MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

MATUKIO KATIKA PICHA YALIYO WEZA KUVUTIA DUNIANI KOTE

Asante kwa kututembelea mbeyagreennews kwa taarifa zaidi endelelea kututembela kila siku ,saa,dakika usipitwe na matukio kem kemu

Thursday, 24 March 2016

Juan Mata asema haya kuhusu Zlatan Ibrahimovic kujiunga Man United


March 23 headlines za nahodha wa timu ya taifa ya Sweden anayeichezea klabu yaParis Saint Germain ya Ufaransa Zlatan Ibrahimovic, jina lake limerudi kwenye headlines baada ya kiungo wa kimataifa wa Hispania anayeichezea klabu ya Man United Juan Mata kuzungumzia ujio wake Man United.
Juan Mata amezungumzia kuhusu tetesi za muda mrefu kuwa Zlatan atajiunga na Man United mwishoni mwa msimu huu akitokea Paris Saint GermainMata ameongea maneno haya baada ya kusikia tetesi hizo.
all-of-zlatan-ibrahimovics-26-league-goals-for-psg-this-season-video
Zlatan Ibrahimovic
Zlatan ni mchezaji mzuri na siku zote nimekuwa nikipenda kucheza na wachezaji wazuri, sina mamlaka ya kuamua ajiunge na Man United au vinginevyo, nafikiri huo ni uamuzi wake na klabu, kwangu itakuwa faraja kucheza nae ila sijui kama yeye ataamua kujiunga na Man United au kuendelea na PSG” >>> Mata
Bado haijajulikana kama Zlatan atajiunga na Man United mwishoni mwa msimu ila amekuwa akihusishwa kujiunga na vilabu kadhaa ikiwemo Arsenal, Chelsea na Man United. Kwa sasa Zlatan anatajwa kukaribia kumaliza mkataba wake na PS
G

Waziri Atoa Siku Moja Manispaa Kujieleza kwa taarifa ya mchanganuo wa fedha ( vinginevyo litakuwa jibu)


 
Manispaa ya Kigoma Ujiji katika Mkoa wa Kigoma imepewa masaa 24 kupeleka taarifa ya mchanganuo wa fedha iliyopokea kutoka Tamisemi katika bajeti ya mwaka 2014/2015 kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi ili kuhakiki matumizi.

 Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, Angela Kairuki baada ya kukagua miradi ya Tasaf na Serikali za mitaa katika Kata ya Majengo, Machinjioni na Kagera zilizopo katika Manispa hiyo.

Hatua hiyo ilikuja baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Sekondari ya Kirugu iliyopo Kata ya Machinjioni yaliyojengwa na Tasaf kwa gharama ya shilingi 40 milioni.

 Baada ya Shule hiyo kuomba msaada wa kupewa umeme kwa ajili ya kuongeza ari ya wanafunzi kujisomea, ndipo ilibainika shule huyo kupangiwa mgawo wa fedha kiasi cha shilingi 53 milioni kwa ajili ya kuingiza umeme na kujenga matundu ya vyoo ili kuondoa changamoto ya upungufu wa vyoo.

 Mkurugenzi msaidizi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Enock Nyanda alisema katika bajeti ya mwaka 2014/2015 Wizara hiyo ilitoa shilingi 2.46 bilioni kwa Halmashauri za Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, nyumba za Walimu na kuingiza umeme katika Shule za Sekondari.

 “Shule hii ya Kirugu ilipangiwa mgawo wa shilingi milioni 53 kwa ajili ya kujenga vyoo na kuingiza umeme, sasa wanapolalamika kwamba hawana umeme na vyoo havitoshi ni jambo linalohitaji ufuatiliaji kuona hiyo fedha iliyotolewa na Wizara ilipelekwa wapi,” alisema Nyanda.

 Waziri huyo aliyefuatana na Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya utawala bora na serikali za mitaa alimuagiza Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, John Shauri kuhakikisha taarifa ya mchanganuo wa fedha hiyo unafanyika.

 “Tunajua Mkurugenzi wa Manispaa hayupo ana wewe ni Kaimu tu lakini nakuagiza uandae taarifa kamili ya amatumizi yote ya fedha mliyopokea kutoka mgawo huo wa shilingi 2.46 bilioni mueleze nyie Manispaa mlipata kiasi gani na mlizitumiaje, hadi kesho saa tisa mchana muwe tayari mmetuma kwa Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene,” alisema Kairuki.

 Alisema hali ya miundombinu katika Shule hiyo ni mbaya na inabidi kurekebishwa haraka kutokana na baadhi ya madarasa kujengwa chini ya kiwango kutokana na kuta zake kuwa na nyufa miaka michache baada ya kukamilika kwa ujenzi.

 Kaimu Mkurugenzi huyo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya mifugo na uvuvi alisema hajui lolote kuhusu mchanganuo wa fedha iliyotolewa na Tamisemi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za Walimu, vyoo, madarasa na kuingiza umeme shuleni ingawa aliahidi kutekeleza agizo la Waziri Kairuki.

 Mbunge wa Mbulu mjini, Zakaria Essau alisema ipo haja kwa Serikali kutoa waraka kuonyesha umuhimu wa kutunza majengo ya Serikali ambayo mengi yamekuwa yakiharibika muda mfupi baada ya kujengwa.

Uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji La Dar es Salaam Kufanyika Baada ya Sikukuu ya Pasaka



Baada ya kumpata Meya wa Jiji la Dar es Salaam, mchakato wa kumchagua naibu meya umeanza.

Juzi, Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), Isaya Mwita alichaguliwa kuwa umeya akimshinda mpinzani wake Yusuph Yenga (CCM) kwa kura 84 dhidi ya 67.

Akizungumza jana, Meya Mwita alisema tarehe rasmi ya uchaguzi wa kumpata naibu meya haijafahamika na kwamba leo atashauriana na uongozi wa jiji na kwamba mara tu baada ya Sikukuu ya Pasaka ataitisha kikao cha baraza.

Mchakato wa kumpata naibu meya ni tofauti kwani idadi ya wajumbe watakaopiga ni ndogo ikilinganishwa na ile ya juzi ambayo madiwani wote na wabunge wote wa Mkoa wa Dar es Salaam walipigakura.

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe alisema jana kuwa wajumbe watakaomchagua naibu meya hawatazidi 25 kutokana na kanuni zilizopo .

Alisema naibu meya atapatikana katika kikao cha kwanza cha Baraza kitakachoongozwa na meya.

Alisema wajumbe watakaoshiriki kikao hicho ni wabunge wa majimbo, kila manispaa; Ilala, Temeke na Kinondoni itatoa wajumbe watatu watakaoteuliwa na mameya wao na Meya wa Jiji atateua watatu.

Mwenyekiti wa Kijiji Auawa na Kuchomwa Moto

Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Makibo Wilayani Sikonge Mkoani Tabora, Petro Ntakulo,  ameuawa kwa kuchomwa na moto na kundi la watu wasiojulikana kisha kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issah alisema tukio hilo limetokea usiku katika kijiji hicho kilichopo kata ya Nyahua.

Akielezea tukio hilo, alisema kulitokea sintofahamu iliyosababisha watu kukusanyika kufahamu kilichotokea na ndipo watu wasiojulikana wakamvamia mwenyekiti huyo na kumkata mapanga na kuuchoma mwili wake kwa moto.

Kamanda Issa alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana ambapo Jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi wanazidi kufanya uchunguzi ili kuweza kubaini chanzo cha mauaji hayo.

Kwa mujibu wa mmoja wa wakazi wa eneo hilo,Daud Musa, mbali ya kufanya mauaji hayo,watu hao pia walibomoa nyumba za marehemu na kuchoma mali zake .

Alizidi kueleza kuwa watu hao walikuwa wakidai kuwa hawataki kuwaona viongozi wa serikali eneo lao na kwamba hata wazee nao hawatakiwi.

