Tuesday, 1 March 2016

Trump na Clinton watawala Jumanne Kuu

Clinton


  •  
Image copyrightReuters AFP
Image captionBw Trump na Bi Clinton wote wawili wameshinda majimbo saba kufikia sasa
Mgombea wa Democratic Hillary Clinton na mgombea wa Republican Donald Trump wamechukua uongozi wa mapema katika mchujo wa kuteua wagombea urais Marekani katika vyama vyao.
Wagombea wote wawili wameshinda majimbo saba kila mmoja. Wameshinda wote wawili majimbo ya Alabama, Georgia, Tennessee na Virginia.
ClintonImage copyrightGetty
Image captionClinton ameshinda majimbo matano
Bi Clinton pia ameshinda Arkansas na Texas, naye Bw Trump akashinda Massachusetts.
Bw Trump hata hivyo ameshindwa na Seneta Ted Cruz majimbo ya Texas na Oklahoma.
Mgombea wa Democratic Bernie Sanders naye ameshinda kwake nyumbani katika jimbo la Vermont, Minnesota, Colorado na pia katika jimbo la Oklahoma.
TrumpImage copyrightReuters
Image captionDonald Trump anaongoza chama cha Republican
Mchujo wa Jumanne Kuu hushuhudia majimbo 11 yakifanya mchujo kwa pamoja huku maandalizi ya uchaguzi mkuu tarehe 8 Novemba yakiendelea kushika kasi.
Bi Hillary Clinton, aliyekuwa wakati mmoja waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, pamoja na mfanyabiashara tajiri kutoka New York Donald Trump walipigiwa upatu kushinda majimbo mengi Jumanne Kuu.
Utafiti wa maoni ya paada ya kura ulikuwa umeonyesha Trump na gavana wa Ohio John Kasich wakikabiliana vikali katika mchujo wa chama cha Republican jimbo la Vermont, lakini baadaye Trump aliibuka mshindi.
Bi Clinton na Bw Sanders pia walikabiliana vikali katika jimbo la Massachusetts, kaskazini mashariki mwa Marekani lakini Clinton akaibuka mbabe
Matokeo kutoka majimbo yaliyosalia yanatarajiwa kutolewa katika saa chache zijazo.
Matokeo kwa sasa:
• Donald Trump (Republican): Alabama, Georgia, Massachusetts, Tennessee, Virginia, Arkansas, Vermont
 Ted Cruz (Republican): Texas, Oklahoma
• Marco Rubio (Republican): Minnesota
• Hillary Clinton (Democrat): Alabama, Georgia, Tennessee, Virginia, Arkansas, Texas, Massachusetts
• Bernie Sanders (Democrat):Vermont, Oklahoma, Minnesota, Colorado

0 comments: