MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Monday, 12 August 2013

DIWANI AWEKA TAA ZA BARABARANI NA MBUGE AGAWA KOMPYUTA 28

Moshi — DIWANI wa Longuo B, Raymond Mboya (CHADEMA), amejitolea kuweka taa kwenye barabara za Mtaa wa Kitandu ambao upo karibu na Hospitali ya Rufaa ya KCMC baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi kufanyiwa vitendo vya ubakaji na wizi.

Diwani Mboya alisema alipokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa udaktari wanaosoma KCMC kwenye mkutano alioufanya Juni mwaka huu juu ya kuwapo kwa matukio hayo. Alisema waliweka ulinzi jamii, lakini ilionesha kutozaa matunda hivyo kuamua kuweka nguzo pamoja na taa kwenye barabara ya mtaa huo.

Mmoja wa wananchi wa Mtaa wa Kitandu akizungumza na Tanzania Daima, Alex Mbaga alisema vitendo vya 
wizi vilikuwa vimekithiri kutokana na barabara hizo kutokuwa na taa za barabarani na kuwa na giza, hivyo majambazi kutumia nafasi hiyo kuwaibia watu. Alisema kwananchi waliokuwa wahanga wa matukio hayo ni wanafunzi wanaosoma udaktari kwenye Chuo cha KCMC, wale wa Ushirika (MUCoBS) pamoja na Mwenge ambao wamepanga nje ya vyuo kwenye mtaa huo. (Rodrick Mushi, Moshi — TanzaniaDaima)
---

Mbunge agawa kompyuta 28 jimboni mwake

Babati — MBUNGE wa Jimbo la Babati Vijijini, mkoani Manyara, Vrajilal Jituson kupitia Mfuko wa Ofisi yake ameazimia kutoa kompyuta mpakato 28 kwenye maeneo tofauti ya jimbo lake kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi wa taasisi mbalimbali.

Jituson ambaye ni Mwanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa huo, (MAMEC) alisema alitoa kompyuta mbili mpakato (laptop) kwa ajili ya waandishi wa habari wa mkoa huo, ili waweze kuandika habari za vijijini.

Akizungumza jana mjini Babati, mbele ya Rais wa Muungano wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Keneth Simbaya, mbunge huyo alisema amejitolea kompyuta hizo kwa lengo la kurahisisha teknolojia ya mawasiliano: “Pamoja na kuwapa waandishi wa habari hizo laptop mbili pia tumetoa laptop mbilimbili kwenye vituo vya polisi vya mjini Babati na Magugu ili waweze kusaidia jamii kuandika taarifa zao,” alisema Jituson.

Alisema katika kompyuta hizo 28, amepanga kugawa kompyuta tano kwa kila tarafa ili zipelekwe kwenye shule za sekondari, kwani lengo lake ni kila shule ya sekondari katika kata ipate kompyuta yake.

Kwa upande wake, Simbaya alipongeza hatua ya mbunge huyo kugawa kompyuta hizo kwa waandishi wa habari kwani amekuwa tofauti na wabunge ambao wanawathamini waandishi kwenye kipindi cha uchaguzi pekee. (MWANANCHI)
 


ILANI KWA WANYWAJI WA KINYWAJI CHA CHILLY WILLY NA TATIZO LA MOYO

Picture
Ushauri umetolewa na Meneja Uhusiano wa Super Market ya TSN, Meshack Nzowah, wakati wa promosheni ya kinywaji cha Chilly 
Willy iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo amewataka watu wenye matatizo na maradhi ya moyo kutotumia kinywaji hicho ili kujiepusha na matatizo ambayo yanaweza kuwapata kama wanatumia kinywaji hicho pasipo kujua madhara yake.

Watu wengine ambao hawatakiwi kutumia kinywaji hicho ni watoto walio chini ya miaka 10.

Akizungumza katika hafla hiyo Nzowah alisema Chilly Willy ni kinywaji kisicho na kilevi kinatumika kwa watu mbalimbali na kinaongeza nguvu kwa watumiaji, lakini kwa watu wenye matatizo ya moyo hakiwafai.

Aliongeza kuwa kinywaji hicho kinachotengenezwa Dubai, kinapendwa na watu mbalimbali duniani hususan wanamichezo na kimekuwa kikiwaongezea nguvu.

“Baada ya kuona kinywaji cha Chilly Willy kinatumiwa na watu wengi duniani, tumeamua kukileta Tanzania ili watu waanze kukitumia kwa kweli ni kinywaji bora na kinakata uchovu wa pombe,”alisema Nzowah. ---
source MAJIRA

 

AJARI ILIYOTOKEA KATIKA BASI LA MERIDIAN WAWILI WAFARIKI DUNIA

 
Taarifa via JamiiForums na HabariLeo — Basi la Meridian ililokuwa na abiria 60 likitokea Tarakea, Rombo, mkoani Kilimanjaro kwenda Dar es Salaam lilipata jali jana kwenye eneo la Kimange, Mbwewe, mkoani Pwani na kusababisha vifo vya watu wawili huku wengine 40 wakiachwa na majeraha mbalimbali katika miili yao.

Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha, shirika linalosimamia Hospitali ya Tumbi, Dk Cyprian Mpenda alithibitisha kuwa watu wawili walikufa katika ajali hiyo na kuwataja kuwa ni Gerald Laswai (43) na Musin Mwaliko ambaye umri wake haujafahamika. Aidha, Dk Mpenda alisema katika Hospitali ya Tumbi, walipokea maiti hao wawili na majeruhi 22, mchana jana, ambapo 12 ni wanawake na 10 ni wanaume na majeruhi mmoja kati ya hao, yuko mahututi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema jana kuwa, ajali hiyo ilitokea saa 5.40 asubuhi baada ya dereva aliyefahamika kwa jina moja la Rajab akiendesha basi hilo lenye namba za usajili T956 ABX kushindwa kulihimili gari kutokana na mwendo kasi baada ya kugonga kigingi na gurudumu kupasuka.

Kamanda Matei alisema katika eneo la tukio, hakukuwa na mtu aliyekufa lakini majeruhi walikuwa 40 na watu 20 walitoka wazima. Alisema majeruhi wengine walipelekwa katika Hospitali ya Lugoba na Chalinze.

