krosi ya Awadh Juma.
Baada ya mabao hayo manne, kocha Mcroatia akawapumzisha wachezaji wake nyota Messi, Amri Kiemba na Tambwe na kuingiza wachezaji wa kwenda kuulinda ushindi huo. 
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, William Lucian ‘Gallas’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Donald Mosoti, Joseph Owino, Jonas Mkude, Haroun Chanongo, Awadh Juma, Amri Kiemba/Uhuru Suleiman dk64, Amisi Tambwe/Abdulhalim Humud na Ramadhani Singano ‘Messi’/Said Ndemla dk55.
JKT Oljoro; Mohamed Ali, Paul Malipesa, Ali, Omar, Nurdin Mohamed, Sabri Makame, Babu Ally, Jacob Masawe, Amir Omar, Shijja Mkina na Majaliwa Mbaga/Shaibu Nayopa dk38.

CHADAMA NDANI YA MOROGORO WAMNADI SELEMANI MSINDI (AFANDE SELE)


Mwenyekiti wa Chama ch Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiwahutubia maelfu ya wakzi wa mji wa Mtibwa katika mkutano wa Operesheni M4C pamoja Daima jana.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akimtambulisha mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Dama, uliofanyika katika Kata ya Tungi mjini Mororgoro jana.

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Afande Sele akiwahutubia wananchi wa Kata ya Tungi mjini Morogoro leo, katika mkutano wa hadhaa wa Operesheni M4C Pamoj Daima. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe alihutubia pia


Baadhi ya wa mji wa Ifakara wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakati wa mkutano wa Operesheni M4C Pamoja Daima, ambao ulihutubiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana. 

HUYU NDIE MWANA DADA MWENYE SEHEMU 2 ZA SIRI


A British woman who's become a celebrity in the U.K. because she was born with two fully formed vaginas may finally be able to cash in on her crotch ...

Her name is Hazel Jones -- and the 27-year-old beauty has been making the media rounds across the pond to discuss "uterus didelphys" ... a condition which caused her to develop 2 sets of female reproductive organs. In other words, two vaginal canals with two openings.

Hazel recently told British tabloid The Sun that she's not shy about her condition -- insisting she and her husband have shown it off at sex clubs around the U.K.

Enter Vivid Entertainment honcho Steve Hirsch ... who heard Hazel's story ... and immediately reached out to the woman with a MASSIVE offer to film her double hoo-hah in action.

In the letter, Hirsch writes, "You are obviously an extraordinary woman and I would like to make you an offer to star in an upcoming Vivid production. We would pay you up to $1 million for your services."

For the mathematically challenged, that's $500k per vagina.

To sweeten the deal, Hirsch says Jones can pick any XXX partner she wants in her movie -- adding, "We would fly you out to L.A. as soon as you are available and provide you with first class accommodations."

ANGALIA HISTORIA YA KOCHA ALIYEIPA SPAIN UBINGWA WA ULAYA ALIYE FARIKI DUNIA LEO HII

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania Luis Aragones amefariki dunia, akiwa na miaka 75, jumamosi ya leo katika clinic moja jijini Madrid, daktari Pedro Guillen amethibitisha.
Kocha huyu atakumbukwa kwa kuiongoza Hispania katika awamu mpya ya mafanikio mnamo mwaka 2008, alipoiwezesha timu hiyo kutwaa kombe la EURO na baada ya hapo alistaafu na kumpisha Del Bosque. Aliifundisha Spain kuanzia mwaka 2004 - 2008.


WASIFU WA ARAGONES


BARCELONA WAKANUSHA KUJARIBU KUMPA MKATABA MPYA VICTOR VALDES ANAYETAKA KUONDOKA CAMP NOU

 


Barcelona wamekanusha madai kwamba wamempa mkataba mpya golikipa Victor Valdes.

Msimu uliopita golikipa huyo wa kihispania alitangaza uamuzi wake wa kuondoka Camp Nou wakati mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.


Lakini Radio Marca ilisema kwamba mabingwa watetezi wa la liga wamejaribu kubadili uamuzi wa kipa huyo mwenye miaka 32 kwa mara ya mwisho.

Taarifa kutoka Barca ilisema: "FC Barcelona inakanusha taarifa iliyotolewa jioni(jana) na radio Marca kuhusu ofa ya mkataba mpya wa Victor Valdes.


