MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Monday, 5 August 2013

WAFANYA BIASHARA WA MANISPAA YA SONGEA WATANGAZA MGOMO

 

 Hawa ni wafanya biashara wa masoko ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakiwa katika kikao 
 
Na Nathan Mtega,Songea


UMOJA  wa wafanyabiashara wa masoko ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma umeendelea kuulalamikia uongozi wa Manispaa ya Songea kwa kuongeza gharama za pango la vibanda na gharama za leseni za biashara kwa wafanyabiashra pamoja na utaratibu usioridhisha wa baadhi ya watumishi wa halmashauri hali hiyo imepelekea wafanyabiashara hao kuazimia kugoma.


Wakizungumza katika mkutano wa dharula wanachama zaidi ya themanini wa umoja huo wamesema hawakubaliani na utaratibu wa uendeshaji wa masoko yaliyopo ndani ya manispaa hiyo ikiwa ni pamoja na ogezeko la pango lililoamriwa na uongozi wa manispaa bila kuwashirikisha wafanyabiashara hao.


Wamesema uwezo wa wafanyabiashara katika masoko ya Manispaa ya songea na mzunguko wa fedha uliopo hauendani na ongezeko hilo la kodi,ushuru na utaratibu wa kuwataka wafanyabiashara hao  kuomba tenda ya kuendelea kufanya biashara katika vibanda hivyo walivyokuwa wakifanyia biashara zao.


Wakizungumza wafanyabiashara Christian Kayombo na Hamis Machaku katika mkutano huo wamesema kuwa utaratibu unaofanywa na uongozi wa Manispaa wa kuongeza pango la vibanda na kutangaza tenda kwa ajili ya vibanda hivyo ambavyo wao wamekuwa wakivitumia kwa mkataba wa muda  mrefu bila kushirikishwa kwenye maamuzi hayo mapya ni ishara ya unyanyasaji kwao na hawajatendewa haki kwa sababu walishaomba kupunguzwa kwa kodi pamoja na malipo ya leseni lakini kabla maombi hayo hayajafanyiwa kazi wanaletewa ongezeko la kodi.


 Wamesema kuwa ni vyema uongozi wa Manispaa ukaona umuhimu wa kuwashirikisha wafanyabiashara kwa kupitia viongozi wa umoja wao katika kutoa na kufikia maamuzi yanayowahusu badala ya uongozi huo kukaa na kuamua juu ya wafanyabiashara wakati ukijua hali za biashara katika Manispaa ya Songea na mzunguko wa fedha ulivyo.


Aidha wafanyabiashara hao wametangaza kugoma siku ya Jumanne 6 Agosti 2013  kwa muda usiojulikana kuendesha biashara ikiwa malalamiko hayo hayatafanyiwa kazi kwa sababu kumekuwepo na vitendo vingi vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa halmashauri dhidi ya wafanyabiashara na hususani wafanyabiashara wadogo .


Akizungumza makamu mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara wa masoko ya Manispaa ya Songea Leornad Chiwangu alisema wafanyabiashara wameazimia kuanza mgomo huo siku ya Jumanne na utaendelea kwa muda usiojulikana ikiwa malalamiko na maombi yao hayatafanyiwa kazi.

 
Na Nathan Mtega,Songea
Habari kwa hisani ya www.demashonews.blogspot.com

CLOUDS MEDIA GOUP NA WADAU WAKE WANDAA FTARI WEEKEND

 Kampuni ya Clouds Media Group mwishoni mwa wiki iliandaa Ftari ya
pamoja kwa wafanyakazi wake na baadhi ya wadau mbalimbali, maeneo ya
Sinza-jijini Dar es Salaam. 


Picture
 

 Jiachie Blog imetushrikisha picha zifuatazo.

