MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Friday, 5 July 2013

BAADA YA MUAFAKA WA KUPATA MKOA MPYA WA MBEYA KUPATIKANA SASA KUITWA SONGWE WATU WATOAMAON YAO


  MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO AKIFUNGUA MKUTANO WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA(RCC)  JIJINI MBEYA

 NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI PHILIPO MULUGO AKICHANGIA JAMBO WAKATI WA KIKAO HICHO

 MKUU WA WILAYA WA MBEYA  DR. NORMAN SIGARA  AKIZUNGUMZA  KATIKA MKUTANO HUO
 
 MEYA WA JIJI MBEYA ATANAS KAPUNGA AKICHANGIA JAMBO KATIKA MKUTANO HUO
 
WAJUMBE  WAKIWA WANAFUATILIA MKUTANO HUO
 
Songwe ndilo jina lililopendekezwa kuitwa kwa Mkoa Mpya utakao gawanywa kutoka Mkoa wa Mbeya ambao utakuwa na Wilaya za Ileje, Chunya, Mbozi na Momba ambapo Makao makuu ya Mkoa huo utakuwa Mkwajuni Wilayani Chunya.

Mkoa wa zamani Mkoa wa Mbeya utabaki na Wilaya za Rungwe, Mbarali, Mbeya na Kyela ambapo Makao makuu yatabaki pale pale Jijini Mbeya.

Kupatikana kwa jina hilo na mwafaka huo umetokana na Mkutano wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa uliofanyika jana katika ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro.

Jina la Mkoa huo Mpya limetokana na uwepo wa Uwanja wa Ndege wa Songwe na Mto mkubwa unaoitwa Songwe ambao umezipitia Wilaya zote zinazounda Mkoa huo mpya.

Hata hivyo kuhalalishwa kwa jina na Mkoa huo unategemewa na Mamuzi ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete baada ya kupelekewa mapendekezo hayo ya RCC.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Baada ya kupatikana kwa mkoa mpya wa mbeya baadhi ya wananchi wametoa maoni yao kupitia mtandao huu kwa jina lililochaguliwa ni zuri ila makao makuu yangekuwa wilaya ya mbozi ili iwe rahisi kwa wananchi wote na hasa wa wilaya ya Momba kupata huduma muhimu za kimkoa bila kusafiri umbali mrefu wa kwenda chunya. Bwana Wifred Ngajilo ambae yeye ni mkazi wa Mbozi amelalamika kuwa chunya itakuwa mabli kwenda toka mbozi.
Kazi kwenu wasomaji toa maoni yako. 
  

BASI LA KWANZA LIENDALO KASI LATARAJIWA KUWA BARABARANI JULAI 2015 (DSM)

UONGOZI wa Mradi wa Mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (DART), umesema basi la kwanza la kutoa huduma hiyo litaanza kusafirisha abiria Julai mwaka 2015. Kaimu Mwenyekiti Mtendaji wa DART, Asteria Mlambo, alisema hayo juzi mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Kassim Majaliwa.

Alisema baada ya kukamilika kwa mradi huo na kuanza shughuli zake, utaondoa daladala zaidi ya 3,000 katikati ya Jiji. Alisema wamiliki wa daladala hizo, wanaombwa kuunda umoja wao, utakaotambuliwa rasmi ili kuwa na mabasi maalumu, yatakayotumika kwa usafiri huo wakiwa kama ni wabia.

Kaimu Mkurugenzi wa Usafirishaji na Maendeleo wa DART, Hassani Uledi alisema usafi huo pia utakuwa ni rafiki kwa watu wenye ulemavu wa viungo, ambao wanaweza kuingia ndani ya mabasi yaendayo haraka na baiskeli zao za magurudumu manne au matatu.

 

PESA YA KITANZANIA: NOTI YA TSH 500 SASA KUBADILISHWA KUWA SARAFU

KUTOKANA na kuchakaa haraka kwa noti ya shilingi 500 na kiwango chake kudumu kwenye mzunguko kwa miezi sita tu, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imesema inatarajia kubadili noti hiyo na kuwa ya sarafu.

Akizungumza na gazeti la Tanzania Daima jana kwenye viwanja vya maonesho ya kimataifa ya biashara, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Fedha, Abdul Dollah, alisema mabadiliko hayo yatafanyika hivi karibuni na sarafu hiyo itadumu kwenye mzunguuko kwa zaidi ya miaka 20 huku ikiwa na ubora wake.

Dollah alitaja sababu nyingine ya uchakavu huo ni kutokana na noti hiyo kushikwa na watu wengi kwenye mzunguko huku baadhi yao wakishindwa kuzihifadhi vizuri: “Tofauti na noti nyingine kama vile zile za sh 5,000 na 10,000 hizi utakuta mara nyingi uchakavu wake si kama ule wa sh 500 kwa sababu noti hizi watumiaji wake wengi ni wale wenye akaunti benki.”

Source: Tanzania daima gazeti

Thursday, 4 July 2013

PEMBE ZA NDOVU HARAMU KUTOKA UGANDA ZA KAMATWA NCHINI KENYA

 
Bara la Asia lina soko kubwa sana la pembe za Ndovu

Pembe haramu za ndovu zilizokuwa zinasafirishwa kutoka Uganda hadi Malaysia, zimenaswa katika bandari ya Mombasa pwani ya Kenya.
Pembe hizo zilikuwa zimefunikwa kiasi cha kufanana na samaki waliokaushwa.
Mzigo huo wa takriban pembe 770 kutoka nchi Uganda, ulikuwa unapelekwa Malaysia.
Walanguzi hao pia walikuwa wamebeba samaki waliokuwa na harufu mbaya ambayo huwachukiza Mbwa maalum wa uchunguzi, kulingana na msemaji wa shirika la ulinzi wa wanyapori nchini Kenya Paul Udoto.
Pembe za Ndovu zina soko kubwa sana barani Asia, ambazo hutumiwa kwa vitu vya urembo.