Alieleza kuwa ulipigwa mwano (ishara ya hatari) na wananchi kukusanyika na ndipo baadhi yao waliokuwa wamejiandaa kufanya mauaji kutekeleza malengo yao.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Peter Nzalalila, amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkonono na badala yake wafuate sheria kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi.
"Wananchi wanapaswa kutii mamlaka zilizopo na sio kujichukulia sheria mkononi bali waache vyombo vya dola vifanye kazi yake’’ alisema Nzalalila.

Tukio hilo limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa eneo hilo, wakisema marehemu alikuwa kiongozi mzuri na aliyejua wajibu wake.

Hukumu ya Mbunge wa ubungo Saed Kubenea kutolewa April 13 2014

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda inayomkabili Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, Aprili 13, mwaka huu.

Hukumu hiyo itatolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya upande wa mashtaka unaowakilishwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa na upande wa utetezi ukiongozwa na Peter Kibatara kuwasilisha hoja zao za mwisho.

Uamuzi huo ulitolewa jana na mahakama hiyo baada ya Kubenea na mashahidi wake watatu, akiwamo mwandishi wa New Habari 2006, Shabani Matutu na Josephat Isango wa Mwanahalisi kutoa ushahidi wao.

Akitoa ushahidi wake, Matutu alidai kuwa Desemba 14, 2016 katika Kiwanda cha Tooku Garments Co. Ltd kilichopo Mabibo External kwenye mgomo wa wafanyakazi, hakusikia Kubenea akimuambia Makonda kuwa ni mjinga, mpumbavu, kibaka na cheo chenyewe kapewa.

Alidai alimsikia mbunge huyo akimuuliza Makonda “kwa nini unafunga mkutano bila ya kunipa nafasi ya kuongea wakati mgogoro nimeuanza mimi kuutatua, mimi siyo kibaka nimekuja baada ya kuitwa na wananchi walionichagua kwa kura 87,000”.

Kubenea anadaiwa kumtolea lugha chafu Makonda alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Walinzi Watatu wa Suma JKT Mbaroni Kwa Wizi wa Kompyuta 50 Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM )



Walinzi watatu wa Suma JKT na askari mmoja wa Kituo  Kikuu cha Polisi Mkoa wa Dodoma, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za wizi wa kompyuta zinazokadiriwa kufikia 50 mali ya Chuo Kikuu Dodoma (Udom).

Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa wizi huo ulitokea juzi baada ya chuo hicho kufungwa kwa ajili ya mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka.

Inadaiwa kuwa katika wizi huo baadhi ya walinzi wa Suma JKT ambao wanajukumu la kulinda chuo hicho, walihusika huku watatu wakishikiliwa na polisi.

Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa baadhi ya askari wa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma wanadaiwa kuhusika na kuzua mkanganyiko katika uchunguzi wa tukio hilo.

“Katika wizi huo, pia kuna  askari kutoka mjini ametajwa na walinzi wa Suma JKT kuhusika, sasa baada ya kupata taarifa hizo ndiyo wanafanya mpango wa kumkamata,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Ofisa Habari wa Udom, Beatrice Baltazar jana alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba, bado hawajajua idadi kamili ya kompyuta zilizoibiwa.

“Ni kweli kuna wizi wa kompyuta hapa chuoni, lakini sijajua idadi kamili ya kompyuta zilizoibwa, ila kuna walinzi watatu wa Suma JKT wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano,” alisema Beatrice.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa naye alithibitisha kuwapo kwa taarifa za tukio hilo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani kwa kuwa yupo likizo.

Hata hivyo, Mambosasa alikanusha kuwa hakuna polisi aliyehusika katika tukio hilo bali ni walinzi wa Suma JKT.

“Hakuna askari wetu aliyehusika katika tukio hilo, wenye jukumu la kulinda chuo hicho ni Suma JKT ndiyo wanaoshikiliwa kwa mahojiano zaidi,” alisema Mambosasa.