MASHINDANO YA KUSOMA NA KUHIFADHI QUR ANI MKOA WA MBEYA YA FANIKIWA VEMA


Mtoto Habibu Abdulrahman(8) ambaye amehifadhi juzuu ya kwanza akionesha umahiri wake wa kuhifadhi na kusoma Koran katika mashindano yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Tausi Hotel ya Rift Valley Jijini Mbeya jana mchana, Abdulrahman amekuwa mshindi wa kwanza kwa kusoma na kuhifadhi koran juzuu moja.



Mtoto Abubakar Muharram(12) akionesha umahiri wa kusoma Koran na kuhifadhi Juzuu saba wakati wa mashindano ya yaliyofanyika Ukumbi wa Tausi Hotel ya Rift Valley Jijini Mbeya, Abubakar amekuwa mshindi wa kwanza katika kundi la wanafunzi waliojitokeza kusoma na kuhifadhi Juzuu Saba amepewa zawadi ya Msahafu maalum unaotumia umeme na fedha taslimu Sh.80,000


Majaji wakifuatilia kwa makini mashindano ya kusoma Koran kabla ya kupatikana washindi


Mgeni rasmi Shekh Said Jabir pamoja na baadhi ya maimamu wakifuatilia mashindano hayo


Majaji wakiwa kazini kumtafuta mshindi




Mgeni rasmi Shekhe Said Jabirakitoa nasaha kabla ya kupatikana kwa mshindi


Mgeni rasmi akimpa mkono mmoja wa majaji wa mashindano hayo Shekhe Abbas Mshauri






Mgeni rasmi akimpongeza mshindi wa kwanza wa kusoma na kuhifadhi Koran na Juzuu moja

Mshereheshaji wa mashindano hayo Shekhe Ibrahimu Bombo akiwaongoza wasomaji na wahifadhi wa Koran


Mshindi wa kwanza wa kusoma Koran juzuu saba Abubakar Muharam akiwa na msahafu wake wa Digital


 Baadhi ya waumini na wanafunzi wa madrasa mbalimbali waliohudhuria mashindano ya kusoma Koran
Picha zote na  Rashid Mkwinda 

WANAFUNZI 8,805 WA KWAMA KUCHAGULIWA NA TCU

 
 
 

Dar es Salaam. 
 Wanafunzi 8,805 walioomba kujiunga na masomo ya shahada ya kwanza katika vyuo vya elimu ya juu nchini kwa mwaka wa masomo 2013/14, wameshindwa kuchaguliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya kufanya makosa kwenye fomu zao za maombi, lakini wamepewa nafasi zaidi hadi Agosti 9, mwaka huu kurekebisha kasoro.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Sifuni Mchome imetaja moja ya sababu za baadhi ya wanafunzi hao kutokuchaguliwa ni sifa zao kutokukidhi masomo waliyoomba.
Alisema watatakiwa kuomba kwa kupitia mfumo wa udahili wa TCU ambao ulifunguliwa Julai 29, mwaka huu hadi Agosti 9, mwaka huu utakapofungwa.

Kutokana na hali hiyo, TCU katika taarifa hiyo imesema wanafunzi wana nafasi nyingine ya kuomba kwa kuchagua kusoma fani ambazo wana sifa nazo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwanafunzi anatakiwa kuangalia jina lake katika orodha ya ambao hawakuchaguliwa ambayo inapatikana kwenye tovuti ya tume hiyo na kisha kufuata utaratibu.

“Baada ya mwanafunzi kuthibitisha jina lake kwenye orodha ya wanafunzi ambao hawakuchaguliwa iliyoko kwenye tovuti ya TCU, anatakiwa kuchagua programu moja tu kutoka kwenye orodha ya programu inayopatikana kwenye tovuti ya TCU,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Pia mwanafunzi anatakiwa kufungua mwongozo wa udahili unaopatikana kwenye tovuti hiyo na kuthibitisha kwamba anayo sifa stahiki ya kujiunga na programu aliyoichagua.
Masharti hayo pia yanamtaka mwanafunzi ambaye hakuchaguliwa, kuingia kwenye sehemu ya taarifa za mwanafunzi (profile) kwa kuingiza jina analotumia na namba yake ya siri, kubofya kitufe cha kuomba, kuchagua programu moja tu, kubofya kwenye makasha ya kuthibitisha na hatimaye kuwasilisha maombi yake.