“Klabu inaheshimu uamuzi wa mchezaji. Tungependa kuonyesha shukrani, ueledi kwenye suala hili."

Barcelona bado wamekuwa wakihusishwa na magolikipa kadhaa kama wabadala wa Valdes, akiwemo golikipa wa Borussia Monchengladbach Marc Andre ter Stegen.

CHAN 2014: LEO NI FAINALI=GHANA v LIBYA! NA MSHINDI WA 3 NI ZIMBABWE v NIGERIA!!


Jumamosi Februari 1CHAN2014_LOGO
[SAA za Bongo]
[Cape Town Stadium]
1800 MSHINDI WA 3
Zimbabwe v Nigeria  
2100 FAINALI
Libya v Ghana
 
HUKO Afrika Kusini Mjini Cape Town, Ghana na Libya zitakumbana kwenye Fainali ya CHAN 2014 ambayo ni Mashindano ya CAF ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ndani za Nchi zao tu.
Kabla ya Fainali hiyo kwenye Uwanja wa Cape Town itachezwa Mechi ya kusaka Mshindi wa Tatu kati ya Zimbabwe na Nigeria.
Kwenye Fainali, hii itakuwa mara ya tatu kwa Ghana na Libya kupambana kwenye michuano hii na mara ya kwanza ilikuwa Mwaka 2009 kwenye Kundi B na Mwaka huu walikuwa pamoja Kundi C na katika Mechi zote hizo matokeo ni Sare ya 1-1.
 
NJIA KWENDA FAINALI:
GHANA
-Kundi C:
Ghana 1 Congo 0
Ghana 1 Libya 1
Ghana 1 Ethiopia 0
-Robo Fainali
Ghana 1 Congo DR 0
-Nusu Fainali:
Ghana 0 Nigeria 0 [Pia 0-0 Baada Dakika 120, Ghana yashinda Penati 4-1]
LIBYA
-Kundi C:
Libya 2 Ethiopia 0
Libya 1 Ghana 1
Libya 2 Congo 2
-Robo Fainali:
Gabon 1 Libya 1 [Pia 1-1 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 4-2]
-Nusu Fainali:
Zimbabwe 0 Libya 0 [Pia 0-0 Baada Dakika 120, Libya yashinda Penati 5-4]
 
Ghana na Libya ndio Timu pekee kwenye michuano ya safari hii huko Afrika Kusini ambazo hazijaonja kipigo na zote zimetinga Fainali hii kupitia Mikwaju ya Penati kwenye Nusu Fainali zao ambazo zote zilitoka 0-0.
Kwenye Nusu Fainali, Ghana iliitoa Nigeria kwa Penati 4-1 na Libya kuibwaga Zimbabwe Penati 5-4.
Wakati Libya ina Kikosi chao kamili, Ghana itakuwa na upungufu kwa kumkosa Beki wao Kwabena Adusei ambae alitolewa kwa Kadi Nyekundu walipocheza na Nigeria na pia upo wasiwasi wa kumkosa Straika Yahaya Mohammed alieumia Goti kwenye Mechi hiyo hiyo.

MOHAMED MORSI KUFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

 
Mtu akimbeba mtoto wanakimbia kutokana na gesi ya tukowa machozi wakati wa mapambano kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa rais wa zamani  Mohamed Morsi mjini Cairo, Jan. 17, 2014.
Mtu akimbeba mtoto wanakimbia kutokana na gesi ya tukowa machozi wakati wa mapambano kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa rais wa zamani Mohamed Morsi mjini Cairo, Jan. 17, 2014.
Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani  Mohammed Morsi anatarajiwa kufikishwa mahakamani  jumanne  ikiwa  ni moja ya  mashtaka ya uhalifu yanayomkabili kiongozi wa chama cha kiislamu.

Bwana Morsi na zaidi ya wanachama 100 wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood wanakabiliwa na mashtaka kwa kutoroka jela mwaka 2011 na shutuma za kuua polisi wakati wa mapinduzi ambayo yamemuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu  Rais Hosni Mubarak na kumuingiza madarakani bwana Morsi.

Washtakiwa wengi wametambuliwa kuwa ni wanachama wa kundi la wanamgambo wa kipalestina la Hamas, kundi la wanamgambo la Hezbollah lenye makao yake nchini Lebanon na kikosi cha Revolutionary Guard cha Iran.
Morsi na wafuasi wake wakiwa mahakamani Nov. 4, 2013Morsi na wafuasi wake wakiwa mahakamani Nov. 4, 2013
Bwana Morsi na wanachama wengine waandamizi wa kundi la Brotherhood pia wanakabiliwa na mashtaka kwa shutuma za kuchochea mauaji ya waandamanaji wa upizani wakati akiwa madarakani.