Wednesday, 23 March 2016

Kiti cha UPDP chayeyuka Zanzibar....ZEC Yasema Yalifanyika Makosa ya Kiufundi Wakati wa Kujaza Karatasi ya Matokeo














Ofisa mdhamini wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Ali Mohammed Dadi amesema mshindi wa uwakilishi katika Jimbo la Ziwani ni Suleiman Ali wa CCM na si Asaa Hamad wa UPDP aliyetangazwa awali.

Dadi kutoka ofisi ndogo ya Pemba alisema jana kuwa msimamizi wa uchaguzi katika Wilaya ya Chakechake, Othman Hamisi alikosea wakati wa kujaza karatasi ya matokeo ya mshindi wa jimbo hilo.

“Nimezungumza naye na amesema kwamba alitoa ufafanuzi kuwa walifanya makosa katika kuandika matokeo, hivyo aliyeshinda ni mgombea wa CCM,” alisema.

Katika karatasi hiyo ya matokeo iliyokuwa imebandikwa ukutani, Asaa Ali Hamad alionekana kuwa amepata kura 221 dhidi ya 121 za mgombea wa CCM, lakini kwa ufafanuzi huo wa ZEC hakuna chama cha upinzani kilichoshinda nafasi ya uwakilishi au udiwani.

Kwa matokeo hayo, CCM imeshinda majimbo yote ya uwakilishi Unguja na Pemba na hivyo kuzidisha utata kwa Rais mteule, Dk Ali Mohamed Shein anayeapishwa leo, kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwa mujibu wa ibara ya 9 (3) ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 toleo la 2010.

Awali, kulikuwa na uwezekano wa UPDP kutoa mteule wa nafasi ya makamu wa kwanza wa Rais kwa kuwa kilitangazwa kimakosa kupata kiti cha uwakilishi baada ya CCM lakini baada ya ufafanuzi huo wa ZEC matumaini hayo yameyeyuka. 
 
Kuyeyuka kwa ndoto hiyo ya UPDP kunamaanisha kwamba hakuna chama kilichoshika nafasi ya pili kwa kupata kura asilimia 10 au zaidi, ambacho kwa mujibu wa Katiba hiyo kingekuwa na nafasi ya moja kwa moja kutoa makamu wa kwanza wa rais na baadaye mawaziri wa upinzani kuunda SUK. 
 
Tangu Dk Shein atangazwe kushinda urais katika uchaguzi wa marudio baada ya matokeo ya ule wa awali kufutwa, mjadala mkubwa kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii umekuwa ni jinsi gani atateua Serikali yake kukidhi matakwa ya Katiba ya kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ili kuendeleza maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa baina ya CCM na CUF kabla ya uchaguzi wa 2010.

Wakati Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akisema Rais Shein atatumia busara zake kumpata makamu wa kwanza wa rais, baadhi ya wanasheria wamesema hawaoni ufumbuzi wa moja kwa moja kutokana na upungufu huo wa kikatiba.

Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar, Rais atateua makamu wa kwanza wa Rais kutoka chama kilichoshika nafasi ya pili na mgombea wake wa urais kupata asilimia 10 ya kura za urais, au nafasi ya makamu wa kwanza itaenda kwa chama chochote cha upinzani kilichoshika nafaso pili kwa wingi wa viti vya majimbo katika Baraza la Wawakilishi.

RC Kijuu: Watumishi HEWA Anzeni Kujiondoa Kabla Sijawakamua Majipu

 


Mkuu  mpya  wa  Mkoa  wa  Kagera,Meja  Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amewaagiza  watumishi  wasio  na  sifa za  kuajiriwa kujiondoa  kabla  ya March  31  mwaka  huu.

Kijuu  alitoa  kauli  hiyo  jana  wakati  wa  Makabidhiano  ya  ofisi baina  yake  na  mkuu  wa  mkoa  wa  zamani,John Mongella ambapo alisema  kwamba  Tanzania  inawatumishi  hewa  zaidi  ya 2000, hivyo ana imani  hata  Kagera  wapo.