“Baada ya kuwasilisha maombi yako, mfumo wenyewe utakutaarifu kuwa ama unastahili kuomba programu hiyo au la na uchaguzi utakaoegemea kwenye msingi wa kwanza mwombaji huyo ndiye atakayehudumiwa mwanzo.”
“Pindi programu moja itakapojaa, haitaonyeshwa kwenye orodha ya programu zinazohitaji kujazwa kwenye mfumo wa udahili, hivyo utahitajika kujaza programu nyingine.”
Na Mwandishi Wetu, Mwananchi  
Posted  Jumatatu,Agosti5  2013 

SADC,AU,EU,WATOFAUTIANA USHINDI WA MUGABE

 

 
Wafuasi wa Chama cha Zanu-PF kinachoongozwa na Robert Mugabe ambaye juzi alitangazwa kwa  mara ya saba kuliongoza Taifa la Zimbabwe wakifurahia baada ya kutolewa kwa matokeo hayo

Harare. Baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Zimbabwe huku Rais Robert Mugabe akiibuka kidedea kwa mara ya saba, waangalizi wa Umoja wa Ulaya (EU), Umoja wa Afrika (AU), na Jumuiya ya Kiuchumi ya Kusini mwa Afrika (SADC), wametofautiana kuhusu matokeo hayo.
Wakati waangalizi AU na SADC wakisema uchaguzi huo ulikuwa huru na haki, wenzao wa EU wamesema kulikuwa na kasoro kadhaa.

Hata hivyo, AU na SADC walisema kulikuwa na hitilafu katika daftari la wapigakura kwani baadhi hawakuruhusiwa kupiga kura wakati walikuwa na haki ya kufanya hivyo.
Waangalizi wa EU wameeleza wasiwasi wao juu ya kutokukamilika kwa ushiriki wa wapigakura na kwamba kulikuwa na udhaifu kwenye mchakato wa upigaji kura pamoja na ukosefu wa uwazi.
Kwa upande wake, Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC), ilisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, licha ya hitilafu mbalimbali zilizojitokeza.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Solomon Zwana, alisema iwapo kuna chama ambacho hakijaridhishwa na matokeo, kinaweza kufuata njia za kisheria.
“Tuna imani vyama vitaheshimu ahadi walizoweka kwamba watafuata njia za kisheria na si kuanzisha vurugu. Hilo ndilo tumaini letu na ujumbe wetu kwa wadau wa kisiasa,” alisema Zwana.


Zuma wa kwanza kumpongeza Mugabe
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amempongeza Rais mteule wa Zimbabwe, Robert Mugabe kwa kuchaguliwa tena kuliongoza taifa hilo la Kusini mwa Afrika.
Katika salamu zake, Rais Zuma aliwataka wapinzani kukubaliana na matokeo hayo kwa ajili ya kudumisha amani nchini humo.”

Zuma anaonekana kutofautiana na misimamo ya Marekani, Uingereza na Australia, zilizokataa kukubaliana na ushindi wa Mugabe.
Uchaguzi wa Zimbabwe umemrudisha madarakani Mugabe kwa ushindi wa asilimia 61 dhidi ya aliyekuwa Waziri wake Mkuu, Morgan Tsvangirai aliyeambulia asilimia 34.

 Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
 Posted  Jumatatu,Agosti5  2013   

Saturday, 3 August 2013

MPAKA SASA MUGABE AONGOZA UCHAGUZI ZIMBABWE

 

NA kayanda manyanya

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe aonekana kuelekea kupata ushindi wa kipindi cha saba cha utawala baada ya ushindi katika uchaguzi wa bunge, ambao umepuuziwa na upinzani kuwa umesheheni udanganyifu.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa pande zote kuwa watulivu.
 