Rais huyo wa zamani na watu wengine 35 pia watashtakiwa kwa shutuma za upelelezi kwa kushirikiana  na kundi la wapalestina la Hamas.


Jeshi la Misri lilimuondoa mamlakani bwana Morsi mwezi July mwaka jana. Hosni Mubarak aliondolewa madarakani kufuatia upinzani wa umma ambao ulianza Januari mwaka 2011.
SAUTI YA AMERIKA( VOA)

UPINZANI WATATIZA UCHAGUZI THAILAND

 
Maandamano yanayotatiza mchakato wa uchaguzi Thailand
Waandamanaji nchini Thailand wanazuia usambazaji wa karatasi za kupigia kura siku moja tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu unaosusiwa na upinzani.
Makundi ya waandamanaji wanaopinga serikali yalizingira ofisi moja ya serikali katika mji mkuu wa Bangkok ,ambapo karatasi za kupigia kura katika zaidi ya vituo 100 zimewekwa.
Karatasi kama hizo pia zimezuiliwa katika ngome ya upinzani kusini mwa taifa hilo.
Upinzani unataka kuondolewa kwa kile inachokitaja kama serikali fisadi ya waziri mkuu Yingluck shinawatra ambaye wamekuwa wakidai ni kibaraka wa kakaake mkubwa Thaksini Shinawatra.
Thailand inajiandaa kwa uchaguzi mkuu siku ya Jumapili,licha ya upinzani kuususia na hata kutatiza maandalizi yake. Inaarifiwa huenda bwana Yingluck shinawatra akachaguliwa tena, kitu kinachowaudhi wapinzani.
Mamia ya waandamanaji walipiga kambi katika vituo vya kusambazia karatasi za kupigia kura mjini Bangkok ili kuzuia shughuli ya kusambaza karatasi hizo kabla ya uchaguzi mkuu Jumapili.
Polisi walijitahidi kuwatawanya wafuasi wa serikali na wapinzani baadhi waliokuwa wamejihami kwa vijiti na vyuma huku hali ya taharuki ikitanda mjini Bangkok.

TAARIFA KUFANYA MITIHANI WA KIDATO CHA NNE NA MAARIFA(QT) 2014

Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwakumbusha watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT)  mwezi Novemba,  2014  kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kilichoanza rasmi tarehe 1 Januari, 2014 kwa ada ya Shilingi 50,000/=kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT  kitaishia tarehe 28 Februari, 2014.

Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au Mpesa.

Imetolewa na:

KAIMU KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA.

 

DK.SHEIN AWASILI NCHINI INDIA LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mashada ya mauwa   wakati wa mapokezi nyake alipowasili katika uwanja wa ndege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo mkewe Mama Mwanamwema Shein katika ziara rasmi.[Picha na Ramadhan Othman, India.] TA1A1406 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana  na Kiongozi wa Ulinzi  wakati wa mapokezi  yake alipowasili  katika uwanja wa ndege  wa Jaipur  Nchini India katika Jimbo la Rajastan,akiwa na ujumbe aliofuatana nao akiwemo mkewe  Mama Mwanamwema  Shei.[Picha na Ramadhan Othman, India.]
TA1A1408 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein  wakisalimiana na Viongozi   wakati wa mapokezi  alipowasili katika uwanja wa ndege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,pamoja na   ujumbe  waliofuatana katika ziara rasmi nchini India[Picha na Ramadhan Othman, India.] TA1A1412 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Uhusiano wa Mambo ya Nje Mam Raj Behamni,  mara baada ya mapokezi na Mkewe Mama Mwanamwema Shein  wakilipowasili katika Uwanja wa dege wa Jaipur Nchini India katika Jimbo la Rajastan,pamoja na   ujumbe   katika ziara rasmi nchini India[Picha na Ramadhan Othman, India.]