Serikali ya Kenya iliharamisha biashara za pembe za ndovu mwaka 1989, huku viwango vya uwindaji haramu wa Ndovu vikipungua pakubwa, lakini pameanza kuonekana ongezeko la uwindaji haramu tena wa Ndovu katika miaka ya hivi karibuni.

Bwana Udoto alisema stakabadhi kuhusu pembe hizo zilolionyesha kuwa zilisafirishwa kutoka Uganda kwa gari tarehe 12 mwezi Juni.
Gari hilo kisha likaegeshwa katika kituo cha mafuta mjini Mombasa, eneo la kufanyia biashara hadi mzigo huo ulipofikishwa bandarini.
Thamani ya pembe hizo badi haijabainika kwa mujibu wa bwana Udoto.

BAADA YA RAIS WA MISIRI KUVURIWA MADARAKA NA JESHI JANA RAIS MPYA KUAPISHWA LEO SHEREHE ZA ANZAAA


Sherehe za baada ya kumuondoa mamlakani Morsi

Jaji mkuu wa mahakama ya kikatiba nchini Misri Adli Mansour anatarajiwa kuapishwa kama rais wa mpito wa nchi hiyo baada ya jeshi kumng'oa madarakani rais Mohammed Morsi, ambaye ni kiongozi wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini humo.
Mkuu wa jeshi Generali Abdul Fattah al-Sisi alitoa tangaza hilo kupitia televisheini Jumatano jioni, katika kile Morsi, alisema ni mapinduzi ya kijeshi.
Generali Sisi alisema kuwa Morsi,ambaye ni rais wa kwanza kuchaguliwa amekosa kutimiza mahitaji ya watu.
Hatua hiyo inakuja baada ya siku nyingi ya maandamano, dhidi ya rais Morsi wa chama cha Musolim Brotherhood.
Waandamanaji walimtuhumu yeye na chama chake kwa kusukuma ajenda ya kiisilamu kwa taifa hilo na kukosa kusuluhisha matatizo ya kiuchumi yanayokumba taifa hilo.
Chama cha Muslim Brotherhood kimesema kuwa bwana Morsi pamoja na washauri wake wako chini ya kifungo cha nyumbani na hawana mawasiliano ya nje.


Hapo awali mkuu wa majeshi alisema kuwa katiba ya nchi hiyo imeahirishwa na kwamba jaji mkuu wa taifa hilo atachukuwa mamlaka ya rais.
Maelfu ya waandamanaji wanaompinga bwana Morsi mjini Cairo walisherehekea kwa shangwe na vifijo kufuatia taarifa hiyo ya jeshi lakini wale wanaomuunga bwana Morsi wanasemekana kubaki kimya huku wakisubiri matukio yatakayofwata.

Rais Obama amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusiana na matukio yaliyopo nchini Misri huku katibu mkuu wa umoja wa mataifa Banki Moon akitaka kuwe na utulivu.

MKURUGENZI MOSHI AVUNJA NYUMBA ZILIZO JENGWA BILA VIBALI

 



MKURUGENZI wa Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro Bernadeta Kinabo,ametelekeze agizo la baraza la madiwani la kumtaka kuvunja nyumba iliyojengwa katika eneo la wazi bila kibali kuvunjwa.

  MTANDAU HUU imefika katika eneo la tukio leo asubuhi na kushuhudia shughuli ya kuvunja nyumba hiyo ikiwa ikekwisha fanyika ambapo baadhi ya mashuhuda walisema tukio hilo lilitokea majira ya saa 7:00 usiku.

Nyumba hiyo  inayolalamikiwa na madiwani hao kujengwa katika eneo la wazi ipo katika mtaa wa “Police Mess” barabara ya Mawenzi karibu na makao makuu ya Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro.

Katika baraza la madiwani lililo kaa juzi katika ukumbi wa Manispaa mkurugenzi huyo alitakiwa kuvunja nyumba hiyo pamoja na baadhi ya nyumba nyingine zilizo jengwa kinyume cha sheria.

Diwani wa kata ya Kiusa Steven Ngasa amedai katika kikao hicho kuwa nyumba hiyo ilijengwa kinyume cha sheri na kwamba madiwani wamekuwa wakilaumiwa kuchukua rushwa kutoka kwa wamiliki hao jambo ambalo si kweli.

Alisema kuwa kumekuwa na ujenzi holela unaoendelea ndani ya manispaa hiyo huku watendaji wa Halmashauri hiyo wakiwa hawatambukii chochote kinacho endelea jambo ambalo ni uzembe.

“tabia hii ya ujenzi holela imekuwa ikishamiri siku hadi siku na mbaya zaidi wanakiuka sheria jambo hili hatuta livumili kuona linaendela katika manispaa yetu”Alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa  Kinabo alisema kuwa baadhi ya madiwa wamekuwa wakipita kwa wamiliki wa majengo hayo huku wakichukua rushwa jambo ambalo limekuwa likikwamisha shughuli hizo kuendelea.