 
 

Saturday, 10 August 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU SHEIKHE ALIYE CHOMWA KISU AKIENDESHA IBADA YA IDD MKOANI MBEYA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Diwani Athumani

Msikiti wa Ijumaa wa mjini Kyela ambao Shekhe wa msikiti huo alivamiwa na kupigwa wakati wa swala ya Idd leo asubuhi

 

TAARIFA YA JESHI LA POLISI

WILAYA YA KYELA - WATUHUMIWA SITA WADHIBITIWA NA WAUMINI KWA USHIRIKIANO NA MAKACHERO WA POLISI WALIPOTAKA KUANZISHA FUJO.

MNAMO TAREHE 09.08.2013 MAJIRA YA SAA 08:30HRS HUKO ENEO LA BONDENI KATIKA MSIKITI MKUU WA IJUMAA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. NURU S/O MWAFILANGO,MIAKA 77,KYUSA,SHEKHE MKUU WA WILAYA YA  KYELA, MKAZI WA BONDENI  AKIWA ANAONGOZA IBADA YA  SWALA YA IDD EL FITRI  MSIKITINI HAPO ALIVAMIWA NA BAADHI YA  WAUMINI WANAOJIITA WAISLAM WENYE ITIKADI KALI NA KUANZA KUMSHAMBULIA KWA KUTUMIA FIMBO,NONDO,MKASI NGUMI NA MATEKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE. CHANZO NI 
MADAI KUWA HAWAMTAKI SHEKHE HUYO KWA MADAI KUWA HANA UWEZO. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVAMIA MHANGA WAKATI WAUMINI WOTE WAKIWA WAMEINAMA WAKISWALI NA KUANZA KUMSHAMBULIA. MHANGA HAKUPATA MADHARA BAADA YA BAADHI YA WAUMINI WALIOSHIRIKIANA NA POLISI/MAKACHERO WA-KIISLAMU KUMUOKOA.   KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA SITA AMBAO WALIKUWA VINARA WA VURUGU HIZO WAMEKAMATWA AMBAO NI 1.MASHAKA S/O KHASIMU,MIAKA 30,MUHA,MKULIMA MKAZI WA NDANDALO 2. ISSA S/O JUMA, MIAKA 37, MRANGI, MKULIMA,MKAZI WA BONDENI 3.AHMED S/O KHASIMU @ MAGOGO,MIAKA 35,MPOGORO,MKULIMA/MGANGA WA KIENYEJI, MKAZI WA MBUGANI [ALIKUTWA NA MKASI] 4. IBRAHIM S/O SHABAN,MIAKA 17,KYUSA,MWANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI KYELA DAY KIDATO CHA NNE MKAZI WA NDANDALO [ALIKUTWA NA FIMBO KUBWA NA NDIYE ALIYEMNYANG’ANYA SHEKHE KIPAZA SAUTI] 5. AMBOKILE S/O MWANGOSI @ ALLY,MIAKA 19,KYUSA,MWANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI  KYELA DAY KIDATO CHA TATU, MKAZI WA BONDENI [ALIKUTWA NA KIPANDE CHA NONDO] NA 6. SADICK S/O ABDUL, MIAKA 28, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA NDANDALO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WAFIKISHWE MAHAKAMANI. KATIKA TUKIO HILO HAMIS S/O HUSSEIN, MIAKA 50, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA BONDENI ALIPATA MAJERAHA KIDOGOKWA  KUKATWA MKASI  JUU YA  SIKIO LA KUSHOTO WAKATI AKIWA KATIKA HARAKATI ZA KUMUOKOA MHANGA ASIPATE MADHARA  NA AMEPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA. HALI  YA  USALAMA NA AMANI  ILIREJEA MUDA MFUPI NA   WAUMINI WALIENDELEA NA IBADA YAO CHINI YA  UONGOZI WA SHEKHE HUYO NA KUMALIZA SALAMA. HAKUNA UHARIBIFU WA MALI ULIOTOKEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WAUMINI NA JAMII KWA UJUMLA KUTATUA MATATIZO/KERO/MALALAMIKO YAO KWA NJIA YA   KUKAA KWENYE  MEZA YA MAZUNGUMZO BAADA YA   KUYAWASILISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA  ILI KUEPUSHA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANASISITIZA  KUWA KWA YEYOTE ATAKAYEJARIBU /ATAKAYEVUNJA SHERIA HATAFUMBIWA MACHO.

   
Imesainiwa na,

[ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
 
 Mbeya — WAUMINI wa dini ya Kiislamu waliokuwa katika ibada ya Swala ya Idd El Fitri katika msikiti mkuu wa Ijumaa uliopo Wilayani Kyela mkoani Mbeya wamekumbwa na taharuki baada ya Shekhe wao aliyekuwa akiongoza ibada kuvamiwa kibla wakati akiendesha ibada na kujeruhiwa.

Tukio hilo la aina yake limetokea majira ya asubuhi ambapo Shekhe huyo aliyetambuliwa kwa jina la Nuhu Mwafilango alishambuliwa akiwa katikati ya sijida baada ya mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Kyela, Ally Mwangosi kuchoma Shekhe huyo na kitu chenye ncha kali.

Taarifa kutoka msikitini hapo zinadai kuwa mara baada ya tukio hilo, Shekhe alipiga kelele wa kuomba msaada na ndipo waumini waliokuwa wakiswali msikitini hapo waliposhikwa na taharuki.

Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Waislamu Wilayani Kyela Bw. Daudi Mwenda alisema kuwa waumini walimuokoa na kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Bw. Mwenda alisema kuwa Shekhe huyo ameumizwa vibaya kichwani na kutokwa na damu nyingi. Waumini wawili waliojaribu kumuokoa Shekhe huyo nao walijeruhiwa kwa kuchomwa na kisu ikiwa ni pamoja na mweka hazina wa BAKWATA wilaya Ustadhi Khamis Hussein ambaye alijeruhiwa kichwani na sikioni.

Nao baadhi ya waumini waliokuwepo katika ibada hiyo walisema kuwa tukio hilo lilitokea wakati waumini wote wakiwa wamesujudu, ndipo waliposikia kelele na vurugu.