HII NDIO SHOW YA HADIJA KOPA ALIYO IFANYA JANA MKOANI MBEYA


Malkia wa Taarab nchini Bi. Hadija Kopa akiimba mbele ya umati wa watu kwenye ukumbi maarufu wa City Pub mjni Mbeya.
Baadhi ya wanamuziki wa TOT Taarab wakiimba kwa hamasa wakati band hiyo ya muziki wa taarab ilipotumbuiza kwenye ukumbi wa City Pub mjini Mbeya.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimpongeza bi Hadija Kopa kwa umahiri wake wa kuimba taarab kwenye ukumbi wa City Pub Mbeya.
Umati wa watu ukiwa umefurika wakati Malkia wa Taaarab Hadija Kopa na Band ya Taarab ikitoa burudani kwa wakazi wa Mbeya mjini.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI MWAFUNZI AGONGWA NA GARI

DSC00207

MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA BARABARANI.
GARI AMBALO HALIKUWEZA KUFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA JINA LA DEREVA WAKE LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI KATIKA SHULE YA MSINGI MBUYUNI ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA DAIMA FAIDA (08) MKAZI WA MBUYUNI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. AJALI HIYO ILITOKEA MAJIRA YA SAA 06:55HRS ASUBUHI WILAYANI MBARALI MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI HIYO NI MWENDO KASI, DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEKABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA MAZISHI. JUHUDI ZA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

HOT NEWsssssss MWENYEKITI UVCCM MKOA WA IRINGA ATANGAZA KUJIUZULU

  KISA WAJUMBE KUGOMA KUCHOMEKEA AJENDA YA KUMTEUA MUME WAKE KUWA MJUMBE


                              Tumaini Msowoya  akiwa na meme  wake Frank  Kibiki  wakati wa harusi yao
                     Aliyekuwa mwenyekiti UVCCM mkoa  wa Iringa Tumain Msowoya 
.....................................................................................................................


MWENYEKITI wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa mwanahabari Tumain Msowoya ametishia kujiuzulu nafasi yake hiyo baada ya wajumbe wa baraza kuu la UVCCM mkoa kupinga uamuzi wake wa kuchomoka ajenda ya kumteua mume wake kuziba nafasi tano ambazo anapaswa kuteua kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM. 

 Msowoya alifikia uamuzi huo wa kutangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo jana katika baraza kuu ya UVCCM mkoa lililofanyika katika ukumbi wa CCM mkoa wa Iringa . Kamujibu wa kanuni ya UVCCM ilipaswa ateue wajumbe watano wa baraza la UVCCM mkoa ambapo wajumbe wanne alikwisha teua katika baraza la vijana lililofanyika Desemba 8 mwaka 2012 hivyo kubaki nafasi moja ambapo jana alipaswa kuiziba nafasi hiyo na kumteua mume wake Frank Kibiki aliyekuwa katibu wa UVCCM Iringa vijijini ambae kwa sasa yupo rikizi. Hata hivyo wajumbe walionyesha kuwa na maswali mengi kuliko majibu ya kuhoji hasa ukizingatia katibu wa wilaya ni mjumbe halali wa baraza kuu la mkoa hivyo hapaswi kuteuliwa nafasi nyingine kuwa mjumbe mara mbili hali wanachama wengine wapo . 
 Hivyo wajumbe walihoji sababu ya mwenyekiti wao huyo kuingiza ajenda ya uteuzi wa nafasi hiyo moja ambayo mwanzoni haikuwepo katika ajenda za baraza hilo na kumtaka kusubiri baraza lijalo jambo ambalo ajenga hiyo ingeingizwa na si kuchomekea katika baraza hilo.
 hatua hiyo ilimfanya mwenyekiti huyo kuingiwa na jazba na hivyo kutangaza kujiuzulu nafasi yake huku akitoka nje ya ukumbi na kupelekea kamati ya utekelezaji ya mkoa kumfuata nje ya ukumbi na kumwolekeza kanuni zinasemaje juu ya uteuzi na namna ya ajenda kujulikana kwa wajumbe na baada ya hapo aliingia ndani ya ukumbi na kurejea kauli yake ya kujiuzulu na kutoka kabisa eneo la mkutano kwa hasira huku akisisitiza kuwa hakushinikizwa na mtu kujiuzulu nafasi hiyo bali ni maamuzi yake binafsi . 

Hata hivyo jazba ya mwenyekiti huyo ilitulizwa na wajumbe wa baraza hilo waliopinga uamuzi wake huo. 