Naye Meya wa manispaa hiyo Jafari Michael aliwataka madiwani kuacha tabia ya kuwa “mawakala wa nyumba” na kutanguliza maslahi mbele kwani wao ndio chanzo cha migororo inayo endelea ndani ya mansipaa hiyo.

Akizungumzia tukio la kuvunjiwa nyumba yake, mmiliki wa Nyumba hiyo, John Ambrose Mwase amesema hapo mwanzoni alikuwa anafanya biashara ya mgahawa katika eneo hilo kabla ya kuiomba manispaa imbadilishie leseni ya biashara na kibali cha kufanya biashara tofauti katika eneo hilo.

Amesema anashangazwa kusikia kuwa ujenzi wa nyumba hiyo umefanyika bila kibali na kuhoji ni kwa nini manispaa ichukue uamuzi wa kuvunja majira ya usiku na kuharibu mali bila taarifa.

Mwasi amesema leseni alipewa na Afisa biashara wa manispaa ambaye pia alifika na kukagua eneo hilo kabla ya ujenzi kuanza. ameongeza kuwa gharama aliyotumia kujenga nyumba hiyo ambayo ni mkopo wa benki ya KCB ni kubwa mno ambayo ni sh milioni 85 pamoja na nyingine za kuendeshea biashara ambazo ni sh. milioni 165.

Mwandishi: KIJA ELIAS, Moshi-Kilimanjaro

Wednesday, 3 July 2013

MCHUNGAJI WA KINISA LA (EAGT) IWAMBI MBEYA AHUKUMIAWA MIAKA 30 NA VIBOKO 12 KWA KOSA LA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI WA MIAKA 19

 MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.
Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi

   MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe   akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela

Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini  baadaya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 3
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na viboko 12 baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Ndugu Gilbert Ndeuruo amesema Mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na Shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni(19).

Amesema Mtuhumiwa huyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.


Kutokana na ushahidi huo Hakimu Ndeuruo alidai kuwa Mahakama yake imemkuta Mtuhumiwa na makosa mawili ya Ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na Mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai kuwa Shtaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.

Kwa upande wake Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana nan mtuhumiwa kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti anaumri wa Miaka 19 ili hali Mtuihumiwa akiwa na Miaka 57.

Pia alidai kuwa Mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha malishtakiwa.

Hata hivyo Hakimu alimuuliza Mtuhumiwa kupunguziwa adhabu ambapo Mshtakiwa huyo aliomba kupunguziwa adhabu kwa madi kuwa ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.

Aidha kutokana na utetezi huo Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo c ha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza ili hali katika kosa la pili amehukumiwa kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.

Ameongeza kuwa Mtuhumiwa anahaki ya kukata rufaa katika Mahakama kuu ya Mbeya kama hatakuwa ameridhika na adhabu aliyopewa na mahakama yake.
 chanzo na Mbeya yetu Blog 

KUMBE KUNATOFAUTI KUBWA KATI YA TANZANIA NA MAREKANI ?



Ndugu zangu, Picture

Katika saa 20 na zaidi Rais Obama alipokuwa katika ardhi ya Tanzania, sikusikia mahali popote akitamka jina la chama chake cha Democrat. Obama ametamka ' AMERICA!' mara zisizohesabika.

Kwa kweli ujio wa Obama umetusaidia Watanzania kupumzika na kelele za vyama, maana, kwa siku kadhaa, kabla na wakati wa ujio wa Obama, Watanzania tumepata kupumzika na kusikia habari za vyama vya siasa na malumbano yasio na hoja za msingi, mara nyingi yasio na tija kwa nchi na maendeleo yake.

Hakika, siasa ni kitu kizuri sana kwa nchi. Lakini siasa za ' ovyo ovyo' ni kitu kibaya kwa nchi. Na mara nyingi, 
siasa za ' ovyo ovyo' ni kitu cha hatari kwa nchi na mustakabali wake.

Picha hiyo hapo juu ina mengi ya kutufundisha; kuwa siasa si uhasama. Uchaguzi ukiisha watu mnarudi kwenye kufanya kazi. Kupigania maslahi ya taifa. Si kuendeleza migogoro ya kisiasa na hata kuwepo kwa vurugu. Hayo hayana tija kwa nchi.

Unapomwangalia Obama na Bush kwenye picha ya pamoja wakiwa Dar na kwenye kutoa heshima kwa wahanga wa ugaidi kwenye mlipuko ulitokea kwenye Ubalozi wao mwaka 1998, inadhihirisha ukomavu wa kisiasa. 

Unachotumainia hapa, kuwa ifike siku, hata hapa kwetu Tanzania, kwa Rais aliye madarakani na Rais Mstaafu kutoka vyama viwili tofauti, tuone picha yao wakiwa wamesimama pamoja kwenye makaburi ya kumbukumbu ya mashujaa wetu wa Vita Vya Kagera kule Uganda.

Ndio, picha hiyo hapo juu ni somo kwetu. Hawa wawili; Bush na Obama, ndio tuliowaona kwenye kampeni zao wakipambana kiasi huwezi kufikiri wanaweza kusimama pamoja kama ndugu wa taifa moja.

Lakini, kwa wenzetu Marekani, siasa si uhasama wala mambo ya kuwindana. Wanachogombania kwenye siasa ni kupewa heshima ya kuitumikia Marekani. 

Na heshima hiyo akipata mpinzani wako, basi, kwa wenzetu wanachofanya ni kuungana mkono kwenye kazi ya maslahi ya Marekani bila kujali tofauti zao za kiitikadi. Na ndicho tunachofundishwa kwenye picha hiyo.