Mmoja wa waumini aliyejitambulisha kwa jina la Idd Hussein alisema kuwa liliibuka kundi la watu waliomsaidia kijana huyo, na kuibua vurugu kubwa iliyosababisha ibada ya swala ya Idd kuvunjika.

Akizungumzia tukio hilo Katibu wa BAKWATA mkoa wa Mbeya Shekhe Juma Killah alisema kuwa vurugu hizo zimetokea katika swala ya Idd na wahusika wa vurugu hizo ni  Waislamu ambao...   Read more

Wednesday, 7 August 2013

ANGARIA PICHA ZA UWANJA WA NDEGE JOMOKENYATA ULIVYO UNGUA MOTO NA CHANZO CHA MOTO HUO



JKIAPicture
  Moto ukiwaka JKIA Agosti 7, 2013. Picha/HISANI 
Imepakiwa - Wednesday, August 7  2013 at 

Wazimamoto kutoka KDF, Kaunti ya Nairobi na Kampuni za kibinafsi walifanikiwa kuzima moto huo baada ya masaa karibu manne. Chanzo chake bado hakijabainika.
Rais Uhuru Kenyatta alizuru eneo la mkasa mwendo wa saa tatu asubuhi lakini akaondoka bila kusema lolote.

Katibu wa Wizara ya Masuala ya Ndani Mutea Iringo amewashauri waliopanga kusafiri kupitia uwanja wa huo kuwasiliana na mashirika ya ndege husika.
Shirika la Msalaba mwekundu lilisema mfanyakazi mmoja wa shirika la ndege la Kenya Airways na abiria wameathiriwa na moshi na kukimbizwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi wa kimatibabu.


Mkasa huo umetokea siku moja tu baada ya shughuli kutatizika kutokana na kukosekana kwa mafuta ya ndege jambo lililopelekea safari nyingi kukatizwa na ndege kulazimika kutua viwanja vingine jirani.
Waziri wa Uchukuzi Michael Kamau alisema ni mapema sana kusema uwanja huo utafunguliwa lini.
“Siwezi kusema uwanja wa JKIA utafunguliwa tena lini. Ni mapema sana. Chanzo cha moto hakijajulikana. Uchunguzi unaendelea,” akasema.
Bw Kamau aliwataka watu wasifunge safari kuelekea uwanja huo wa ndege ila tu vikosi vya kutoa huduma za dharura na wazimamoto.

Usalama
Waziri wa Usalama Joseph ole Lenku alisema usalama umeimarishwa na kuwataka wananchi na wageni wasiwe na wasiwasi.
“Mnaweza kuona vikosi vilivyofika hapa, ardhini na angani kuhakikisha eneo ni salama na anga pia. Hili linafaa kutosheleza Wakenya na wageni kwamba usalama wao unahakikishwa.  Hatukusudii kuufunga muda mrefu lakini lazima tuhakikishe usalama. Tunaelewa umuhimu wa uwanja huu kwa taifa.


“Tunazima moto na pia kupunguza hasara kuhakikisha hauathiri uchumi sana.”
Afisa Mkuu Mtendaji wa Kenya Airways kupitia taarifa kwa vyombo vya habari alisema abiria wote wa shirika hilo wako salama.
“Tungependa kuwajulisha wateja na wadau kwamba abiria waliokuwa wakiwasili JKIA na waliokuwa wakiondoka wako salama,” akasema.


Alieleza kuwa ni dhahiri kwamba shughuli zitatatizika lakini akasema maelezo mengi yatatolewa baadaye.
Ndege tano za shirika hilo zilizopangiwa kutua JKIA zimehamishiwa uwanja wa ndege wa Moi, Mombasa na wale waliokuwa safarini kuelekea viwanja vingine kupitia Nairobi wamepelekwa mahotelini.
Ndege zilizoelekezwa Mombasa ni KQ117, KQ331, KQ311, KQ863 na KQ203.

swahilihubblog
Imepakiwa - Wednesday, August 7  2013 at

MAHAKAMA YAMUACHIA HURU MKENYA ALIYETUHUMIWA KUMTEKA DK ULIMBOKA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imemwacha huru Raia wa Kenya, Joshua Muhindi (22) aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kumteka na kujaribu kumwua Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Stephen Ulimboka.

Hata hivyo, baada ya kuachwa jana, muda mfupi baadaye alikamatwa tena na kusomewa mashitaka ya kutoa taarifa za uongo kwa Ofisa wa Jeshi la Polisi.

Muhindi aliachwa na Hakimu Waliarwande Lema baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) kuwasilisha hati ya kufuta kesi hiyo kwa kuwa hana haja ya kuendelea nayo.

Alikamatwa tena, na saa 6.15 mchana akapandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Aloyce Katemana na kusomewa mashitaka mapya.

Katika mahitaka hayo mapya, Wakili wa Serikali Tumaini Kweka alidai kuwa Julai 3 mwaka jana katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, Muhindi alitoa taarifa za uongo Polisi, kuwa yeye na wenzake ambao hawajulikani, walikodishwa kumteka na kumwua Dk Ulimboka jambo ambalo si kweli.

Mshitakiwa huyo alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashitaka kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo
 umekamilika na kuomba tarehe ya kutajwa kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali.

Muhindi aliiomba Mahakama impe dhamana, kwa kuwa ana wadhamini, hata hivyo upande wa mashitaka ulipinga ombi hilo ukidai ni kutokana na usalama wake kwa kwa kuzingatia mazingira ya kesi hiyo na maslahi ya umma.

Aidha, Wakili Kweka alidai kuwa mshitakiwa si raia wa Tanzania pia hana makazi maalumu hivyo itakuwa vigumu kumpata. Hata hivyo, Muhindi alidai kuwa ameshakaa rumande tangu mwaka jana na kitendo cha kumrudisha gerezani ni kujaribu kumpoteza ili kutuliza umma na Bunge na kudai endapo atarudi gerezani, atagoma kula na ataandamana.

"Hawa watu wanataka kunipoteza mimi kijana mdogo wa miaka 22 na mashitaka yanayonikabili si ya kweli, naumia sana Mheshimiwa" alidai Muhindi mbele ya Hakimu.