“Hatukubaliani na uamuzi aliotaka kuuchukua; hawezi kuucha umoja wa vijana katika kipindi hiki ambacho chama kinaelekea kwenye chaguzi ndogo tatu za udiwani mkoani hapa,” alisema mmoja wa wajumbe katika baraza hilo 


Aidha mjumbe huyo alisema Msowoya hawezi kujiudhulu nafasi yake hiyo kwa jazba kutokana na kile alichokiita ‘majungu’ yanayopikwa na baadhi ya wajumbe wa baraza hilo. “


Kilichopelekea atishie kujiuzulu ni pamoja na majungu yanayopikwa dhidi yake na baadhi ya wajumbe wa baraza hilo; wengi wa wajumbe hawakubaliani wamekataa azma ya mwenyekiti kutaka kujiuzulu na kuwa kufanya hivyo ni kuonyesha ukomavu mdogo wa kisiasa na sawa na kuwa msaliti ndani ya UVCCM na iwapo wangejua basi wangemchagua mgombea mwingine kata ya waliogombea . 


Mwanahabari Tumaini Msowoya alikuwa mwakilishi wa gazeti la Mwananchi mkoani Iringa kabla ya kuhamia gazeti ya Uhuru na Mzalendo mkoa wa Iringa alipata kushinda kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa mkoa wa Iringa Oktoba, 2012.

 Katika uchaguzi huo, jumla ya kura 302 zilipigwa ambapo Msowoya alipata kura 188 akifuatiwa kwa mbali na mwanahabari Abba Ngilangwa aliyepata kura 76 huku Ramadhani Baraza akiambulia kura 36.
 Alipopewa nafasi ya kuwashukuru wajumbe kwa kumpatia ushindi huo, Msowoya alisema anafahamu kazi ngumu aliyoanayo mbele yake ya kuwaangunisha vijana wa mkoa mzima wa Iringa ili kukiletea ushindi chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.
 “Uongozi unapimwa kwa mambo mengi lakini unapokuwa katika siasa sifa kubwa ni kukisaidia chama chako kupata ushindi,” alisema huku akiomba ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wanahabari.
 Katibu wa UVCCM mkoa wa Iringa Alawi Haidar ametibitisha kutangaza kujiuzulu kwa mwenyekiti huyo japo alisema hadi sasa hajapokea barua rasmi kwa mujibu wa kanuni za UVCCM kutokana na kiongozi anapohitaji kujiuzulu ni lazima kuandika barua .

MUENDELEZO WA SHUGHULI ZA MIAKA 37 YA CCM MKOAN MBEYA WAENDELEA VIZURI

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia katika shamba la Mage Kolimwa (wapili kulia), katika Kijiji cha Mlimanyoka, Kata ya Nsalanga, wilala ya Mbeya mjini. Kinana alifika kumsaidia mkulima huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, inayofanyika Kitaifa Jumapili hii mjini Mbeya.  2. Nape akisaidiana na vijana kupanga jukwaa la mapokezi ya matembezi 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisaidiana na vijana kuandaa jukwaa litakalotumika wakati wa mapokezi ya matembezi ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Sokine mjini Mbeya. Matembezi hayo yanaongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete 3. Maandalizi ya halaiki 
Vijana wakiwa kwenye mazoezi ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yatakayofanyika Jumapili hii mjini Mbeya.1 
Vakila vijana wa Chipukizi wakila kiapo cha utii kwa CCM wakati wa mazoezi yao leo asubuhi. 3 

BIASHARA YA NDIZI YASHAMIRI KATIKA SOKO KUU LA MANISPAA YA IRINGA

 
ndindi_2_a5b87.jpg
Wafanya biashara wa Ndizi katika soko hilo wamesema kuwa biashara ya Ndizi inawapa faida kubwa sana kwa kuwa watu wengi wamekuwa wakinunua sana bidhaa hiyo katika kipindi hiki na pia walitaja bei ya mikungu ya Ndizi, mkungu mmoja mkubwa ni sh 16,000/= na mdogo ni sh 14,000/=.
mtu_19a09.jpg
mfanya biashara wa bidhaa hiyo akiwa anapakia minkungu ya ndizi katika mkokoteni tayari kwa kuifanyia biashara katika eneo hilo la soko kuu la manispaa ya Iringa.
ndindi_3_84846.jpg
baadhi ya mikungu ya ndizi ambayo ipo sokoni tayari kwa biashara katika eneo la soko kuu la manispaa ya Iringa.
mkungu_324f3.jpg