Swali linabaki, Watanzania tuko tayari kubadilika kifikra kwa maslahi ya taifa letu?

MUHUBIRI FAKE AKAMATWA BAADA YA KUDAI PESA KABLA YA HUDUMA


PictureMtuhumiwa Richard Mwangusi
Jeshi la  polisi mkoa wa Iringa limemkamata na kumtupa mahabusu mhubiri  Richard Mwangusi, raia wa nchini uganda kwa  tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii baadhi ya watu wameeleza kusikitishwa na  kito cha utapeli kinachofanywa na  mhubiri huyo ambaye  amekuwa akiishi katika nyumba ya kulala  wageni ya Wihanzi mjini  Iringa kuwa amekuwa akiwataka  watu kutuma pesa kwa  njia ya  M-PESA kuanzia TSh 10,000 na kuendelea iwapo wanahitaji kupanga muda wa kuongea na mhubiri  huyo kupitia simu ya kiganjani.

Baadhi ya  wananchi  ambao  walitoa malalamiko yao leo  walidai kuwa  mhubiri  huyo amekuwa akitumia namba ya simu ya Lodge ya Wihanzi ambayo ni 0262700222 kwa kuwataka   watu  wenye matatizo  kupiga simu kwa namba hiyo na mara  baada ya  kupiga simu mhudumu  ambaye  yupo  zamu amekuwa akimtaka  mtu aliyepiga   simu  kueleza shida yake na mara  baada ya kueleza iwapo anataka kuongea na mhubiri  huyo amekuwa akitaka kutumiwa kwanza kiasi cha fedha kwa namba ya mhubiri huyo ndipo apewe huduma anayotaka.

Mmoja kati ya watu ambao  wamepata  kulizwa na mhubiri huyo amedokeza  kuwa namba  za mhubiri  huyo amezipata  kupitia kituo kimoja  cha  Radio  mjini Iringa  na kutokana na baadhi ya watu kutoa ushuhuda  kuwa  wamepona magonjwa sugu  ndio sababu ya kuchukua namba yake  ili  kuweza  kuombewa  pia ila baada ya kuchukua namba  hiyo amejikuta akiishia  kuliwa  pesa bila kupewa huduma husika.

Pia  alisema  kila anapomtafuta mhubiri huyo kwa njia ya simu  ili kuombewa amekuwa akimtaka  kuongeza pesa zaidi  ili  kuombewa hadi kupona jambo ambalo amekuwa akijiuliza kama kwa sasa injili ya biashara na kama  biashara  basi  ni  vyema wahubiri watangaze  bei  kamili  ili mtu anunue kulingana na uwezo wake.

Tuesday, 2 July 2013

USHURU WAWALIZA WAKULIMA WA MPUNGA (MOROGORO)

 


WAKULIMA wa mpunga wilayani Kilombero, Morogoro wamesema licha ya serikali kuwapiga mabomu wakati wakidai kupunguziwa ushuru, imeendelea kutoza ushuru kwa zaidi ya asilimia 200.
Awali mpunga ulikuwa ukitozwa sh 1,000 kwa gunia la kilo 100 lakini kwa sasa ushuru umepanda hadi sh 5,000 kwa gunia hilo au asilimia tano ya bei iliyopo sokoni kwa gunia.


Wakizungumza kwenye mkutano wa wadau wa kilimo cha mpunga Kilombero ulioandaliwa na Taasisi ya Maendeleo Mijini na Vijijini (RUDI) kwa kushirikiana na Jukwaa la Kilimo (ANSAF), walisema ushuru mkubwa ni kikwazo kwa wakulima katika kujikwamua kiuchumi.

Ushuru unatozwa asilimia tano ya bei ya soko ambapo gunia la kilo 100 linatozwa ushuru wa sh 5,000 huku wilaya nyingine zikitoza sh 3,000 kwa gunia la uzito huo.
Masumbuko Francis, mkulima wa mpunga alisema wanakumbana na ushuru kwa zaidi ya mara tatu na kwamba walipigwa mabomu walipokuwa kwenye maandamano lakini halmashauri ya wilaya hiyo inaendelea kutoza ushuru mkubwa.
“Wanunuzi wanakimbilia wilaya nyingine zenye ushuru mdogo… lakini pia kushusha bei ya mpunga kwa kuwa wametozwa ushuru mkubwa na serikali ni kumuumiza mkulima.

Alisema madiwani wanashindwa kuwatetea wananchi na kuwaacha wakandamizwe na ushuru mkubwa.
Mwekahazina wa Halmashauri ya Kilombero, Mbwana Msangi, alisema licha ya ushuru mkubwa wanalazimika kufanya hivyo ili kupata fedha za kujiendesha.
Wadau na wakulima waliofika kwenye mkutano huo walipendekeza kushirikishwa kwa wakulima katika suala la ushuru na kuupunguza hadi asilimia tatu.

na Rodrick Mushi, Morogoro Tanzania daima

KUJA KWA RAIS OBAMA TANZANIA KWA WASOTESHA ABIRIA WA MIKOANI

BAADHI ya abiria wanaosafiri kwenda na kuingia jijini Dar es Salaam wanatarajia kukumbwa na adha ya usafiri leo kwa muda wa saa kadhaa wakati Rais wa Marekani, Barack Obama, atakapotembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion Power iliyopo eneo la Ubungo.