Matokeo kamili yalitarajiwa kupatikana jioni ya leo Jumamosi(03.08.2013) lakini chama cha rais Mugabe cha ZANU-PF kinasema kuwa tayari kimeshinda viti 140 katika bunge, ambavyo vinatosha kuweza kuendelea na mabadiliko yenye utata katika katiba.

Zimbabwe's President Robert Mugabe addresses a media conference at State house in Harare, on the eve of the country's general elections, July 30, 2013. Heavily armed riot police deployed in potential election flashpoints in Zimbabwe on Tuesday on the eve of a poll showdown between Mugabe and Prime Minister Morgan Tsvangirai that remains too close to call. REUTERS/Philimon Bulawayo (ZIMBABWE - Tags: POLITICS ELECTIONS) Rais Robert Mugabe
"Tumekwisha pata zaidi ya theluthi mbili ya viti. Ni wingi wa kutosha," afisa wa ngazi ya juu wa chama hicho ameliambia shirika la habari la AFP kwa masharti ya kutotajwa jina.
 

Wakati majimbo 186 kati ya majimbo ya uchaguzi 210 tayari yamemaliza rasmi zoezi la kuhesabu kura baada ya uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatano, Chama cha Mugabe tayari kina wingi wa kutosha, kikishinda viti 137 katika bunge.
Msemaji wa chama hicho Rugare Gumbo ameliambia shirika la habari la AFP: "Wapinzani wetu hawafahamu kile kilichowasibu", na kuongeza kuwa Mugabe anaweza kushinda asilimia 70 hadi 75 ya kura ya urais.
 

Kiongozi wa upinzani Morgan Tsvangirai ameueleza uchaguzi huo kuwa ni wa bandia na udanganyifu mkubwa na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) kimeapa kutokubali matokeo, hali inayozusha hofu ya kurejewa kwa ghasia zilizomwaga damu ambazo zilitokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2008.

Zimbabwe Prime Minister and leader of the opposition Movement for Democratic Change (MDC) Morgan Tsvangirai speaks at a news conference in Harare, June 13, 2013. Tsvangirai on Thursday rejected a plan by President Robert Mugabe to hold an election on July 31, accusing his rival of breaking the constitution and formenting a political crisis in the southern African nation. REUTERS/Philimon Bulawayo (ZIMBABWE - Tags: POLITICS ELECTIONS) Kiongozi wa chama cha MDC Morgan Tsvangirai
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezitaka pande zote mbili "kutoa ujumbe wa wazi wa utulivu" kwa wafuasi wao wakati hali ya wasi wasi ikiongezeka.
 

Ban ana matumaini kuwa hali hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa shwari na ya amani katika siku ya uchaguzi , itaendelea wakati wa zoezi la kuhesabu kura na hata baada ya kukamilika zoezi hilo," amesema msemaji wa katibu mkuu Martin Nesirky.

Bildnummer: 59927292 Datum: 01.07.2013 Copyright: imago/Xinhua
United Nations Secretary-General Ban Ki-moon addresses a press conference after attending the opening ceremony of the High-level Segment of United Nations Economic and Social Council (ECOSOC) Substantive Session 2013 in Geneva, Switzerland, July 1, 2013. Ban Ki-moon on Monday called to end the violence in Syria and said that an international conference on Syria was the best chance for reaching a political solution to end the conflicts. (Xinhua/Wang Siwei) (zw) SWITZERLAND-GENEVA-UN-SYRIA PUBLICATIONxNOTxINxCHN people xas x0x 2013 quer premiumd
59927292 Date 01 07 2013 Copyright Imago XINHUA United Nations Secretary General Ban KI Moon addresses a Press Conference After attending The Opening Ceremony of The High Level Segment of United Nations Economic and Social Council ECOSOC Substantive Session 2013 in Geneva Switzerland July 1 2013 Ban KI Moon ON Monday called to End The Violence in Syria and Said Thatcher to International Conference ON Syria what The Best Chance for Reaching a Political Solution to End The conflicts XINHUA Wang Siwei ZW Switzerland Geneva UN Syria PUBLICATIONxNOTxINxCHN Celebrities x0x 2013 horizontal premiumd Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC ambayo ina ushawishi mkubwa pia imewataka "Wazimbabwe wote kuwa na uvumilivu,na utulivu."
 