Hakimu Katemana alisema kama upande wa mashitaka unataka kupinga dhamana uwasilishe hati mahakamani kabla ya saa 7.30 mchana jana, lakini ulishindwa kufanya hivyo.

Muhindi aliachiwa kwa dhamana ya wadhamini wawili, mmoja akifanya kazi katika taasisi inayojulikana ambapo walisaini hati ya Sh milioni tano na yeye kusaini ya Sh milioni tano na kuwasilisha pasipoti yake.

Kesi itatajwa Agosti 20. Mara ya kwanza Muhindi alifikishwa mahakamani hapo Julai 13, mwaka jana akidaiwa kuwa Juni 26 mwaka huo, katika eneo la Leaders Club, alimteka Dk Ulimboka.

Katika mashitaka mengine, ilidaiwa kuwa siku hiyo hiyo, akiwa eneo la Msitu wa Mabwepande, Dar es Salaam, kinyume cha sheria alijaribu kumsababishia kifo Dk Ulimboka, alikana mashitaka hayo.

Rejea: HabariLeo

 

KICHANGA CHAZALIWA NA JINSIA MBILI TOFAUTI

 

 
Mganga mfawidhi wa Hospitali ta Wilaya ya Tunduru Dkt. Joseph Ng'ombo akimuangalia mtoto huyo aliyezaliwa akiwa hana macho, pua na Shavu linalo shika mdomo wa juu, kushoto ni mkunga wa zamu katika Hospital hiyo Rukia Nguo akiwa akiwa amekishika kichanga
Huu ndiyo muunekano wa kichanga hiki usoni.

Mkono wa mkunga huyo ukionyesha maungo ya kichanga hicho kilichozaliwa kikiwa na sehemu nyeti mbili ikiwepo ya kiume kwa juu na ya kike kwa chini.
----------------------------------------------
Na Steven Augustino, Tunduru
 
MAJONZI na Simanzi zilitawala kwa wanafamilia na Wauguzi katika hosipitali ya Wilaya ya Tunduru baada ya ndugu yao mkazi wa Kijiji cha Kadewele Mjini hapa aliyetambuliwa kwa jina la Rehema Safi (42) kujifungua Mtoto wa ajabu mbaye pamoja miongoni mwa maajabu hayo nipamoja na kuzaliwa akiwa na Jinsia Mbili.

Aidha Kichanga hicho ambacho kimezaliwa kikiwa na uzito wa kilo 1.8 pia kimezaliwa kikiwa hakina Pua,macho na Shavu ambalo hushikilia mdomo wa juu.  

Tukio hilo ambalo lilisababisha mshtuko na taaharuki kwa wataalamu wanaotoa huduma ya kiafya limetokea katika Hospitali ya serikali ya Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma Agosti 5 mwaka huu.

Mkunga wa zamu katika Wodi ya wazazi iliyopo katika hospitali hiyo Rukia Nguo alisema kuwa pamoja na uzowefu wake wa muda mrefu katika kada hiyo hajawahi kuona kiumbe cha aina hiyo.

Alisema baada ya tukio alilazimika kuwaita waganga na wauguzi wenzake ili wamsaidie kutazama kichanga hicho ili kujiridhisha juu ya tukio hilo akidai kuwa awali akiwa peke yake akishindwa kukitambua kiumbe hicho kama ni binabamu ama la ingawa kilionekana kuwa na viungo vingine vya kibinadamu.

Kufuatia hali hiyo Mkunga huyo akatoa wito kwa wanawake wenzake kuachana na tabia ya kutumia dawa za kienyeji na badala yake waende hospital kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa maafisa tabibu.
“unajua sisi wanawake wengi tumekuwa na tabia ya kuchukua na kuanza kuzitumia dawa kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki “ alisema Nguo na kuongeza kuwa matumizi ya dawa za aina hiyo zinaweza kusababisha madhara makubwa yakiwemo yanayo sababisha kuzaliwa kwa watoto wenye upungufu wa viungo.    

Akizungumza kwa unyonge juu ya tukio hilo mama mzazi wa Mtoto hoyo ambaye hadi sasa hajapatiwa jina, Reheme Safi ambaye uzazi huo ni wa tano alisema kuwa hana budi kulipokea tukio hilo kama changamoto ya maisha kwani mtoaji nimungu na kwa hatua hiyo hawezi kubishana na uumbaji huo.

  ukilinganisha na tukio la Kutunza mimba ya Mtoto kwa Miezi 9 huku ukiwa na matumaini ya kupata mtoto atakaye kusaidia maishani,sijisikii vizuri kupata Mtoto wa aina hii lakini sinanjia ya kuyabadilisha matokeo hayo “ alisema Reheme na kuongeza kuwa yeye anamuachia mungu juu uumbaji huo.

Akizungumzia histolia ya jinsi ulivyo patikana ujauzito huo alisema kuwa kwanza yeye hakutarajia kuupata kwavile kwa zaidi ya miaka miwli alikuwa akitumia Dawa za uzazi wa Mpango aina ya (DEPO PROVELA) ya sindano ambayo wanawake wengi wanaopanga uzazi huitumia kwa kuchoma sindao moja kila baada ya miezi mitatu.

Alisema akiwa katika hali hiyo ghafla alishangaa kuona tumbo lake linakuwa zito na baadae kitu kikaanza kucheza tumboni na alipokwenda hospitali na kupimwa alishangaa kuelezwa kuwa huo ni ujauzito na kinachocheza ni Mtoto.

Mganga Mfawidhi wa hospitali ya serikali ya Wilaya ya Dkt. Joseph Ng’omboa amedhibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa maafisa tabibu wanaendelea kufanya utafiti wa chanzo cha tukio hilo kwa kumpima mama huyo kama ana magonjwa ya kuambukiza ama la.

Alisema mtoto kuzaliwa akiwa katika hali hiyo kunaweza kusababishwa na mambo mengi yakiwemo magonjwa ya zinaa, kukosekana kwa virutubisho Fulani wakati wa uumbwaji wa viungo mwilini ama mama mzazi kutumia madawa wakati akiwa na mimba changa.