Akizungumza na gazeti laTanzania daima jana, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga, alisema kuwa kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo (UBT), kitafungwa kuazia saa 3:00 asubuhi hadi saa 7:00 mchana.

Alisema kituo hicho kitasitisha safari zake kutokana na kufungwa kwa Barabara ya Morogoro ambako kipo kituo hicho
.“Kituo hicho kinafungwa ili kupisha msafara wa rais huyo wakati atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Symbion Power,” alisema Mpinga bila kufafanua kama kutakuwa na njia mbadala.
Licha ya kufungwa kwa muda kituo hicho vilevile mabasi yanayotoka mikoani yatazuiwa kuingia mjini hadi saa 7:00 mchana wakati rais huyo atakapokuwa amemaliza ziara yake kwenye mitambo hiyo.
Mpinga aliongeza kuwa mbali na UBT, pia kituo kidogo cha daladala na magari ya shamba kitafungwa kuanzia asubuhi hadi baada ya kumalizika kwa ziara hiyo, ambapo madereva wote wanatakiwa kutafuta njia nyingine za ndani ili kuepuka usumbufu kwa abiria.

Kamanda huyo aliwaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu utakaojitokeza kutokana na kufungwa kwa barabara hizo.


chanzo  na Shehe Semtawa Tanzania daima

MAELFU WALIA KUTOMWOANA BARACK OBAMA

 
Umati wa wananchi ukiwa umekusanyika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya kumwona Rais Barack Obama.
Picha na Venance Nestory 
0
DAR ES-Salaam. Maelfu ya wakazi wa D Dar es Salaam, walijitokeza kwa wingi jana kumlaki Rais wa Marekani, Barack Obama aliyewasili nchini kwa ziara ya siku mbili inayohitimishwa leo huku wakilalamikia kutomwona.Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, msafara wake ulipitia Barabara za Nyerere, Nkrumah, Samora, Magogoni hadi Ikulu.


Ukonga Majumba SitaWakazi wa maeneo ya Gongo la Mboto, Ukonga, Kitunda, na Tabata walifurika eneo la Majumba Sita kwa ajili ya kumwona, lakini hali ilikuwa tofauti.Magari yalizuiwa kuanzia Njia panda ya Segerea na hayakuruhusiwa kusogea karibu na barabara inayotoka uwanja wa ndege. 

“Mimi nimefika hapa kwa ajili ya kumwona, sikumwona jamani yaani nimepigwa na jua bure,” alilalamika dada mmoja akiwa na wenzake huku ameshikilia kandambili mkononi.Naye Mkazi wa Tabata Mawezi, aliyejitambulisha kwa jina la Jana Kamanzi alilalamikia mwendo kasi wa magari hayo na kushindwa kumuona kiongozi huyo.Kipawa/Jeti LumoMaeneo hayo walijitokeza watu wengi huku wengine wakiwa na mikeka ya kukalia tayari kumlaki kiongozi huyo.

Gazeti hili lilishuhudia umati huo kwa wakazi kutoka maeneo ya Jeti, Kipawa, Karakata waliofika kumlaki Rais huyo wa Marekani.Baadhi ya mama lishe walitumia nafasi hiyo kuuza chakula kwenye ndoo za plastiki kwa kificho, huku wafanyabiashara ya maji na wao wakitumia nafasi hiyo kupandisha bei ya maji huku wakiuza kwa kificho.VingungutiKatika maeneo ya Vingunguti, umati ulifurika pande zote mbili za barabara kwa wakazi wa Vingunguti na Kijiwe Samli wakiwamo wafanyakazi ambao ofisi zao ziko karibu na Barabara ya Nyerere. 

Chanzo mwananchi gazeti


OBAMA NA BUSH WA ONANA ANA KWA ANA NDANI Y A TANZANIA


 
 
Rais Obama ameweka rekodi ya kuwa mtu wa kwanza mweusi kuchaguliwa kuongoza Marekani, akipokea wadhifa huo kutoka kwa Rais Bush, ambaye aliiongoza taifa hilo kuanzia mwaka 2000-2008.

Kitendo cha vigogo hao kukutana nchini ni cha
kihistoria na kinadhihirisha jinsi Marekani ilivyoipa kipaumbele Tanzania kwa masuala ya diplomasia.
Viongozi hao wawili, wapo Tanzania wakati Rais Obama akimalizia ziara yake ya Afrika na Bush atakuwa na mkewe, Laura, watahudhuria mkutano wa wake za marais wa Afrika unaodhaminiwa na Taasisi ya Bush Foundation.


Pia, Michelle Obama, atahudhuria mkutano huo kabla ya kuondoka kurejea Marekani.
Balozi mbili za Marekani za Dar es Salaam na Nairobi, Kenya zilishambuliwa kwa wakati mmoja Agosti 7, 1998.

Obama ataweka shada kama sehemu ya kumbukumbu ya tukio hilo na Bush ataungana naye katika shughuli hiyo.
Hata hivyo, viongozi hao hawatahutubia wakati wa shughuli hiyo.

Rais Obama ametoa pongezi kwa sera za Bush Afrika hasa kwa kuongoza mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ukimwi.
Hata hivyo, utawala wa Rais Obama umejikita zaidi katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Kuna kamandi ya Jeshi ya Africom, ambayo ina kazi kubwa ya kukabiliana na ugaidi barani humu.