Macho yote sasa yanaelekezwa kwa chama cha MDC ambacho kilitarajiwa kutoa taarifa yake leo Jumamosi(03.08.2013) kufuatia mkutano wao wa siku mbili.
Kabla ya mkutano huo , afisa wa ngazi ya juu wa MDC Roy Bennett alitoa wito wa kampeni ya upinzani wa chini kwa chini, akiwataka watu "kuifikisha nchi hiyo katika hali ya kutoweza kufanya lolote".

** FILE ** In this Monday June 23, 2008 file photo Roy Bennett, a senior member of the Zimbabwean opposition Movement for Democratic Change in neighboring Zimbabwe, speaks during an interview with the Associated Press in Johannesburg, Bennett, an ally of Prime Minister Morgan Tsvangirai who was expected to join Zimbabwe's unity government was arrested Friday Feb. 13, 2009, the party said _ an early indication the country's new political partnership will be rocky. (AP Photo/Denis Farrell, File) Afisa wa ngazi ya juu wa chama cha MDC Roy Bennett
Waangalizi wanaonekana kutofautiana kuhusiana na jinsi uchaguzi huo ulivyoendeshwa.
 

Mkuu wa ujumbe wa uangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika , Olusegun Obasanjo , amesema muda mfupi baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa kuwa uchaguzi huo umekuwa wa "amani , uliofuata utaratibu, huru na wa haki".
SADC imeshindwa kuutangaza uchaguzi huo kuwa wa "haki" lakini imesema ulikuwa " huru na wa amani".
 

"Tumesema uchaguzi huu ulikuwa huru, kwa hakika ulikuwa huru," amesema kiongozi wa kundi la uangalizi la SADC Bernard Membe. "Hatujasema ulikuwa wa haki... hatukutaka kutoa maamuzi katika wakati huu."
Membe alikutana na Mugabe siku ya Ijumaa, "kumtakia kila la kheri wakati akijitayarisha na hatua ya kuapishwa," aliwaambia baadaye waandishi habari.

Aussenminister Tansania Bernard Membe Waziri wa mambo ya kigeni wa Tanzania na mkuu wa ujumbe wa SADC Bernard Membe
SADC ilijadili kuundwa kwa serikali ya kugawana madaraka baada ya uchaguzi uliomwaga damu wa mwaka 2008. Kukiwa na waangalizi 600 katika uchaguzi huo, uamuzi wao na hatua inayofuata itaangaliwa kwa karibu na mataifa ya magharibi ambayo yamekataliwa kuangalia uchaguzi huo.
 

Hata hivyo wanadiplomasia wa mataifa ya kigeni wameueleza uchaguzi huo kuwa umeendewa kinyume kimsingi na mtandao wa usaidizi wa uchaguzi nchini Zimbabwe umeripoti kuwa zaidi ya wapiga kura milioni moja walizuiwa kupiga kura katika maeneo ambayo ni ngome kuu ya Tvangirai. Lakini imesisitiza kuwa wasi wasi ambao umeelezwa kuhusiana na maeneo fulani ya hatua za uchaguzi yanapaswa kufuatiliwa kupitia njia sahihi za utaratibu wa

UCHAGUZI WA ZIMBABWE ULIKUA HURU"OBASANJO ASEMA '