Aidha Dkt. Ng’ombo pia akatumia nafasi hiyo kuwahamasisha akina mama wajawazito kuhudhulia Kliniki katika kipindi chote baada ya kupata ujauzito na kwenda kujifungulia hospitali kwa ajili ya kupata msaada wa maafisa tabibu wakati wote.  
Habari kwa hisani ya Demashonews.blogspot.com

WAZAZI WAKATAZA WALIMU KUWAFUNDISHA WATOTO MBINU ZA KUJIKINGA NA VVU/UKIMWI

PictureMsimamizi wa mradi, M. Herman akitoa maelezo
Imeelezwa kuwa Baadhi ya wazazi na walezi wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamekuwa wakiwazuia walimu kutoa elimu ya njia ya kujikinga na ukimwi kwa watoto wao wa sule za msingi ikiwemo matumizi sahihi ya condom.

Hayo yamebainika leo katika semina iliyoandaliwa na shirika la UNESCO iliyojumisha wakuu wa shule za msingi na sekondari pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali iliyofanyika katika ukumbi wa Golden Valley Mjini Kahama.

Akichangia hoja katika semina hiyo Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Korogwe Bi Ashura Rugakingira amesema kuwa wamekutana na tatizo hilo toka kwa baadhi wazazi hao licha ya kuwa somo hilo lipo katika mtaala wa Serikali.

Rugakingira amesema kuwa changamoto hiyo inawafanya walimu wengi kukata tamaa ya kutoa elimu hiyo ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa wanafunzi hao.

Awali akifungua semina hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ushetu Bi Isabela Chilumba amewataka walimu hao kuvunja ukimya na kuwa wawazi kuzungumza na wanafunzi wao kuhusu Maambukizi ya virusi vya ukimwi na UKIMWI.

Sambamba na hayo Chilumba ametoa angalizo kwa wananchi kutodanganyika na takwimu za maandishi zinazotolewa na kwamba kila mtu awe mstari wa mbele kupima afya yake mwenyewe.

Naye Msimamizi wa mradi huo wa Elimu ya Afya ya UKIMWI, uzazi na maadili kwa vijana kutoka UNESCO Mathius Herman amesema lengo la mradi huo ni kujenga mahusiano rasmi kati ya Mashirika yasiyo ya serikali na shule.

--- Imeandikwa na William B via, KB blog

Picture
Washiriki

Tuesday, 6 August 2013

MAKADA WA CHADEMA WAFUTIWA SHTAKA LA UGAIDI

 
KWA mara nyingine Mahakama Kuu, imetupilia mbali mashtaka ya ugaidi yaliyofunguliwa dhidi ya viongozi na wananchama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
 
Jana, Mahakama Kuu Kanda ya Tabora iliwafutia shtaka la ugaidi wanachama watano wa CHADEMA ikisema kosa lao ni la jinai na halipaswi kuitwa la ugaidi.
 
Katika uamuzi wake, Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Simon Lukelelwa, aliwaonya waendesha mashtaka kuacha tabia ya kutumia maneno makali ya ugaidi katika kesi za jinai, hatua aliyosema inaogofya wageni wanaotarajia kuja Tanzania.
 

“Suala hili la ugaidi kwa siku za hivi karibuni limeshika kasi, linazungumzwa kwa mapana ndani na nje ya nchi, lakini inavyoonyesha mazungumzo hayo hayajaeleweka undani wa madhara yake. Nchi ikiwa imekithiri kwa ugaidi kama inavyodaiwa vitu vingi vingeathirika, uchumi, utalii na mambo mengine.
 

“Ni vizuri mambo haya yakapewa nafasi yake na kwa umakini mkubwa, yasije yakaleta madhara kwa nchi pasipo ulazima wowote. Hata neno ugaidi tafsiri yake haijajulikana vizuri, kila mtu anatafsiri zake. 

Mtu unayemuona ni gaidi, anaweza kuwa mpigania uhuru kwa mwingine,” alisema Jaji Lukelelwa.
 
Hii ni mara ya pili kwa Mahakama Kuu kufuta mashtaka kama hayo kwa viongozi wa CHADEMA ambapo Mei 8, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilimfutia mashtaka matatu ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Lwakatare.


Jaji Lawrance Kaduri alitoa uamuzi huo akisema ulitokana na kukubaliana na hoja ya mawakili wa Lwakatare, Tundu Lissu, Peter Kibatara na Mabere Marando.
 
Makada hao wa CHADEMA waliofutiwa shtaka hilo la ugaidi jana mkoani Tabora ni Henry John Kilewo, ambaye ni Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Kinondoni, Evodius Justinian, Oscar Kaijage, Rajabu Daniel na Seif Magesa Kabuta.
 

Vijana hao walipandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Igunga na kusomewa mashtaka mawili, moja la ugaidi na lingine la jinai.
 

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mawakili wao, Peter Kibatala na Profesa Abdallah Safari walipambana kuwanusuru na mashtaka hayo.
Mawakili hao walihoji uhalali wa mashtaka hayo, wakidai kuwa hakuna vigezo vya kutosha kuonyesha kuwa kuna ugaidi, huku pia wakihoji utaratibu wa kuwafungulia mashtaka katika mahakama hiyo badala ya kule walikokamatiwa.
 
Hivyo, waliiomba Mahakama Kuu ama iwafutie mashtaka hayo au iamuru kila mshtakiwa arudishwe na kushtakiwa katika mahakama za mahali walikokamatiwa.
Katika uamuzi wake, Jaji Lukelelwa aliongeza kuwa sheria za makosa ya jinai zipo wazi na zinaelekeza na kufafanua makosa na mashtaka yanayoweza kufunguliwa kwa wananchi wanaokwenda kinyume cha sheria zilizotungwa.
 

Jaji aliamru watuhumiwa hao warejeshwe wilaya ya Igunga walikotenda makaosa yao na wafunguliwe shtaka la kufanya matendo ya kusababisha madhara makubwa mwilini kwa kuzingatia sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
 
Aliongeza kuwa hakimu atakayesikiliza shauri hilo awape dhamana kwa kutoa masharti atakayoona yeye yanalingana na shtaka linalowakabili watuhumiwa.
Wakili wa washtakiwa hao, Peter Kibatala, akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama na kumshukuru jaji kwa kupitia marejeo yao waliyoomba na kuyatolea maamuzi.
 

Awali wananchama hao watao wa CHADEMA kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini walikuwa wanatuhumiwa kwa makosa mawili likiwemo la ugaidi kwamba walimteka na kummwagia tindikali raia mkazi wa mjini Igunga.
 

Katika shtaka la kwanza walishtakiwa chini ya Sheria ya Kuzuia Ugaidi, wakidaiwa kumteka kwa nia ya ugaidi Mussa Tesha huko Igunga, Tabora na la pili wanashtakiwa chini ya Sheria ya Kanuni za Adhabu wakidaiwa kumdhuru Tesha kwa kummwagia tindikali.
Walidaiwa kutenda makosa hayo mwaka 2011, wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga.
 
Upande wa mashtaka uliongozwa na wakili wa serikali, Juma Masanja, akisaidiana na wakili mwingine wa serikali, Idelfonce Mukandara, waliodai mashtaka hayo ni halali

 Tanzania daima gazeti
.na Thomas Murugwa, Tabora

BAADA YA KUTEULIWA KWA MSAJILI MPYA WA NYAMA WAPINZANI WASEMA NENO;;;;;;;




JAJI wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Francis Mutungi, ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Taarifa ya uteuzi huo iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ilisema kuwa uteuzi huo ulianza Agosti 2, mwaka huu.
Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.
Uteuzi huo unamfanya Jaji Mutungi kuwa msajili wa tatu tangu kurejeshwa tena mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.
Aliyekuwa wa kwanza kukalia ofisi hiyo ya msajili ni Jaji mstaafu, George Liundi, kisha akafuatiwa na Tendwa, ambaye amerithiwa na Jaji Mutungi.
Jaji huyo aliwahi kuwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
 
Wapinzani wasifu
Kufuatia uteuzi huo mpya, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa Tendwa alipaswa kuwa ameondoka ofisini tangu mwaka 2008 alipofikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Tarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya chama hicho imesema kuwa Tendwa alitumia muda huo wa miezi kadhaa alipoongezewa mkataba kuropoka na kuharibu demokrasia kwa manufaa ya Rais Kikwete na CCM.
CHADEMA iliongeza kuwa kutokana na mwenendo wake mbovu, chama hicho kilitangaza kutokumpatia ushirikiano wowote kwa vile alikuwa adui wa demokrasia nchini.
“Kwa muda wote huo, CHADEMA ilikuwa ikitoa ushirikiano kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Badala ya kuifuta CHADEMA na kufanikisha dhamira ovu ya kuharibu amani ya nchi, ameondoka yeye,” ilisema taarifa ya 

CHADEMA.
CHADEMA ilisema kuwa wanamkaribisha Jaji Mutungi kwenye kazi na majukumu yake mapya. Kwamba, wapenda demokrasia na maendeleo nchini wanamtarajia atatimiza wajibu wake kwa kuzingatia haki, sheria na utawala bora, asije akapita njia ya Tendwa.

“Kupitia mchakato wa Katiba mpya unaojadiliwa sasa hivi, CHADEMA tunapendekeza Ofisi ya Msajili ipewe uhuru zaidi na uteuzi wake usiwe suala la rais kuamka tu na kuamua kuteua bila wahusika kuomba, kuchujwa na kuthibitishwa na mamlaka nyingine tofauti na iliyoteua,” walisema.
Jaji Mutungi, anapaswa kuonesha kwa maneno na vitendo kwamba hatakuwa kama Tendwa, kwa kuanza kushughulikia matendo ya kiharamia yaliyofanywa na Green Guards wa CCM kwenye chaguzi za madiwani zilizomalizika hivi karibuni.
Naibu Mkurugenzi wa Uenezi na Haki za Binadamu wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya, alisema ni jambo zuri ingawa aliyemteua vilevile ni Mwenyekiti wa CCM, hatua ambayo inaleta hofu kidogo.
“Tunadhani ni mtu mweledi, sisi hatupigi ramli kuhusu utendaji wake, mpaka tutakapomwona akianza kazi. Wakati wa Tendwa tumefanya kazi katika mazingira magumu, hasa sisi wapinzani, tunaomba huyu asifuate hayo. 

Tendwa aliiogopa sana CCM,” alisema.
Naye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Sam Ruhuza, alisema wanamtakia kila jema Tendwa na kumkaribisha kwa furaha Jaji Mutungi, japokuwa wateule wote huwa wanafanya kazi ya kumpendeza aliyewateua.

TENGA ASHUKURU KUSAJILIWA KWA KATIBA YA TFF

TengawaTFF 1a5bdRais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amemshukuru Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo nchini kwa kusajili Katiba ya TFF toleo la 2013 kutokana na marekebisho yaliyofanywa na Mkutano Mkuu Maalumu uliofanyika Julai 13 mwaka huu.

POLISI MKOANI KIGOMA WAKAMATA SILAHA ZA KIVITA


Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma Frasser Kashai akiwaonesha waandishi wa habari, Moja ya silaha ya kivita aina ya SMG iliyotelekezwa na wahalifu baada ya kukurupushwa na polisi.


Silaha mbili za kivita aina ya SMG zilizokamatwa na polisi baada ya watuhumiwa walikuwa wakizimiliki kinyume cha sheria na kuzitumia kwa uhalifu, kukimbia na kuzitelekeza baada ya kuwaona polisi katika wilaya ya Kibondo.

TASO YAGOMEA SERIKALI KUAHIRISHA SHEREHE ZA NANENANE KUPISHA SIKUKUU YA IDDI.


Mwenyekiti wa TASO Kanda ya nyanda za juu Kusini Kepten mstaafu Nkoswe 
Siku chache zikiwa zimebaki ili kufikia kilele cha maadhimisho ya s kumeibuka mgongano  baina ya Chama cha wakulima (TASO)na serikali kuhusu maadhimisho hayo yafanyike Agosti 7au 8, mwaka huu.

Mgongano huo umekuja baada ya serikali kutaka maadhimisho hayo yafanyike  Agosti  7 mwaka huu huku chama cha wakulima kikiweka msimamo wake wa kusherehekea  maadhimisho hayo agosti,  8 mwaka huu .