MWANAFUNZI (15)AMBAYE ANASADIKIWA KIBAKA ANUSURIKA KUAWAWA

KIBAKA Rajabu Hamisi Juma (15), Mwanafunzi wa shule ya Sekondari ya Msasani, iliyoko Manispaa ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, amenusurika kuuwawa na wananchi wenye Hasira kali baada ya kufamaniwa mchana wa leo akiiba katika Duka la mfanyabiashara Paulo Maile.

Kibaka huyo ambaye ni mkazi wa Pasua, amekutwa na masahibu hayo baada ya kuingia dukani hapo kwa kudhani kuwa mhudumu wa duka yuko mbali na ndipo alipokutwa akiwa tayari ameshaiba Simu, aina ya Nokia huku akijaribu kuficha Laptop iliyokuwa dukani hapo.

Akizungumzia mkasa huo, kibaka Rajabu huyo aliamua kufanya hivyo kwa ajili ya kukosa ada ya kulipa shule kutokana na wazai wake kukataa kumlipia ada anayodaiwa shuleni hapo.



Tukio hilo lililowaacha mdomo wazi baadhi ya mashuhuda waliofika dukani hapo , limetokea leo majira ya saa 6:10 mchana katika duka la Nguo lililloko katika mtaa wa double Road, barabara kuu ya Moshi-Dar es salaam linalomilikiwa na mfanyabiashara Paulo Maile mkazi wa Soweto.


Kamera ya .MTANDAO HUU  ilifika katika eneo la tukio na kukuta kijana huyo akishushiwa kipondo na mhudumu wa duka hilo aliyefahamika kwa jina moja la George.Huu hapa ni mkanda mzima wa tukio lenyewe:
Amando Tarimo ambaye ni mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo akishusha kipondo kwa kijana Rajabu Hamisi aliyekutwa akijaribu kuiba katika duka la mfanyabiashara Paulo Maile, Leo Mchana.



Gari la Polisi likiondoka na mhalifu katika eneo la tukio


Vijana wa Boaz wakiondoka na Kibaka huyo aliyenusirika kufa mikononi mwa Raia Wema


George akitoa Maelezo kwa mashuhuda wa tukio la wizi nje ya duka hilo


George aendelea na Maelezo


Kibaka  Rajabu Hamisi (Jezi ya Manchester Utd) akiomba msamaha baada ya kufumaniwa dukani katika jaribio la wizi, Paulo Maile ambaye ndiye mmiliki wa Duka (shati la mistari), George (shati jekundu katikati) na mmoja wa mashuhuda wakimsikiliza kibaka huyo dukani hapo


Rajabu akipakizwa kwenye gari la polisi leo mchana


Mwenye duka akitoa kipondo kwa Kibaka huyo...


kipondo kikiendelea...


 

Mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo, Amando Tarimo akiendeleza kipondo kwa kibaka huyo....

   

Monday, 1 July 2013

BAADA YA HISPAIN KUA HOI KWA BRAZIL 3-0, WAJIPANGA KWA KOMBE LA DUNIA

 



Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar, ameshinda tuzo ya Mpira wa Dhahabu kama mchezaji bora wa Kombe la Mabara, Confederations Cup. 
 
Katika michezo mitano ya timu yake kwenye Kombe la Dunia, Neymar, alifunga kwenye mechi nne, ikiwemo ya jana ya fainali, ambapo Brazil iliibwaga Hispania kwa mabao 3-0. Kiungo wa Hispania, Andres Iniesta, alipata tuzo ya Mpira wa Fedha, na mwenzake wa Brazil, Paulinho, akashinda Mpira wa Shaba. Mshambuliaji wa Uhispania, Fernando Torres, ameshinda Kiatu cha Dhahabu kwa kufunga mabao 5 katika michunao hiyo. 
 
Mshambuliaji wa Brazil, Fred, alikuwa wa pili kwa kupata Kiatu cha Fedha, akiwa pia na magoli 5, ingawa alicheza kwa dakika nyingi zaidi. Neymar alifunga magoli 4 na kushinda Kiatu cha Shaba. Mlinda mlango wa Brazil, Julio Cesar, alishinda Glavu ya Dhahabu, huku timu ya Uhispania ikipewa tuzo ya mchezo mzuri.
 

BAADA YA HAKUNAGA, HAJUI ATOE IPO.. SUMA LEE

 



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgSTvhNbN0FPeDo_yyBh9ss8ztqXYWr3s8lKOepQ3p5tmrjyFZl7pKHv9I0RvDxvkWk1MqEMu743sFxdMCvuDxiRJjlk-k4Y72TK0F2VrrlbUTnlQtSpEjUWQqXWX4s8bq41ZqN_zfDgQ/s1600/sumalee.jpgBAADA ya kutamba na wimbo wake wa ‘Apate Raha’, msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ismail Sadick ‘Suma Lee’, anajipanga kuachia wimbo wake mmoja kati ya nyimbo tano ambazo ameziandaa.

Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Suma Lee alisema katika stoo yake ana nyimbo zaidi ya nne  alizoandaa na hajui aanze kuitoa ipi kutokana na ubora zilizonazo.

Alisema baadhi ya nyimbo ambazo tayari amezirekodi ni ‘UK Dubai’, ‘Moyo Safi’, ‘Nimekaa’, ‘Hesabu za Mapenzi’ na ‘Ndoa’, hivyo bado yupo kwenye wakati mgumu, aanze na upi.

http://www.angalia-bongo.com/wp-content/uploads/2011/10/sum.jpg“Baadhi ya mashabiki wanasema nimeishiwa mistari, wengine wanasema sitaki ‘Hakunaga’ ichuje ndiyo maana sitoi wimbo mwingine, naomba mkae mkao wa kula, vitu vizuri vinakuja,” alisema Suma Lee.
 