 
Masanduku ya kupigia kura

Mkuu wa ujumbe wa uangalizi kutoka Muungano wa Afrika nchini Zimbabwe, Olusegun Obasanjo amesema uchaguzi mkuu wa hapo Jumatano ulikua huru na haki. Matokeo ya awali yanaoyesha Rais Robert Mugabe na chama tawala cha Zanu PF wakiongoza kwa kura nyingi
Chama hicho tayari kimedai ushindi. Msemaji wa chama hicho Rugare Gumbo alisema chama hicho kilitarajiwa kushinda kiasi ya asilimia 70 ya kura hizo.
Lakini mpinzani wa Mugabe, Morgan Tsvangirai, amesema uchaguzi huo ni wa uongo na kusema udanganyifu uliofanyika una maana uchaguzi huo haukubaliki.
Waangalizi kutoka Umoja wa Afrika na jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika wanatarajiwa kutoa tamko rasmi hii leo kuhusu uchaguzi huo.

Bw. Obasanjo amesema kulikua na visa kadhaa wakati wa shughuli ya kupiga kura. Hata hivyo amesema visa hivyo haviwezi kutajwa kuwa na uzito wa kubatilisha au kufuta matokeo ya kura.

Msimamo wa Muungano wa Afrika unatofautiana na ule wa kundi la uangalizi la Zimbabwe Election Support Network.
Kundi hilo ambalo ndilo kubwa zaidi linalochunguza kura ya Zimbabwe limekashifu uchaguzi mkuu na kusema ulikuwa na dosari nyingi. Hii ni kwa sababu watu milioni moja walizuiwa kupiga kura.

Huku upande wa Rais Mugabe ulitangaza kushinda uchaguzi na Morgan Tsvangirai akipinga ni dhahiri kwamba Zimbabwe ingali na mgawanyiko mkubwa wa kisiasa..

USAJILI WA WACHEZAJI SASA MWISHO AGOSTI 5

 
Usajili wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2013/2014) sasa utafungwa Jumatatu (Agosti 5 mwaka huu) badala ya Agosti 3 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Uamuzi wa kusogeza mbele umetokana kuchelewa kupata disc ya usajili msimu huu ambayo ndiyo inayotumika kwa usajili wa elektroniki unaofanywa kwa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom. Disc hiyo ambayo hutolewa na kampuni ya NAS Technology ya Tunisia tayari imeshawasili.

Kutokana na mabadiliko hayo, sasa kipindi cha pingamizi kitakuwa kati ya Agosti 6 na 12 mwaka huu wakati Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itakutana Agosti 13 na 14 mwaka huu kupitia na kufanyia uamuzi usajili wa wachezaji wenye matatizo.

Hatua ya pili ya usajili itaanza tena Agosti 15 mwaka huu ikihusisha wachezaji ambao watakuwa hawajasajiliwa katika Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu. Timu zitakazoruhusiwa kusajili ni zile ambazo zitakuwa hazijajaza nafasi zote za usajili. Dirisha dogo za usajili litafunguliwa kuanzia Novemba 15 mwaka huu hadi Desemba 15 mwaka huu.

Pia klabu za Ligi Kuu ya Vodacom zinapowasilisha usajili wao zinatakiwa kuambatanisha nyaraka zinazoonesha viwanja vyao vya mazoezi, nakala za bima kwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Masuala hayo yameelezwa kwenye Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom

KAMISHNA RWIZA KUSIMAMIA MECHI YA CHAN
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Alfred Rwiza wa Tanzania kuwa kamishna wa mechi ya raundi ya pili ya michuano ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN).

Rwiza atakuwa kamishna katika mechi ya kwanza ya raundi hiyo itakayohusisha mshindi wa mechi kati ya Msumbiji na Namibia dhidi ya Angola itakayochezwa kati ya Agosti 9 na 11 mwaka huu. Mechi hiyo itachezeshwa na refa Noram Matemera kutoka Zimbabwe.