"Hao watumishi  hewa  endapo  watang'ang'ania kubaki katika vitengo  walivyopo  nitawashughulikia wahusika  wakuu  wa  vitengo  hivyo," alisema

Aidha, aliagiza wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kusimamia uundwaji wa mabaraza  ya  usuluhishi kuanzia ngazi za kata hadi  mkoa  ili  kusimamia  haki  za  wananchi.

Pia  aliwataka  watumishi  wa  serikali  mkoani  humo kufahamu maudhui ya "Hapa Kazi Tu", kwa kufanya kazi kwa kasi,haraka, nguvu, maarifa  na  uadilifu.

Aliwataka  kutosubiri  kusukumwa, lakini wajitambue wao ni akina  nani na  wanapaswa  kufanya  nini  kutokana  na  majukumu  waliyopewa.

Alisema  ili  kufikia  lengo  la  Rais John Magufuli la kuwatumikia wananchi  kwa  uaminifu  ni  lazima  kushikiria  uadilifu  na  kutambua  kwamba watumishi wapo kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii.

Maalim Seif: CUF haitashiriki uchaguzi wowote chini ya Tume ya Jecha Salim Jecha


SIKU mbili tangu kufanyika kwa uchaguzi wa marudio Zanzibar, na siku moja kabla ya kuapishwa Dk Ali Mohamed Shein, Maalim Seif Shariff Hamad, Mgombea wa Urais wa Zanzibar katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana kupitia Chama cha Wananchi (CUF), amesema CUF haitashiriki uchaguzi wowote chini ya Tume ya Jecha Salim Jecha. 

Akizungumza na MwanaHALISI Online Hoteli ya Serena ambapo yupo kwa mapumziko baada ya kulazwa, Maalim Seif amesema kuwa kama yatatokea maridhiano yatakaoongozwa na kusimamiwa na taasisi huru za kidemokrasia, bila vitisho vya majeshi na polisi, kuwa na vyombo huru vya habari na tume huru sio hii iliyopo Zanzibar chini ya Jecha, hapo CUF kitaweza kufikiri kushiriki uchaguzi.

Ameongeza kuwa harakati za kudai haki, zitaendelea kwa njia ya amani ili marekebisho ya tume yafanyike kwani kwa utaratibu uliopo hata mwaka 2020 upinzani ukishinda Tanzania bara, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitang’gang’ania madaraka.

“CUF tunaamini katika amani, tusichafue amani, tusichafue nchi yetu, tuendeleze mapambano kwa kutoitambua serikali iliyojiweka madarakani katika uchaguzi haramu wa Machi 20 mwaka huu, wala hatutaipatia ushirikiano wowote katika mambo yote” alisema na kuongeza :

"Uchaguzi wa 20 Machi, sio halali. Jecha hakuwa na uwezo wa kisheria wala kikatiba kufuta uchaguzi, mgogoro uliopo sasa umesababishwa na Jecha, ukapewa baraka za CCM, sababu CCM hawataki kushindwa, na hawataki wapinzani kuongoza. Kila CCM ikishindwa hutoa visingizio.

“Kabla Kikwete (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) hajaondoka madarakani, aliniambia kuwa Maalim CCM wanakuogopa, wanajua ukishinda utaweza kuvunja Muungano, lakini nilimwambia, CCM ndio wenye jeshi, wenyewe ndio wenye dola mimi nitavunjaje Muungano?

"Hiyo ni hofu na visingizio tu ili waendelee kukwapua madaraka.”Alisema.

Ameweka bayana kuwa kwa sasa CCM imewarejesha wananchi miaka 20 iliyopita, kwani uhasama wa watu kutengana kwenye shughuli za kijamii kwa sababu za tofauti za kisiasa zimeanza kurejea baada ya CCM kulazimisha kukwapua madaraka ya wananchi kwa kufuta uchaguzi wa 25 Oktoba mwaka jana.