Akizungumza jijini Mbeya katika viwanja vya John Mwakangale Mwenyekiti wa Chama cha wakulima (TASO) kanda ya nyanda za juu kusini,Kapten Mstaafu Noel Nkoswe wakati wa majumuisho na waandishi wa habari baada ya kuibuka vuta nikuvute  na serikali  kuhusu kilelele cha maadhimisho hayo ya wakulima.

Kapten Nkoswe amesema kuwa wao kama chama cha wakulima msimamo  wao upo pale pale wa sherehe hiyo  ya wakulima kufanyika Agosti 8 mwaka huu kama ilivyopangwa kila mwaka.

Amesema Wakulima wao  lazima l washerekee sikukuu yao kama kawaida  hivyo mpango wa kubadilisha tarehe  haupo ambapo chama hicho kwa msimao wake kitafanya   tarehe 8 na zawadi za wakulima kutolewa   agosti 8 kama ilivyo pangwa.

        Kapten mstaafu Nkoswe  amesema mwenyekiti wa TASO taifa aliyemtaja kwa jina moja amemwelekeza kuwa maadhimisho ya kilele cha sikukuu hiyo yatafanyika kitaifa katika kanda ya kati Dodoma Agosti 7 mwaka huu ambapo katika kanda zingine zitafanya kama kawaida Agosti 8 mwaka huu.

Hata hivyo  kwa upande wake Mkuu wa Mkoa  wa Iringa Dkt.Christine Ishengoma amesema kuwa wamepokea barua ya serikali inayotaarifu sherehe za kilele cha nane nane zifanyike Agosti 7 mwaka huu kutokana na sikukuu ya Idd kuwa agosti 8 mwaka huu .

Hata hivyo katika barua iliyotumwa na wizara ya kilimo chakula na ushirika yenye kumbu kumbu namba AE 18/196/01 ya julai 30 mwaka huu  kwenda kwa waziri wa nchi sera uratibu na bunge ofisi ya waziri mkuu iliyoandikwa  na waziri wa kilimo na chakula Eng Christopher Chiza  na nakala kwa wakuu wa mikoa yote minne ya kanda ya nyanda za juu kusini.

Aidha nakala ya barua hyo iliyotumwa kwa katibu mtendaji Taifa  imesema kuwa  sherehe za kilele cha nane  nane  imeamliwa zifanyike Agosti 7 mwaka huu  kutokana na mwingiliano wa sikukuu ya Idd ambapo Waziri wa nchi Mh.William Lukuvi  atakuwa mgeni rasmi katika sherehe  hizo.

NA mbeya Yetu Blog

MAFUTA YAOK NAVIKING NI SALAMA SERIKALI YA ZANZIBAR IMESAEMA

Hafsa Golo na Asya Hassan — SERIKALI imesema mafuta ya kupikia ya OKI na Viking yako salama kwa matumizi ya binadamu.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, alisema Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi imefanya uchunguzi wa kina na kugundua kuwa mafuta hayo hayana tatizo na yanafaa kwa matumizi ya binadamu.

Alisema tangazo lililotolewa na Mamlaka ya Viwango Tanzania (TBS) kuwa mafuta hayo hayafai ni miongoni mwa mikakati ya kuua soko la wafanyabiashara wa Zanzibar.

Alisema baada ya uchunguzi huo alizungumza na Waziri wa Biashara wa Tanzania Bara na kumpa uthibitisho wa matokeo ya uchunguzi.

Alikuwa akijibu hoja mbali mbali za Wawakilishi baada ya kujadili na kuichangia bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/2014.

Kuhusu matumizi ya nembo ya TBS, alisema mamlaka hiyo inashindwa kudhibiti nembo yake hali
inayosababisha wafanyabiashara kuitumia vibaya hata kwa bidhaa zilizopitwa na wakati.

Aidha alisema TBS inakiuka sheria na taratibu huku ikikubali kutumiwa katika kudhoofisha biashara za Zanzibar kwa kuwalinda baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi binafsi huku wananchi wakiathirika na vyakula vilivyopitwa na muda.

Sambamba na hayo alikiri kwamba kuna baadhi ya wafanyabiashara wadanganyifu ambao wanaingiza bidhaa zisizo na kiwango na kughushi nembo.

Katika kupambana na wafanyabiashara hao, alisema wizara imekusudia kuongeza kikundi kazi cha kufuatilia kwa kina na kuhakikisha wanadhibitiwa.

Aidha alisema mradi wa kiwanda cha maziwa cha kampuni ya Azam una umuhimu mkubwa katika taifa ambapo utawezesha kutoa fursa mbali mbali za ajira nchini na kuinua ya uchumi wa wafugaji.

"Muekezaji huyu ana malengo mazuri hivyo ni vyema tukampa mashirikiano aweze kufikia dhamira ya kuleta maendeleo nchini, ikiwa mataifa mengine yanamuhitaji," alifahamisha.

Kuhusu kiwanda cha sukari Mahonda, Mazrui alisema kiwanda hicho kipo katika hatua zuri na mwishoni mwa mwaka huu kitaanza uzalishaji wa sukari.

Akizungumzia mzozo baina ya kiwanda hicho na wakulima wa mpunga katika mashamba yanayomilikiwa na kiwanda, alisema hana taarifa lakini aliahidi kufuatilia kwa kushirikana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya
Kaskazini ‘B’.

Nae Naibu Waziri, Thuwaiba Edington Kisasi alisema wizara ina lengo ya kurudisha maonesho ya biashara ili kuitangaza Zanzibar kibiashara.

Alisema serikali imetenga eneo katika kijiji cha Dimani na kinachofanywa ni kuboresha miundombinu ya barabara na huduma za maji na umeme.

Bajeti ya wizara hiyo ilipitishwa juzi.

--- Rejea ya habari: ZanziNews.com
 

 

MZEE APORWA ARDHI NA MAAFISA WA ARDHI WILAYANI BUNDA

 MZEE mmoja (80) Benedicto Marwa mkazi wa Kitongoji cha Mashine ya maji kata ya Bunda Stoo mjini Bunda Mkoani Mara amelalamika nyumba zake kubomolewa na kutishiwa kupelekwa polisi kwa kudai fidia ya mali zake kutoka kwa idara ya ardhi wilayani Bunda licha ya ofisi ya Waziri Mkuu kutoa barua ya kufatilia suala lake lakini imekuwa kimya.
 