Matemera atasaidiwa na Wazimbabwe wenzake Tapfumaney Mutengwa atakayekuwa mwamuzi msaidizi namba moja, Ncube Salani ambaye ni mwamuzi msaidizi namba mbili wakati mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Ruzive Ruzive.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

WANANCHI NA WAKAZI WA MBALIZI MBEYA WAGOMBANIA MAFUTA BAADA YA LORI KUPINDUKA

 

 Lori lenye namba za usajili  T97 AJL lenye tela namba T746 BKF lilipo acha njia na kupinduka na kuziba njia

Lori  likishindwa kupita baada ya Mafuta kumwagika Barabarani na kusababisha barabara kushindwa kupitika
Magari yakipita kwa shida baada ya Lori kudondoka
Askari wakijitahidi kukabiliana na watu waliokuwa wanachota mafuta
Shughuli za uokoaji zikiendelea kulia ni Dereva wa Lori hilo baada ya kunusurika
Dereva wa gari hilo Hassan Abdi (35) akiwa haamini kilicho tokea baada ya Kunusurika kifo


YALE YALE!!! Wananchi  wenye ndooo Haya.... Wenye Madumu haya .... wenye Masefuria haya... wote walikuwepo kuchota Mafuta kama inavyo onekana ... bila kujali kama yaweza kulipuka 
Wananchi Mbalimbali wakiwa wanapata shida kupita baada ya Lori kudondoka

Askari wa zima moto wakiwa wanaendelea na Juhudi za kuondoa mafuta barabarani kwa maji 
Wananchi mbalimbali wakiwa wanaondoka na Mafuta... huku wengine wakiendelea kuchota
Wakina mama... Watoto... Vijana na wazee wakiwa wanapata shida jinsi ya kupita baada ya ajali



Ezekiel Kamanga
Watu wawili wamenusurika kifo baada ya roli la mafuta lenye namba za usajili T 978 AJL lenye tela namba T 746 BKE Aina ya SCANIA walilokuwa wakisafiria kutoka DAR ES SALAAM kwenda ZAMBIA kuacha njia na kupinduka katika mteremko wa MBALIZI barabara MBEYA TUNDUMA.
Dereva ametambuliwa kwa jina la HASSAN ABDI 35 na msaidizi wake SAIMON SOVELA 23 ambao walikuwa wametokea DAR ES SALAAM kuelekea ZAMBIA likiwa limejaa shehena ya mafuta
Kwa mujibu wa Dereva amesema kuwa gari hilo ghafla lilipoanza kuteremka mteremko liliharibika mfumo wa breki na mbele yake kukiwa na magari matano baada ya kuona kuwa angesababisha maafa makubwa aliamua kulichepusha pembeni ndipo lilipoacha njia na kupinduka na kumwaga shehena ya mafuta.
Kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio na kuhakikisha usalama wa eneo hilo kuhofia mlipuko wa moto ambao ungeweza kutokea kutokana na baadhi ya wananchi kuanza kuchota mafuta yaliyokuwa yanatiririka.
Pamoja na juhudi za Jeshi la Polisi kudhibiti wananchi kutochota mafuta lakini wananchi walikaidi na kuendelea kuchota mafuta.
Ajali hiyo ilisababisha adha kubwa kwa wasafiri waliokuwa wana pita barabara hiyo wakiwemo wagonjwa na waliokuwa wanawahi usafiri wa ndege majira ya saa saba mchana.

Habari na mbeya yetublog

KODI YA SIMU IHAMISHIWE KENYE WAMILIKI WA NYUMMBA ZA KUPANGISHA

   NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, amesema badala ya kuwatoza wananchi kwenye laini za simu serikali ihamishie kodi hiyo kwa wamiliki wa nyumba wanaopangisha bila kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Makamba alisema kuwa malalamiko ya wananchi yalikuwa ya kweli na ya msingi hivyo basi serikali iweke mbadala wa tozo hizo kwa wenye nyumba za kupangisha.

Naibu waziri huyo aliongeza kuwa aliwahi kulizungumza hilo na kutoa ushauri kwa serikali na hata kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusiana na suala hilo la kutaka wenye nyumba kulipa kodi ili ziweze 
kusaidia wananchi katika maeneo  mbalimbali ya maendeleo.