Akizungumzia suala la Muungano kama ambavyo amekuwa akihusishwa Maalim seif amesema kuwa sasa Muungano utavunjwa na CCM, sio CUF wala yeye kama wanavyosingizia.

Ameongeza kuwa kwa sababu CCM ya bara ndio inalazimisha kuweka viongozi waliokataliwa na wananchi wa Zanzibar na chama chao kwa kutumia majeshi na polisi wao ndio husababisha wananchi wachukie Muungano.

Aidha kuhusu uchaguzi wa marudio wa Machi 20, Seif amesema kuwa CUF imeshinda, kwani wananchi wa Zanzibar waliitikia wito wa CUF, wakasusa, hawakujitokeza kupiga kura. 

“Mimi nilishasema tangu awali, kuwa matokeo yameshajulikana kabla ya uchaguzi, sababu ni ya kupika, namhurumia Dk Shein kwa kujisifu kupata kura ambazo hazipo, mawakala waliweka wao na wasimamizi na kuna taarifa kuwa wapigakura walikuwa wanapewa rundo la kura, wapige na kutumbukiza ili kukidhi matakwa ya CCM.” Amesema Maalim Seif.

Maalim Seif amewatakia utulivu Wazanzibar wote, na kuwaarifu kuwa afya yake ni imara, na atarejea Zanzibar wakati wowote kuungana nao

CCM na CUF Watwangana Ngumi Pemba Wakati Wakisherehekea Ushindi wa Dr. Shein

Jeshi la Polisi jana walitumia mabomu ya machozi kurejesha hali ya amani baada ya wananchi kuanza kupigana kwa sababu za kisiasa wakati wakisherehekea ushindi wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, katika kijiji cha Mjini Wingwi Wilaya ya Micheweni, Pemba.

Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Micheweni, Rashid Khalid Salim, alidai vurugu hizo zimesababishwa na wanachama wa CCM kutoka katika kijiji cha Kwale wilayani humo.

Alisema baada ya Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa marudio, wanachama wa CCM katika kijiji cha Kwale, walianza kukusanyika na ngoma zao na kuanza safari ya kuingia katika kijiji cha Mjini Wingi, sehemu ambayo ni ngome ya wanachama wa CUF, huku wakisherehekea kwa kurusha 'vijembe' (maneno ya kejeli) na matusi.

“Pamoja na kutakiwa kuacha matusi wakati wakisherehekea ushindi wa Dk. Shein, waliendelea na kusababisha wenzao kupandwa na ghadhabu kuwachemka na kuanza kupigana,” alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema baada ya kutokea vurugu hizo, wanachama wa CCM kutoka kijiji cha Kwale, walilazimika kukimbilia Kituo cha Polisi Micheweni.

Alisema askari walipofika eneo la tukio, walianza kupiga mabomu ya kutoa machozi na kuvunja milango ya nyumba.

Mwenyekiti huyo alisema nyumba 15 zilivunjwa milango wakati wakiwasaka watu waliokuwa wakihusishwa na vurugu hizo ambazo zilianza kufanyika saa 10:00 jioni na kuendelea hadi usiku juzi.

Aidha, alisema kwa mujibu wa mabaki ya milipuko, jumla ya mabomu 27 yanadaiwa kupigwa mbali na nyumba kuvunjwa milango na kusababisha watu zaidi ya 28 kuyakimbia makazi yao katika kijiji hicho.

“Watu wanne wamekamatwa akiwamo mtoto mwenye umri wa miaka 13, lakini wananchi wengi wamekimbia makazi yao na kukimbilia katika kisiwa cha Kojani na Maziwang'ombe,” alisema Rashid.

Hata hivyo, alisema jambo la kushagaza polisi wameamua kuwakamata watu waliofanyiwa fujo badala ya kuwakamata waliokuwa chanzo cha vurugu hizo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Hassan Nassir, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kwamba watu watano wanashikiliwa kwa uchunguzi wa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo, alikanusha kuvunjwa milango 15 pamoja na kutumika mabomu 27 kurejesha hali ya utulivu baada ya wananchi kuanza kupigana.