KING MSWATI ATUA TANZANIA (DAR)

 

b2ap3_thumbnail_01.jpg

Mfalme Mswati wa II, alipokuwa akitua nchini kwa ajili ya kuhudhuria
Mkutano wa 'Smat Patnership' 

 b2ap3_thumbnail_03.jpg

TAARIFA YA JWTZ YA KANUSHA KUHUSU TUHUMA UBAKAJI MTWARA

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepokea taarifa kwamba waandishi wa Habari kadhaa wamepelekwa Mtwara kwenda kumhoji msichana mmoja kwa madai ya kubakwa na wananjeshi wa JWTZ.

JWTZ  linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa endapo taarifa hizo zitatangazwa kwenye baadhi ya vyombo vya Habari wazipuuze kwani hazina ukweli  wowote zaidi  ya kuwa ni za upotoshaji.

Msichana huyo amepandikizwa ili kuharibu taswira nzuri ya JWTZ. Ifahamike kwamba maafisa na askari wa JWTZ waliopo huko Mtwara wanafanya kazi kwa uangalizi wa karibu na vitendo hivyo vya aibu hawawezi  kuvifanya.
Jeshi letu linafanya kazi kwa nidhamu na si kama baadhi ya watu wenye maslahi binafsi wanavyolipaka matope.

Tunapenda kuwafahamisha watanzania wote kuwa JWTZ lipo kwa ajili ya maslahi ya watanzania wote.
Tunasikitika sana kama wapo watanzania wenye mawazo hayo machafu ya  kulichafua JWTZ lenye sifa nyingi ndani na nje ya nchi yetu.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

SLP 92023, Simu: 0764 742161


 

MWANAFUNZI WA KIKE AKAMATWA NA WAZAZI WAKE GEUST HOUSE

Mwanafunzi mmoja amefumaniwa katika nyumba moja ya wageni (guest house) hapo juzi, tarehe 29/6/2013 majira ya saa nane mchana katika eneo la Yombo Vituka jijini Dar es salaam.

Hata hivyo mfumaniwa mwenzake hajakamatwa kwani aliponyoka na kukimbia.

(Picha zote na maelezo yameletwa na Dei Misana)
Picture
Wazazi wa uchungu na hasira wakiwa na binti yao mara baada ya fumanizi.
Picture
Hii ndio sura halisi ya binti aliyefumaniwa.
Picture
Chumba kilichotumika kwa kwa mwanafunzi huyo, mwenzake kufanyia ufuska.
Picture
Wazazi wakimpiga binti yao kwa uchungu na hasira mara baada ya fumanizi.

 

ZITTO KABWE ASEMA KUHUSU BARACK OBAMA KUJA TANZANIA (AFRIKA)

     Hatimaye Barack Obama, Rais wa Marekani anatembelea tena bara la Afrika. Hii itakuwa ni mara ya pili Obama kutembelea Bara hili alikotoka baba yake baada ya ziara yake ya kwanza mwaka 2009. Mwaka huo alitembelea Ghana na Misri ilhali mwaka huu anatembelea Senegali, Afrika Kusini na Tanzania. Ziara hiyo itakayoanza tarehe 26 mwezi Juni, itamfikisha Tanzania tarehe 1 Julai na kuondoka siku ya pili yake.

      Uchaguzi wa Obama kuwa Rais wa Marekani ulipokolewa kwa shangwe Afrika nzima. Wakati Waziri wa mambo ya nje wa Nigeria alilia kwa furaha, nchi ya Kenya ilitangaza siku ya mapumziko na Rais wa zamani wa Afrika Kusini ndugu Nelson ‘Madiba’ Mandela alisema ‘ushindi wa Obama unawafanya Waafrika wathubutu kuota ndoto (Jarida la The Economist). Hapa Tanzania kulikuwa kuna shamra shamra za kila namna na magazeti yaliweka vichwa vya habari kana kwamba ni Rais wa Tanzania aliyechaguliwa. Waafrika walikuwa na matumaini makubwa sana na bwana Obama. Yamefikiwa?

     Ni vema ifahamike kuwa Barack Obama ni Rais wa Marekani na siku zote atalinda maslahi ya Marekani tu. Kuwa na matumaini makubwa kwamba labda yeye angeliweza kuiweka Afrika mbele sana ilikuwa ni kujifurahisha tu nafsi. Maslahi ya Marekani ni ya kipaumbele kuliko kitu kingine chochote kwa Rais Obama. Kwa wengi Obama amekuwa kama amewavunja moyo.

       Tanzania inapokea kiongozi wa Taifa kubwa duniani wa pili sasa ndani ya kipindi cha miezi 3 tu. Kwanza 
alikuja Rais wa China na sasa wiki hii anakuja Rais wa Marekani. Maneno ya mtaani na kwenye mabaraza ya majadiliano ni kwamba viongozi hawa wanakuja kugombea maliasili tulizo nazo kama gesi asilia na madini. Nadhani haya ni maneno ya kusema katika kupiga soga maana kunyonywa kwa rasilimali hakuhitaji Rais wa Marekani aje Tanzania.
 
     Makampuni yote makubwa yanayochimba dhahabu hapa nchini ni makampuni ya nje na marais wao hawakuja ili waweze kupata mikataba minono ya kuvuna utajiri wetu.  Katika kitalu namba 2 cha utafutaji wa mafuta na gesi huko Bahari Kuu kampuni ya kimarekani ya ExxonMobil ina ubia na kampuni ya Norway ya StatOil. Kampuni hiyo haikusubiri Rais wa Marekani aje ili wapate mikataba.