Alisema kodi kwenye tozo za simu wananchi walikuwa na hoja lakini aliwaita wabunge kuwa ni wanafiki kwa kuwa walipitisha wenyewe wakiwa kwenye kamati ya bajeti lakini akashangaa kuanza kulalama bila sababu kwa kile alichokiita ni kutaka sifa kwa wananchi.

“Kwa sasa tayari vikao vitatu vimefanyika lakini pia kuna haja ya kuangalia endapo hii itatolewa kutakuwa na mbadala gani wa kufidia hicho kiasi cha sh bilioni 178 kinachohitajika ili kuweza kutekeleza miradi mbalimbali ya wananchi vijijini,” alisema.

Hata hivyo alisema kuwa kikubwa ni kuganga yajayo na kuacha kukumbuka ya nyuma, kwamba wananchi wamelalamika na wamesikika na sasa maagizo aliyotoa rais wameanza kuyatekeleza.

Akijibu swali kuhusu kuongezeka kwa makato katika miamara ya kutuma na kupokea fedha kupitia simu za mikononi, Makamba alisema hana uhakika nalo, lakini ni wajibu wao kuliangalia upya suala hilo.

Source: Imeandikwa na Asha Bani, TanzaniaDaima

Friday, 2 August 2013

BREAKING NUUUUUZ: LORI LA MAFUTA LADONDOKA MTELEMKO WA MBALIZI MBEYA MUDA HUU.

 

Picha ya Mlima Mbalizi
Live!
Kwa Taarifa Tulizo pokea sasa kutoka mlima wa Mbalizi zinasema kwamba kuna Lori la mafuta limedondoka muda huu na kusababisa watu waanze kuyachota mafuta hayo bila kujali kama Linaweza kulipuka.

Timu ya Mtandao  ipo eneo Hilo kwa sasa... taarifainakuja endelea kusomaa

MKUU WA MAGEREZA NA MSAIDIZI WAKE WAFUKUZWA KAZI KWA KOSA LA UJANGILI

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imewafukuza Mkuu wa Gereza la Kiteto mkoani Manyara na
Msaidizi wake, kwa kosa la kutumia vibaya madaraka yao na kutumia mali za Serikali, kwenda kufanyia ujangili na kuiba nyara za Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam JUMATANO Msemaji wa wizara hiyo, Isaac Nantanga, alisema maofisa hao ni pamoja na Mrakibu wa Magereza Ally Ramadhani Sauko na msaidizi wake ambaye ni Mratibu Msaidizi wa Magereza Joseph Kimaro.

Alisema maofisa hao walifukuzwa rasmi kazini Julai 29, mwaka huu na Katibu Mkuu wa wizara hiyo
kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya kifungu cha 34(6) cha Kanuni za Utumishi wa Magereza za mwaka 1997.

“Kufukuzwa kwao kunatokana na matumizi mabaya ya 
madaraka kwa kuruhusu mali za Serikali, ilikiwemo gari na silaha kutumika katika kufanyia ujangili,” alisema Nantanga.

Maofisa hao Julai 23, mwaka huu wakiwa na wenzao wengine wawili ambao ni askari magereza wa gereza hilo la Kiteto Koplo Sylvester Dionice na Wada Barick, walikamatwa na kikosi cha kuzuia ujangili Kanda ya Kati wakiwa na gari la jeshi la Magereza na silaha na kupakia nyara za Serikali huku dereva wa gari hiyo Sajenti Ketto Ramadhan akitoroka.

Baada ya uchunguzi wa awali, Jeshi la Magereza lilitoa taarifa ya kuwafukuza kazi askari hao watatu waliohusika kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi la Magereza na watafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi wa Polisi kukamilika.

Maofisa wawili ambao walikuwa wakuu wa gereza hilo, pamoja na kushtakiwa walivuliwa nafasi ya uongozi wao wakisubiri hatua zaidi za Wizara ambao nao sasa wamefukuzwa kazi na wanasubiri kesi yao mahakamani.

Source