Waliokamatwa katika mkasa huo ni Kombo Khalfan Faki, Salim Hassan Khamis, Mjawiri Faki, Khatib Dawa Juma na Assaa Bakar Ali, wakazi wa kijiji hicho.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa huo, Omar Khamis Othman, alisema hali katika kijiji hicho imerejea kuwa ya kawaida na kuwataka wananchi kuendelea na sherehe za kumpongeza Dk. Shein bila ya kuvunja sheria.

Alisema wananchi waliokimbia makazi yao na kukimbilia katika kisiwa cha Kojani na Maziwang'ombe, watakuwa ndiyo waliohusika na vurugu na kwamba raia mwema hana sababu ya kukimbia askari.

Maamuzi mengine leo kutoka kwa Waziri wa Magufuli


March 23 2016 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekutana na Baraza la Wazee wa Dar es salaam na kusikiliza changamoto zinazowakabili katika jamii.
Katika kutatua changamoto zinazowakabili wazee, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeonyesha imedhamiria kutoa kipaumbele kwa wazee na imesisitiza kusimamia Sera ya Serikali ya kutoa huduma za afya bure kwa wazee.Waziri  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy  Mwalimu amezungumza na waandishi wa habari na kusema….
>>’kuhusu huduma kwa wazee hasa matibabu tunataka kuwathibishia bado inabaki kuwa ni sera ya Serikali  na kwamba wazee Tanzania wanatakiwa  kupata matibabu bure, kuanzia gharama ya kumuona Daktari, vipimo na Dawa. Naendelea kuziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatekeleza Sera ya Serikali ya kutoa huduma za afya bure ikiwemo kuanzisha dirisha la wazee‘.
>>>’na kuonyesha kwamba nimedhamiria nimeshaongeas na watu wa bima ya afya mwezi ujao tutatoa matangazo ambayo tutaweka katika vituo vyote vya Serikali ‘Mzee kwanza, Mzee alikuwa kama wewe na wewe utakuwa kama yeye, tafadhali toa kipaumbele cha huduma kwa wazee’ tayari tumeshaaanza tunatafuta siku ya kuyazindua ili kuendelea kuhamasisha kipaumbele kwa wazee

Tuesday, 22 March 2016

FIFA kuchunguza Beckenbauer, 5 wengine


Image copyrightAP
Image captionBeckenbauer na wengine 5 kuchungwa na FIFA
Aliyekuwa Nahodha na kisha kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani iliyotwaa kombe la dunia Franz Beckenbauer ametajwa katika orodha ya watuhumiwa 6 wanaoshukiwa kutoa hongo kununua kombe la dunia la mwaka wa 2006 huko Ujerumani.
Kamati ya maadili ya FIFA imetoa orodha wa watu 6 waliongoza kampeini hiyo ya kutwaa uwenyeji wa kombe la dunia.
Shirikisho la soka la Ujerumani lilipasua mbarika lilipofichua ripoti ya upelelezi ambayo ilimpelekea Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani kukiri kuwa alifanya makosa wakati wa kuwania zabuni ya wenyeji wa kombe hilo la dunia.
Mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita, Beckenbauer, 70, aliomba msamaha kwa hatua na kauli alizotoa wakati wa kuwania uwenyeji wa mashindano hayo.
Ujerumani wakati huo iliishinda Afrika Kusini kwa kura moja pekee.
Image copyrightREUTERS
Image captionMnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita, Beckenbauer, 70, aliomba msamaha kwa hatua na kauli alizotoa wakati wa kuwania uwenyeji wa mashindano hayo.
Ujerumani ilipata kura 12 dhidi ya 11 za Afrika Kusini katika uchaguzi uliofanyika mwaka wa 2000.
Orodha kamili
  1. Franz Beckenbauer
  2. Wolfgang Niersbach
  3. Helmut Sandrock
  4. Theo Zwanziger
  5. Horst Schmidt
  6. Stefan Hans