         Kuna makampuni mengi sana ya kichina yanajenga barabara zetu hapa nchini yakiwa na mikataba minono sana. Kule Mchuchuma na Liganga kuna kampuni ya kichina inajiandaa na uchimbaji wa chuma na makaa ya mawe. Makampuni yote haya hayakusubiri Rais wao aje.

        Hoja inayojengwa hapa ni kwamba ujio wa Marais mbalimbali nchini ni ujio wa kujijenga kidiplomasia na wakati mwingine kama sehemu ya kutuma ujumbe Fulani kwa dunia. Nchi inayotembelewa pia inaweza kuona kuwa diplomasia yake inaheshimiwa na mataifa yanayoitembelea.

 
 
Hata hivyo hii haiondoi ukweli kwamba Obama anakuja kwa ajili ya maslahi ya nchi yake kama ilivyo kwa wachina walivyokuja. Tumesikia Rais Obama ataambatana na mamia ya wafanyabishara kutoka Marekani kwa ajili ya kupata fursa za kuwekeza nchini. Pia tutasikia matangazo kuhusu msaada wa pili wa Millenium Challenge ambapo Wamarekani wanaendelea kumwaga pesa nchini kusaidia miundombinu lakini pia kushawishi kuungwa mkono na nchi zetu kwenye maamuzi Fulani Fulani jumuiya za kimataifa.

Tumesikia Obama atakwenda kutembelea mitambo ya kampuni ya Symbion. Hii ni mitambo ambayo miaka 4 iliyopita ilipigiwa kelele kuwa ni mitumba na hivyo TANESCO wasiinunue. Hawakununua na badala yake kampuni hiyo ya kimarekani ikainunua, wakaingia  mkataba na TANESCO kuwauzia umeme unaozalishwa na mitambo hiyo hiyo chakavu. Wakati tunasuburi kulipa takribani tshs 105 bilioni kwa Dowans baada ya kutubwaga kwenye kesi, tunasubiri kuona wanasiasa watakaokwenda kumsindikiza Obama kwenye matembezi hayo ya kutembelea mitambo chakavu.

Kampuni kubwa ya kutengeneza mitambo ya kuzalisha umeme ya GE imetangaza kuingia ubia na kampuni ya Symbion kuzalisha umeme nchini. Takribani 400MW zitazalishwa kutoka Mtwara na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa. Pia sehemu kubwa ya umeme utakaozalishwa Mtwara tayari umepata soko kwenye kiwanda cha kuzalisha udongo ulaya (simenti) cha bwana Dangote kule Mtwara. Mtendaji Mkuu wa GE bwana Jeff Immelt ametangaza kuwa kampuni yake itauza mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi mingi zaidi Afrika Mashariki kuliko Marekani katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Ni biashara tu!

Nishati naona ni kipaumbele kikubwa sana kwa ziara ya Rais Obama. Kwa nchi kama yetu yenye watu asilimia 21 tu wenye umeme, ni dhahiri kipaumbele hiki watu wengi watakiiunga mkono. Hata hivyo Obama ni lazima asimame kidete kuhakikisha kuwa kampuni za nchini mwake zinazopata miakataba hapa nchini ziweke wazi mikataba hiyo na kulipa kodi inavyostahili. Makampuni ya mafuta kutoka Marekani hayana historia nzuri duniani na hivyo ni lazima tulisisitize mapema kabisa. Uwazi wa mikataba na uwezo wa kupambana na ukwepaji kodi ni muhimu sana katika vita dhidi ya Ufisadi na ubadhirifu.

Rais Obama atambue kuwa iwapo Tanzania ingekuwa inakusanya nusu ya kodi zinazokwepwa na makampuni makubwa yanayotumia mbinu kali, basi tungehitaji misaada ya Marekani na hapa nchini angekuja kama mbia wa kweli na sawa katika dunia. Hivyo ni vema aungane na Waziri Mkuu wa Uingereza kuhakikisha kuwa makampuni makubwa hayatumii ‘tax havens’ kukwepa kodi katika nchi kama Tanzania. Uwazi wa mapato yao na kilicholipwa kwa Serikali ni vema usisitizwe sana na Obama mwenyewe ili makampuni yao yasikie na yaache kupora utajiri wa Afrika kiujanja ujanja.

Mwisho ni vema kama Rais Obama ataomba radhi kwa ushiriki wa Marekani kwenye mauaji wa Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo Patrice Lumumba. Hivi Tanzania inahangaika zaidi ya uwezo wake kupeleka majeshi huko mashariki ya Kongo kulinda amani.                                 
 
 
   Waafrika wengi tunaamini kuwa mauaji ya Lumumba ilikuwa ni kama laana kwa Taifa lile na hivyo limekuwa ni taifa la vurugu na vita licha ya utajiri mkubwa ulioko nchini humo. Nyaraka za CIA zinaonyesha dhahiri kuwa Rais wa Marekani wa wakati huo Lyndon Johnson aliagiza kuuwawa kwa mwanamapinduzi Patrice Lumumba. Kuwaomba radhi Waafrika na hasa Wakongo kuhusu mauaji ya Lumumba ni jambo litakaloweza kusaidia sana kurejesha amani Kongo.

Karibu Afrika, Karibu Tanzania ndugu Barack Hussein Obama.