Akitoa malalamiko yake hivi karibuni kwa Waandishi wa Habari Mjini Bunda,Marwa alidai licha ya kuwasilisha malalamiko yake kwa wakati tofauti katika ofisi mbalimbali za serikali bado maofisa wa aridhi waliovamia maeneo yake wameendelea kuyashikilia huku wakiwa wamejenga nyumba zao na kukahidi maelekezo yaliyotolewa.
 
Alitaja ofisi alizowahi kuwasilisha kero zake kuwa pamoja na  Ofisi ya mkuu wilaya ya Bunda, Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara, Baraza la ardhi, nyumba na Makazi mkoani Mara na Kamishna ya Ardhi Wizarani lakini bado maamuzi hayafanyiwi kazi huku akiendelea kuangaika kuitafuta haki yake ya kurudishiwa maeneo.
 
Akionesha vielelezo  kwa Wandishi wa Habari, alisema Mahakama ya Ardhi, Nyumba na Makazi ya wilaya ya Musoma  mkoani Mara ilihukumu kesi hiyo MISC Application No.85 ya mwaka 2010, kwa kutoa siku 30 kwa maofisa wa ardhi kumrejeshea eneo lake katika Kitongoji cha mashine ya maji mjini humo.
 
Alisema agizo lilitolewa Novemba 5, 2010 ambapo Kampuni ya UBAPA LTD and Tribunal Broker ilitakiwa  kubomoa nyumba zilizojengwa katika eneo lake lakini anashangazwa na kampuni kuendelea kuwa na kigugumizi cha kutekeleza agizo lililotolewa huku akidai huenda kampuni hiyo inashindwa kufanya hivyo kwa kuwa inategemea kazi nyingi kutoka katika idara ya ardhi ya Bunda.
 
Vielelezo vimebaini kuwa hiyo ni hukumu ya pili ambapo hukumu ya kwanza ya kurejeshewa eneo lake lilitolewa na Baraza la ardhi la Kata ya Bunda Na.77 mwaka 2009 lakini Ofisa ardhi ya wilaya ya Bunda wakati huo (jina tunalo ) hakuridhika na kukata rufaa kuhamisha hukumu hiyo kwenda mahakama ya ardhi nyumba na makazi wilayani Musoma.
 
Kutokana na hatua hiyo April 4, mwaka huu Mahakama ya Ardhi Nyumba na Makazi Musoma iliagiza Kampuni ya UBAPA and TRIBUNAL BROKER kutekeleza agizo la Mahakama hiyo Na.85 ya mwaka 2010.
 
 Marwa alidai  kwamba kwa  muda huo wote, maofisa hao wanatumia fedha ili agizo la mahakama hiyo isitekelezwe huku wakiendeleza eneo hilo licha ya kuzuiliwa na  badala yake waliamua kumfikisha  polisi kuwa ni mvamizi na kudai anasikitishwa na na anavyofanyiwa licha ya kuwa na umri mkubwa na kuviomba vyombo vya juu kumsaidia kuipata haki yake ambayo anadai vielelezo vyote anavyo huku akikabidhi nakala ya vielelezo hivyo katika Gazeti hili ikiwemo barua kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.


CHANZO  shommi b blog

MKOA WA NJOMBE WAONGOZA KWA MAMBUKIZI YA UKIMWI TAKWIMU ZA TACAIDS ZA ONYESHA

TUME ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS) imesema mkoa wa Njombe unaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya Virusi vya UKIMWI kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1.

Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya nne kwa asilimia tisa ukifuatiwa na Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).

Msemaji wa TACAIDS, Glory Mziray alisema hayo jana Dar es Salaam na wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Mikoa mingine na viwango vyake ni Mara (4.5), Mwanza (4.2),Mtwara (4.10), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).

Alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya UKIMWI yamepungua kwa kasi ndogo.

Alisema watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya ukimwi na UKIMWI wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.

Kuhusu tohara kwa wanaume endapo inapunguza maambukizi ya UKIMWI alisema inapunguza kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja kutoa elimu zaidi juuya uelewa wa ugonjwa huo.

---via Habari Leo

 

Monday, 5 August 2013

JINSI BARACK OBAMA ALIVYOSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA,ATIMIZA MIAKA 52,

 

RAIS BARACK OBAMA AKIONDOKA IKULU YA MAREKANI KWENDA CAMP DAVID MARYLAND KUSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA


AKIWA LIVE KWENYE KIPINDI CHA TELEVISION


RAIS BARACK OBAMA AKIWA KWENYE VIWANJA VYA GOLF HUKO CAMP DAVID

RAIS BARACK OBAMA AKITUA KWA CHOPA IKULU YA MAREKANI AKITOKEA CAMP DAVID MARYLAND KUSHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA
Rais Barack Obama amesherehekea siku yake ya kuzaliwa jana huko Marekani.Rais Obama ambae ametimiza miaka 52,alitumia siku yake ya jana kusherehekea na marafiki zake huko Camp David Maryland.

Ikulu ya Marekani imesema Rais Obama aliisherehekea siku yake hii maalum kwa kucheza Golf na marafiki zake siku ya Jumamosi huko Hawaii na Chicago,wengine waliungana nae jana huko Camp David Maryland.

Wakati huo huo Mrs Michelle Obama amemtakia birthday njema kwenye ukurasa wake wa  tweeter kupitia account yake ya @FLOTUS wenye watu 450,000  wanaomfuatilia,,na ujumbe wake huo ulisomeka kama ifuatavyo
"Happy birthday, Barack! Your hair's a little grayer, but I love you more than ever"
" Hongera kwa siku yako ya kuzaliwa Barack,nywele zako zimeanza kuwa na mvi kidogo, lakini nakupenda sana",alisema Michelle.
Ujumbe huo uliambatana na Picha ya zamani ya wawili hao enzi za ujana wao wakiwa wameketi kwenye SOFA kama inavyoonekana hapa chini


Picha ambayo Michelle Obama ameiweka kwenye mtandao wa Tweeter kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa mumewe ambae ni Rais wa Marekani Barack Obama ambae ametimiza m